Monday, November 18, 2013

Tanzania na Kuwait zasaini Mkataba wa Kulinda na Kukuza Vitega Uchumi pamoja na Mkataba wa Kushitrikiana katika Masuala ya Utalii

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe {Mb} aliye kushoto akiongea na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Khalid Al-Sabah kabla ya shughuli ya kusaini Mikataba kuanza.
 




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe {Mb} na Waziri mwenzake wa Kuwait wakisaini Mikataba ya Kukuza na Kulinda Vitega Uchumi; na Kushirikiana katika Masuala ya Utalii. Uwekaji saini huo ulifanyika nchini Kuwait siku ya Jumapili tarehe 17 Novemba, 2013.

Picha zaidi za uwekaji saini huku Maafisa kutoka Wizara za Mambo ya Nje za Tanzania na Kuwait wakishuhudia. kushoto ni Bw. Benedict Msuya kutoka Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe {Mb} na mwenzake wa Kuwait wakipongezana baada ya kukamilisha kazi ya kuweka saini Mikataba, Wanaopiga makofi ya furaha kutoka kushoto ni Mhe. Prof. Abdillah Omar, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia ambaye anawakilisha pia Kuwait na Qatar na anayefuata ni Mhe. Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Waheshimiwa Mawaziri wakibadilishana Mikataba mara baada ya kuisaini huku Balozi Yahya akipiga makofi kwa furaha.

Waheshimiwa Mawaziri wakiteta jambo baada ya kukamilisha kazi ya kusaini Mikataba.

Mhe. Membe akiongea na ujumbe wake, Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Clifford Tandari , Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Fedha, Bw. Charles Samanyi, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia ambaye pia anashughulikia masuala ya Afro Arab, Mhe. Naimi Aziz na Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.