Wednesday, April 13, 2016

Mhe. Rais apokea Hati za Utambulisho za Mabalozi wa Brazil, Czech na Sudan Kusini nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Brazil nchini, Mhe. Carlos Alfonso Iglesias Puente. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Aprili, 2016.
Mhe. Rais akimtambulisha  kwa Balozi Puente Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga
Balozi mpya wa Brazil, Mhe. Puente akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Mhe. Rais.
Mhe. Balozi Puente akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga
Mhe. Balozi Puente akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Anthony Mtafya.
Mhe. Rais akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Puente, Waziri Mahiga, Balozi Sokoine, Msaidizi wa Rais masuala ya Diplomasia, Balozi Zuhura Bundala (kulia) na Afisa kutoka Ubalozi wa Brazil (kushoto)
Mhe. Rais Magufuli akiwa kwenye mazungumzo na Balozi Puente

Balozi Puente (katikati) akipokea heshima ya wimbo wa Taifa lake mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana.

.......Hati za Utambulisho za Balozi wa Jamhuri ya Czech

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Jamhuri ya Czech mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Pavel Rezac. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tareje 13 Aprili, 2016.
Mhe. Rais Magufuli akimtambulisha kwa Balozi Rezac Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga.
Waziri Mahiga akimtambulisha kwa Balozi Rezac Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.
Balozi Rezac akisalimiana na  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga
Mhe. Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Rezac
Mhe. Rais Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi Rezac
Waziri Mahiga ( wa kwanza kushoto) pamoja na Wajumbe kutoka Ikulu na Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Rais Magufuli na Balozi Rezac (hawapo pichani).
Balozi Rezac akiagana na Kiongozi wa Bendi ya Polisi mara baada ya kuwasilisha Hati zake za utambulisho kwa Rais

...........Hati za Utambulisho za Balozi wa Sudan Kusini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Sudan Kusini, Mhe. Mariano Deng Ngor. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tareje 13 Aprili, 2016.
Mhe. Rais Magufuli akimtambulisha kwa Balozi Ngor Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga.
Waziri Mahiga akimtambulisha kwa Balozi Ngor Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Samwel Shelukindo.
Balozi Ngor akisalimiana na  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga
Picha ya pamoja
Mhe. Rais Magufuli akizungumza na Balozi wa Sudan Kusini nchini, Mhe. Ngor.
Balozi Ngor akisikiliza wimbo wa taifa lake mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana.
Mhe. Balozi Ngor akisaini kitabu cha wageni  mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais.


Picha na Reginald Philip


Makamu wa Rais afungua rasmi Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Oman

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Oman lililofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku mbili litawakutanisha Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman.
Katika hotuba yake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alisema Tanzania itaendelea kushirikiana na Oman katika masuala ya biashara na uwekezaji pamoja na kudumisha ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akifuatilia Mkutano wa kukuza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Oman unaoendelea katika Hoteli ya Hyatt Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Mhe. Charles Mwijage (kushoto kwa Makamu wa Rais); Waziri wa Biashara na Viwanda wa Oman, Mhe. Dkt. Ali Masoud Al Sunaidy (kushoto kwa Makamu wa Rais) pamoja na baadhi ya Viongozi na watendaji wa Serikali ya Tanzania na Oman. Waliosimama ni baadhi ya Wabunge waliohudhuria mkutano huo.
Mmoja wa wajumbe wa Mkutano akichangia hoja.


Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman wanaokutana jijini Dar es Salaam leo katika kongamano la siku moja, wamehimizwa kufanya majadiliano yatakayoweka misingi na mikakati ya kutumia fursa lukuki za uwekezaji zinazopatikana katika nchi zao. 


Hayo yalisemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa anafungua kongamano hilo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.


Makamu wa Rais alieleza kuwa Oman ina uzoefu, ujuzi, teknolojia na mtaji mkubwa, wakati Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi na nguvu kazi ya kutosha, hivyo nchi hizo zikishirikiana kupitia wafanyabiashara wao, hatua kubwa ya maendeleo itafikiwa kwa muda mfupi kwa faida ya pande zote mbili.

Mhe. Hassan alibainisha kuwa malengo ya Tanzania ni kuwa nchi yenye uchumi wa kati kupitia maendeleo ya viwanda ifikapo mwaka 2025. Ili kufanikisha malengo hayo, mchango mkubwa wa wafanyabiashara wakiwemo kutoka Oman unahitajika kwa kiasi kikubwa kupitia uwekezaji wao.

Mhe. Makamu wa Rais alihitimisha hotuba yake kwa kupongeza uwekaji saini wa Mkataba wa Kulinda na Kuhimiza Vitega Uchumi (Protection and Promotion of Investments Agreement) kati ya Tanzania na Oman na kusisitiza umuhimu wa kukamilisha uwekaji saini wa Mkataba wa Kuepuka Tozo ya Kodi Mara Mbili (Avoidance of Double Taxation Agreement). Alisema mikataba hiyo itachochea biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

Akitoa salamu za ukaribisho katika kongamano hilo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage (Mb) aliweka wazi dhamira ya Serikali ya kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi kupitia maendeleo ya viwanda. Alisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika viwanda ili nchi iweze kuziongezea thamani malighafi zinazozalishwa nchini kabla ya kuuzwa nje ya nchi.

Kwa upande wake, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Oman, Dkt. Ali Masoud Al Sunaidy aliongelea ujenzi wa  Bandari ya Bagamoyo utakaofanywa kwa ushirikiano baina ya Mfuko Mkuu wa Akiba wa Oman, Serikali ya Tanzania na Serikali ya China kupitia Kampuni ya China Merchant International. Alisema mradi huo utakapokamilika utafungua na kuongeza kiwango cha biashara baina ya Tanzania na nchi za Kiarabu na dunia nzima kwa ujumla.

