Wednesday, June 5, 2019

Maandalizi Ya Mkutano Wa Jumuiya Ya Maendeleo Ya Nchi Za Kusini Mwa Afrika (SADC) Yaanza

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, Dkt Stagomena Tax kabla ya kuanza kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati) akishauriana jambo na Katibu Mtendaji wa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC Dkt. Stagomena Tax (kulia) wakati wa kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019,kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC Dkt. Stagomena Tax (kulia) wakati wa kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019,kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019
Maafisa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC walioambatana na Dkt. Stagomena Tax wakisikiliza kwa makini mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo nao wakifuatilia kwa makini, katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Grace Martine, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Stephen Mbundi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Agness Kayola. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati) akiongoza  kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019


Prof. Kabudi azungumza na Idara ya Itifaki ya Wizara yake.

Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akizungumza na Watumishi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) alipokutana nao kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nafasi hiyo tarehe 3 Machi 2019. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Prof. Kabudi aliwataka Watumishi wa Wizara kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu miongozo na maelekezo mbalimbali pamoja na kuwa wazalendo na kufanya kazi zao kwa kushirikiana na  kwa weledi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Balozi Grace Martin na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Katika Wizara ya Mambo ya Nje. Aidha, mazungumzo hayo ni mwendelezo wa Vikao vya Prof. Palamagamba John Kabudi na Watumishi wa Wizara yake, ambapo yamefanyika katika Ofisi ndogo jijini Dar es Salaam tarehe 04 Juni, 2019 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akutana kwa mara ya kwanza na kiting cha Itifaki cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Grace Martini akitoa maelezo ya majukumu ya kitengo hicho kwa Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi alipokutana na Kitengo hicho kwa mara ya kwanza katika ofisi ndogo za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Idara ya Itifaki wakimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi ambaye hayupo pichani alipozungumza nao
Sehemu nyingine ya Watumishi wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani)
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye mkutano wao na Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (hayupo pichani).
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Idara ya Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.








Dkt. Mnyepe afanya mazungumzo na Balozi wa Msumbiji hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Msumbiji hapa nchini Mhe. Monica Patricio Clemente. Mazungumzo yao yamefanyika katika Ofisi Ndogo zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 04 June, 2019
Mazungumzo kati ya Dkt. Mnyepe (wa pili kutoka kulia) na Balozi Clemente (wa pili kutoka kushoto) yakiendelea, wa kwanza Julia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Wilbroad Kayombo akifuatilia kwa making mazungumzo hayo. 

Tuesday, June 4, 2019

Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi,na Utamaduni (UNESCO) nchini Bw. Tirso Dos Santos. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 04, Juni 2019
Bw. Santos akimweleza jambo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi,na Utamaduni (UNESCO) nchini.



TAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA

Dodoma, 04 Juni 2019

TANGAZO KWA UMMA

TAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kwamba, kuanzia tarehe 20 Mei, 2019 malipo yoyote Kwa Wizara yanafanyika kwa njia ya Kielektroniki kupitia mfumo wa GOVERNMENT ELECTRONIC PAYMENT GATEWAY (GePG).

Hivyo, wateja wote watakao hitaji kufanya malipo ya uthibitisho wa nyaraka mbalimbali zikiwemo; vyeti vya talaka, ndoa, kuzaliwa, Kifo n.k wanapaswa kabla ya kufanya malipo yoyote kuwasiliana na ofisi za Wizara kupitia vituo vyake vilivyopo Dodoma, Dar es salaam na Zanzibar ili kupatiwa ‘Control Number’ ili kufanikisha malipo husika kupitia Akaunti ya Benki ya CRDB.

Wateja wanaoleta nyaraka hizo kwa uthibitisho, wanaendelea kukumbushwa pia kukamilisha hatua muhimu kabla ya kupatiwa ‘Control Number’ ikiwemo kupelekwa kwanza katika Mamlaka na Taasisi husika zilizotoa vyeti/nyaraka hizo ili vihakikiwe na kuthibitishwa.

UMMA WOTE UNAOMBWA KUZINGATIA RAI KWAMBA, MALIPO YOYOTE YATAKAYOFANYIKA KINYUME NA MAELEKEZO BAADA YA TANGAZO HILI, HAYATOPOKELEWA


Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Friday, May 31, 2019

PRESS RELEASE

Dodoma, 31 Mei 2019

PRESS RELEASE
Job Announcement at the African Commission for Nuclear Energy
The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the African Commission for Nuclear Energy (AFCONE) inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Desk Officer available at the AFCONE.

