Friday, May 6, 2016

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje azungumza na Balozi wa China nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Mlima akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Balozi Lu Youqing alipofika Wizarani kwa mazungumzo yao yaliyojikita kwenye kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika masuala ya Biashara, Uchumi na Elimu. Katika mazungumzo hayo Balozi Mlima alimshukuru Balozi Youqing kupitia nchi yake kwa kuisaidia Tanzania kwenye ujenzi wa miundombinu. 
Balozi Youqing naye akizungumza na kumweleza Balozi Mlima kuwa nchini yao itaendelea kuboresha mahusiano ya kihistoria yaliyopo kati ya Tanzania na China.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto) na Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo kati ya Balozi Mlima na Balozi Youqing (hawapo pichani)   
Mazungumzo yakiendelea
Katibu Mkuu Balozi Aziz Mlima akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Lu Youqing

Picha na Reginald Philip

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa akutana na Mjumbe Maalum kutoka Thailand

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimaaifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) akimkaribisha Mjumbe Maalum kutoka  nchini Thailand, Mhe. Kobsak Chutikul alipokuja Wizarani kuwasilisha ujumbe maalum kutoka Serikali ya Thailand kuhusu masuala ya ushirikiano wa kimataifa.
Mhe. Kobsak Chutikul akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kukaribishwa Wizarani
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza na Ujumbe kutoka nchini Thailand (haupo pichani). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga.
Mhe. Kobsak Chutikul naye akizungumza na kuwasilisha ujumbe
Mazungumzo yakiendelea
Mhe. Chutikul (wa pili kutoka kushoto), Balozi Mushy (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo

Picha na Reginald Philip

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza huku Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustine Mahiga wakisikiliza.

Thursday, May 5, 2016

Wizara ya Mambo ya Nje yafanya Mkutano na Vyombo vya Habari

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bi. Mindi Kasiga, akiongea na waandishi wa habari kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, ambapo alizungumzia Mkutano wa Tume ya pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda uliofanyika nchini Rwanda pamoja tarehe 28 hadi 1 Mei, 2016 na Kikao cha Serikali ya Tanzania na Zambia kilichojadili utatuzi wa changamoto za mipaka  kilichofanyika tarehe 27 Aprili, 2016.
Mkurugenzi wa Masomo katika Chuo cha Diplomasia, Dkt. Watengele Kitojo (kushoto) akiwa na Maafisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na Taasisi zake wakati wa  Mkutano kati ya Wizara na Waandishi wa Habari. 
 Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Msemaji wa Wizara.
Wakati Mkutano ukiendelea.
================================================

Kikao cha Kumi na Nne cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda, 29 Aprili – 1 Mei, 2016

Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilifanyika kuanzia tarehe 29 Aprili hadi Aprili, 2016, Mjini Gisenyi, Rwanda, ambapo wataalam wa sekta mbalimbali waliazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

Kikao hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

Wakati wa ziara hiyo, wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.
Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania aliwakumbusha wajumbe wa pande zote mbili kuendesha mazungumzo na mjadala kwa kuzingatia maagizo ya viongozi hao na vilevile kuchangamkia fursa za ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za wananchi wa pande zote mbili baada ya mindombinu ya kikanda kuimarika.

Kwa upande wake, Balozi Jeanine Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda na mwenyeji wa kikao hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea malengo yanayotekelezeka na tarehe za ukomo kwenye maeneo yote watakayokubaliana ili kusukuma utekelezaji na kupata matokeo ya haraka.

Pamoja na mambo mengine, pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta muhimu kama vile miundombinu ya ushoroba wa kati (central corridor), kuharakisha ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha kimataifa (standard gauge), kukuza ushirikiano katika sekta ya anga hususan baina ya mashirika ya ndege ya Rwandair na ATCL, kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, afya, kilimo na ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.

Mkutano huo pia umekubaliana kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Utekelezaji (Joint Implementation Committee) kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo mbili, itakutana kila robo mwaka.

Aidha, Serikali ya Rwanda imeonesha utayari wake wa kuleta nchini Maafisa na Watumishi wa Serikali kwa lengo la kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo vya kitaalamu nchini kama vile Chuo cha Diplomasia  (CFR), Chuo cha Taifa cha Utalii na Wanyamapori  (Mweka) na Chuo cha Usafirishaji (NIT).

Kwa upande wa Tanzania, Serikali imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa mitaala ya elimu kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye upande wa kuandaa mitaala ya elimu ya tehama kwenye shule za awali, msingi na sekondari.

Mkutano ujao wa kumi na tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda utafanyika mwaka 2018, nchini Tanzania.

WAKATI HUO HUO, Kikao cha pamoja cha Makatibu Wakuu kati ya Tanzania na Zambia kwa ajili ya kujadili utatuzi wa changamoto za mpaka wa Nakonde Tunduma kilifanyika Lusaka Zambia 25 hadi 27 Aprili, 2016.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano  huo uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dkt. Servacius Likwelile na kwa upande wa Zambia uliongozwa na Bw. Bright Nundwe, Katibu Mkuu wa Jimbo la Muchinga.

Miongoni mwa changamoto zilizojadiliwa na ufumbuzi wake wakati wa mkutano huo ni pamoja na:- Msongamano wa magari ambapo kwa  upande wa Zambia huduma kwa  magari ya mizigo zinafanyika hadi saa nne usiku na kwa magari ya abiria huduma inatolewa kwa masaa 24. Ili kupunguza msongamano, Tanzania imeiomba Zambia kutoa huduma kwa magari ya aina zote kama Tanzania inavyotoa huduma ya masaa 24; na Kuimarisha usalama mpakani ili kukabiliana na biashara haramu za kubadilisha fedha, biashara za magendo na biashara haramu za binadamu.

