Thursday, January 14, 2016

Waziri Mahiga akutana kwa mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia), akimsikiliza Rais wa Mahakama ya Afrika  Jaji Mstaafu, Mhe. Augustino Ramadhani alipofika kumtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Waziri. Pia kuzungumzia masuala mbalimbali yanayoihusu Mahakama hiyo likiwemo suala la ujenzi wa Mahakama hiyo katika Jiji la Arusha.
Waziri Mahiga naye akieleza jambo ambapo alimpongeza Mhe. Ramadhani kwa juhudi anazozifanya kwenye Mahakama hiyo.

Afisa Mambo ya Nje, Bw. Elisha Suku naye akielezea jambo katika mazungumzo kati ya Waziri Dkt. Mahiga na Mhe. Ramadhani (hawapo pichani), wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Baraka Luvanda, na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizarani, Bi. Mindi Kasiga. 
Mazungumzo yakiendelea
Picha na Reginald Philip

Wednesday, January 13, 2016

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Syria

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,  Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Balozi wa Syria hapa nchini Mhe.Abdulmonem Annan, baada ya Balozi huyo kumtembelea Naibu Waziri kwa ajili ya kumpongeza na kuzungumzia namna ya kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili.

 Balozi wa Syria hapa nchini Mhe.Abdulmonem Annan, akizungumza jambo na Mhe. Naibu Waziri wakati wa mazungumzo hayo.
 Msaidizi wa Naibu Waziri, Bw. Adam Isara (kulia), akifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
=======================================
Picha na Reuben Mchome.

Balozi wa Tanzania nchini Kenya azindua safari za ndege za Fastjet kutoka Dar es Salaam-Nairobi

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule akikata utepe kuzindua safari za ndege za Shirika la  Fastjet kati ya Dar es Salaam na Nairobi. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Balozi Ami Mpungwe (kushoto) na Meneja Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Jimmy Kibati (kulia)
Balozi Haule, Balozi Mpungwe(kushoto), Bw. Lawrence Masha na Bw. Kibati wakishangilia baada ya uzinduzi rasmi wa safari hizo.
Abiria waliowasili na ndege hiyo
Wakikata keki kuashiria uzinduzi huo.
Picha ya pamoja ya Balozi Haule na Maafisa wa Fastjet.

====================================
Kampuni ya safari za ndege za bei nafuu iliyosajiliwa Tanzania, Fastjet, imezindua safari zake za Dar es Salaam-Nairobi tarehe 11 Januari, 2016.

Ndege ya Fastjet kutoka Dar es Salaam ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi asubuhi ya tarehe 11 Januari, 2016 na kulakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule. 

Aidha, Wakurugenzi wawili wa kampuni hiyo, Balozi Ami Mpungwe na Bw. Lawrence Masha, pamoja na Meneja Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Jimmy Kibati, walijumuika kwenye safari hiyo. 

Kwa kuanzia, Fastjet itafanya safari za Dar es Salaam-Nairobi-Kilimanjaro na baadae itaanzisha safari za Dar es Salaam-Mombasa-Zanzibar.

Mhe. Haule alipongeza uanzishwaji wa safari hizo, akisema zitaimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Tanzania na kukuza utalii na biashara.

Waziri Mahiga ashiriki Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi walioshiriki katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium leo akiwa katika gari maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi lililoandaliwa rasmi katika kilele cha sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Susan Kolimba (kushoto), na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mhe. Sophia Simba wakifuatilia matukio wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Shen akiwapungia mkono vijana waliokuwa wakipita mbele yake (hawapo pichani).
Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakibeba Picha la Marehemu Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Karume wakati wa Maandamano ya kusherehehekea Kilele cha Mapinduzi Kutimia miaka 52 leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.  
Rais Shen akiwahutubia wananchi wa Zanzibar wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52  
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi (katikati juu), akiwa pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.  
Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa kilele cha sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja. 
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (mwenye tai nyekundu) akifurahia jambo na na Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mwenye Tai Nyeusi yenye mistari meupe), pamoja na Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba kichwani).
Waziri Mahiga (katikati) akisalimiana na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mohammed Othmani Chande (wa kwanza kushoto), wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Silima Haji Kombo.
Waziri Mahiga (katikati) akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa Sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kulia ni Balozi Silima Haji Kombo 
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto)  akisalimiana na Balozi Silima


