Wednesday, June 27, 2018

RAIS WA ZIMBABWE ZIARANI NCHINI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa kuhusu ziara ya Rais wa Zimbabwe nchini

Mheshimiwa Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe atafanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania tarehe 28 hadi 29 Juni, 2018. Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Mheshimiwa Rais Mnangagwa nchini Tanzania tangu aingie madarakani mwezi Novemba, 2017.

Lengo la ziara hii ya Rais wa Zimbabwe ni kujitambulisha kwa Rais na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu aingie madarakani, Mheshimiwa Rais Mnangagwa ameshafanya ziara katika nchi za Namibia, Zambia, Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Botswana.

Ziara hii ni muhimu kwa Tanzania kwani itatoa fursa ya kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano mazuri yaliyopo ya kidiplomasia, kihistoria, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili. Ziara hii pia itatoa fursa kwa viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili ya kikanda na kimataifa.

Wakati wa ziara hiyo,  Mhe. Rais Mnangagwa atafanya  mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 

Rais Mnangagwa anatarajiwa pia kutembelea Chuo cha Kilimo cha Wazazi Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Bara la Afrika na Mhe. Rais Mnangagwa ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho. 

Mhe. Rais Mnangagwa anatarajiwa kuondoka tarehe 29 Juni 2018 kurejea chini Zimbabwe.
-Mwisho-


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 27 Juni, 2018

Tuesday, June 26, 2018

Balozi Migiro azindua rasmi Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza-ATUK

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro akiitazama keki iliyoandaliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza (Association of Tanzanians in the UK-ATUK)
Mhe. Balozi Migiro akifurahia jambo na sehemu ya Watanzania walioshiriki uzinduzi huo

Sehemu ya Watanzania na wageni waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria 

===================================================



UZINDUZI WA  ASSOCIATION OF TANZANIANS IN THE UK – ATUK 

Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uzinduzi wa Jumuiya Mwamvuli ya Watanzania waishio nchini Uingereza na Ireland ya Kaskazini iitwayo ATUK –Association of Tanzanians in the UK zilizofanyika mjini Reading tarehe 23 Juni, 2018. Jumuiya hii inatokana na muungano wa jumuiya za diaspora kutoka mikoa mbalimbali ya hapa Uingereza na wanachama wa kujitegemea.

Wajumbe wa Kamati ya Muda iliyoratibu kuanzishwa kwa ATUK walipongeza na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kupambana na ufisadi, kusimamia uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na kuongeza kasi ya kujenga uchumi wa viwanda. Kauli mbiu ya hafla hii ilikuwa “UMOJA NI NGUVU, TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA”. Hivyo mojawapo ya malengo ya kuanzishwa kwa ATUK ni kujenga umoja na kukusanya nguvu za kuchangia jitihada za kujenga uchumi wa viwanda nchini mwetu.

Akihutubia hadhara hiyo Balozi Migiro aliwapongeza ATUK na alihimiza umoja na kukumbusha kwamba wakati wote Mhe. Rais amekuwa akisisitiza umoja wa Watanzania bila kujali tofauti zao kwani umoja ni nyenzo muhimu ya kujiteletea maendeleo. Hivyo Balozi Migiro aliwashukuru kwa Muungano huo na kueleza kwamba wakiendeleza mshikamano wataweza kuchangia  kwa ufanisi jitihada kubwa za Mhe. Rais  Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea maendeleo Watanzania wote.






Katibu Mkuu akutana na wadau mbalimbali kutoka Serikalini na Taasisi za Umoja wa Mataifa kujadili SDGs.


   

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda akisistiza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa na Taasisi zake kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo  Endelevu. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tarehe 26 Juni2018.
Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia(SDGs) yako 17 yenye shabaha 169 na  Viashiria 232, malengo hayo yanatekelezwa kwa pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kwa kushirikisha kila sekta na utekelezaji wake unahimiza ushiriki wa kila kundi kwenye jamii.
 Katibu Mkuu Prof. Mkenda( wa pili kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Faustine Kamuzora, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (mwisho kulia) na wa mwisho kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, wakifuatilia majadiliano ya Mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akielezea malengo ya Mkutano huo.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akitoa taarifa ya ufunguzi kwa upande wa Umoja wa Mataifa.
 Sehemu ya washiriki wakifuatilia mkutano huo.
 Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar na washiriki wengine kutoka Serikalini walioshiriki katika mkutano huo.
 Sehemu ya Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mkutano huo.
 Katibu Mkuu Prof. Mkenda akiwaelezea wanahabari kuhusu mpira uliondikwa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia, aliokabidhiwa na Bw. Rodriguez kuashiria  utekelezaji wa malengo hayo kwa kasi na kuzingatia Muktadha wa mazingira ya Tanzania.
Picha ya pamoja baada ya mkutano.

