Friday, August 7, 2020

TANZANIA YASAINI MKATABA WA MAPITIO WA GEORGETOWN WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA, CARIBBEAN NA PACIFIC

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TANZANIA  YASAINI MKATABA WA MAPITIO WA GEORGETOWN WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA, CARIBBEAN NA PACIFIC

 

Dodoma, 06 Agosti 2020

Tanzania imesaini Mkataba wa mapitio wa Georgetown unaosimamia mahusiano na uendeshaji wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific ambayo zamani ilikuwa ikiitwa  ACP na sasa Organisation of African, Carribean and Pacific States (OACPS) iliyo na nchi wanachama 79.


Mkataba huo ulisainiwa na balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,  Mhe. Jestas Abuok Nyamanga kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Brussels, Ubelgiji tarehe 31 Julai 2020. Hivyo Tanzania inakuwa nchi ya 42 kati ya nchi 79 kusaini Mkataba wa mapitio wa Georgetown.

Mkataba wa Georgetown umefanyiwa mapitio ili uweze kuendana na wakati kwa kuzingatia mabadiliko makubwa yanayoendelea kutokea duniani katika nyanja za  kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimazingira tangu kuanzishwa kwa ACP mwaka 1975. Mchakato wa kufanya mapitio ya mkataba huu ulianza mwezi Machi 2013 kupitia timu maalum iliyoanzishwa kukusanya maoni na kuleta mapendekezo chini ya Uenyekiti wa Rais Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Olusegun Obasanjo.

Aidha, Mwaka 2019 mchakato wa mapitio hayo ulihitimishwa kwa  kuridhiwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za OACPS katika mkutano wao uliofanyika mwezi Desemba 2019 jijini Nairobi, Kenya.

Mkataba wa Georgetown ndiyo ulianzisha ACP mwaka 1975 katika mji wa Georgetown nchini Guyana.  Tanzania ilisaini Mkataba huo wa awali tarehe 11 Desemba 1975 na imedumu ikiwa mwanachama wa ACP tangu wakati huo.

Pamoja na kuwa mwanachama Tanzania imekuwa ikinufaika katika masuala ya kiuchumi, kijamii, biashara, na uwekezaji kupitia ushirikiano maalum baina ya nchi za ACP na Umoja wa Ulaya unaosimamiwa na mikataba ya Lome na Cotonou. Vilevile miradi ya ubia wa maendeleo na ile ya mtangamano wa nchi za ACP chini ya ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya. Pia ushirikiano katika masuala ya kubadilishana ujuzi na uzoefu na nchi za ACP, mshikamano wa kisiasa na kidiplomasia katika kutetea maslahi ya Tanzania kimataifa kupitia jukwaa la ACP.

 

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

==============================================

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga akisaini Mkataba wa Mapitio wa Georgetown mjini Brussels, Ubelgiji tarehe 31 Julai, 2020


Mhe. Nyamanga, Maafisa wa Ubalozi na Mwanasheria wa Jumuiya ya OACPS, Dkt. Emmanuel Opoku wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha zoezi la kusaini Mkataba.


Thursday, August 6, 2020

TANZANIA YACHAGULIWA KUWA RAIS WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA, CARRIBEAN NA PACIFIC

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 


TANZANIA YACHAGULIWA KUWA RAIS WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA, CARRIBEAN NA PACIFIC

 

Dodoma, 6 Agosti 2020

Serikali ya Tanzania imechaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Carribean na Pacific (Organisation of African, Carribean and Pacific States-OACPS)  kwa kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe 1 Agosti 2020 hadi tarehe 31 Januari 2021.

 

Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alikabidhiwa rasmi nafasi hiyo iliyopokelewa kwa niaba yake na Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro,  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 28 Julai 2020.

 

Tanzania inakuwa Rais wa Baraza hilo kutokana na Balozi  wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga kuchaguliwa kwa kauli moja kuwa Mwenyekiti wa Mabalozi wa Nchi za OACPS waliopo Brussels. Kwa mujibu wa Jumuiya ya OACPS,  nchi inayotoa Mwenyekiti wa Mabalozi wa Jumuiya hiyo, Waziri wake anayesimamia masuala ya OACPS ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje moja kwa moja anakuwa Rais wa Baraza la Mawaziri. Uamuzi wa kuichagua Tanzania ulifanywa na Mabalozi kutoka nchi 15 za Ukanda wa Mashariki mwa Afrika kwenye kikao kilichofanyika tarehe 2 Julai 2020 na kuthibitishwa kwa kauli moja na mabalozi wote wa nchi 79 wa OACPS kupitia kikao chao kilichofanyika Brussels tarehe 14 Julai 2020.

