Sunday, November 10, 2013

Mhe. Membe akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa katika mazungumzo  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed (hayupo pichani) ambaye alifika nchini tarehe 8 Novemba, 2013 kama Mjumbe Maalum wa Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta kuja kutoa pongezi kwa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa hivi karibuni Bungeni kuhusu msimamo wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mhe. Membe na Mhe. Mohammed pia walijadili  masuala mengine ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili. 
Mhe. Mohammed (katikati) na Ujumbe wake wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao.
  Mhe. Membe (Mb.) akiendelea na mazungumzo huku Mhe. Mohammed na Ujumbe wake wakimsikiliza. Wengine katika picha waliofuatana na Mhe. Membe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (kulia kwa Mhe. Membe), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana ( wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Dora Msechu na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Robert Kahendaguza.
Mhe. Mohammed (katikati) nae akielezea dhumuni la ziara yake hapa nchini
Mhe. Membe na Ujumbe wake wakimsikiliza Mhe. Mohammed (hayupo pichani)
Bw. Togolani Mavura (kulia), Katibu wa Waziri Membe na Bw. Leonce Bilauri, Afisa Mambo ya Nje wakisikiliza kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Mhe. Membe na Mhe. Mohammed (hawapo pichani)


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.