Waziri Mahiga akutana kwa pamoja na Balozi wa Uingereza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akisalimiana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania  Dkt. Inmi Patterson akiwa amefuatana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Sarah Cooke mara walipomtembelea na kufanya nae mazungumzo kwenye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje zilizopo Jijini Dar es Salaam 
Dkt. Mahiga akisalimiana na Mhe. Balozi Cooke.
Dkt. Mahiga akimsikiliza Mhe. Balozi Cooke alipokuwa akimweleza jambo wakati wa mazungumzo yao
Sehemu ya ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe Waziri Mahiga na Balozi Cooke (hawapo pichani). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga, Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu ( kulia) pamoja na Anthony Mtafya, Afisa Mambo ya Nje
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dkt. Patterson ( kulia) pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Ubalozi wa Marekani na Uingereza nchini wakisikiliza kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Cooke (hawapo pichani).
Mkutano ukiendelea.



Monday, June 25, 2018

Washindi wa TBL watembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi

Balozi wa Tanzania nchini Urusi Mhe. Simon Mumwi amekutana na Washindi wa shindano la Tanzania Breweries Ltd. kupitia bia rasmi ya Kombe la Dunia - Kilimanjaro Premium Lager siku chache mara baada ya kuwasili jijini Moscow Urusi, kwa ajili ya kushuhudia Mechi za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini humo.

 Pichani katikati ni Balozi Mumwi, 
watatu kutoka kulia ni Bw. Charles John, wa pili kutoka kulia ni Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi Dkt. Mkama, na wa kwanza kulia ni Joel Terry. 
Wa kwanza kushoto ni Bw. Leodigard Isack,  Bw. Kironde Mwijage (wa pili kushoto), Bi. Mary Mushi (wa tatu kutoka kushoto),  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili ubalozini hapo.
Balozi Mumwi akifanya mazungumzo na washindi hao.
Balozi Mumwi akipokea zawadi ya Majani ya Chai yanayotengenezwa nchini Tanzania kutoka kwa mmoja wa washindi wa shindano hilo Bw. Leodigard Isack kwa niaba ya Kundi la Washindi wa Shindano la TBL kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ambapo washindi hao walidhaminiwa safari ya Urusi kushuhudia mojawapo ya Mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini humo.

Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa kufanyika jijini Arusha

Mhandisi Abdillah Mataka Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Kijamii kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akichangia jambo kwenye mkutano wa  15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa unaoendelea jijini Arusha. Mkutano huu unafanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.



Mkutano huu unaofanyika kila mwaka, mwaka huu pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa za utelelezaji wa mapendekezo, maagizo na maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na kuamuliwa katika mikutano ya ngazi mbalimbali na vyombo vya kisera vya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sekta zinazotarajiwa kujadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na sekta ya miundombinu ya uchukuzi inayojumuisha aridhi, anga na maji, mawasiliano na hali ya hewa. 

Utelezaji wa maagizo, mapendekezo na maamuzi mbalimbali yaliyotolewa ili kuboresha maeneo haya unatarajiwa kuleta mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii katika nchi wanachama za Jumuiya Afrika Mashariki.

Mkutano huu unaoendelea jijini Arusha na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika katika ngazi tatu ambazo ni; ngazi ya Wataalam, ngazi ya Makatibu Wakuu na hatimaye ngazi ya Mawaziri.
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipokuwa ukiimbwa na wajumbe kabla ya kuanza kwa mkutano.
Sehemu ya wajumbe kutoka Tanzania wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kuanza kwa mkutano. Kushoto ni Mhandisi Abdillah Mataka Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Kijamii, Mhandisi Julius Chambo (katika) Mkurugenzi Sekta ya Ujenzi kutoka  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Bw. Moses Malipula kutoka Wizara ya Fedha na Mipango

Meza kuu ikiongoza majadiliano wakati wa mkutano

Sehemu ya wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa.

Bibi Edna Chuku (wa kwanza kulia) Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea.