 

Tanzania ambayo inachukua nafasi hiyo kutoka kwa Gambia, imejipanga kutekeleza masuala mbalimbali yenye maslahi kwa Nchi za OACPS ikiwa ni pamoja na kusimamia ukamilishwaji wa majadiliano kuhusu Mkataba mpya wa ushirikiano wa Nchi za OACPS na Umoja wa Ulaya (EU) unaotarajiwa kuanza kutumika mwezi Januari 2021 baada ya mkataba wa sasa wa Cotonou (Cotonou Partnership Agreement) kufikia ukomo mwezi Desemba 2020, pamoja na kuhakikisha  maslahi ya nchi za OACPS yanaingizwa kwenye mkataba huo mpya. Aidha, Tanzania imejipanga kusimamia utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya Jumuiya ya OACPS katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa COVID-19 na madhara yake kiuchumi kwa nchi wanachama.

 

Kadhalika, maeneo mengine ya kipaumbele yatakayosimamiwa na Tanzania katika kipindi cha Urais wa Baraza hilo ni kusimamia  mikakati ya kuongeza mtangamano na ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya; kusimamia mabadiliko ya kiutendaji na mifumo ili kuendana na wakati pamoja na kudumisha mshikamano na umoja miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya.

 

Vilevile miongoni mwa manufaa ya Tanzania kuwa Rais wa Baraza hilo  ni pamoja na kuongeza ushawishi wa nchi yetu katika kupanga na kutekeleza mikakati, miradi na programu mbalimbali za Jumuiya ya OACPS ambazo ni pamoja na zile zinazotekelezwa kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya na wabia wengine wa maendeleo kama vile kilimo, uwekezaji, biashara na ujasiriamali, mazingira, miundombinu, vijana na utamaduni.

 

Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kuwa Rais wa Baraza la Mawaziri na Mwenyekiti wa Mabalozi  wa nchi za OACPS tangu ilipojiunga mwaka 1975. Miongoni mwa sababu zilizopelekea Tanzania kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo ni kutokana na kuongozeka kwa ushawishi wake kwenye Jumuiya ya OACPS, Sera na hatua thabiti zinazochukuliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimamia masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa pamoja na utendaji madhubuti wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kusimamia Sera ya Mambo ya Nje  ikiwemo ushiriki mahiri wa Tanzania katika masuala yanayogusa maslahi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya OACPS.

 

 

 

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.

Wednesday, August 5, 2020

TROIKA YAJADILI NAMNA YA KUIMARISHA HALI YA USALAMA NCHINI DRC

Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama (OrganTroika) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imekutana na kujadili namna ya kurejesha hali ya amani, ulinzi na usalama nchini DRC ili nchi hiyo iweze kupiga hatua katika maendeleo.

 Akiongea katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao (Video Conferencing) na kujadili masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama nchini Kongo DRC, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amesema kuwa mkutano huo ulizihusisha nchi za utatu wa siasa ulinzi na usalama pamoja na nchi tatu ambazo zinazotoa askari wa kikosi maalumu kinachoshughulikia masuala ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (Force Intervention Brigade). 

 “Tangu mwaka jana SADC na Umoja wa Mataifa tumekuwa katika mazungumzo ya jinsi ya kuimarisha kikosi hicho pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama nchini DRC hasa upande wa Mashariki mbapo umekuwa ukipambana na vikundi vyenye misimamo mikali na kuifanya DRC kukosa utulivu na amani,” Amesema Prof. Kabudi 

Waziri ameongeza kuwa Tanzania kwa muda mrefu ikiwa ni sehemu ya SADC imepeleka askari wake upande wa mashariki mwa DRC, ambapo pamoja na mambo mengine mkutano wa leo ulikuwa ni nwebdelezo wa mazungumzo kati ya Tanzania na nchi nyingine za SADC ili kuwa na msimamo wa pamoja katika mazungumzo yake yanayoendelea na Umoja wa Mataifa (UN) kwa lengo moja la kusisitiza suala la kurejesha hali ya amani nchini Kongo hasa Mashariki mwa Kongo.