Taasisi mbalimbali zikiwemo TIC, ZIPA, EPZA ziliwasilisha mada katika kongamano hilo ambazo zililenga zaidi vivutio na fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini.
 

Waziri Mahiga na Balozi Mark Childress wa Marekani wafanya mazungumzo


Tuesday, April 12, 2016

Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule wa Sudani Kusini na Jamhuri ya Czech

Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Pavel Rezac, na kisha kufanya nae mazungumzo yaliyojikita katika kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Czech.  
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi Mteule Mhe. Pavel Rezac
Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Czech Mhe. Pavel Rezac

=============================================

Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Mariano Deng Ngor, na kisha kufanya nae mazungumzo yaliyojikita katika kukuza Ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya Tanzania na Jamhuri ya Sudani Kusini. 
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi Mteule Mhe. Mariano Deng Ngor
Waziri Mahiga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Sudani Kusini Mhe. Mariano Deng Ngor (wa tatu kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Balozi Samwel Shelukindo (wa kwanza kushoto), Afisa Ubalozi wa Sudani Kusini nchini (wa pili kutoka kulia) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Eric Ngilangwa (wa kwanza kulia).

Picha na Reginald Philip

Monday, April 11, 2016

Waziri Mahiga akutana na Viongozi Wakuu wa Mahakama ya MICT


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Rais wa  Mahakama ya Kimataifa ya Masalia ya kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (Mechanism for International Criminal Tribunals-(MICT) inayojengwa katika eneo la Lakilaki jijini Arusha, Mhe. Theodor Meron. Rais huyo alifika Wizarani kwa ajili ya kujitambulisha kwa Mhe. Waziri, kumweleza maendeleo ya ujenzi wa Mahakama hiyo pamoja na kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na mchango mkubwa inaotoa katika kufanikisha ujenzi huo. Pia aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia utawala wa sheria na haki.
Sehemu ya ujumbe uliofuatana na Mhe. Meron, Rais wa MICT.
Picha ya pamoja
Mhe. Mahiga na Mhe. Meron
Mhe. Mahiga akiagana na Mhe. Meron

...........Mkutano wa Waziri na Mwendesha Mashitaka wa MICT

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Masalia ya kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (Mechanism for International Criminal Tribunals- (MICT), Mhe. Dkt.Serge Bremmertz. Katika mazungumzo yao Mwendesha Mashtaka huyo aliipongeza Tanzania kwa mchango wake mkubwa wa kuridhia taasisi za Umoja wa Mataifa zinazosimamia sheria kujengwa nchini na kuielezea Arusha kama  makao makuu ya kimataifa ya haki kwa Ukanda wa Afrika. Pia aliahidi ushirikiano hususan katika kuwajengea uwezo wataalam wa masuala ya sheria za kimataifa hapa nchini.
Sehemeu ya Wajumbe waliofuatana na Mwendesha Mashtaka wa MICT.
Mazungumzo yakiendelea. Kushoto kwa Mhe. Mahiga ni Bw.  Elisha Suku, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Mhe. Dkt. Mahiga akiagana na Mwendesha Mashtaka wa MICT, Dkt. Bremmertz.
Picha na Reginald Philip

Wednesday, April 6, 2016

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda afanya mazungumzo na Balozi wa Namibia nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Innocent Shiyo akizungumza na Balozi wa Namibia nchini Mhe. Theresia Samaria alipomtembelea leo katika ofisi za Wizara.Katika mazungumzo yao alieleza juu ya umuhimu wa kuimarisha Uhusiano baina ya maitaifa hayo sambamba na kuahidi kuwa Wizara itaendelea kusimamia diplomasia ya Uchumi kama Sera ya Mambo ya Nje inavyoeleza

Mhe. Samaria pia katika mazungumzo hayo alieleza nia ya dhati ya Serikali ya Namibia katika kuimarisha ushirikiano ambapo alieleza umuhimu wa kufanyia utekelezaji makubaliano yanayo sainiwa baina ya mataifa hayo,  hususan katika masuala yanayogusa uchumi, vilevile aliainisha masuala kadhaa ya mafanikio yaliyopatikana katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
Maafisa Mambo ya Nje katika Wizara ya Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakifuatilia mazungumzo.
Mazungumzo yakiendelea
Wakiagana mara baada ya mazungumzo.

Picha na Reginald Philip

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia afanya ziara nchini Tanzania

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Mhe. Dkt. Mario Giro ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 5 Februari, 2016, ambapo alitembelea ofisi za Wizara kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Mhe. Dkt. Mario Giro akizungumza na Mhe. Dkt. Susan Kolimba ambapo katika mazungumzo yao walijadili uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo hasa katika sekta ya uchumi na kusisitiza juu ya suala la kukuza na kuendeleza sekta binafsi. Pia nafasi ya Italia katika kusaidia sekta ya elimu ambapo kwa upande wa Tanzania nchi hiyo imekuwa ikitoa ufadhili kwa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT)
Kushoto ni Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia, Dkt. Raffaelle De Lutio  na Balozi wa Italia nchini Mhe. Luigi Scotto ambao waliambatana na Mhe. Dkt. Mario Giro.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,  Balozi Innocent Shio (kushoto) kwa pamoja na  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga ( wa pili kushoto) wakiwa na Bi. Olivia Maboko,  Afisa Mambo ya Nje na Bw. Adam Isara, Msaidizi wa Naibu Waziri wakifuatilia mazungumzo
        Sehemu nyingine ya Wajumbe wakifatilia mazungumzo
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo
Balozi Innocent Shio akijadili jambo na Mhe. Dkt. Mario Giro huku Mhe. Kolimba na Bi. Kasiga wakishuhudia.