Sunday, February 19, 2023

MKUTANO WA KAWAIDA WA 43 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC KUFANYIKA BURUNDI


Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unatarajiwa kufanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 23 Februari 2023.

 

Mkutano huo ambao umeanza kwa Ngazi ya Wataalam tarehe19 hadi 20 Februari 2023 utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 21 na 22 Februari 2023 na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 23 Februari 2023.

 

Mkutano wa Wataalam utapitia na kujadili agenda mbalimbali muhimu kuhusu masuala ya mtangamano wa Jumuiya hiyo ambazo baadaye zitawasilishwa kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 21 na 22 Februari 2023 kwa majadiliano na hatimaye agenda hizo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya  Mawaziri unaotarajiwa kufanyika jijini hapa tarehe 23 Februari 2023.

 

Miongoni mwa agenda hizo ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara na forodha, miundombinu, ulinzi na usalama, sheria, utalii, ajira na utawala na fedha; Kupokea taarifa ya mwaka ya Ukaguzi wa Hesabu za Jumuiya kwa mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2022; Taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya; Taarifa kuhusu Taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kupitia na kupitisha ratiba ya shughuli za Jumuiya kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2023.

 

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. Ujumbe huo pia unajumuisha Wajumbe kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Katiba na Sheria.

 

Kadhalika Mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama ambazo ni Burundi ambaye ni mwenyeji wa mkutano, Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya mtandao.

Mwenyekiti wa Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam kutoka Burundi (kushoto) akiongoza kikao hicho kilichofanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 19 Februari 2023 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masahriki unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Februari 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango na Utawala, Mhandisi Steven Mlote.
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam uliofanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 19 Februari 2023 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masahriki unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Februari 2023. Mkutano kwa ngazi ya wataalam unafanyika kuanzia tarehe 19 hadi 20 Februari 2023 na utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 21 na 22 Februari 2023. Kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Haji Janabi

Ujumbe wa Burundi ukishiriki Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaofanyika jijjini Bujumbura, Burundi kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa EAC. Burundi ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kiongozi wa Ujumbe wa Rwanda akishiriki Mkutano wa Wataalam
Ujumbe wa Uganda ukishiriki Mkutano huo
Ujumbe wa Kenya nao ukiwa katika Mkutano
Kiongozi wa Ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nae akishiriki mkutano wa wataalam
Wajumbe kutoka Taasisi za Jumuiya ya Afrika wakishiriki mkutano wamaandalizi ya mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa EAC

Wajumbe kutoka Sekreatarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishiriki Mkutano wa Wataalam jijini Bujumbura
Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Sera, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi Agnes Meena akishiriki Mkutano wa Wataalam
Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw.  Bernard Haule akishiriki mkutano wa wataalam

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki Mkutano wa Wataalam
Sehemu ya Wajumbe wa Sekretarieti ya EAC wakifuatilia mkutano
Mkutano ukiendelea
Wajumbe kutoka Tanzania katika mkutano
Mkutano ukiendelea



















 

Thursday, February 16, 2023

TANZANIA, ANGOLA ZASAINI HATI ZA MAKUBALIANO

Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola zimesaini Hati mbili za Makubaliano (MoU) kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Ushirikiano kati ya Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania (CFR) na Chuo cha Venancio de Moura cha Angola.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mara baada ya kusaini Hati hizo za Makubaliano, Dkt. Tax alisema Tanzania na Angola zimekuwa zikishirikiana kwa muda mrefu, na Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuzisaidia nchi za Kusini mwa Bara la Afrika kujikomboa na tangu wakati huo imeendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali.

“Leo tumeona ni vyema turasimishe ushirikiano wetu kwa sababu dunia inakwenda mbele na kuna mambo mengi ya kufanya pamoja na hivyo tumesaini Hati mbili za Makubaliano ya kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja itakayotuwezesha kukutana na kujadili masuala mbalimbali yenye manufaa kwa pande zote mbili.