 “Tunashukuru kusema kwamba DRC ambayo ni sehemu ya SADC msimamo wake umekuwa ni ule ule unaofanana na wa nchi za SADC, pili Nchi za SADC na umoja wa Mataifa tumeazimia jambo linalofanana kuhakikisha kwamba Kongo inamaliza migogoro yake, Kongo inarejea kuwa na Amani na utulivu na Kongo inakuwa na mshikamano ili wananchi wa Kongo waweze kupiga hatua kubwa katika maendeleo,” Amesema Waziri Kabudi.

Kongo imekuwa ni muhanga wa machafuko na vita kwa muda mrefu ni imani ya Tanzania na nchi za SADC kwamba wakati umefika sasa kwa Kongo na hasa kwa Mashariki ya Kongo kupewa nafasi yake ya utulivu na mshikamano ili iweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo. 

Mkutano umehudhuriwa na Jamhuri ya Afrika Kusini, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Malawi, Zimbabwe, Botswana, Zambia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati) akiwa na Waziri wa Ulinzi Mhe.Dkt. Husseni Mwinyi (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Brigadia Generali, Balozi Wilbert Ibuge (kulia kwa Prof. Kabudi).  Wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi Dkt. Faraji Mnyepe (wa kwanza kushoto) pamoja na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Mkutano wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama (Organ Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao (Video Conference). 

Mkutano ukiendelea 


                                   Mkutano ukiendelea 

BALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI NA MWAKILISHI KATIKA UMOJA WA ULAYA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO


Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Mwakilishi katika Umoja wa Ulaya, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Mhe. Ursula von der Leyen katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Umoja huo jijini Brussels, Ubelgiji tarehe 30 Julai 2020.

Wakizungumza baada ya kukamilika kwa makabidhiano hayo viongozi hao waliazimia kudumisha na kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano mzuri uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 baina ya Serikali ya Tanzania na Umoja wa Ulaya.

Kadhalika, Mhe. Nyamanga alieleza Tanzania na Umoja wa Ulaya zimekuwa na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote mbili hususan katika eneo la ubia wa maendeleo kwenye sekta za kilimo, miundombinu, elimu, nishati, afya na mazingira. Hivyo, ushirikiano huo pia umehamasisha uwekezaji, biashara na kutembeleana baina ya watu wa pande zote na kuzidi kuongeza fursa kwa wananchi wake.

Tanzania na Umoja wa Ulaya pia zinashirikiana katika mikakati mbalimbali ya kutafuta na kudumisha amani, usalama na utulivu katika ukanda wa nchi za Maziwa Makuu, barani Afrika na duniani kwa ujumla.


Balozi Nyamanga akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Ursula von der Leyen kabla ya kuwasilisha rasmi Hati za Utambulisho.


Picha ya pamoja baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwasilisha Hati za Utambulisho.


MKUTANO MAALUM WA 41 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Kutoka Kushoto; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) wakiwa katika Mkutano Maalum wa 41 uliokuwa ukiendelea kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing). 



Wajumbe wa Mkutano wakifuatilia wa Mkutano Maalum wa 41 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing). 


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akifuatilia Mkutano wa Maalum wa 41 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masahariki uliokuwa ukiendelea

Kutoka Kushoto; Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Mhe. Balozi Stephen Mbundi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) wakiwa katika Mkutano Maalum wa 41 uliokuwa ukiendelea kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing). 

Mkutano ukiendelea



Sunday, August 2, 2020

BALOZI MTEULE WA MAREKANI NA BALOZI MTEULE WA VIET NAM WAKABADHI NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akipokea nakala ya hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Viet Nam Nchini Tanzania Mhe.Nguyen Nam Tien,na baadae kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Viet Nam Nchini Tanzania Mhe.Nguyen Nam Tien,muda mfupi kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Balozi Mteule wa Viet Nam Nchini Tanzania Mhe.Nguyen Nam Tien akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mara baada ya kumkabidhi nakala ya hati za utambulisho

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Mteule wa Viet Nam Nchini Tanzania Mhe.Nguyen Nam Tien wakiwa katika mazungumzo pamoja na baadhi ya maafisa na Wakurugenzi kutoka pande zote mbili 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akipokea nakala ya hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Marekani Dkt. Donald John Wright na baadae kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Balozi Mteule wa Marekani Nchini Tanzania Dkt. Donald John Wright akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mara baada ya kumkabidhi nakala ya hati za utambulisho


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Viet Nam Nchini Tanzania Mhe.Nguyen Nam Tien,muda mfupi kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Mteule wa Marekani Nchini Tanzania Dkt. Donald John Wright wakiwa katika mazungumzo pamoja na baadhi ya maafisa na Wakurugenzi kutoka pande zote mbili 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisalimiana na Balozi Mteule wa Viet Nam hapa Nchini Mhe. Nguyen Nam Tien muda mfupi kabla ya kukabidhi nakala ya hati za utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
 

