Sunday, October 18, 2015

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wamuaga Rais Kikwete





Picha zote za juu zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakati alipowasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha cha Mikutano cha Julius Nyerere ambapo Wizara ya Mambo ya Nje ilifanya hafla ya kumuaga Mhe. Rais.

Rais Kikwete akifunua kitambaa ambapo nyuma yake kuna picha ya Jengo la Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje linalokusudiwa kuanza kujengwa hivi karibuni. Rais Kikwete alifunua kitambaa hicho kuashiria kuanza ujenzi wa jengo hilo.


Rais Kikwete akipiga makofi kuonesha furaha yake kuwa Wizara ya Mambo ya Nje itapata ofisi za kisasa hivi karibuni

Rais Kikwete akiongozwa kuelekea ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya kufanya hafla ya kumuaga. Wanaomuongoza ni Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe wa kulia kwa Rais Kikwete na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga akitoa neno la kuwakaribisha wageni waalikwa akiwemo Rais Kikwete katika hafla ya kumuaga.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akitoa utambulisho wa wageni waalikwa wakiwemoWaheshimiwa Mabalozi waliostaafu.

Balozi Mstaafu akisalimia wajumbe baada ya kutambulishwa

Watumishi wa Wizara wakiwemo Wakuu wa Idara/Vitengo, Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi wakiwa wameketi kwa ajili ya kushuhudia matukio ya hafla ya kumuaga Rais Kikwete.

Sehemu ya watumishi wa Wizara waliohudhuria hafla ya kumuaga Rais Kikwete

Watumishi wa Wizara katika hafla ya kumuaga Rais Kikwete

Mtumishi wa Wizara akisoma utenzi wa kumsifu na kumpongeza Rais Kikwete namna alivyoongoza Taifa la Tanzania kwa umahiri mkubwa katika kipindi chake cha miaka 10 ambacho kinakamilika Oktoba 2015.

Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Bernard K.Membe akisoma hotuba yake katika hafla hiyo. Hotuba ya Waziri Membe iligusia mafaniki ambayo Serikali ya awamu ya nne imeyapata katika kipindi cha miaka 10 ikiwa ni pamoja na kuvutia wawekezaji wakubwa, kuongeza uwakilishi nje ya nchi,kujenga ofisi za kibalozi na utatuzi wa migogoro.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Membe wakionesha Tuzo aliyotunukiwa Rais Kikwte na Wizara ya Mambo ya Nje.



Picha za juu zinaonesha zawadi mbalimbali ambazo Rais Kikwete amekabidhiwa wakati wa hafla hiyo

Rais Kikwete akiongea na watumishi wa Wizara na wageni waalikwa. Katika mazungumzo yake Rais Kikwete alisisitiza umuhimu wa watumishi wa Wizara kudumuisha na kuimarisha mahusiano mazuri na nchi zote duniani. Alisema katika kipindi cha uongozi wake mafanikio makubwa ya kidiplomasia yamepatikana hivyo ni vyema watumishi wa Wizara wakayaendeleza kwa kiwango cha juu zaidi.

Picha ya pamoja kati ya Mhe. Rais Kikwete, Mhe. Waziri Membe, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje,Wakuu wa Idara/Vitengo na Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi


Mhasibu Mkuu wa Wizara, Bw. Paul Kabale akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  watumishi wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu



Saturday, October 17, 2015

Rais Kikwete Azindua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Bandari kubwa ya Bagamoyo.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wa tatu waliosimama kutoka kushoto, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Wengine kutoka kwa Rais Kikwete ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youqing, Mtendaji Mkuu wa Mfuko Mkuu wa Akiba wa Oman, Mhe. Abdulsalam Murshidi, Mawaziri na viongozi mbalimbali wote kwa pamoja wakiwashuhudia Wawakilishi wa nchi za Tanzania,Oman na China wakiweka saini Makubaliano ya kujenga Bandari kubwa na ya kisasa ya Bagamoyo.
Wawakilishi hao wakionyesha nyaraka za mmakubaliano walizosaini na kubadilishana kama ishara ya wazi ya kuanza kwa ujenzi wa Bandari hiyo.
Mhe. Rais Kikwete akiweka rasmi jiwe la msingi la Bandari hiyo huku Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda pamoja na viongozi wengine wa Oman, Tanzania na China  wakishuhudia.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), Makamu wa Rais wa kampuni ya China Merchants Group, Dkt. Hu Jianhua (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mfuko Mkuu wa Akiba wa Oman Mhe. Abdulsalam Murshidi,  (kulia) wakichanganya udongo,kama ishara ya kukubaliana kuanza rasmi ujenzi wa mradi huo wa Bandari.
Mhe. Rais akiwa katika picha ya pamoja mara tu baada ya kuweka jiwe la msingi na kuchanganya udongo.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza muda mfupi kabla ya kutiliana saini na kuweka jiwe la msingi ili kubariki ujenzi wa Bandari ya kisasa ya Bagamoyo.

