Tuesday, September 8, 2015

Tanzania mwenyeji Mkutano wa Kimataifa kuhusu masuala ya Lishe na Chakula

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akimpokea Mfalme wa Lesotho,  Mhe. Letsie III (kulia) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Kilimanjaro (KIA).  Mfalme Letsie ambaye pia ni Kiongozi wa kuhamasisha masuala ya Chakula na Lishe wa Umoja wa Afrika yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kwanza wa Dunia kuhusu umuhimu wa kuongeza Virutubisho kwenye Chakula. Mkutano huo unafanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 09 hadi 11 Septemba, 2015.
Waziri Mkuu Mhe. Pinda (katikati) akimtambulisha Mkurugenzi wa TANAPA Dkt. Allan Kijazi (wa kwanza kulia) kwa Mfalme Letsie (wa kwanza kushoto).
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (wa kwanza kulia) akimtambulisha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu CCM Arusha Mhe. Catherine Magige (wa pili kutoka kushoto) kwa Mfalme Letsie (wa pili kutoka kulia).
Mfalme Letsie akiwapingia Mkono moja ya vikundi vya ngoma vulivyokuwepo uwanjani hapo
Mhe. Pinda akimwongoza Mfalme Letsie III mara baada ya kumpokea. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Daudi Felix Ntibenda.
Mhe. Waziri Mkuu kwa pamoja na Mfalme Letsie III wakiwa wameongozana pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Ntibenda na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Itifaki katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. James Bwana (mwenye tai nyeupe)


Mhe. Pinda akizungumza na Mfalme Letsie mara tuu baada ya kuwasili uwanjani hapo

Picha na Reginald Philip
=====================================


Tanzania imekuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Dunia kuhusu umuhimu wa kuongeza Virutubisho kwenye Chakula kwa ajili ya Lishe Bora utakaofanyika kwa siku tatu Jijini Arusha kuanzia tarehe 09 hadi 11 Septemba, 2015.

Mkutano huo ambao utahudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, utafunguliwa rasmi na Mfalme wa Lesotho Letsie III ambaye ni Kiongozi wa kuhamasisha Lishe na Chakula Bora wa Umoja wa Afrika.

Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika, utajadili masuala mbalimbali yanayohusu umuhimu wa kuongeza virutubisho kwenye chakula ikiwemo vitamini na madini muhimu ili  kuwawezesha watu duniani kote kuwa na afya bora kwa ajili ya uzalishaji na kuleta maendeleo na hatimaye kuondokana na umaskini. 

Pia Mkutano huu ni sehemu ya jitihada za kimataifa katika kukomesha lishe duni na utapiamlo uliokithiri katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

Aidha, Mkutano huo utawashirikisha wadau na wataalam mbalimbali kutoka Mashirika ya Kimataifa, Sekta Binafsi na Serikalini. Mashirika hayo ni pamoja na  Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Chakula Duniani (WFP) na Umoja wa Afrika  (AU).

Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) ya Uingereza.

-Mwisho-



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.