Thursday, September 10, 2015

Waziri Membe azungumza na Mabalozi kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.), akizungumza na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, kuhusu nafasi na majukumu yao katika uchaguzi mkuu ujao, pamoja na jinsi Serikali ilivyojipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani, huru na haki kwa vyama vyote.
Waheshimiwa Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini,wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), wakati wa mkutano huo uliofanyika leo 10-09-2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIC) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Mambo ya Nje Balozi Celestine Mushy na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Bi Rosemary Jairo (kushoto) wakimsikiliza Mheshimiwa Waziri.
Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage Juma, akiwatambulisha Mabalozi waliowasili nchini hivi karibuni ambao ni mara yao ya kwanza kuhudhuria Kikao cha aina hii, Wizara ya Mambo ya Nje. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye pia alikua muendeshaji wa mkutano huo Bi. Mindi Kasiga, akiratibu kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao hicho. 
Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini Mhe.Thamsanga Dennis Mseleku akiuliza swali katika mkutano huo.
Balozi wa Namibia hapa nchini Mhe. Japhet Isaack, akiuliza swali katika mkutano huo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi, akiuliza swali katika mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), akijibu Maswali ya Waheshimiwa Mabalozi, kushoto kwa Mhe. Waziri ni Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini Mhe. Juma Khalifan Mpango, Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (kulia kwa Mhe. Waziri) na Mwisho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.

Baadhi ya Mabalozi wakisikiliza majibu yanayotolewa na Mhe. Waziri Membe katika mkutano huo.

Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Paulo Kabale (kulia), Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara hiyo Bw. Abisai Mathias (katikati), na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa wizara hiyo, Bw. Lucas Suka wakibadilishana mawazo baada ya mkutano kuisha.
 Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini Mhe. Juma Khalfan Mpango, akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, ambaye pia alikua muendeshaji wa mkutano huo.
 (pichani juu na chini) Baadhi ya  Mabalozi wakibadilishana mawazo na kusalimiana muda mfupi kabla ya mkutano huo kuanza. 
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Mambo ya Nje Balozi Celestine Mushy akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi.
Waheshimiwa Mabalozi wakibadilishana mawazo.
Mkutano ukiendelea
 Mkutano ukiendelea....
Mhe. Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano huo kumalizika.
Picha ya pamoja.
=======================
PICHA NA REUBEN MCHOME.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  
Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wamehimizwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC). Hayo yamesemwa leo Septemba 10, 2015 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), alipokutana na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wa hapa nchini kwenye Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Tanzania inatarajiwa kupokea waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa kati ya 400 hadi 600 katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015.
“Tunatarajia kupokea waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi kati ya 400 na 600 kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), nchi za SADC, Jumuiya ya Ulaya (EU), Marekani, Uingereza, Norway na nchi nyingine. Hivyo, kupitia kwenu (Mabalozi) nawaomba muwasisitize wazingatie sheria na kanuni kama zilivyoainishwa na NEC na ZEC”. Waziri Membe alisikika akisema.
Waziri Membe alitaja baadhi ya kanuni ambazo waangalizi wa Kimataifa wanatakiwa kuzingatia kuwa ni pamoja na kutotoa taarifa kwenye vyombo vya habari wakati wa zoezi la uchaguzi linaendelea; kutoingilia zoezi la uchaguzi kwa maana ya kwamba, wanatakiwa kuwa waangalizi wa uchaguzi na sio kushiriki zoezi la uchaguzi; kuandaa ripoti baada ya uchaguzi na kuziwasilisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Tume za Uchaguzi na mamlaka nyingine zinazohusika pamoja na kuainisha kwa maandishi kasoro zote zitakazojitokeza wakati wa zoezi hilo.
Aidha Mhe. Membe aliwahakikishia waangalizi wa uchaguzi kuwa Serikali itatota uhuru wa kutembelea majimbo yote ya uchaguzi bila kikwazo chochote kwani Serikali imejipanga kuendesha uchaguzi wa huru, haki na wazi, hivyo, haina chochote cha kuficha.
Kuhusu utulivu wakati wa uchaguzi, Waziri Membe aliongeza kuwa Serikali imejipanga vyema kuhakikisha uchaguzi wa Oktoba unafanyika kwa amani na utulivu, kama ilivyokuwa mila na desturi ya taifa la Tanzania. Alisisitiza kuwa vyombo vya usalama havitashiriki katika uchaguzi huo, isipokuwa vitahakikisha kuwa amani inakuwepo wakati wote wa uchaguzi. Pia usalama wa Watanzania kwa ujumla na mali zao utaimarishwa.
Katika hatua nyingine, Waziri Membe alisema kuwa yeye kama mwana CCM ana uhakika chama chake kitaibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi Mkuu ujao. Alisema haoni sababu ya CCM kushindwa kwani tofauti na vyama vingine vinavyoshiriki uchaguzi huo ni CCM pekee ndio chama kinachojivunia rekodi nzuri na madhubuti; mpango kazi unaoainisha shughuli zilizotekelezwa, zinazotekelezwa na zinazotarajiwa kutekelezwa pamoja na kuwa na mgombea bora wa nafasi ya Rais ukilinganisha na wagombea wengine wote nane wanaowania nafasi hiyo.
Waziri Membe alihitimisha mkutano wake kwa kulishukuru Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Washirika wengine wa maendeleo kwa kuchangia gharama za uchaguzi huo ambazo ni Shilingi bilioni 265 za Kitanzania.
Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Urais utafanyika nchini tarehe 25 Oktoba 2015 na Watanzania takriban milioni 23.7 wamejiandikisha kushiriki uchaguzi huo.   

