Friday, February 8, 2019

Naibu Mawaziri watembelea Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Mtukula.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Julius Wandera Maganda katika Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani cha Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda Tarehe 7 Februari 2019. Mara baada ya kukutana walipata fursa ya kutembelea na kujionea namna kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani cha Mtukula (OSBP) kinavyofanya kazi na kufanya Mkutano wa pamoja uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Tanzania na Uganda. Mkutano huo umefanyia Mpakani mwa Tanzania na Uganda eneo la Mtukula.

Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Waganda kabla ya kufanya mkutano wa pamoja na wadau mbalimbali. Wengine katika picha ni wajumbe walioongozana na Naibu Mawaziri hao.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.Ndumbaro (Mb.) akizungumza kwenye Mkutano na wadau mbalimbali pamoja na jumuiya ya wafanya biashara walio hudhuria mkutano huo.

Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Maganda naye akizungumza na wadau pamoja na jumuiya ya wafanya biashara walio hudhuria mkutano huo

Wadau kutoka upande wa Tanzania wakisikiliza kwa makini  wakati Naibu Mawaziri, Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Maganda walipokuwa wakizungumza kwenye mkutano uliyofanyika mpakani wa Tanzania na Uganda-Mtukula
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwa na Mhe. Maganda wakisikiliza kwa makini michango mbalimbali ya wadau iliyokuwa ikiwasilishwa kwenye mkutano.
Mwakilishi wa jumuiya ya wafanya biashara akichangia mada kwenye mkutano
Mmbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Uganda naye akichangia mada wakati wa mkutano huo ukiendelea.

Ujumbe wa Uganda nao wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.
Viongozi wa pande zote mbili walipata fursa ya kuzungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo na kuwaelezea yaliyojiri kwenye mkutano.
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano.
Viongozi hao wakifanya ziara kwenye maeneo mbalimbali ya kituo hicho cha pamoja na kujione namana watendaji wanavyo fanya kazi kwa umakini kwa kutumia vifaa vya kisasa katika kupambana na mambo mbalimbali ikiwemo namna ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko.
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakimsikiliza Afisa wa ukusanyaji mapato kutoka Tanzania Bw. Mohamed Shamte alipokuwa akielezea namna kituo hicho cha pamoja kinavyo fanya kazi. Naibu Mawaziri hao walijione namna watendaji wanavyofanya kazi kwa umakini kwa kutumia vifaa vya kisasa katika kupambana na mambo mbalimbali, ikiwemo udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola..
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Julius wakiendelea na kukagua  Kituo ili kujionea namna watendaji wake wanavyotoa huduma kwa wananchi wa pande zote mbili.
Katika picha ni jengo la Kituo cha kutolea hudmua kwa pamoja Mtukula mpakani mwa Tanzania na Uganda.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe. Dkt. Ndumbaro alisema lengo la ziara yao katika kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja Mtukula ni pamoja na kujionea mafanikio na kubaini changamoto zinazokabili utendaji wa kazi na kuzipatia ufumbuzi. 

Akiainisha mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kituo hicho , Dkt. Ndumbaro alieleza namna mizigo mbalimbali ikipita kwa wakati kwa kuzingatia taratibu zote zilizopo pamoja na wafanyabiashara kati ya nchi hizi mbili wakifanya biashara zao bila vikwazo vyovyote vile.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kuwajulisha wadau mbalimali waliohudhuria mkutano huo, kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeanzisha safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kutoka Dar es Salaam, Arusha mpaka Enttebe, Uganda. Mafanikio hayo yametokana na mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyopo baina ya Tanzania na Uganda na pia kupitia Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Kwa upande wake Mhe Maganda, alifurahishwa na hali ya kituo hicho namna huduma zinavyotolewa. Aidha, aliahidi kuwa Serikali ya Uganda itaongeza watendaji kazi kwenye kituo hicho ili kuwezesha upande wa Uganda kufanya kazi masaa 24 kama ilivyo kwa upande Tanzania. Pia alisisitiza nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya Ushirikiano.
    
