Tuesday, September 8, 2015

Rais Kikwete Apokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki kutoka kwa taasisi ya East Africa Book of Records yenye makao yake makuu jijini Kampala Nchini Uganda. Pichani ni kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt. Paul Bamutize akimkabidhi Rais Kikwete tuzo hiyo wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Sambamba na Tuzo hiyo, Rais Kikwete pia amepokea tuzo ya kuitambua Tanzania kama taifa bora Afrika Mashariki kwa kudumisha Amani na Utulivu, Huduma bora za kijamii na Maendeleo makubwa ya kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake.
(Picha na Freddy Maro).
=================


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Amani na utulivu ulioko nchini , umechangiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wote wa Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo leo Ikulu wakati akipokea nishani ya Amani kutoka kwa Dr. Paul Bamutize, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya East Africa Book Records yenye makao yake makuu nchini Uganda.
Rais amepokea nishani mbili leo ambazo ni kwa ajili ya nchi na ingine kwa ajili yake kama Kiongozi wa Tanzania.
Dr. Bamutize amesema Tanzania imekua mfano wa kuigwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ambapo pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi kama chama ambacho kimesimamia Amani hiyo hapa nchini.
“Amani hii tuliyonayo hapa nchini imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Tanzania ambao napenda kupokea nishani hii kwa niaba yao kwa sababu wao ndiyo watunzaji na walinzi wakubwa wa Amani hii” Rais Kikwete amesema.
Dr. Bamutize amempongeza Rais Kikwete na kuelezea kuwa amani hiyo imeleta matumaini kwa wawekezaji na majirani wa Tanzania na hivyo kuwa mfano wa kuigwa na majirani zake wote katika ukanda huu na Afrika kwa ujumla.
Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na mabalozi wa Burundi, Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Watu wa Congo na  Uganda.
Wakati huo huo Rais Kikwete amepokea Ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi.
Ujumbe huo umeletwa Ikulu na Mheshimiwa Rajiv Pratap Rudy Waziri wa Nchi anaeshughulikia Maendeleo ya Ujasiriamali ambaye pia amefanya mazungumzo na Rais Kikwete kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na ushirikiano katika biashara na ujasiriamali.
……………………………Mwisho……………………………
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-Dsm

8 Septemba, 2015

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.