Friday, November 15, 2013

Mhe. Rais Kikwete akutana kwa mazungumzo na Rais wa Sri Lanka


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa alipomtembelea jana kwa mazungumzo kabla ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola (CHOGM 2013).  Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye jengo la Temple Trees jijini Colombo, Sri Lanka.

Mhe. Rais Kikwete akisaini kitabu cha wageni, wakati Rais wa Sri Lanka Mhe. Rajapaksa  (mwenye nguo nyeupe) na Mhe. Bernard K. Membe (Mb) (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakishuhudia tukio hilo. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa wakati alipomtembelea jana kwenye jingo la Temple Trees jijini Colombo.

Mazungumzo ya Viongozi hao yakiendelea, wakati Mhe. Bernard K. Membe (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mhe. Balozi John Kijazi  (kushoto) wa Tanzania nchini India na Sri Lanka wakiwasikiliza kwa makini. 



Picha zote na Ikulu




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.