Katika uzinduzi huo Mhe. Rais amesisitiza serikali ihakikishe wananchi wote waliopisha eneo lao ili kujengwa kwa bandari hiyo wanalipwa fidia stahiki ikiwa ni pamoja na kujengewa nyumba nzuri za kisasa.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda akizungumza katika mkutano huo.
Balozi wa China hapa nchini,Mhe. Lu Youqing akitoa hotuba fupi katika mkutano huo wa uzinduzi na uwekaji jiwe la msingi ili kujenga Bandari kubwa na ya kisasa ya Bagamoyo.
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Samwel John Sitta akitoa hotuba yake kuhusu mambo ya uchukuzi,kabla ya kuzinduliwa kwa ujenzi wa Bandari hiyo.
Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni inayojenga mradi huo wa Bandari ya Bagamoyo ya China Merchants Group, Dkt. Hu Jianhua, akizungumza katika mkutano huo.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko Mkuu wa Akiba wa Oman, Mhe. Abdulsalam Murshidi akizungumza na kutoa shukrani za kipekee kwa Rais Kikwete kwa kukubali kuzindua na kuweka jiwe la msingi la mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akizungumza machache kuhusu mambo ya uwekezaji hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo akitoa hotuba fupi wakati wa uzinduzi huo wa Bandari ya Bagamoyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kulia) akizungumza na  Mkuu wa Itifaki, Balozi Juma Mohammed Maharage wakati wa uzinduzi huo.
Mabalozi mbali mbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Wakurugenzi na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya  Nje pamoja na Wananchi waliohudhuria kushuhudia uzinduzi wa ujenzi wa Bandari hiyo ya Bagamoyo.

Moja ya picha inayoonyesha ramani ya Bandari hiyo itakavyokua.

Mkutano huo ukiendelea.
 Mabalozi mbalimbali wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mheshimiwa Rais.
Mabalozi mbalimbali wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mheshimiwa Rais. 
 Mabalozi mbalimbali wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mheshimiwa Rais.
 Kikundi cha ngoma cha kabila la Wakwere, kikitumbuiza katika uzinduzi huo.
==========================
PICHA NA: REUBEN MCHOME.

Thursday, October 15, 2015

Flyover ya TAZARA kuanza kujengwa mwezi ujao

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale (kulia) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya SUMITOMO MITSUI, Bw. Ichiro Aok kutoka Japan wakiweka saini Mkataba wa kuanza ujenzi wa barabara ya juu (flyover) katika eneo la TAZARA. 

SUMITOMO MITSUI ni kampuni iliyoshinda zabuni ya kujenga barabra hiyo, ambao ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Novemba 2015 na kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu. 

Wengine katika picha waliosimama watatu kutoka  kulia ni  Waziri wa Ujenzi na Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, kushoto kwake ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida na Mwakilishi Mkazi wa JICA nchini Tanzania.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale (kulia) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya SUMITOMO MITSUI, Bw. Ichiro Aok kutoka Japan wakibadilishana mikataba baada ya kuweka saini.
Waziri wa Ujenzi na Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiongea kabla ya uwekaji saini kukamilika. Dkt. Magufuli alieleza kuwa barabara hiyo itakapokamilika itakuwa ni ya kwanza ya aina yake katika nchi za Afrika Mashariki.
Mshauri mwelekezi wa kampuni hiyo Bw. Keigo Konno akionyesha jinsi mradi huo utakavyokuwa huku Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akifuatilia 
Sampuli ya barabra ya juu ya TAZARA itakavyokuwa baada ya ujenzi kukamilika.
Barabara ya juu
Waziri wa Ujenzi na Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akiteta jambo na Balozi wa Japan hapa nchini.
======================
PICHA NA: REUBEN MCHOME.

Wednesday, October 14, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI





Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia

Mahujaji wengine wawili kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki  dunia. Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini na mbili (22). Majina kamili ya mahujaji hao na vikundi vilivyowasafirisha kwenda Makkah katika mabano ni Hafsa Sharrif Saleh Abdallah (TCDO) na Khadija Hamad Hemed (Ahlu Daawa).  
Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za kuwatambua mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
14 Oktoba, 2015

Tuesday, October 13, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI





Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia



Mahujaji wengine wanane kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki  dunia. Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania walipoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini (20). Majina kamili ya mahujaji hao na vikundi vilivyowasafirisha kwenda Makkah katika mabano ni Hamida Llyas Ibrahim (Khidmat Islamiya), Farida Khamis Mahinda (Ahlu Daawa), Archelaus Anatory Rutayulungwa (Khidmat Islamiya) na Said Abdulhabib Ferej (Ahlu Daawa).


Wengine ni Awadh Saleh Magram (Khidmat Islamiya), Salama Rajab Mwamba (Khidmat Islamiya), Nuru Omar Karama (Ahlu Daawa) na Saida Awaadh Ali (Ahlu Daawa).

Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za  mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.



Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

Dar es Salaam

13 Oktoba, 2015