For more details and application instructions, candidates are advised to visit: https://www.pnet.co.za/cmp/en/African-Commission-on-Nuclear-Energy-AFCONE-27508/work.html.

Application deadline is 16th June 2019.

Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

Bunge laidhinisha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge wakati wa kujadiliwa Bajeti ya Wizara yake May 30, 2019
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Willium Lukuvi (Mb.) wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani ) alipokuwa akijibu maswali  Bungeni.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Kangi Lugola (Mb.) naye akichangia hoja kwenye Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Willium Lukuvi (Mb.)  naye akichangia hoja  kwenye Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia kwa hoja zilizokuwa zikichangiwa na wabunge mbalimbali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) akijibu maswali mbalimbali Bungeni  wakati wa  kupitisha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro akifafanua jambo wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya wizara hiyo. Aliyekaa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi na nyuma kabisa ni sehemu ya baadhi ya menejimenti ya Wizara hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi  pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro wakipongezwa na Wabunge Mbalimbali mara baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma. May 30, 2019.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro (Mb.) akipongezwa na Mhe. Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya Mjini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro, Katibu Mkuu Dkt. Faraji Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan Mwinyi wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.









Thursday, May 30, 2019

Wizara ya Mambo ya Nje yawasilisha Bajeti Bungeni

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akiwasilisha Bungeni Bajeti ya Wizara yake May 30, 2019
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe akiwa na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje, Zanzibar Balozi Mohamed Hamza(kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi. May 30, 2019.
Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishaji wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri Profesa Palamagamba John Kabudi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019
Juu na Chini ni sehemu ya wabunge wakipitia moja ya machapisho ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, yanayoonyesha namna Mabalozi wa Tanzania waliopo Nje ya Nchi wanavyoliwakilisha Taifa vyema


 Sehemu nyingine ya Wabunge wakiendelea kusoma baadhi ya Machapisho ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki



Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia uwasilishaji wa hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo iliyowasilishwa na Waziri Profesa Palamagamba John Kabudi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akipongezana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro mara baada ya kuwasilisha bajeti ya Wizara hiyo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (kushoto) wakijadiliana jambo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro (katikati) pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Augustine Mahiga(kulia). May 30, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi  akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro wakisikiliza hoja za Wabunge wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma. May 30, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akipongezwa na Dkt. Detlef Wrätcher Balozi wa Ujerumani hapa Nchini mara baada ya Waziri kuwasilisha hotuba ya Bjaeti ya Wizara yake. May 30, 2019.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akipongezwa na Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, waliokuja wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe akipongezwa na Mwakilishi wa Ubalozi wa China hapa Nchini Bw Lin Liang. May 30, 2019.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi wanaoziwasilisha Nchi zao hapa Nchini mara baada ya kuwasilishwa hotuba ya bajeti ya wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma. May 30, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa pamoja na baadhi ya wazazi na watoto walioshinda katika mashindano ya uandishi wa insha kwa nchi za Afrika ya Mashariki,watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraji Mnyepe,May 30, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro, Katibu Mkuu Dkt. Faraji Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan Mwinyi wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Nchini pamoja na Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania 














Wednesday, May 29, 2019

Tanzania na Namibia kushirikiana katika maswala mbalimbali ya kuleta maendeleo

 Profesa Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  (Mb) pamoja na Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah  Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano (Mb) wakitia saini tamko la pamoja la mashirikiano kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo baina ya Tanzania na Namibia Mjini Windhoek,Namibia May 28,2019.

Profesa Palamagamba John Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  (Mb) pamoja na Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah  Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano (Mb) wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini tamko la pamoja la mashirikiano kuhusu masuala mbalimbali baina ya Tanzania na Namibia Mjini Windhoek,Namibia May 28,2019.

         Profesa Palamagamba John Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  (Mb) pamoja na Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah  Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano (Mb) wakionesha kwa waandishi wa habari nyaraka za tamko la pamoja la mashirikiano kuhusu masuala mbalimbali baina ya Tanzania na Namibia walizotia saini  Mjini Windhoek,Namibia May 28,2019

     Profesa Palamagamba John Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  (Mb) pamoja na Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah  Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano (Mb) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutia saini na kubadilishana nyaraka za tamko la pamoja la mashirikiano kuhusu masuala mbalimbali baina ya Tanzania na Namibia walizotia saini  Mjini Windhoek,Namibia May 28,2019. Kushoto ni kaimu balozi wa Tanzania Nchini Afrika ya Kusini anayesimamia pia Namibia Bw. Richard Lupembe na kulia ni Balozi wa Namibia nchini Tanzania Theresia Samaria.