Sunday, November 17, 2013

Naibu Waziri atunukiwa Shahada ya Uzamivu

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akitafakari wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo Mhe. Dkt. Maalim alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika masuala ya Sheria.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Balozi Nicholaus Kuhanga akimtunuku Shahada ya Uzamivu (Ph.D) Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) katika Mahafali ya 43 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani tarehe 16 Novemba, 2013. Mhe. Dkt. Maalim alikuwa miongoni mwa Wahitimu 41 waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu siku hiyo.

Mhe. Dkt. Maalim na Wahitimu wengine wa Shahada ya Uzamivu wakiwa wenye nyuso za furaha.

Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, Mhe. Balozi Fulgence Kazaura (katikati mwenye joho jekundu) akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Rwekaza Mukandala (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Wahadhiri wengine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo hicho.

Wahitimu wa Shahada na Stashahada mbalimbali.

Picha ya pamoja



Mhe. Dkt. Maalim (katikati) akiwa na Wahitimu wenzake. Kushoto ni Dkt. Adelardus Kilangi na Dkt. Mramba Joseph (kulia)

Mhe. Dkt. Maalim akiwa na Wahitimu wengine wakiimba Wimbo wa Taifa.

Mhe. Dkt. Maalim akiwa na Mke wake mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu.

Mhe. Dkt. Maalim na Familia yake.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.