Pia katika Mkutano huo wadau walitoa pongezi kwa viongozi wa Serikali za pande zote mbili kwa kuanzisha kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Mtukula, ambapo walisema kuanzishwa kituo hicho kumeongeza chachu ya maendeleo kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambapo wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao kwa wingi bila kupata changamoto kulinganisha na hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa kituo hicho.

 Kadhalika wadau walitoa pongezi kwa watendeji waliopo kituoni hapo kwa upande wa Tanzania, kwa kutoa huduma nzuri kwa masaa 24 kwenye kituo hicho ambapo, imepelekea wafanyabiashara kutokupoteza muda mwingi wafikapo mpakani hapo. 


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
9 Februari 2019















Thursday, February 7, 2019

Wabunge wa EALA walivyotoa Elimu ya Mtangamano wa EAC

Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga akitoa mada kwa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kuhusu shghuli za taasisi hiyo. Alisema taasisi yake inashirikiana na Serikali kuboresha miundombinu mbalimbali kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa biashara katika nchi za EAC inafanyika bila vikwazo.

Waheshimiwa Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakijadili kwa pamoja na Mkurugenzi wa TMEA kuhusu mchango wa taasisi hiyo katika kuboresha mwenendo wa biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine za EAC.

Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakijadili mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkazi wa TMEA.

Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam

Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la EALA, Mhe. Dkt. Abdallah Makame (kulia) akijadili jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar Es Salaam mara baada ya kuwasili katika chuo hicho kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu EAC. 

Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la EALA, Mhe. Dkt. Abdallah Makame (kulia) akipata chakula cha mchana na wanafunzi wa UDSM katika Cafteria Namba moja ya Chuo hicho. Mwenye nguo za bluu ni Mbunge mwenzake wa EALA, Mhe. Pamela Maasay.

Wanafunzi wa UDSM wakipata chakula cha mchana ambapo Wabunge wa EALA walijumuika nao katika chakula hicho.

Mbunge wa EALA, Mwalimu Josephine Sabastian (kushoto) akibadilishana mawazo na wanafunzi wa UDSM wakati wakipata kwa pamoja chakula cha mchana Cafteria.
Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakiwa katika meza kuu kwenye Ukumbi wa Nkurumah kwa ajili ya kuongea na wanafunzi kuhusu fursa za EAC.
Mbunge wa EALA, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe akiwasilisha mada kuhusu EAC kwa wanafunzi wa UDSM.

Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakiongea na wanafunzi wa UDSM kuhusu fursa za Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wanafunzi walioshiriki kwenye mazungumzo na Wabunge wa EALA. Mwenye suti ya bluu ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Washiriki wengine katika mazungumzo hayo.


Wanafunzi wakiuliza maswali na kutoa maoni namna Watanzania watakavyofaidika na Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki



Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakikabidhi bendera ya EAC kwa viongozi wa UDSM ili iwe inapeperushwa chuoni hapo. Walitoa wito kwa taasisi nyingine, hususan za Serikali kupeperusha bendera hiyo.
Mkutano na Asasi za Kiraia
Mbunge wa EALA, Mwalimu Josephine Sabastian akitoa elimu kuhusu EAC kwa wawakilishi wa Asasi za Kiraia zilizopo hapa nchini.



Majadiliano baina ya Wabunge wa EALA na wawakilishi wa Asasi za Kiraia kuhusu ushiriki wa asasi hizo katika masuala ya EAC.

Wabunge wa EALA na wawakilishi wa Asasi za Kiraia wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wabunge walisisitiza umuhimu wa wimbo huo kupigwa katika shughuli rasmi za Serikali.
Mdau akifanya tafrisi ya lugha ya ishara kwa watu wenye ulemavu wa kusikia.

Wednesday, February 6, 2019

Vacancy announcement




PRESS RELEASE

Job Announcement at the Commonwealth Secretariat

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Business Analyst available at the Commonwealth Secretariat.

In line with the Comonwealth’s commitment to gender equality, the Commonwealth Secretariat encourages applications from appropriately qualified women for this post.

Application details can be found on the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobs. Closing date for application is Sunday 17th February, 2019.

Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
6th February, 2019.

Tuesday, February 5, 2019

Jengo la Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje lasonga kwa kasi Dodoma


Mafundi wakiwa katika harakati kuhakikisha kuwa jengo linamalizika kwa wakati.