………lakini sisi kwa kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) tutaweza kujadili yanayojiri katika Kanda zetu na Kimataifa na kuona tunavyoweza kufanyia kazi kwa pamoja kwani umoja ni nguvu,” alisema Dkt. Tax

Kuhusu Makubaliano ya Ushirikiano wa Vyuo vya Diplomasia kati ya Tanzania na Angola, Waziri Tax alisema kupitia makubaliano hayo vyuo hivyo vitaweza kubadilishana uzoefu, utaalamu na wanafunzi ili kuboresha taasisi hizo za diplomasia.

“Kupitia makubaliano tuliyosaini leo, vyuo vyetu vya Dioplomasia vitabadilishana uzoefu, utaalamu na wanafunzi ili kuboresha zaidi taasisi zetu hizi za diplomasia,” alisema Waziri Tax.

Kwa Upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António amesema Angola imefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya Tanzania kukubali kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na kuelezea utayari wake wa kushirikiana katika nyanja mbalimbali kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Tanzania na Angola ni marafiki wa siku nyingi, kupiti makubaliano tuliyosaini leo tumefungua ukurasa mpya wa ushirikiano baina ya mataifa yetu, tunayo mengi ya kushirikiana.

Kadhalika, kuhusu ushirikiano wa vyuo vyetu Waangola tumekuwa tukija kujifunza masuala mbalimbali ya kidiplomasia katika Chuo cha Diplomasia (CFR) na kuwa wanadiplomasia, hivyo kupitia makubaliano ya leo tutaweza kubadilishana uzoefu wa kidiplomasia na kuwanoa wanadiplomasia wengi zaidi,” alisema Balozi António.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António wakisaini Hati za Makubaliano (MoUs) za kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Hati ya Ushirikiano kati ya Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania (CFR) na Chuo cha Venancio de Moura cha Angola. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António wakibadilishana Hati za Makubaliano (MoUs) za kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Hati ya Ushirikiano kati ya Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania (CFR) na Chuo cha Venancio de Moura cha Angola baada ya kuzisaini katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akieleza jambo baada ya kusaini Hati za Makubaliano (MoUs) za kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Hati ya Ushirikiano kati ya Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania (CFR) na Chuo cha Venancio de Moura cha Angola katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António baada ya kusaini Hati za Makubaliano (MoUs) katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa serikali za Tanzania na Angola katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023


UBALOZI AUSTRIA WAFANIKISHA UWEKAJI SAINI HATI YA MAKUBALIANO SEKTA YA AFYA

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika (wa pili kushoto); Naibu Mkuu wa Chuo cha Tiba cha Vienna, Dkt. Michaela Fritz na Mkurugenzi wa Idara ya Urolojia katika Hospitali Kuu ya Vienna, Prof. Shahrokh Shariat wakiweka saini Hati ya Makubaliano kuhusu kushirikiana katika masuala ya tiba za kibingwa. Kulia ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Austria, Bi. Elizabeth Rwitunga.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika (wa pili kushoto); Naibu Mkuu wa Chuo cha Tiba cha Vienna, Dkt. Michaela Fritz na Mkurugenzi wa Idara ya Urolojia katika Hospitali Kuu ya Vienna, Prof. Shahrokh Shariat wakibadilishana Hati ya Makubaliano kuhusu kushirikiana katika masuala ya tiba za kibingwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Hosiptali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Open Medical Institute yenye makao makuu Austria, Prof. Wolfgang Aulitzky. 


Wednesday, February 15, 2023

DT. TAX AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA 42 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA UMOJA WA AFRIKA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023.  

Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 18-19 Februari 2023.

Pamoja na mambo mengine, mkutano wa Mawaziri utajadili masuala ya kimkakati yanayohusu Bara la Afrika ikiwemo utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika-AfCFTA, uhakika wa chakula, hali ya ulinzi na usalama, mabadiliko ya tabianchi, pamoja na masuala ya kiutawala na usimamizi wa rasilimali za Umoja wa Afrika.

Akichangia katika mkutano huo, Dkt. Tax alisisitiza umuhimu wa Kamisheni na Taasisi za Umoja wa Afrika kusimamia vyema rasilimali za Umoja wa Afrika kwa kuchukua hatua za kuondoa mapungufu yaliyobainika kwenye taarifa ya ukaguzi wa rasilimali za Umoja wa Afrika. 

