Wednesday, November 13, 2013

ZIARA YA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA NCHINI KENYA


Mhe. Batilda S. Birian, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya akitoa taarifa fupi kwa wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu majukumu ya Ubalozi, utendaji na changamoto tunazokumbana nazo katika kufanikisha majukumu ya kila siku.

Mhe. Balozi Batilda S. Burian akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kupata taarifa ya utendaji wa ubalozi.


ZIARA YA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA NCHINI KENYA
Kamati ya Bingr ya Katiba, Sheria na Utawala iko nchini Kenya kwa ajili ya ziara maalum ya kimafunzo katika Bunge la Jamhuri ya Kenya.  Ziara hiyo ya kimafunzo imejikita katika maeneo yafuatayo
(i)                  Namna Bunge la Kenya linavyofanya kazi katika mchakato wakatiba mpya na utungaji wa katiba
(ii)                Ushiriki wa Wananchi katika utungaji wa katiba
(iii)               Utaratibu uliyotumika katika kupitisha katiba; na
(iv)               Utaratibu wa kura ya maoni ( Referundum)
Ujumbe huo mzito ambao una jumla ua wajumbe 20 unaongozwa na Mh. Pindi Hazara Chana (Mb), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba. Wakiwa katika ziara hiyo, wajumbe walipata fursa ya kutembelea ubalozi leo asubuhi na kuonana na Mhe. Balozi Batilda S. Burian.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.