Monday, September 14, 2015

Rais Kikwete apokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Sudani.


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimpokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudani Prof. Ibrahim Ahmed Ghandour Ikulu jijini Dar es Salaam, alipowasilisha ujumbe rasmi kutoka kwa Rais wa Sudan Mhe. Omar Al-Bashir leo tarehe 14-08-2015.
 Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudani Prof. Ibrahim Ahmed Ghandour, akimkabidhi rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ujumbe rasmi kutoka kwa Rais wa Sudan Mhe. Omar Al-Bashir leo tarehe 14-08-2015, ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mhe. Rais Kikwete akisoma ujumbe huo kutoka kwa rais wa Sudan Mhe. Omar Al-Bashir.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (wa kwanza kushoto), pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo na Ikulu wakifuatilia mazungumzo hayo.

Ujumbe ulioambatana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudani Prof. Ibrahim Ahmed Ghandour, nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
picha ya pamoja
===========================

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) pamoja na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudani Prof. Ibrahim Ahmed Ghandour wakizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na Mheshimiwa Rais.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga (kulia) na Ujumbe wa Waziri ya Mambo ya Nje wa Sudani Prof. Ibrahim Ahmed Ghandour, nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo na waandishi wa habari.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe wakifurahia jambo na  mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudani Prof. Ibrahim Ahmed Ghandour, wakati wakizungumza na waandishi wa habari.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudani Prof. Ibrahim Ahmed Ghandour, akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Zuhura Bundala (kushoto) muda mfupi kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, akiteta jambo na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Dkt. Yassir Mohamed Ali, huku Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga akifuatilia mazungumzo hayo.
=======================
PICHA NA REUBEN MCHOME.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.