Mhe. Waziri pia alieleza hatua ambazo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inachukua katika kutekeleza Mikataba ya Uenyeji ya Taasisi za Umoja wa Afrika zilizopo Tanzania ambazo ni Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Umoja wa Posta Afrika na Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri dhidi ya Rushwa.

Awali akiwasilisha hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mhe. Moussa Faki Mahamat alisisitiza umuhimu wa Umoja wa Afrika kuendelea kutoa kipaumbele kwenye masuala yanayowagusa wananchi wa Afrika ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za mabadiliko za kijamii, kiuchumi na kiusalama. Alisisitiza umuhimu wa Afrika kupunguza utegemezi wa chakula kutoka nje kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za vyakula ndani ya bara la Afrika pamoja na kutumia fursa za mkataba wa AfCFTA katika kukuza Mtangamano wa Kiuchumi.

Bw. Faki aliongeza kuwa Umoja wa Afrika umeendelea kusimamia masuala ya amani na usalama katika bara la Afrika katika nchi za Ethiopia, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Libya ambapo jitihada zilizofanyika zimelenga zaidi kupata suluhisho la amani kwa mataifa hayo.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Demeke Mekonnen amesema Ethiopia ameshukuru Umoja wa Afrika kwa mchango na ushirikiano wake ambao umewezesha kupatikana amani na utulivu nchini Ethiopia na kumaliza mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka miwili. “Ethiopia inaamini kuwa kupitia Umoja wa Afrika amani, ulinzi na usalama vitailetea Afrika maendeleo zaidi,” alisema Mhe. Mekonnen.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Shiyo alipokuwa akimfafanulia jambo wakati wa Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sudan Kusini, Mhe. Deng Dau Deng Malek katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Demeke Mekonnen akijadili jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja

Mawaziri mbalimbali walioshiriki Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023. 





TANZANIA MWENYEKITI WA SEKTA YA UVUVI NA UCHUMI WA BULUU KATIKA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI



 

Tuesday, February 14, 2023

MKUTANO WA MAJADILIANO YA KIMKAKATI YA NGAZI YA JUU KATI YA SERIKALI NA WADAU WA MAENDELEO WAFANYIKA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Sterrgomena Tax wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.

 Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo katika meza kuu wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.


Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki balozi Joseph Sokoine (wa pili kulia) akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo  uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.

Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.

Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023 ukiendelea.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023 katika picha ya pamoja.

Meneja ratiba wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023 bi Ellen Maduhu akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kuzungumza katika mkutano huo.



Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati ya Ngazi ya Juu ulioshirikisha watendaji wakuu wa Serikali na wadau wa maendeleo wafanyika jijini dar es Salaam.

Akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax , Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amewahakikishia wadau wa maendeleo ushirikiano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza kwa pamoja mipango ya maendeleo.

Balozi Mbarouk amesema kufanyika kwa kikao hicho kunadhihirisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau wa maendeleo na Taasisi za Umoja wa Mataifa.

“Uwepo wenu hapa katika kikao hiki unadhihirisha ushirikiano usliopo kati ya Tanzania na wadau wa maendeleo, Sio kwamba uwepo wenu unachochea ubia wetu na kuimarisha nia yenu ya kuhakikisha tunatekeleza kikamilifu Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo ambao umelenga kutekeleza malengo Endelevu ya Milenia ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya Addis Ababa ya kuchangia maendeleo na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Balozi Mbarouk

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye uwakilishi wao hapa nchini, wadau wa maendeleo , sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikal.

 

 


TANZANIA, COMORO KUANZIASHA TUME YA KUDUMU YA PAMOJA

 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal wakisaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili.  Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal wakionesha Mkataba wa Makubaliano (MoU) uliosainiwa kwa ajili ya kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili. Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal wakionesha Mkataba wa Makubaliano (MoU) uliosainiwa kwa ajili ya kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili. Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal wakipongezana baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) kwa ajili ya kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili. Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili. Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na Comoro baada ya kusaini Mkataba wa kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na Comoro. Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.