MWISHO.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,


10 Septemba, 2015

Wednesday, September 9, 2015

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Mabalozi kutoka Uswisi, Uturuki, Finland na Sweden

.........Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Uswis
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Uswis hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli, katika hafla iliyofanyika leo 09-09-2015, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Uswis hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli (wa pili kushoto), pamoja na mumewe ambaye ni balozi mteule wa nchi hiyo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, na afisa mwandamizi ( wa kwanza kushoto) walioambatana naye kuwasilisha hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi mpya wa Uswis hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli, akisaini kitabu cha wageni ikulu, katika hafla fupi ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais akifanya mazungumzo na Balozi mpya wa Uswis na ujumbe wake, baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), (wa kwanza kushoto) Bi. Tunsume Mwangolombe, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Marekani, na Mshauri wa Rais masuala ya Diplomasia Balozi Samuel Shelukindo wakifuatilia mazungumzo.
Mhe. Florence Tinguely Mattli, Balozi mpya wa Uswis hapa nchini akisikiliza wimbo wa taifa lake muda mfupi baada ya kuwasili ikulu jijini Dar es Salaam.
====================
 .........Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Uturuki.
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Uturuki hapa nchini Mhe. Yasemin Eralp, katika hafla iliyofanyika leo 09-09-2015, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete akimtambulisha Mhe. Yasemin Eralp.

Mheshimiwa Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Uturuki hapa nchini Mhe. Yasemin Eralp (wa pili kushoto), Maofisa waandamizi kutoka Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania, pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb), katika picha ya pamoja.
Rais akifanya mazungumzo na Balozi mpya wa Uturuki na ujumbe wake, baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho.
Mshauri wa Rais masuala ya Diplomasia Balozi Shelukindo (katikati) Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na Bi. Tunsume Mwangolombe, wakifuatilia mazungumzo ya Mhe. Rais na Balozi mpya wa Uturuki (hawapo pichani).
Balozi mpya wa Uturuki hapa nchini Mhe. Yasemin Eralp, akisaini kitabu cha wageni Ikulu, katika hafla fupi ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
 Mhe. Yasemin Eralp , Balozi mpya wa Uturuki hapa nchini akisikiliza wimbo wa taifa lake muda mfupi baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
=================
.........Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Finland
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Finland hapa nchini Mhe. Pekka Hukka, katika hafla iliyofanyika leo 09-09-2015, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi mpya wa Finland hapa nchini Mhe. Pekka Hukka, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), katika hafla hiyo.

Balozi mpya wa Finland hapa nchini Mhe. Pekka Hukka, akisalimiana na Bi. Tunsume Mwangolombe Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Marekani, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 



Mhe. Rais akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Finland hapa nchini Mhe. Pekka Hukka.

Rais akifanya mazungumzo na Balozi mpya wa Finland na ujumbe wake, baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho.
        Balozi mpya wa Finland hapa nchini Mhe. Pekka Hukka, akisaini kitabu cha wageni ikulu, katika hafla fupi ya kuwasilisha hati zake za utambulisho.
                                =================
.............Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Sweden.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Sweden hapa nchini Mhe. Katarina Rangnitt, katika hafla iliyofanyika leo 09-09-2015, ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi mpya wa Sweden hapa nchini Mhe. Katarina Rangnitt,akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga wakati wa hafla hiyo.
Mheshimiwa Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Sweden hapa nchini Mhe. Katarina Rangnitt (wa pili kushoto), pamoja na Maofisa wake walioambatana naye kuwasilisha hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais akifanya mazungumzo na Balozi mpya wa Sweden hapa nchini na ujumbe wake, baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho.

  Mhe.Katarina Rangnitt, Balozi mpya wa Sweden hapa nchini akisikiliza wimbo wa taifa lake muda mfupi baada ya kuwasili ikulu jijini Dar es Salaam.
                                    ==================
PICHA NA REUBEN MCHOME.