Linapendeza kweli kweli.

Palasta inaendelea kupigwa.

Kumenoga, tazama mwenyewe.

Kazi nje na ndani. Usiku na mchana. Mtumba Oyeeeee.

Monday, February 4, 2019

Wabunge wa EALA watoa elimu ya Mtangamano wa EAC

Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Abdallah Makame na Katibu wake, Mhe. Josephene Sabastian wakiwa katika kikao na Wabunge wenzao wa Tanzania, maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bunge la EALA na Trade Mark East Africa katika Hoteli ya Serena. Mkutano huo ni maandalizi ya zoezi la siku nne la kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu fursa za Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuanzia tarehe 04 hadi 07 Februari 2019 jijini Dar Es Salaam. 

Mhe. Habib Mnyaa, Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mhe. Maryam Ussi wakishiriki kikao cha maandalizi ya zoezi la kutoa elimu kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe. Pamela Maasay (kulia) na Mhe. Happiness Legiko wakijiandaa kukutana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya Mtangamano.

Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao Wizara yao ndio mratibu w masuala ya Mtangamano wakiwa katika kikao cha maandalizi cha kutoa elimu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Maafisa kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika kikao cha maandalizi ya zoezi la kutoa elimu kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe. Dkt. Abdallah Makame akitoa maelekezo kwa Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa dawati la Bunge.

Kikao kinaendelea

Mkutano wa Waandishi wa Habari

Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuwaeleza zoezi walilopanga la kuelimisha wadau kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Waandishi wamefurika kusikiliza Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu zoezi la kuelimisha wadau kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Waheshimiwa wabunge (kushoto) na waandishi wa habari wkiendelea na mkutano wao.

Bandari ya Dar Es Salam 
Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar Es Salaam akiwakaribisha Wabunge wa EALA katika Bandari ya Dar Es Salaam. Waheshimiwa Wabunge walienda Bandari ya Dar Es Salaam kuona maboresho yanayofanywa na bandari hiyo pamoja na kusikiliza wadau wanotumia bandari hiyo changamoto wanazokutana nazo.

Waheshimiwa Wabunge walienda kutembelea gati namba moja ambalo ni moja ya mageti ynayofnyiwa maboresho makubwa.

Siku ya Kuzaliwa
Mheshimiwa Maryam akisherehekea Siku yake ya kuzaliwa tarehe 04 Februari kwa kuwalisha keki Wabunge wenzake.

Happy Birthday kwa Mhe. Maryam Ussi kutoka kwa Mhe. Fancy Nkuhi.

Friday, February 1, 2019

Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa EAC wamalizika Arusha

Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiwa wamesimama kutoa heshima wakati wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiimbwa kabla ya kuanza rasmi Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutsno cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 1 Februari 2019. Katika picha ni Mhe. Yoweri Kaguta Museveni (wa nne kulia), Rais wa Uganda, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (wa tatu kulia), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Paul Kagame (wa nne kushoto), Rais wa Rwanda, Mhe. Uhuru Kenyatta (wa tatu kushoto), Rais wa Kenya, Mhe. Gaston Sindimo (wa pili kulia), Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi ambaye alimwakilisha Rais wa nchi hiyo Mhe. Pierre Nkurunziza, Mhe. Paul Mayom Akechi (wa pili kushoto), Waziri wa Biashara, Viwanda na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Sudan Kusini ambaye alimwakilisha Rais wa nchi hiyo Mhe. Salva Kiir. Wengine katika picha ni Mhe. Kirunda Kivejinja (kulia), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Uganda ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo na Dkt. Liberat Mfumukeko (kushoto), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda alikabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye amemaliza muda wake. Pia Wakuu hao walishuhudia kuapishwa kwa Jaji mpya wa Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Jaji Sauda Mjasiri kutoka Tanzania.
Marais wanne walioshiriki Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama wanavyonekana kwenye picha. Kutoka kulia ni Mhe. Dkt. Magufuli, Mhe. Rais Museveni, Mhe. Rais Kagame na Mhe. Rais Uhuru
Mkutano ukiendelea