Picha na Reginad Philip

Tuesday, January 12, 2016

Waziri Mahiga awataka Watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa kuzingatia maadili

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akizungumza kwa mara ya kwanza na Watumishi wote wa Wizara kwa ajili ya kuwatakia heri ya mwaka mpya, kufahamiana nao na kuwapatia mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Mkutano huo umefanyika  hivi karibuni katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) naye akitoa salamu zake wakti wa mkutano huo wa kwanza na Watumishi wote wa Wizara.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakimsikiliza Naibu Waziri (hayupo pichani)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima akizungumza machache wakati wa mkutano na Watumishi wa Wizara 
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani)
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akitoa ratiba ya mkutano huo wa Waziri na Watumishi wote.
Baadhi ya Wakurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Masahriki, Kikanda na Kimataifa nao wakifuatilia matukio wakati wa mkutano kati ya Waziri na Watumishi wa Wizara.
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi wa Wizara nao wakifuatilia matukio
Bw. Abdallah Mtibora, Afisa Mambo ya Nje akiuliza swali kwa Mhe. Waziri wakati wa mkutano huo.
Bw. Octavian Kivyiro, Afisa kutoka Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji nae akiomba ufafanuzi wa baadhi ya mambo wakati wa mkutano huo
Mhe. Waziri Mahiga akijibu baadhi ya hoja zilizowasilishwa na Watumishi wa Wizara. Kushoto ni Mhe. Dkt. Kolimba, Naibu Waziri, Balozi Mlima (wa pili kulia), Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (kulia)
==================================================


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia nidhamu, uadilifu na kuweka mbele maslahi ya Watanzania wote ili kuliletea Taifa maendeleo.

Mhe. Dkt. Mahiga aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa mkutano wake wa kwanza na Watumishi wote wa Wizara hiyo wakiwemo wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mahiga ambaye kwenye mkutano huo aliongozana na Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Aziz Ponary Mlima na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi alisema kuwa lengo la kukutana na Watumishi wote ni kuwatakia heri ya mwaka mpya, kufahamiana, pamoja na kuwapa mwelekeo wa utendaji wa Wizara kufuatia kuunganishwa kwa Wizara mbili.

Dkt. Mahiga alieleza kuwa kuunganishwa kwa Wizara hizi mbili kuna lengo la kuboresha utendaji na kuimarisha ushirikiano hususan katika masuala ya Kikanda na hivyo kuwataka Watumishi wote kufanyakazi zao kwa ushirikiano wa hali ya juu huku wakizingatia nidhamu, uadilifu, kuheshimiana, kujali utu, kutunza mali ya umma na kuwa wabunifu.

“Watumishi wenzangu kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu ambayo imeasisiwa na Rais wetu ina tafsiri pana sana. Moja ya tafsiri hiyo ni kufanya kazi kwa malengo na weledi wa hali ya juu huku tukizingatia nidhamu, uadilifu na kuepukana na ubadhirifu na matumizi mabaya ya mali ya umma” alisema Waziri Mahiga.

Waziri Mahiga aliongeza kusema  kwamba, katika kutekeleza kaulimbiu hiyo Watumishi wa Umma wanatakiwa kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyowekwa ili kuepukana na vitendo viovu na kutanguliza maslahi ya taifa mbele katika kuwatumikia wananchi. Aidha, Mhe. Mahiga alisisitiza umuhimu wa kufanyakazi kwa uwazi na ubunifu huku akihimiza Watumishi kujiendeleza kimasomo ili kujiongezea ujuzi.