Friday, June 22, 2018

MINISTER MAHIGA’S DAY VISIT TO ROMANIA; SIGNS AN MOU FOR BILATERAL CONSULTATIONS

   






PRESS RELEASE
Tanzania’s foreign minister Hon. Dr. Augustine Mahiga, and his Romanian counterpart Hon. Teodor Melescanu have signed a Memorandum of Understanding, redefining bilateral relations that exist between Tanzania and Romania. 
The two leaders held extensive talks prior to the signing ceremony which was held at Ministry of Foreign Affairs in Bucharest in front of members of the press. The timely signing came at a time when the two parties are working to establish strong economic ties, with different nations around the world.  
The signed MoU between the two countries’ Foreign Ministries provides a platform to hold regular strategic consultations on political, economic, commercial, scientific, technical and cultural aspects of bilateral relations, regional and international matters.
The platform is envisaged to further develop and strengthen friendly relations while increase mutual understanding and cooperation between Tanzania and Romania.
“During the liberation struggle of Africa, many Tanzanian students came to Romania to study medicine and pharmaceutical. With the signing of this MoU, now Romania and Tanzania are strategic partners. We anticipate diversification in the area of training and capacity building to include new sectors such as agronomy for Tanzanian students” Hon. Mahiga remarked. 
Hon. Melescanu explained that ever since the new Government of Romania came into leadership one year ago, the focus has been to re establish relations and partnerships with countries outside Europe. 
“But Tanzania and Romania have been friends for the longest time, and we witnessed many of your colleagues receiving education in Romania. The number kept decreasing year after year due to the closing of our embassy in the 90’s. I believe now things will be better, for our people” announced Foreign Minister Melescanu. 
Diplomatic relations between the two countries were established on 5th May 1964. The relations were very active until 18th November, 1999, when the government of Romania closed its embassy in Dar es Salaam, due to financial difficulties. The relations were mainly based on education particularly scholarship to Tanzania students. 
The platform for political discussions will provide an opportunity to discuss both priority issues, including migration issues, business opportunities, investments, various development projects, capacity building and tourism promotion.
Hon. Mahiga and his delegation, made a one-day visit to Bucharest on their way back to Tanzania after concluding another working visit in the region. Permanent Secretary of Romania Foreign Ministry is also expected to visit Tanzania as a follow up of this signed MoU within the coming month. 

ENDS

Issued by:
Government Communication Unit, 
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation, 
Bucharest, Romania June 21 2018

African envoys plug business on the continent

Ambassadors and diplomats from Sierra Leone, Tunisia, Kenya, Tanzania, Ethiopia, Nigeria, Sudan, Ghana, Angola, Rwanda, Egypt, Gabon, Senegal, Morocco, the Ivory Coast and Zambia; and Korean lawmakers and investors attend the Africa Business Seminar at the FKI Tower in western Seoul on Wednesday. 

Africa is changing and Korea should get on board, ambassadors of African nations said at a forum in Seoul on Wednesday to celebrate Africa Day.

“Currently, six of the world’s 10 fastest growing economies are in Africa,” said Albino Malungo, ambassador of Angola and dean of the African Group of Ambassadors. “The African train has already left the station. The message to our Korean business partners is that Africa is the new global growth pole and the next market.”

The Korea-Africa Foundation, African Diplomatic Corps in Korea and Federation of Korean Industries hosted the Africa Business Seminar at the FKI Tower in western Seoul, on Wednesday. Organizers highlighted the African Continental Free Trade Area, which includes 44 countries and intends to pool together African goods and services into a single market with free movement of people and investment.

The free trade area “is aware that there are other economic communities in the regions where it will [have] impact,” said Rwandan Ambassador Emma-Francoise Isumbingabo, who chaired the preparation committee for this year’s Africa Day celebration in Korea. “[The free trade area] will work closely with existing communities, aligning itself with their goals and objectives, and ensuring that cooperation with foreign and outside investment in the African market is made easy and approachable.”

Investors noted budding Korean interest in the African market.

“Korea’s Ministry of Foreign Affairs has what’s called the Country Partnership Strategy for each recipient country of its funds,” said Jun Woo-hyung, director of trade information at the Korea Trade-Investment Promotion Agency, “which in Africa are Ethiopia, Ghana, Mozambique, Uganda, Rwanda, Senegal and Tanzania. There is budding interest in the African market here. Recall that the African Development Bank held its annual meeting in Busan this past May.”

Some ambassadors said Korean companies can do more in Africa.

“We all think there is a huge potential that is underutilized,” said Egyptian Ambassador Hazem Fahmy. “Korea is leading in high technology and the fourth industrial revolution, and I think it could make huge profits by investing in Africa in these areas.”

