Tuesday, April 6, 2021

MAPOKEZI YA KATIBU MKUU, NAIBU KATIBU MKUU KATIKA OFISI NDOGO ZA WIZARA - DAR

 Na Mwandishi wetu, Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameendelea kumuamini Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika nafasi ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Balozi Ibuge aliteuliwa Februari 06, 2020 kuwa katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki nafasi anayoendelea kuishikilia mpaka sasa.

Kabla ya wadhifa huo, Balozi Ibuge alikuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Balozi Fatma Mohammed Rajab kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Balozi Fatma aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Qatar Desemba 03, 2016 nafasi aliyokuwa akiishikilia hadi alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Hayupo Pichani) akimuapisha Balozi Fatma Mohammed Rajab kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo Ikulu Jijini Dar es Salaam



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab wakipokelewa na baadhi ya watumishi katika Ofisi Ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab mara baada ya kuwasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wizara wakati wa mapokezi katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 



  

 

Thursday, April 1, 2021

WAZIRI NA NAIBU WAKE WAWASILI WIZARANI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula akiwasili katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma muda mfupi baada kula kiapo cha kutumikia nafasi hiyo. Mhe. Balozi Mulamula na Naibu wake Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wamepokelewa na Watumishi na Wakuu wa Idara na Vitengo wakiongozwa Katibu Mkuu Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula akikaribishwa Wizarani muda mfupi baada ya kula kiapo cha kutumikia nafasi hiyo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akikaribishwa Wizarani muda mfupi baada ya kula kiapo cha kutumikia nafasi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula na Naibu wake Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk wakisikiliza maelezo ya Katibu Mkuu Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge mara baada ya kuwasili Wizarani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula akiongea na Watumishi na Menejimenti ya Wizara (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Wizarani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula akisaini kitabu cha wageni alipowasili Wizarani
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha wageni alipowasili Wizarani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula na Naibu wake Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi, Menejimenti na Viongozi wa Wizara mara baada ya mapokezi ya kuwakaribisha Wizarani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula na Naibu wake Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi, Menejimenti na Viongozi wa Wizara mara baada ya mapokezi ya kuwakaribisha Wizarani.

 

WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WATEULE WAAPA KUWA WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA



Waziri Mteule wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberatha Mulamula akiapa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Naibu Waziri Mteule wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiapa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania






 

Tuesday, March 30, 2021

Balozi Brigedia Jenerali Ibuge: Tuendelee Kudumisha Mahusiano ya Kidiplomasia na Biashara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge amehimiza Ofisi za Balozi zinazoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nje ya Nchi kuendelea kukuza na kudumisha ushirikiano wa Kidiplomasia na biashara katika maeneo yao ya uwakilishi. Balozi Brigedia Jenerali Ibuge amesema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Qatar Mhe. Fatma M. Rajab na Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Abdallah Abas Kilima. 

“Mnadhamana na jukumu kubwa la kuendelelea kudumisha na kukuza mahusiano ya kidiplomasia na biashara katika maeneo yenu ya uwakilishi ili kuendelea kuvutia kwa uwingi wawekezaji na watalii nchini. Jukumu letu la kutumikia wananchi wa Tanzania tulifanye kwa moyo, kujituma, maarifa na uzalendo”. Amesema Balozi Brigedia Jenerali Ibuge.

Balozi Brigedia Jenerali Ibuge vilevile ameeleza dhamira ya Wizara ya kuendeleza viwanja vya Serikali vilivyopo maeneo mbalimbali nje ya nchi ili viweze kuiingizia Serikali mapato na kuipunguzia matumizi yanayotokana na gharama za pango la ofisi na makazi kwa watumishi wanaofanya kazi katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Balozi Abdallah Kilima na Fatma Rajab kwa nyakati tofauti wameishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano mzuri wanaoendelea kuupata na kuahidi kuwa wataendelea kufanyakazi kwa bidii na weledi katika kulinda na kutetea maslahi ya nchi na kuleta manufaa kwa nchi.  


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge na Mhe. Abdallah Abas Kilima Balozi wa Tanzania nchini Oman wakiwa kwenye mazumgumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge na Mhe. Fatma M. Rajab Balozi wa Tanzania nchini Qatar wakiwa kwenye mazumgumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge na Mhe. Fatma M. Rajab Balozi wa Tanzania nchini Qatar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge na Mhe. Abdallah Abas Kilima Balozi wa Tanzania nchini Oman wakiwa katika picha pamoja baada ya mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma






Monday, March 29, 2021

MABALOZI WANAOIWAKILISHA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NJE YA NCHI WAHIMIZWA KUONGEZA JUHUDI ZA KUTAFUTA MASOKO

Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nje ya Nchi wameelekezwa kujipanga, kushiriki na kutafuta fursa zitakazowezesha bidhaa mbalimbali za Tanzania kupata masoko ya uhakika katika nchi walizopo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akizungumza na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na kuongeza kuwa , Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatamka bayana juu ya diplomasia ya uchumi sambamba na kuimarisha sauti ya Tanzania na taswira yake katika medani ya uhusiano wa kikanda na kimataifa. 

Prof. Kabudi ameongeza kuwa ili kufanikisha hilo Balozi zinapaswa kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika jumuiya nyingine za kimataifa zikiwemo, Indian Ocean Rim Association, Indian Ocean Tuna Commission, South South Commission, South West Indian Ocean Fisheries Commission.

Aidha amewataka Mabalozi hao kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoyatoa wakati akizundua Baraza la Wawakilishi ya kutaka Uchumi wa Bluu kupitia uvuvi wa Bahari Kuu unakuwa na manufaa kwa Wananchi hususani katika kuongeza mapato, ajira na kukuza uchumi kwa kuzingatia kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni ya Muungano. 

Pia Prof. Kabudi amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) katika maendeleo ya Taifa na kuzielekeza Balozi zianze na ziboreshe kanzi data ya Diapora ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kuanzisha Jumuiya zao. 

“Natambua kazi hiyo inaendelea na kwa sasa tuna data za diaspora takriban 98,658 na kuna jumuiya 77 za diaspora. Nichukue fursa kusisitiza umuhimu wa Balozi zetu kuboresha na kuharakisha zoezi hili kwa kubuni njia mbalimbali za kuwaandikisha”. Amesema Prof. Kabudi

Mkutano huo wa Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi umehudhuriwa pia na Naibu Waziri, Mhe William Tate Ole Nasha, Katibu Mkuu Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akisisitiza jambo kwenye Kikao kazi na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kilichofanyika jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.  William Tate Olenasha (Mb) akizungumza na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoiwakilisha nchi sehemu mbalimbali Duniani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kwenye kikoa kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisisitiza jambo katika Kikao kazi katika ya Mhe. Prof Kabudi na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kilichofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya Mabalozi na Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) kwenye Kikao Kazi kilichofanyika jijini Dodoma. 

Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) kwenye Kikao Kazi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani mara baada ya Kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo baada ya Kikao Kazi kilichofanyika jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani mara baada ya kuhitimisha Kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

TANGAZO LA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO