Mazungumzo yakiendelea |
Wednesday, March 17, 2021
TANZANIA–CHINA KUENDELEA KUDUMISHA USHIRIKIANO
Monday, March 15, 2021
TANZANIA, VATICAN KUHIMIZA AMANI
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tanzania
na Vatican zimeahidi kuendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye
changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa
unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kuhimiza amani, utulivu na usalama duniani.
Ahadi
hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa
Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski leo jijini Dar es Salaam.
Prof.
kabudi amesema kuwa
Tanzania na Vatican kwa kutambua umuhimu wa amani, zimeahidi kuendelea kushirikiana
katika mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhimiza amani, utulivu na mshikamano
katika masuala mbalimbali yenye changamoto kwa binadamu duniani.
“Tumeongelea umuhimu wa kulinda amani, utulivu
na usalama duniani kote hasa katika maeneo yanayokumbwa na matatizo ya vita……..
katika hilo pia tuliongela suala la amani na usalama katika ukanda wa nchi za
maziwa makuu, Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika tukijua kuwa kuna maeneo
yanayohitaji amani ikiwemo eneo la kaskazini mwa Masumbiji, na mashariki ya
Demokrasia ya Kongo,” Amesema Pro. Kabudi
Prof.
Kabudi ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni na hata sasa dunia
inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji mshikamano wa mataifa yote
duniani ili kuweza kuyakabili hii ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu amani,
utulivu, majanga, na magonjwa ya mlipuko kama vile Covid 19, na yale yanayohusu
umasikini na hali yamaisha ya watu kubaguliwa na kuonewa.
“Mfano
katika mapambano dhidi ya Uviko 19, Vatican na Baba Mtakatifu wanayo nafasi
kubwa ya kutoa mchango wao katika eneo hilo katika kuhakikisha kuwa mapambano
dhidi ya Covid 19 hayageuzwi kuwa katika masuala ya kibiashara na kisiasa na
badala yake mapambano hayo yazingatie utu, undugu na imani, Ameongeza Pro.
Kabudi
Kwa
upande wake Balozi wa Vatican hapa Nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski
amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na
Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya haki, utu, amani na utulivu.
“Maongezi
yangu na Mhe. Waziri yalikuwa mazuri kwani tuliongelea masuala mbalimbali yenye
maslahi kwa binadamu yakiwemo masuala ya kukuza diplomasia yetu pamoja na
masuala ya amani na usalama duniani,” Amesema Askofu Mkuu Solczynski.
Baba
Mtakatifu Papa Francisko alimteua, Askofu Mkuu Marek Solczyński kuwa Balozi
mpya wa Vatican nchini Tanzania mwezi Aprili, 2017. Kabla ya uteuzi huu, Askofu
mkuu Solczyński alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Georgia, Armenia na
Azerbaijan.
Katika
tukio jingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. William Tate Olenasha amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria
hapa nchini Mhe. Ahmed Djellal ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi
hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu kuimarisha diplomasia baina ya
Tanzania na Algeria.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi,
(Mb) akisalimiana na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski
wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar
es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi,
(Mb) akiongea na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski wakati
walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
Salaam
Balozi
wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski akimuelezea jambo Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb)
wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar
es Salaam
Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, Mhe. William
Tate Ole Nasha akiongea na Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal wakati
walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
Salaam
Balozi
wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo
ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, Mhe. William Tate Ole Nasha wakati
walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
Salaam
WATUMISHI WA WIZARA WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA UWELEDI NA NIDHAMU.
Shemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo |
Shemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo |
Friday, March 12, 2021
TANZANIA YAJIVUNIA MIAKA 40 YA MAFANIKO SADC
Na Mwandishi wetu,
Tanzania
imejivunia mafanikio iliyoyapata katika kipindi cha miaka 40 ya uanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) ameyataja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na miaka 40 ya uanachama wa
SADC tangu 1979, lugha ya kiswahili kutumika katika mikutano yote ya kisekta ya
SADC pamoja na kutengenzwa sanamu maalumu ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius
Kambarage Nyerere.
“Pamoja
na mambo mengine, mkutano wetu wa leo wa Baraza la Mawaziri wa SADC tunategemea
kujadili masuala mbalimbali anayohusu jumuiya hiyo likiwemo suala la matumizi
ya lugha ya Kiswahili katika mikutano yote ya kisekta,” Amesema Prof. Kabudi.
Mambo
mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na suala la kutengeneza sanamu maalumu ya
Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambapo sanamu hiyo itawekwa
katika jengo la Amani Addis Ababa nchini Ethiopia, pamoja na maadhimisho ya
miaka 40 ya SADC.
“Hivyo
kupitia mkutano huu tutakamilisha mchakato wa kumpata mtu atakae ifua sanamu
hiyo ya Mwl. Nyerere ambapo itawekwa katika jingo la Amani Ethiopia,” Amesema
Prof. Kabudi
Prof. Kabudi ameendelea kueleza kuwa katika mkutano huo suala la maadhimisho ya miaka 40 ya SADC pia limejadiliwa ikiashiria umoja wa SADC kudumu kwa miaka 40.
