Monday, July 20, 2015

Ujumbe wa Maafisa Waandamizi kutoka Nigeria watembelea Wizara ya Mambo

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akiukaribisha Ujumbe wa Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi ya Taifa ya Mafunzo ya Sera na Stratejia ya Nigeria walipotembelea Wizarani  tarehe 20 Julai, 2015. Ujumbe huo upo nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku 12 ambapo watatembelea Wizara na Taasisi mbalimbali za hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu kuzungumza na ujumbe huo kutoka Nigeria.
 JUU NA CHINI:
Baadhi ya wajumbe wa msafara huo wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

 Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Simba akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa msafara huo Bw.Hamakim Jonny Godwin. 
Picha ya pamoja.

Sunday, July 19, 2015

Wizara yawapokea Madaktari kutoka Marekani


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akiwakaribisha nchini Timu ya Madaktari kutoka Marekani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam hivi karibuni. Madaktari hao wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa magonjwa mbalimbali katika Hospitali za Mwananyamala ya Jijini Dar es Salaam na Mnazi Mmoja, Zanzibar. Ziara ya Madaktari hao ambao wametoka Majimbo ya Washington DC, Maryland na Virginia imeratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani (Diaspora).
Rais wa Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani, Bw. Iddi Sandaly ambaye amefuatana na Madaktari hao kutoka Marekani akielezea jambo mara baada ya kuwasili nchini.
Bibi Jairo akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu dhumuni la ziara ya madaktari hao hapa nchini.
Mmoja wa Madaktari kutoka Marekani akizungumza na Waandishi kuhusu  ziara yao hapa nchini
Bw. Sandaly akifafanua jambo kwa waandishi kuhusu ziara ya madaktari hao kutoka Marekani.

Thursday, July 16, 2015

Waziri Membe afuturisha Mashehe na watumishi wa Wizara

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Mhe. Bernard K. Membe akiwakaribisha  Mashehe pamoja na  Watumishi wa Wizara (hawapo pichani)   kabla  ya kushiriki  Futari aliyoiandaa kwa ajili yao nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam  hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza kulia), akiwa pamoja na Mashehe walioudhuria Futari hiyo
Waziri Membe akiendelea kuzungumza na kuwakarisha wageni wote nyumbani kwake
Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Nigel Msangi akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Waziri Membe na Familia yake  kwa niaba ya Watumishi wa Wizara na Wageni wengine walioalikwa  kufuturu pamoja na Mhe. Membe nyumbani kwake
Mhe. Membe akiwa na Kadhi Mkuu walioshiriki futari hiyo
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje walioshiriki futari nyumbani kwa Mhe. Membe
Wageni waalikwa
Mke wa Waziri Membe, Mama Dorcas Membe (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju wakati wa futari iliyoandaliwa na Familia ya Waziri Membe kwa Watumishi wa Wizara.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba wakati wa futari nyumbani kwa Mhe. Membe. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa APRM, Bibi Rehema Twalib, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga na Bi. Aisha Mandia.
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa futari hiyo
Watumishi wa Wizara wakiwa wametulia kabla ya kuanza kufuturu
Waziri Membe akimpongeza Kadhi Mkuu baada ya kuhutubia
Shehe  akitoa dua kabla ya kuanza kufuturu
Dua ikiendelea
Mhe. Membe akiwaongoza wageni wake kuchukua futari

Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Mashehe na Wageni wengine aliwaalika kufuturu pamoja nae.

Picha na Reginald Philip

Monday, July 13, 2015

Press Release

King of Saudi Arabia,  H.H. Salmanbin Abdulaziz Al Saud

PRESS RELEASE

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a condolence message to H. H. Salmanbin Abdulaziz Al Saud, the King of the Kingdom of Saudi Arabia on the passing on of Prince Saud al-Faisal, former Foreign Minister of the Kingdom of Saudi Arabia which occurred on 9th July, 2015. 

The message reads as follows;

“His Highness, Salmanbin Abdulaziz Al Saud
King of the Kingdom of Saudi Arabia,
Riyadh.

Your Highness,

I have learnt with deep sorrow and sadness the passing on of Prince Saud al-Faisal, former Foreign Minister of the Kingdom of Saudi Arabia which occurred on 9th July, 2015.

On behalf of the Government and  the People of the United Republic of Tanzania I wish to convey to you, and through you, to the people of the Kingdom of Saudi Arabia, particularly the royal family of the bereaved our heartfelt condolence  and deep sympathies.
 
In this time of grief, our heartfelt and prayers are with the royal family and the people of the Kingdom of Saudi Arabia in general.

Please accept, Your Highness, the assurance of my highest consideration”.

Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam
13th July, 2015

Friday, July 10, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Palestina

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano  wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akimkabidhi picha yenye mchoro wa Mlima Kilimanjaro Balozi wa Palestina aliyemaliza muda wake wa uwakilishi nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Nasri Abu Jaish. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Wizara ya Mambo ya Nje.
Balozi Simba akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Palestna nchini.
Picha juu na chini ni Mabalozi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Simba (Hayupo pichani)
Balozi Jaish akitoa neno la shukrani kwa ushirikiano na upendo aliokuwa akipata kutoka Wizarani na kwa watanzania kwa ujumla.  
Balozi Jaish akiendelea kuongea. 
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba akimpongeza Balozi Jaish mara baada ya kumaliza kuzungumza
Balozi Jaishi akimkabidhi Balozi Simba zawadi ya Picha yenye mfano wa Nyumba ya Ibada (Msikiti)
Naibu Kaitbu Mkuu Balozi Hassan Simba Yahya akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Palestina aliyemalimaliza muda wake wa uwakilishi nchini Tanzania.
Balozi Simba (Wa tatu kutoka kushoto), Balozi Jaish (Wa nne Kutoka kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Joseph Sokoine (Wa pili Kutoka Kushoto), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Bwa. Elibariki N. Maleko, wa kwanza, wapili na watatu ni Maafisa Mambo ya Nje.


Picha na Reginald Philip

Thursday, July 9, 2015

MEMBE ASISITIZA UMUHIMU WA VIWANDA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.), akiongea kwenye muhadhara kabla ya Mtoa mada mkuu Prof. Justin Yifu Lin hajaongea katika muadhara uliokuwa unazungumzia umuhimu wa viwanda nchini ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje 
Makamu wa Rais wa zamani wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin akitoa mada yake juu ya uwanzishaji wa viwanda nchini Tanzania katika muadhara ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya (Kulia), na kushoto ni Balozi Mstaafu Mhe. Elly Mtango wakisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Dkt. Lin (hayupo pichani). 
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza kwa makini Prof. Lin (hayupo pichani), Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Nigel Msangi, Kushoto ni Afisa Mawasiliano mwandamizi wa Mambo ya Nje Bw. Ally Mkumbwa nao wakifuatilia kwa makini Muhadhara uliokuwa ukiendelea 
Balozi Simba akichangia mada katika muadhara uliokuwa ukiendelea  
Muhadhiri Chuo cha Diplomasia Bw. Innocent Shoo akiuliza swali 
Afisa Mambo ya Nje Bi. Felisita Rugambwa naye akiuliza swali katika muhadhara 
Dkt Lin akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kulizwa.
Picha ya juu na chini ni watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje nao wakisikiliza mada kwa makini
KKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akitoa neno la shukrani kwa Prof. Lin, kwa niaba ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje mara baada ya kumalizika kwa muhadhara huo
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo huku akisikilizwa na Prof. Lin (Kulia) na Mhe. Membe (Katikati). 
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Diaspora Bi. Rosemary Jairo akizungumza jambo kwa Prof. Lin (kushoto) na Katibu Mkuu Balozi Mulamula.

Picha na Reginald Philip



  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, amesema upatikanaji wa gesi ni nyenzo muhimu ya uendelezaji wa viwanda vya kati ili kutengeneza ajira na kuharakisha maendeleo ya nchi.

Mhe. Membe alipongeza uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu za Afrika itakapohamishia baadhi ya viwanda vyake, akazitaka taasisi za uwekezaji na uendelezaji wa viwanda kuweka mikakati madhubuti ya kutumia fursa hiyo kikamilifu.

Mhe. Waziri alisema hayo leo wakati wa mhadhara wa aliyekuwa Mchumi Mkuu na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar Es Salaam, uliohudhuriwa na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na wadau wengine.

Alisema uendelezaji wa viwanda lazima utiliwe mkazo katika mpango wa Tanzania kuingia uchumi wa kati 2025. "Tuache kukimbilia viwanda vikubwa vinavyohitaji mitaji mikubwa, ambayo hatuna.Tuchague viwanda vya kati vitakavyoajiri watu wengi kwa uwekezaji wa wastani."

Mhe. Membe alisema uendelezaji wa viwanda usambae nchi nzima ili kuvutia vijana kuishi vijijini badala ya kukimbilia mijini. "Sasa hivi nchi yetu ina viwanda takriban 3,000 lakini zaidi ya theluthi mbili viko Dar Es Salaam. Lazima umeme upelekwe vijijini kuleta uwiano wa maendeleo ya viwanda," alisisitiza.

Katika mhadhara wake, Prof. Lin alisema nchi nyingi zinazoendelea zilifanya maamuzi yasiyo sahihi kuhusu viwanda. "Nchi nyingi zilifuata kile kinachoitwa Muafaka wa Washington na kuanzisha viwanda vikubwa kwa maelekezo ya nchi tajiri, ambavyo viliwashinda kuendesha kwa kuwa vilihitaji uwekezaji mkubwa sana."

Alisema nchi za Asia zilizoendelea kwa haraka ni zile zilizoamua kuzingatia mazingira halisi na kwenda hatua kwa hatua katika kuanzisha viwanda. "Hii iliimarisha uchumi wao na kuukuza."

Prof. Lin alisema serikali zina wajibu wa kusimamia uendelezaji wa viwanda kwa kuweka sera sahihi, kuhimiza uwekezaji kwenye uzalishaji wa bidhaa zenye masoko ya uhakika na kusaidia sekta binafsi ishiriki kikamilifu.

Akiongelea Tanzania, Mchumi huyo wa Kichina alisema ingawa gharama za ajira ziko chini, gharama za uendeshaji ziko juu, hivyo hazivutii uwekezaji. Alisema moja ya sababu kubwa za Shilingi ya Tanzania kushuka thamani ni uuzaji mdogo wa bidhaa nchi za nje.

(mwisho)