Vile vile Dkt. Mahiga alitumia fursa hiyo kuwaondoa hofu Watumishi wa iliyokuwa Wizara ya Afrika Mashariki kwamba kuunganishwa kwa Wizara hizi hakutaathiri maslahi wala ajira zao kwa namna yoyote ile na kuwataka kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano wakati taratibu za kimuundo, kisheria na kiutumishi zikiendelea kukamilishwa.

“Nawaomba Watumishi wote mfanyekazi zenu kwa ushirikiano na kwa wenzetu kutoka iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki msijisikie unyonge kwani ajira zenu zitabaki zilivyo na maslahi yenu hayataathirika kwa kuungana huku. Zaidi napenda kwasisitiza muwe na mawazo endelevu na utayari wa kupokea mabadiliko” alisisitiza Dkt. Mahiga.

Akichangia neno wakati wa Mkutano huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba alisisitiza Watumishi wa Wizara kufanyakazi kwa bidii huku wakiweka maslahi ya nchi mbele hususan wanapotekeleza jukumu la msingi la Wizara la kuiwakilisha nchi nje ya mipaka yake.

“Naomba niwapongeze Watumishi wote kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuiwakilisha nchi kimataifa. Lakini napenda kuwahimiza kuongeza nguvu zaidi katika kutekeleza majukumu yenu ili kuendelea kutetea maslahi ya nchi yetu vizuri na kuiletea maendeleo” alisema Dkt. Kolimba.

Awali akimkaribisha Mhe. Waziri kuzungumza, Katibu Mkuu, Balozi Aziz Ponary Mlima alisema kuwa Wizara imejiwekea utaratibu wa Watumishi wote kukutana na Waziri katika kila robo ya mwaka yaani mara nne kwa mwaka ili kuweka mikakati ya pamoja na kuwa na utendaji wenye tija.


-Mwisho-







Monday, January 11, 2016

Naibu Waziri awataka Vijana kuiwakilisha vizuri Tanzania wanapopata fursa za kwenda nje ya nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Vijana 12 wa Kitanzania  kutoka Mpango utakaohusisha safari ya meli (the Ship for  World Youth Program) kuzunguka nchi nne Barani Asia ambazo ni India, Sri Lanka, Singapore na Japan kwa lengo la kujadili masuala ya kijamii pamoja na mitazamo mbalimbali kuhusu mwingiliano wa tamaduni pamoja na kuangalia fursa miongoni mwa nchi mbalimbali. Mpango huo ulioandaliwa na Serikali ya Japan unatarajia kuanza tarehe 13 Januari hadi 02 Machi, 2016. 
Mhe. Dkt. Kolimba akizungumza na vijana hao (hawapo pichani) kuhusu ziara yao na kuwataka kuiwakilisha vizuri Tanzania na kuwa mfano miongoni mwa vijana kutoka nchi nyingine zitakazoshiriki mpango huo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima na kushoto ni Balozi wa Japan hapa nchini, Mhe. Masaharu Yoshida.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizarani hapo, Bi. Mindi Kasiga wakimsikiliza Naibu Waziri (hayupo pichani) alipozungumza na vijana 12 watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mpango wa safari ya meli kuzunguka nchi nne Barani Asia.
Sehemu ya Vijana hao
Baadhi ya vijana hao 12
Balozi Yoshida nae akizungumza na vijana hao (hawapo pichani)
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Masahriki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Eva Ng'itu na Bw. Emmanuel Luangisa wakimsikiliza Balozi Yoshida hayupo pichani
Mkutano ukiendelea

Sehemu nyingine ya viajana.

Balozi Mulamula akabidhi Ofisi kwa Katibu Mkuu mpya wa Mambo ya Nje

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima (kulia) akipokea nyenzo mbalimbali za kufanyia kazi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula wakati wa makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika Wizarani tarehe 11 Januari, 2016.
Katibu Mkuu, Balozi Mlima (mwenye tai)  akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Mulamula (kushoto). Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani  Muombwa Mwinyi  (kulia) na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya (wa pili kulia).