Wednesday, January 14, 2015

Waziri Membe amuaga Balozi wa Algeria

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamiliusi Membe (Mb.) akimkabidhi zawadi ya picha yenye michoro ya Tembo  Balozi wa Algeria Mhe. Djelloul Tabel nchini Tanzania wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi huyo ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini. Hafla hiyo ilifanyika Hyatt regency kempinski Hotel jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Algeria Mhe.Djelloul Tabel, kwenye Hafla ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje  kwa ajili ya kumuaga Balozi Tabel ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bi. Zuhura Bundara akizungumza katika ghafla ya kumwaga balozi wa Algeria.
Balozi Djelloul Tabel akitoa neno la shukrani, wakati wa hafla ambapo alitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano aliopata katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini na kuomba ushirikiano huo uendelee.
Balozi Tabel akiendelea kuongea
Wageni waalikwa wakimpongeza Balozi Tabell kwa kumpigia makofi
Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia wizara ya Mambo ya Nje Balozi Mbelwa Kairuki naye akimsikiliza Balozi Tabell wa Algeria 


Waziri Membe akimweleza jambo Mhe. Balozi.
Waziri Membe wakigonga Glasi (Cheers)
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Algeria Mhe Tabell.


Naibu Waziri Mambo ya Nje akutana na Mabalozi wa kundi la nchi nne.



Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) akiwapokea wizarani mabalozi wa kundi la nchi nne (Ujerumani,Brazil,India na Japani)  kwa mazungumzo kuhusu mabadiliko ya muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

 Balozi wa Brazil hapa nchini, Mhe.Fransisco Carlos Luiz akichangia jambo katika mazungumzo hayo,huku Naibu waziri Mhe.Mahadhi pamoja na maofisa wa wizara ya Mambo ya Nje Adam Isara (wa kwanza kulia) na Ramla Khamis wakimsikiliza kwa makini.
Majadiliano ya mabalozi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe.Mahadhi yakiendelea.
Balozi wa Japani, Mhe.Masaki Okada (kulia),Balozi wa India Mhe.Dednath Shaw (katikati) pamoja na Balozi wa Ujerumani Mhe.Egon Kochanke wakati wa mazungumzo hayo.

Tuesday, January 13, 2015

Balozi Kilumanga ashiriki Hafla ya kuwakumbuka Wahanga wa shambulizi la kigaidi Ufaransa



Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Chabaka Kilumanga akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa katika Ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo, jijini Paris, Ufaransa. Kitabu cha maombolezo kimefunguliwa kwenye ubalozi wa Ufaransa nchini Comoro na kusainiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro, Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa pamoja na watu Mashuhuri. 
Balozi Chabaka Kilumanga, akisalimiana na viongozi wa Serikali ya Comoro katika maombolezo hayo.


Rais Kikwete awaandalia Sherry Party Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini katika hafla ya kuwatakia heri ya mwaka mpya, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Januari 9, 2015.
Baadhi ya Mabalozi wakimsikiliza Mhe. Rais katika hafla hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe.Bernard Kamillius Membe (wa kwanza kulia) akiwa pamoja na maofisa wa wizara hiyo wakimsikiliza Mhe. Rais.
Mmoja wa mabalozi waliohudhuria hafla ya mwanzo wa mwaka akisalimiana na Mhe. Rais
Mmoja wa mabalozi waliohudhuria hafla hiyo,akisalimiana na Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe.Bernard Kamillius Membe akiteta jambo na naibu wake, Mhe. Dkt.Mahadhi Juma Maalim na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw.John Haule (Kulia), wakisubiri kuanza kwa hafla ya mwanzo wa mwaka ya mabalozi.
Rais Kikwete (mstari wa mbele,katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa mabalozi wa nchi mbalimbali aliowaandalia hafla ya kufungua mwaka. Kulia kwa Mhe. Rais ni waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Membe,na kushoto kwake ni Naibu waziri wa Mambo ya Nje, Mhe.Dkt.Mahadhi. 
(Picha na Reuben Mchome)

Deputy Minister Presents exequatur to New Zealand Consul

The Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Dr. Maadhi Jima Maalim presents exequatur to the Honorary Consul of New Zealand in Tanzania, Mr. Hatim Karimjee (L).
Dr. Mahadhi exchanges views with Mr Karimjee after the presentation of exequatur.
 Personal Assistant to the Deputy minister, Mr. Adam Isara (left) and Miss. Berthar Makilagi takes notes of the meeting. 
Meeting is in progress

Photo by Reginald Philip.

Saturday, January 10, 2015

Deputy Minister Presents Work Certificates to India, Oman Consuls

The Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Dr. Maadhi Juma Maalim presents exequatur to the Consul General of India in Zanzibar, Mr. Satendar Kumar (Left).
Dr. Mahadhi exchanges views with Mr Kumar after the presentation ceremony.
The Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Dr. Mahadhi Juma Maalim, presents exequatur to the Consul General of Oman in Zanzibar,  Mr. Ali Abdullah Al Rashdi (Left).
Dr. Mahadhi and Mr. Al Rashid in discussions after presentation of exequatur.

The Deputy Minister listens to the Oman Consul General (not in picture) as the minister's Personal Assistant, Mr. Adam Isara (Right) takes notes. 


Photo By: Reginald Philip



Deputy Minister Presents Work Certificates to India, Oman Consuls

The Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Dr Mahadhi Juma Maalim today presented work certificates (Exequatur) to the Indian Consul General in Zanzibar, Mr Satendar Kumar and the Consul General of Oman, Mr Ali Abdullah Sulaiman Al Rashid, in separate ceremonies at the ministry headquarters in Dar es Salaam.

Mr. Kumar informed the Deputy Minister that his government was financing construction of a vocational training centre in Zanzibar while preparations were underway for implementation of other development projects.
Dr Mahadhi commended India for the assistance, saying Tanzania and the Asian country had very strong relations.

The Oman Consul General told Dr Mahadhi that his country was preparing an international donor conference to marshal financial resources for the development of Zanzibar to be held this year. The Deputy Minister said Prime Minister Mizengo Pinda was made aware of the plan during his recent visit to the Sultanate of Oman and that the union government fully supported the idea.

Dr Mahadhi said Zanzibar and Oman had deep-rooted historical ties. "The history of Zanzibar is not complete without Oman and the history of Oman is not complete without Zanzibar," he explained.

Friday, January 9, 2015

Katibu mkuu Mambo ya Nje akutana na Mabalozi waliopanda mlima Kilimanjaro

Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Mataifa Bw. John Haule (Wa tatu kulia) akizungumza na baadhi ya waheshimiwa Mabalozi waliopanda mlima Kilimanjaro mwezi uliopita.
Baadhi ya waheshimiwa Mabalozi waliopanda mlima Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Haule.
Picha na Reuben Mchome.

PRESS RELEASE

François Hollande

President of the United Republic of Tanzania, H.E. Jakaya Mrisho Kikwete has sent the condolence message to H.E. François Hollande, President of the Republic of France following a shooting attack at the Charlie Hebdo offices in Paris which occurred on 7th January, 2015.

The message reads as follows:

‘‘H.E. François Hollande,
President of the Republic of France,
Paris,
FRANCE

Your Excellency,

I have received with great sadness and dismay the devastating news of the tragic attack at the Charlie Hebdo offices in Paris which has claimed the lives of 12 people and injured several others. On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania and on my own behalf, I wish to convey to you our heartfelt condolences and through you to the bereaved families who have been robbed of their loved ones by this heinous act.

France and Tanzania enjoy good relations through which we have worked hand in hand to tackle the most pressing security challenges of our time. To this end, I condemn this senseless attack which aimed at bringing fear and insecurity among the French people and the world at large. We are convinced that under your able leadership, the Government of France will leave no stone unturned in bringing the perpetrators to justice.

       While wishing all the victims fortitude in this difficult time, please accept, Your Excellency, renewed assurances of my highest consideration.


Issued by: THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM

8 January 2015


Thursday, January 8, 2015

Wadau wajadili sera ya Taifa ya Mtangamano ya Afrika Mashariki


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akifungua kikao cha wadau cha kujadili Sera ya Taifa ya Mtangamano wa Afrika Mashariki, katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba yahaya akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Said Seif Mzee  wakifuatilia hotuba
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Irene Kasyanju pamoja na Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA Bwa. Isack Kalumuna wakisikiliza Hotuba ya ufunguzi. 
Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje Bw. James Lugaganya akitoa mada kwa wadau kuhusu mambo muhimu yaliyozingatiwa katika Sera ya Taifa ya Mtangamano ya Afrika Mashariki

Wadau wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Bw. Lugaganya
Sehemu nyingine wadau
Balozi Mstaafu Vincenti Kibwana akichangia jambo katika kikao hicho
Mdau, Bi. Grace Naburi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi naye akitoa mchango wake kuhusi sera hiyo


Mdau, Bw. Justin Moshi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria
Mdau, Bi. Mindi Kasiga kutoka Wizara ya Mambo ya Nje nae akichangia mada
Wadau mbali mbali wakiwa katika kikao.
Kikao kikiendelea





Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akiwa katika Picha ya pamoja na wadau.


Picha na Reginald Philip