Saturday, June 17, 2023

WATUMISHI WA MAMBO YA NJE WAFANYA USAFI HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kuratibu upatikanaji wa madaktari bingwa, vifaa tiba na misaada mingine kutoka kwa wahisani kwa ajili ya kuboresha sekta ya Afya nchini.

 

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17 Juni 2023 na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen P. Mbundi wakati wa zoezi la watumishi wa Wizara hiyo kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.

 

Balozi Mbundi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu, Balozi Samwel Shelukindo, alisema kuwa Wizara kwa nafasi yake inaendelea na mkakati wa kutangaza utalii tiba hasa kwa nchi jirani, na mafanikio yamenza kuonekana kutokana na sekta ya afya nchini kuimarika na kuwa na uwezo wa kutoa huduma za kibingwa kwa gharama nafuu ukilinganisha na maeneo mengine duniani.

 

Aliendelea kueleza kuwa watumishi wa Wizara ni sehemu ya jamii ya Watanzania na uamuzi wa kufanya usafi katika hospitali hiyo ni moja ya jukumu lao la kuhudumia jamii, kwa sababu usafi ni tiba ya magojwa.

 

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Magonjwa Hatarishi, Dkt. Paul Julius Mageni ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo ameishukuru Wizara kwa uamuzi wake huo wa kizalendo. Alisema kitendo kilichofanywa na watumishi wa Wizara ni ibada kubwa na kina lenga kuzuia maambukizi ya magonjwa. “Njia nzuri na rahisi ya kutibu ugonjwa ni kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo na usafi ni moja ya njia za kuzuia magonjwa kusambaa”, Dkt. Mageni alisema.

 

Wizara inaendelea kuadimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili watumishi ili kuchagiza ari na motisha kwa watumishi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen P. Mbundi (mwenye barakoa) akishiriki zoezi la kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Balozi Mbundi  alimwakilisha Katibu Mkuu, Balozi Samwel Shelukindo. Mwenye miwani ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Paul Mageni. Zoezi hilo limefanyika kwenye Hospitali hiyo tarehe 17 Juni 2023. Kaulimbiu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi mwaka huu ni "Kufanikiwa kwa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika kunahitaji usimamizi wa Utumishi wa Umma wenye Mtazamo wa Kikanda".

Balozi Mbundi akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salifius Mligo (kushoto) wakiendelea na zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Kawina Kawina naye akiendelea na zoezi la usafi
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, Bw. Magabilo Murobi (kushoto) akiwa na Afisa Usafirishaji  wa Wizara Bw. Maulid Mkenda wakishiriki zoezi la usafi
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji,  Bw. Athuman Nkungu akiendelea na zoezi la usafi 
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiendelea na zoezi la usafi
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiendelea na zoezi la usafi kwa kuchoma takataka
Zoezi la usafi likiendelea
Watumishi wa Wizara wakijituma katika zoezi la usafi
Zoezi la usafi likiendelea 
Zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma likiendelea
Zoezi la usafi likiendelea
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakiendelea na zoezi la usafi
Zoezi la Usafi likiendelea
Zoezi la usafi likiendelea
Zoezi la usafi likiendelea
Usafi ukiendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Zoezi la usafi likiendelea
Watumishi wa Wizara wakishiriki zoezi la usafi
Usafi ukiendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki wakiwa katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa zoezi la usafi

Balozi Mbundi (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu mara baada ya Wizara kukamilisha zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma Bw. Mageni akitoa neno la shukrani kwa Wizara kwa kutembelea Hospitali hiyo
Picha ya pamoja

....Ushiriki wa Wiki ya Utumishi katika Ofisi Ndogo za Wizara-Dar es Salaam

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao wapo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam nao wakishiriki zoezi la usafi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Zoezi hilo limefanyika tarehe 17 Juni 2023

Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara waliopo Dar es Salaam wakiendelea na zoezi la usafi katika Taasisi ya Sratani ya Ocean Road kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma

........Ushiriki wa Wiki ya Utumishi wa Umma katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar 

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao wapo katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar wakishiriki zoezi la usafi katika Hospitali ya Rahaleo kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Zoezi hilo limefanyika tarehe 17 Juni 2023
Usafi ukiendelea katika Hospitali ya Rahaleo Zanzibar kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma




















 

Thursday, June 15, 2023

MAHAKAMA YA AFRIKA YAISHUKURU SERIKALI YA TANZANIA

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud kutoka Tanzania ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa misaada inayoipatia mahakama hiyo ikiwemo ujenzi wa jengo la ofisi ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilikabidhi eneo la ujenzi kwa Mkandarasi CRJE jijini Arusha tarehe 02 Juni 2023.