Saturday, August 1, 2020

PROF. KABUDI AZINDUA MAONESHO YA NANE NANE MKOANI MOROGORO




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Mhe Jokate Mwongelo alipowasili katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Mkoani Morogoro katika ufunguzi wa siku ya wakulima nanenane

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akivalishwa skafu na mmoja wa maskauti alipowasili katika ufunguzi wa maonesho ya siku ya wakulima nane nane Mkoani Morogoro

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika maonesho ya siku ya wakulima nane nane Mkoani Morogoro.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Abubakar Kunenge
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa bodi ya Sukari katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika maonesho ya siku ya wakulima nane nane Mkoani Morogoro

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiangalia moja ya mashine ya mano ya uzalishaji wa sukari katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika maonesho ya siku ya wakulima nane nane Mkoani Morogoro
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiangalia moja ya teknolojia ya kisasa ya umwagiliaji wa mboga mboga katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika maonesho ya siku ya wakulima nane nane Mkoani Morogoro
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na kaumu ya wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa maonesho ya wakulima nane nane yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Mkoani Morogoro.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na kaumu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere katika ufunguzi wa maonesho ya siku ya wakulima nane nane Mkoani Morogoro

Tuesday, July 28, 2020

HAFLA YA MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS WA AWAMU YA TATU WA TANZANIA- HAYATI BENJAMIN MKAPA



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali wilbert Ibuge(wa kwanza kushoto), akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli katika Viwanja vya Uhuru kwa ajili ya kuongonza hafla ya Kitaifa ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania Mhe. Hayati Benjamin William Mkapa, aliyefariki dunia tarehe 24 Julai 2020, Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi(aliyesimama mwisho kulia), akisoma wasifu wa Mhe, Hayati Mkapa.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Jenerali Alain                   Guillaume Bunyoni, akitoa salam za rambirambi kutoka Nchi ya        Burundi, Jenerali Bunyoni pia ameambatana na Spika wa Bunge la    Nchi hiyo pamoja na viongozi wengine kutoka nchini humo.

Kiongozi(Dean) wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini, Balozi wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih, akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Mabalozi wenzake. 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe          Magufuli akihutubia viongozi na wananchi waliohudhuria hafla ya    Kitaifa ya kumuaga Rais wa awamu ya tatu, Mhe. Hayati Mkapa.   
  akiongea katika hotuba yake alisisitiza Watanzania kuenzi mambo      mengi mazuri aliyoyaacha Hayati Mkapa, Mhe. Magufuli alisema      "Ninamshukuru Mungu kwa zawadi ya Maisha ya Mkapa".

 Baadhi ya Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania Nje ya nchi  pamoja  na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania (waliosimama mistari mitatu ya mwisho) wakiwa katika hafla hiyo

   Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini
   ( mistari miwili ya mwisho) wakifuatilia shughuli hiyo


       Mawaziri waliohudhuria wakifuatilia shughuli hiyo


   Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat                Mfumukeko( wa pili kulia), akiongozwa na Afisa Itifaki Bw. Ishengoma kuingia uwanjani kushiriki shughuli hiyo

    Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakitoa heshima     za mwisho kwa mwili wa Hayati Mkapa

         Mabalozi wakiendelea kutoa heshima za mwisho


     Mabalozi wakiendelea kutoa heshima za mwisho

  Mhe. Kabudi akimuaga Mhe. Magufuli alipokuwa akitoka uwanjani

   Mhe. Kabudi akiagana na Waziri Mkuu wa Burundi, Mhe. Bunyoni


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika                  Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro(Katikati),                              akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe.                  Hamad Masauni(Kulia), baada ya hafla hiyo kumalizika

    








Monday, July 27, 2020

WAZIRI KABUDI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA BURUNDI NA UJUMBE WAKE





Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Burundi, Jenerali Alain Guillaume Bunyoni alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhudhuria mazishi ya Kitaifa ya Hayati Benjamin William Mkapa, yatakayofanyika tarehe 28 Julai 2020, Viwanja vya Uhuru, Jijini Dar es Salaam



Mhe. Kabudi na Mhe. Jenerali Bunyoni wakiwa katika mazungumzo katika chumba maalum cha viongozi (VIP), Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, tarehe 27 Julai 2020