Mwisho, pande zote mbili zilikubaliana suala hilo lishughulikiwe kwa kufanya ukaguzi na ulinzi wa pamoja na kubadilishana taarifa za kiusalama.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,

 05 Mei, 2016

Mhe. Kikwete asaini Kitabu cha Maombolezo Ubalozi wa Kenya

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyeambatana na Mkewe, Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kenya hapa nchini kufuatia kifo cha Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya, Mhe. Nwai Kibaki, Mama Lucy Kibaki kilichotokea wiki iliyopita nchini Uingereza. Mwingine katika picha ni Naibu Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Boniface Muhia. Dkt. Kikwete anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye mazishi ya Mama Kibaki yatakayofanyika Nairobi, Kenya.
Mama Salama Kikwete naye akisaini Kitabu cha Maombolezo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Aziz Mlima naye akisaini kitabu cha maombolezo.
Rais Mstaafu, Dkt. Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Naibu Balozi, Mhe. Boniface Muhia (wa pili kutoka kulia), mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha maombolezo, Mama Salama Kikwete (wa kwanza kushoto) na Balozi Mlima nao wakimsikiliza Naibu Balozi.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Samuel Shelukindo (wa kwanza kushoto) na Maafisa kutoka Ubalozi wa Kenya nao wakisikiliza kwa makini mazungumzo hayo
Dkt. Kikwete akiagana na Naibu Balozi, Mhe. Muhia 

Picha na Reginald Philip

Wednesday, May 4, 2016

Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait awasilisha Hati za Utambulisho

Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Dkt. Mahadhi Juma Maalim (kushoto), akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Shekh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah (kushoto), Amir wa Serikali ya Kuwait katika sherehe zilizofanyika Ikulu ya nchi hiyo tarehe 03 Mei, 2016. Anayeshuhudia tukio hilo ni  Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kuwait, Mtukufu Shekh Sabah Al-khaled Al-Sabah. Tanzania imefungua rasmi Ubalozi nchini humo mwaka 2015.
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim Balozi wa Kwanza Mkaazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait, akiwasilisha Nakala za Hati zake za Utambulisho kwa Mtukufu Sheikh Sabah, Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Serikali ya Kuwait kabla ya kuwasilisha Hati  hizo kwa Amir wa Serikali ya Kuwait.
Balozi Dkt. Mahadhi Juma Maalim (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mtukufu Shekh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah (kushoto), Amir wa Serikali ya Kuwait mara baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho.

Tuesday, May 3, 2016

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati akutana na Balozi wa Palestina

 Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Abdalah Kilima akimkaribisha Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hazem Shabat alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo katika ofisi za Wizara.
Mabalozi walizungumza juu ya kudumisha na kuimarisha mahusiano na ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Mamlaka ya Palestina.
Kushoto ni Afisa Mambo ya Nje katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bw. Tahir Khamis akifuatilia mazungumzo hayo.

Saturday, April 30, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: TUME YA KUDUMU YA PAMOJA YA USHIRIKIANO TANZANIA-RWANDA

Kikao cha Kumi na Nne cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda, 29 Aprili – 1 Mei, 2016

Gisenyi RWANDA

Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilichofanyika kuanzia tarehe 29 – 30 Aprili, 2016, kimekamilika Mjini Gisenyi, Rwanda, ambapo wataalam wa sekta mbalimbali wameazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Kikao hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.
Wakati wa ziara hiyo, wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.
Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania aliwakumbusha wajumbe wa pande zote mbili kuendesha mazungumzo na mjadala kwa kuzingatia maagizo ya viongozi hao na vilevile kuchangamkia fursa za ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za wananchi wa pande zote mbili baada ya mindombinu ya kikanda kuimarika.
Kwa upande wake, Balozi Jeanine Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda na mwenyeji wa kikao hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea malengo yanayotekelezeka na tarehe za ukomo kwenye maeneo yote watakayokubaliana ili kusukuma utekelezaji na kupata matokeo ya haraka.
Pamoja na mambo mengine, pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta muhimu kama vile miundombinu ya ushoroba wa kati (central corridor), kuharakisha ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha kimataifa (standard gauge), kukuza ushirikiano katika sekta ya anga hususan baina ya mashirika ya ndege ya Rwandair na ATCL, kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, afya, kilimo na ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.
Mkutano huo pia umekubaliana kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Utekelezaji (Joint Implementation Committee) kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo mbili, itakutana kila robo mwaka.
Aidha, Serikali ya Rwanda imeonesha utayari wake wa kuleta nchini Maafisa na Watumishi wa Serikali kwa lengo la kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo vya kitaalamu nchini kama vile Chuo cha Diplomasia  (CFR), Chuo cha Taifa cha Utalii na Wanyamapori  (Mweka) na Chuo cha Usafirishaji (NIT).
Kwa upande wa Tanzania, Serikali imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa mitaala ya elimu kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye upande wa kuandaa mitaala ya elimu ya tehama kwenye shule za awali, msingi na sekondari.
Mkutano ujao wa kumi na tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda utafanyika mwaka 2018, nchini Tanzania.
Mwisho.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Gisenyi, Rwanda

30 Aprili, 2016

Friday, April 29, 2016

Ufunguzi wa Kikao cha 14 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda Balozi Jeanine Kambanda akifungua Kikao cha 14 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda katika Hoteli ya Lake Kivu Serena tarehe 29 Aprili 2016

Sehemy ya Ujumbe wa Tanzania (kushoto) na Rwanda (kulia) wakifuatilia hotuba za wakuu wa ujumbe wa pande mbili ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa. 

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania