Balozi Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Al Maadadi mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho |
Wednesday, June 17, 2015
Katibu Mkuu Balozi Mulamula apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Qatar nchini
Saturday, June 13, 2015
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje amuaga Balozi wa Brazil aliyemaliza muda wa kazi nchini
Meza Kuu wakiwemo Mabalozi kutoka nchi mbalimbali zenye uwakilishi hapa nchini |
Balozi Luz pamoja na Mablozi wengine wakimsikiliza Balozi Mulamula ambaye haonekani pichani |
Balozi Luz nae akitoa hotuba yake ambapo aliisifu Tanzania kuwa ni nchi ya amani na kwamba nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula pamoja na Mabalozi wengine wakimsikiliza Balozi Luz (hayupo pichani) |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula na Balozi Luz wakigonga glasi kama ishara ya kuutakia heri ushirikiano kati ya Tanzania na Brazil |
Sehemu ya Mabalozi wakishuhudia Balozi Luz akipewa zawadi (hayupo pichani) |
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Balozi wa Brazil hapa nchini. Kushoto ni Bw. Leonce Bilauri na Bi. Felister Rugambwa |
Balozi wa Namibia hapa nchini akiwa pamoja na Balozi wa Cuba nchini. |
Balozi wa Urusi hapa nchini Mhe. Yuri Fedorovich Popov (kushoto) akimweleza jambo mmoja wa wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Brazil |
Sehemu nyingine ya Wageni waalikwa |
Waziri Membe awaaga Mawaziri wa nchin wanachama wa Umoja wa Afrika
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimtaifa, Mhe. Bernard Membe (Mb.) akisoma Hotuba ya kuwaaga Mawaziri wenzake katika mkutano wa Mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. |
Friday, June 12, 2015
Watanzania wengine 13 warejea kutoka nchini Yemen
Kiongozi wa msafara wa Watanzania kumi na tatu waliorejea leo nchini wakitokea nchini Yemeni, Bw.Faiz Abdulsheikh Said akizungumza na Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Asha Mkuja wakati wa mapokezi ya Watanzania hao walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Shirika la Ndege la Qatar. Serikali imefanikiwa kuwarejesha nchini zaidi ya Watanzania 100 kutoka Yemen baada ya nchi hiyo kukumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Zoezi la kuwarejesha Watanzania hao linaratibiwa na kusimamiwa na Wizara kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman. Watanzania wengine 15 wanatarajiwa kuwasili nchini kesho tarehe 13 Juni, 2015.
Bi. Asha Mkuja akiendelea kupata maelezo kutoka kwa mmoja wa Watanzania hao Mzee Bader Saleh Omar kuhusu hali ilivyo nchini Yemen.
Mazungumzo yakiendelea
Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi.Asha akimsikiliza kwa makini mzee Bader, akimpa maelezo ya hali ilivyo huko Nchini Yemen.
Watanzania hao wakijiandaa kuondoka ndani ya Uwanja wa Ndege baada ya kukamilisha taratibu zote.
Picha na Reuben Mchome
Picha na Reuben Mchome
Wednesday, June 10, 2015
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje aongoza maadhimisho ya siku ya Taifa la Sweden
Mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Taifa la Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa Sweden hapa nchini. Mhe. Lennarth Hjelmaker (hayupo pichani).
Balozi wa Sweden hapa nchini, Mhe.Balozi Lennarth Hjelmaker akifungua hafla hiyo iliyofanyika usiku wa tarehe 09/06/2015 katika Makazi ya Balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
Balozi Lennarth akimkaribisha Balozi Mulamula katika hafla hiyo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filberto Cerian Sebregondi akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula huku Afisa wa Wizara hiyo Bi.Asha Mkuja (kushoto mwenye kilemba).
Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini Mhe.Balozi Juma Halifan Mpango akisalimiana na Balozi Liberata Mulamula.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Katibu Mkuu Mulamula akiendelea na hotuba yake,kushoto ni Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe.Lennarth
Balozi Lennarth na Katibu Mkuu Balozi Mulamula pamoja na wageni waalikwa wakinyanyua glasi kutakiana kheri katika ushirikiano wa nchi hizi mbili.
Balozi wa Sweden Mhe.Lennarth akicheza kwa furaha pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi huo hapa nchini kama ishara ya kufurahia maadhimisho ya siku ya Taifa lao la Sweden sherehe zilizofanyika katika makazi ya balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha watoto wa Maafisa wa Ubalozi wa Sweden hapa nchini walioshiriki hafla hiyo kwa wakiimba kwa ufasaha nyimbo za Mataifa ya Sweden na Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waandishi wa abari katika hafla hiyo.
===================
Picha na Reuben Mchome.
Tuesday, June 9, 2015
Balozi Mulamula akutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa EU hapa nchini
Maafisa Mambo ya Nje Waandamizi wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Sebregondi (hawapo pichani). |
Balozi Mulamula na Balozi Sebregondi wakimsikiliza Balozi Melrose akifafanua jambo |
Kikao kikiendelea
Picha na Reginald Philip
|
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje azungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress pamoja na ujumbe ulioambatana na Mhe. Thomas - Greenfield nao wakifuatilia mazungumzo. |
Balozi Linda akitoa ufafanuzi wa jambo huku Balozi Mulamula akimsikiliza kwa makini. |
Balozi Mulamula (katikati) akimsikiliza Mhe. Linda alipokuwa akizungumza naye kulia ni Afisa Mambo ya Nje Bwa. Lucas Mayenga. |
Picha na Reginald Philip.
Monday, June 8, 2015
Balozi wa China amtembelea Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youquig alipomtembelea Wizarani kwa mazungumzo ya kudumisha ushirikiano wa nchi hizi mbili.
Mkalimani wa Balozi wa China Bi.Wang Fang akisalimiana na Katibu Mkuu
Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youqing akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa China huku Maafisa wa pande zote mbili wakinukuu kile kinachozungumzwa.
Balozi wa China, Mhe.Lu akifurahia jambo na Balozi Mulamula
Balozi Lu Youqing akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Maafisa kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Mr.Dong (kulia), Mr.Lin Liang (katikati) na Bi.Wang Fang wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Lu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw.Nathaniel Kaaya (wa kwanza kushoto) kwa pamoja na Maafisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza (wa kwanza kulia) pamoja na Bi.Ramla Hamis wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Lu (hawapo pichani).
Picha na Reuben Mchome
Subscribe to:
Posts (Atom)