Tuesday, November 12, 2013

Balozi wa Tanzania nchini Kenya awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Seychelles


Mhe. Balozi Batilda S. Burian, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Seychelles mwenye makazi yake nchini Kenya, awasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. James Alix Michel, Rais wa Jamhuri ya Seychelles.  Tukio hilo lilitokea tarehe 5 Novemba, 2013 katika Ikulu ya Rais was Seychelles. 

Mh. Rais James Alix Michel wa Seychelles akiwa katika picha ya pamoja na na MheshimiwaBalozi Batilda S. Burian. Kulia kwa Mh. Rais Michel ni Brig. Gen. E.V. Milinga, Mwambata Jeshi, Ubalozi wa Tanzania, Nairobi Kenya.


MHESHIMIWA BATILDA S. BURIAN, BALOZI WA TANZANIA NCHINI SEYCHELLES AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA
MHESHIMIWA RAIS JAMES ALIX MICHEL  SEYCHELLES

MheshimiwaBalozi Batilda S. Burian, Balozi wa Tanzania nchini Seychelles mwenye makazi yake nchini Kenya, aliwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mheshimiwa James Alix Michel, Rais wa Jamhuri ya Seychelles tarehe 5 Novemba, 2013 katika Ikuluya Rais Seychelles. Hafla ya kuwasilisha hati hizo, imefungua ukurasa mpya wa mashirikiano kati ya nchi hizi mbili. Takriban kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15 hatukuwahi kuwa na Balozi aliyewahi kuwasilisha Hati za Utambulisho nchini Seychelles. Mh. Balozi alifuatana na Brig. Gen. E.V. Milinga, Mwambata Jeshi, Ubalozi wa Tanzania Nairobi
Katika hafla hiyo, Mhe. Balozi alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais James A. Michel, mazungumzo ambayo yalilenga zaidi katika biashara, uwekezaji, mashirikiano ya anga usafiri wa majini, ulinzi na usalama.  
Pia Mhe. Balozi Burian alipata fursa ya kuona  na na Mawaziri wafuatao na kufanya nao mazungumzo:-

(i)  Mhe. Prof. RolphPayet, WaziriwaMazingira naNishati
(ii)   Mhe. Christian Lionnet, Waziri wa Ardhi naNyumba
(iii)  Mhe. Pierre Laporte, Waziri waFedha
(iv)  Mhe. Dkt Patrick S. Herminie, Spika wa Bunge
(v) Bibi Benjamine Rose, Katibu Mkuu, Wizara ya Utalii na Utamaduni.
Ubalozi wa Tanzania Nchni Kenya pia unawakilisha nchi za Sudani, Sudani Kusini, Somalia na Eritrea.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.