 

Jaji Aboud ametoa shukrani hizo wakati wa kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 15 Juni 2023.

 

Rais wa Mahakama ya Afrika na watumishi wengine, wakiwemo Makamu wa Rais; Majaji na Msajili wapo jijini Dodoma kwa ajili ya kikao (retreat) cha kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Mahakama hiyo ili kubaini mafanikio na changamoto kwa ajili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

 

Kwa kutumia fursa ya kikao kufanyika Dodoma, Rais na ujumbe wake wametumia nafasi hiyo kukutana na wadau mbalimbali ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ili kajadili utekelezaji wa majukumu ya chombo hicho muhimu barani Afrika.

 

Kwa upande wake, Mhe. Waziri Dkt. Tax alieleza kufurahishwa na uamuzi wa Mahakama hiyo wa kufanya kikao chao jijini Dodoma ambapo ni makao makuu ya nchi. Aidha, aliwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano unaohitajika ili mahakama hiyo iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi.

 

Mhe. Waziri Dkt. Tax alihitimisha mazungumzo yake kwa kumpongeza Jaji Aboud kwa kuchaguliwa tena kwa kipindi cha awamu ya pili na cha mwisho cha miaka miwili kuwa Rais wa Mahakama hiyo. Jaji Aboud alichaguliwa wakati wa ufunguzi wa Baraza la 69 la Pan-Afrika lililofanyika Arusha tarehe 12 Juni 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa Mkutano kati yake na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (hayupo pichani) alipomtembelea Ofisi kwake jijini Dodoma tarehe 15 Juni 2023. Mhe. Jaji Imani na ujumbe wake, wakiwemo Makamu wa Rais; Majaji na Msajili wapo jijini Dodoma kwa ajili ya kikao cha kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Mahakama hiyo ili kubaini mafanikio na changamoto kwa ajili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa Mkutano kati yake na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (kshoto) alipomtembelea Ofisi kwake jijini Dodoma tarehe 15 Juni 2023. Kulia ni Makamu Rais wa Mahakama hiyo, Mhe. Jaji Sacko Madibo
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud akizungumza wakati wa Mkutano kati yake na Mhe. Dkt. Tax (hayupo pichani)
Mkutano ukiendelea
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Levina Maleo akizungumza wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Waziri Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud hawapo pichani
Afisa kutoka Kitengo cha Sheria, Bi. Elizabeth Bukwimba akichangia jambo wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud hawapo pichani
Mhe. Jaji Aboud akimpatia Mhe, Dkt. Tax zawadi ya nembo ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao
Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud wakijadili jambo baada ya mazungumzo yao
Picha ya pamoja 
Picha ya pamoja

TANZANIA YAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA URUSI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Serikali ya Urusi kuwekeza nchini kwa maslahi ya pande zote mbili na ustawi wa dunia kwa ujumla.

Mwaliko huo umetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) wakati aliposhiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana jioni Jijini Dar es Salaam. 

“Tanzania ina mazingira tulivu ya biashara na uwekezaji yanayotoa fursa za uwekezaji, hivyo natoa rai wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Urusi kuja kuwekeza Tanzania ili kuimarisha zaidi biashara baina ya nchi zetu mbili,” alisema Balozi Mbarouk

 Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Tanzania kwa kushirikiana na sekta binafsi zimeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuhakikisha kuwa uwekezaji unafanyika katika mazingira rafiki na salama na kuwafanya wafanyabiashara kutoka nje kufanya biashara zao katika mazingira salama na rafiki. 

Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Urusi imekuwa mshirika wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiteknolojia na kisiasa nchini Tanzania. Kwa kusainiwa kwa mkataba wa kuanzisha Tume ya Pamoja ya Kiserikali ya Biashara na Ushirikiano wa Kiuchumi, nchi hizo mbili zipo katika nafasi nzuri zaidi ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan alisema kuwa ushirikiano wa Urusi na Tanzania ni wa kihistoria na umekuwa imara wakati wote. Urusi itaeendelea kushirikiana na Tanzania kijamii, kisiasa na kiuchumi wakati wote.

“Tunapoadhimisha siku hii muhimu tunakumbuka pia miaka 62 ya uhusiano kati ya Urusi na Tanzania. Aidha, Balozi Avetisyan aliongeza kuwa Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuendeleza ushirikiano wa kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya pande zote mbili,” alisema Balozi Avetisyan.

“Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania kuboresha biashara na uwekezaji ambapo kwa sasa ukuaji wa biashara baina ya mataifa yetu umeongezeka. Tunaendelea kuboresha biashara licha ya changamoto zinazojitokeza,” aliongeza Balozi Avetisyan. 

Tanzania na Urusi zinashirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi, afya, biashara, viwanda, uwekezaji na utalii ambapo kwa pamoja zimekubaliana kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta tija katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana jioni (tarehe 14 Juni, 2023) Jijini Dar es Salaam. kushoto ni Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiaana na Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan wakati maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana jioni (tarehe 14 Juni, 2023) Jijini Dar es Salaam

Washiriki wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi

Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana jioni (tarehe 14 Juni, 2023) Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan akizungumza na washiriki wakati maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana jioni (tarehe 14 Juni, 2023) Jijini Dar es Salaam



Wednesday, June 14, 2023

TANZANIA, MISRI KUIMARISHA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kuimarisha ushirikiano wake na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri katika sekta za biashara na uwekezaji.

Hayo yamebainishwa wakati wa mazungumzo baina ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) na Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry walipokutana katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mbarouk amesema kuwa ni wakati muafaka kwa Serikali za Tanzania na Misri kuwekeza zaidi katika sekta ya biashara na uwekezaji ili kukuza uchumi wa mataifa yote mawili.

“Ili kukuza na kuimarisha misingi ya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Misri tunahitaji kufanya mkutano wa Mkutano wa Tume ya pamoja ya Ushirikiano ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Misri, pamoja na kuanzisha Baraza la biashara ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara wetu kubadilishana uzoefu na mawazo ya biashara na uwekezaji,” alisema Balozi Mbarouk.

Aidha, Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepanga kufanya Mkutano wa Tume ya pamoja ya Ushirikiano ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Misri mwezi Oktoba, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo utajadili mazingira ya biashara na uwekezaji kwa pande zote mbili.

“Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji kwa kuondoa kero mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wawekezaji hivyo mazingira ya biashara na uwekezaji ni mazuri na yanaridhisha,” aliongeza Balozi Mbarouk.

Naye Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry alisema kuwa kufanyika kwa JPC ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa Misri na Tanzania katika sekta ya biashara na uwekezaji.

“tumejadili na kukubaliana kuanzisha Baraza la biashara kati ya nchi zetu ili kuweza kuimarisha sekta hiyo kwa maslahi ya pande zote mbili,” alisema Balozi Badry

Balozi Badry aliongeza kuwa Misri imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, maji, nishati, utamaduni, utalii, kilimo pamoja na uvuvi na mifugo, hivyo ni wakati muafaka kwa mataifa hayo mawili kujikita zaidi katika sekta ya biashara na uwekezaji.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimkaribisha Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimsikiliza Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry pamoja na Balozi wa Misri Nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry pamoja na Balozi wa Misri Nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail katika picha ya pamoja na ujumbe wake



BALOZI MBAROUK ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA ITALIA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Italia nchini, kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Mhe. Silvio Berlusconi kilichotokea tarehe 12 Juni, 2023.

Mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Balozi Mbarouk amesema Tanzania inamkumbuka Mhe. Berlusconi kwa kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania Italia enzi za uongozi wake.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Italia nchini, kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Mhe. Silvio Berlusconi



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Italia nchini, kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Mhe. Silvio Berlusconi. aliyesimama ni Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akitoa salamu za pole kwa Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Mhe. Silvio Berlusconi