Africa Day is celebrated on May 25 annually and commemorates the foundation of the Organization of African Unity in 1963. In addition to the business forum, embassies of African nations hosted a food and culture fair in central Seoul’s Cheonggye Plaza.

There was injera (sourdough flatbread) made with teff flour; baked goods from the Algerian embassy, including semolina-stuffed makrout and date-filled kaak cookies; figurines from Ghana in traditional dress; handwoven baskets from Sudan and Rwanda; and stone animals from Tanzania.

“Before I knew it, Korea has become my home,” said Audrey Aduol, a 28-year-old Kenyan studying at Seoul National University, who was helping out at the Kenyan booth. “The other time I went home, I felt like a guest in my own country. It’s bittersweet how that happens.”

BY ESTHER CHUNG [chung.juhee@joongang.co.kr]

Naibu Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani M.Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Jasem Ibrahim Al-Najem, alipomtembelea Wizarani tarehe 22 Juni,2018, Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu jinsi ya kuboresha mahusiano yaliyopo katika kati ya Tanzania na Kuwait, nchi ya Kuwait imekuwa ni kati ya wadau muhimu wa Maendeleo hapa nchini kupitia mradi wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait(Kuwait Fund).

            Mhe. Al-Najem akifafanua jambo katika mazungumzo hayo.

 Balozi Mwinyi akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo.
 Mazungumzo yakiendelea, wanaofuatilia kulia kwa Balozi Mwinyi ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Suleiman Salehe, Bw. Hangi Mgaka na Bw. Fidelis Odilo Maafisa wa Mambo ya Nje, wakifuatilia mazungumzo hayo.
Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo.


Thursday, June 21, 2018

WAZIRI MAHIGA AHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI NORWAY


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MAHIGA AHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI NORWAY ASISITIZA UWEKEZAJI WENYE TIJA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Norway kwa mazungumzo na wafanyabiashara huku akiwapa ujumbe mkuu wa kuwekeza Tanzania ambapo tayari kuna mazingira mazuri ya uwekezaji.

Kwenye hotuba yake kwa wanachama wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Norway na Afrika (NABA), Mhe. Mahiga ameelezea ushirikiano uliopo kati ya Serikali za Norway na Afrika kwa ujumla hususan Tanzania, ambapo Norway inasaidiana na nchi nyingi za kiafrika  ikiwemo Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Hii ni ishara nzuri kwa ukuaji wa biashara na mahusiano.

Akitolea mfano wa Tanzania, Mhe. Mahiga alisema kuwa miaka ya hivi karibuni Serikali ya Norway imebadilisha ushirikiano wake na Tanzania kutoka kwenye kutoa misaada kwenda kwenye udhamini wa pamoja wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kuinua uchumi.

“Ushiriki wa Serikali ya Norway nchini kwetu ni wa kipekee, kwani unazingatia vipaumbele na sera za Tanzania na pale wanaongeza nguvu kwa kudhamini mafunzo na hatimaye ujenzi wa mifumo sahihi ya utekelezaji wa sera hizo” Waziri Mahiga alisema.

Waziri Mahiga aliongeza kuwa, kwenye awamu ya tano ya uongozi nchini Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mambo mengine, amejenga mifumo bora ya ukusanyaji kodi, usimamizi wa rasilimali za umma pamoja na uendelezwaji wa rasilimali ya mafuta kwa maendeleo. “Serikali ya Norway inadhamini maeneo yote hayo na mengine mengi, kama mdau wa maendeleo ya Watanzania. Hivyo ni vyema na nyie wafanyabiashara muwekeze pale ambapo Serikali yenu ipo. Kwa sababu hapo ndio mahali salama kwa uwekezaji wenye tija” alihimiza Mhe. Mahiga.

Mkutano huo uliojumuisha taasisi takriban 25, ulifanyika chini ya mwamvuli wa Norfund, Taasisi inayojenga uwezo kwa wafanyabiashara kuendesha biashara kwenye nchi zinazoendelea.

Akielezea mikakati ya taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wake, Bw. Kjell Roland alisema Norfund inajikita zaidi kwenye nchi ambazo upatikanaji wa mitaji ni mgumu kutokana na uchanga wa sekta binafsi.

Kwa upande wake, Mratibu wa umoja huo wa Wafanyabiashara wa NABA, amesema kuwa wapo kwenye maandalizi ya ziara ya biashara Tanzania kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Waziri Mahiga alitumia fursa ya mkutano huo kumtambulisha Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake nchini Sweden, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa ambaye anatarajiwa kukabidhi hati zake  za utambulisho tarehe 21 Juni, 2018.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 21 Juni, 2018