“Miaka
40 ya SADC ina umuhimu mkubwa sana kwa Tanzania kwa sababu miongoni mwa
viongozi nane walioasisi sadc ni Mwl. Julius Nyerere katika mkutano uliofanyika
mwaka 1979 mkoani Arusha ambapo Tanzania iliamua kuingia rasmi katika jumuiya
hiyo,” Ameongeza Prof. Kabudi
Tanzania
itakuwa inasherekea miaka 40 ya SADC ikiwa tayari Kiswahili ni moja ya lugha
rasmi za jumuiya hiyo, lakini pia ikiwa na sanamu maalumu ya kumuenzi na
kumheshimu baba wa Taifa na Muasisi wa SADC Mwl. Julius Nyerere.
Hivyo
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Waziri wa
Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, Waziri wa Fedha na Mipango –
Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe.
Omar Said Shaaba, Naibu Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto, Dkt. Godwin Mollel, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
UShirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge pamoja
na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaban.
Februari
27, 2021 katika mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulifanyika
kwa njia ya Mtandao, wakuu wan chi waliridhia lugha ya Kiswahili iwe lugha ya
tatu katika shughuli za jumuiya hiyo sambamba na lugha ya kifaransa kuwa lugha
ya nne.
Kadhalika,
Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika mkutano wao wa 39 uliofanyika jijini
Dar es Salaam mwezi Augusti, 2019 waliridhia na kuipitisha kiswahili nne ya
mawasiliano, ikiungana na lugha za Kifaransa, Kiingereza na Kireno zinazotumika
katika jumuiya hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akifuatilia Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb), katikati pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na Kaimu
Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agnes Kayola wakifuatilia mkutano
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati wa mkutano
wa baraza la mawaziri
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (anaesoma taarifa) na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed
Mazrui (kulia) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge (kushoto) wakifuatilia
mkutano
Ujumbe
wa Tanzania ukiendelea kufuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri SADC
Ujumbe wa Tanzania ukiendelea kufuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri SADC Mkutano ukiendelea
Wednesday, March 10, 2021
MAKATIBU WAKUU SADC WAENDELEA NA KIKAO
Na Mwandishi wetu,
Makatibu
Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wameendelea na kikao
chao kwa siku ya pili ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa baraza la mawaziri wa
SADC unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 – 13 Machi, 2021 kwa njia ya mtandao
jijini Dar es Salaam.
Ujumbe
wa Tanzania katika kikao hicho unaongozwa na Balozi Brigedia Jenerali Wilbert
Ibuge pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban.
Mkutano
wa Baraza la Mawaziri ujumbe wa Tanzania utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Africa Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ataongoza
ujumbe wa Tanzania.
Mwenyekiti
wa Sasa katika Jumuiya ya SADC ni msumbiji na ndiye atakayeongoza majadiliano ya
Mkutano huu.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akiwasilisha mada katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachoendelea jijini Dar es Salaam kwa
njia ya mtandao. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi.
Amina Shaban. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa
SADC utakafanyika tarehe 12 - 13, Machi 2021 kwa njia ya mtandao jijini Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akiwasilisha mada katika kikao cha Makatibu Wakuu wa
SADC kinachoendelea jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao. Kikao hicho ni
maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakafanyika tarehe 12,
Machi kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge, akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha makatibu
wakuu wa SADC, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi.
Amina Shaban pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agnes Kayola
Washiriki
wa kikao cha makatibu wakuu wakifuatilia kikao kinachoendelea kwa njia ya
mtandao jijini Dar es Salaam
Washiriki
wa kikao cha makatibu wakuu wakifuatilia kikao kinachoendelea kwa njia ya
mtandao jijini Dar es Salaam
Kikao
kikiendelea
Monday, March 8, 2021
KISWAHILI CHAPENDEKEZWA KUTUMIKA RASMI SADC
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Lugha
ya Kiswahili imependekezwa kuanza kutumika rasmi katika majadiliano kwenye
vikao vya ngazi ya baraza la mawaziri na katika utendaji wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Pendekezo
hilo limewasilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika kikao cha
Makatibu Wakuu wa SADC kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam kwa njia ya
mtandao.
“Sisi
kama Tanzania tumependekeza suala la lugha ya Kiswahili kutoka kwenye lugha ya
kazi kwenye ngazi ya baraza la mawaziri hadi wakuu wa nchi na serikali wa SADC
linabadilika na kuiwezesha lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi kwenye utendaji
wa SADC,” Amesema Balozi Ibuge.
Balozi
Ibuge ameongeza kuwa, SADC wamekuwa wakitumia lugha za kikoloni kwa muda mrefu
na kwa busara za wakuu wa nchi na Serikali wameamua kuanza kwa mpangilio ambapo
lugha ya Kiswahili itaanza kutumika katika ngazi ya baraza la mawaziri pamoja
na vikao vya wakuu wa nchi, na kuishusha
lugha hiyo kwenye sekta na kuingia rasmi katika matumizi ya SADC.
Kikao
hicho ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC unaotegemewa
kufanyika tarehe 12, Machi jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akiwasilisha mada katika kikao cha Makatibu Wakuu wa
SADC kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao
Mkutano
ukiendelea
Mkutano
ukiendelea