Tuesday, September 8, 2015

Tanzania mwenyeji Mkutano wa Kimataifa kuhusu masuala ya Lishe na Chakula

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akimpokea Mfalme wa Lesotho,  Mhe. Letsie III (kulia) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Kilimanjaro (KIA).  Mfalme Letsie ambaye pia ni Kiongozi wa kuhamasisha masuala ya Chakula na Lishe wa Umoja wa Afrika yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kwanza wa Dunia kuhusu umuhimu wa kuongeza Virutubisho kwenye Chakula. Mkutano huo unafanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 09 hadi 11 Septemba, 2015.
Waziri Mkuu Mhe. Pinda (katikati) akimtambulisha Mkurugenzi wa TANAPA Dkt. Allan Kijazi (wa kwanza kulia) kwa Mfalme Letsie (wa kwanza kushoto).
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (wa kwanza kulia) akimtambulisha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu CCM Arusha Mhe. Catherine Magige (wa pili kutoka kushoto) kwa Mfalme Letsie (wa pili kutoka kulia).
Mfalme Letsie akiwapingia Mkono moja ya vikundi vya ngoma vulivyokuwepo uwanjani hapo
Mhe. Pinda akimwongoza Mfalme Letsie III mara baada ya kumpokea. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Daudi Felix Ntibenda.
Mhe. Waziri Mkuu kwa pamoja na Mfalme Letsie III wakiwa wameongozana pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Ntibenda na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Itifaki katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. James Bwana (mwenye tai nyeupe)


Mhe. Pinda akizungumza na Mfalme Letsie mara tuu baada ya kuwasili uwanjani hapo

Picha na Reginald Philip
=====================================


Tanzania imekuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Dunia kuhusu umuhimu wa kuongeza Virutubisho kwenye Chakula kwa ajili ya Lishe Bora utakaofanyika kwa siku tatu Jijini Arusha kuanzia tarehe 09 hadi 11 Septemba, 2015.

Mkutano huo ambao utahudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, utafunguliwa rasmi na Mfalme wa Lesotho Letsie III ambaye ni Kiongozi wa kuhamasisha Lishe na Chakula Bora wa Umoja wa Afrika.

Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika, utajadili masuala mbalimbali yanayohusu umuhimu wa kuongeza virutubisho kwenye chakula ikiwemo vitamini na madini muhimu ili  kuwawezesha watu duniani kote kuwa na afya bora kwa ajili ya uzalishaji na kuleta maendeleo na hatimaye kuondokana na umaskini. 

Pia Mkutano huu ni sehemu ya jitihada za kimataifa katika kukomesha lishe duni na utapiamlo uliokithiri katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

Aidha, Mkutano huo utawashirikisha wadau na wataalam mbalimbali kutoka Mashirika ya Kimataifa, Sekta Binafsi na Serikalini. Mashirika hayo ni pamoja na  Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Chakula Duniani (WFP) na Umoja wa Afrika  (AU).

Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) ya Uingereza.

-Mwisho-



Rais Kikwete Apokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki kutoka kwa taasisi ya East Africa Book of Records yenye makao yake makuu jijini Kampala Nchini Uganda. Pichani ni kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt. Paul Bamutize akimkabidhi Rais Kikwete tuzo hiyo wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Sambamba na Tuzo hiyo, Rais Kikwete pia amepokea tuzo ya kuitambua Tanzania kama taifa bora Afrika Mashariki kwa kudumisha Amani na Utulivu, Huduma bora za kijamii na Maendeleo makubwa ya kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake.
(Picha na Freddy Maro).
=================


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Amani na utulivu ulioko nchini , umechangiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wote wa Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo leo Ikulu wakati akipokea nishani ya Amani kutoka kwa Dr. Paul Bamutize, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya East Africa Book Records yenye makao yake makuu nchini Uganda.
Rais amepokea nishani mbili leo ambazo ni kwa ajili ya nchi na ingine kwa ajili yake kama Kiongozi wa Tanzania.
Dr. Bamutize amesema Tanzania imekua mfano wa kuigwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ambapo pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi kama chama ambacho kimesimamia Amani hiyo hapa nchini.
“Amani hii tuliyonayo hapa nchini imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Tanzania ambao napenda kupokea nishani hii kwa niaba yao kwa sababu wao ndiyo watunzaji na walinzi wakubwa wa Amani hii” Rais Kikwete amesema.
Dr. Bamutize amempongeza Rais Kikwete na kuelezea kuwa amani hiyo imeleta matumaini kwa wawekezaji na majirani wa Tanzania na hivyo kuwa mfano wa kuigwa na majirani zake wote katika ukanda huu na Afrika kwa ujumla.
Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na mabalozi wa Burundi, Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Watu wa Congo na  Uganda.
Wakati huo huo Rais Kikwete amepokea Ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi.
Ujumbe huo umeletwa Ikulu na Mheshimiwa Rajiv Pratap Rudy Waziri wa Nchi anaeshughulikia Maendeleo ya Ujasiriamali ambaye pia amefanya mazungumzo na Rais Kikwete kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na ushirikiano katika biashara na ujasiriamali.
……………………………Mwisho……………………………
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-Dsm

8 Septemba, 2015