Wednesday, September 30, 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
 
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

 

 
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
      11466 DAR ES SALAAM, 
                                    Tanzania.


Taarifa za kupatikana kwa majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania waliopotea huko Saudi Arabia

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imepokea majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawaonekani kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 na kusababisha vifo vya watu 769 na wengine 934 kujeruhiwa.

Itakumbukwa kuwa tarehe 28 Septemba, 2015 Wizara ilitoa taarifa kuwa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana huku wengine watano wakiwa wamefariki dunia.

Majina ya baadhi ya Mahujaji wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:-

1. Abdul Iddi Hussein
2. Awadh Saleh Magram
3. Burhani Nzori Matata
4. Yussuf Ismail Yusuf
5. Saleh Mussa Said
6. Adam Abdul Adam
7. Archelaus Antory Rutayulungwa
8. Farida Khatun Abdulghani
9. Rashida Adam Abdul
10. Hamida Ilyas Ibrahim
11. Rehema Ausi Rubaga
12. Faiza Ahmed Omar
13. Khadija Abdulkhalik Said
14. Shabinabanu Ismail Dinmohamed
15. Salama Rajabu Mwamba
16. Johari Mkesafiri Mwijage
17. Alwiya Sharrif Salehe Abdallah
18. Hafsa Sharrif Saleh Abdallah

Mbali na taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kutambuliwa kwa mwili wa hujaji mmoja wa Tanzania anayeitwa Hadija Shekali Mohammed wa kikundi cha Ahlu Daawa.

Aidha, Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha za maiti za Mahujaji waliokufa Makkah ambao wamehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa ajili ya utambuzi. Hivyo, Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission pamoja na vikundi vya Mahujaji unaendelea na zoezi la kuzihakiki picha hizo ili kubaini kama zinalingana na sura za Mahujaji wetu waliopotea.

Vilevile, Mamlaka ya Serikali ya Saudi Arabia imesema kuwa imechukua alama za vidole za Mahujaji waliokufa ili wazilinganishe na zile walizozichukua Uwanja wa Ndege wakati Mahujaji hao wakiingia nchini humo. Wizara inaamini kuwa taarifa za alama za vidole zitakapotolewa zitasaidia sana kuwatambua Mahujaji wetu.

Pamoja na jitihada zote hizo, Ubalozi pia unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji wengine wa Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali zilizohifadhi maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

29 Septemba, 2015

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.