Friday, June 9, 2023

DKT. TAX AZUNGUMZA NA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WA ITALIA JIJINI ROMA


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na mwenyeji wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani walipokutana kwa mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake jijini Roma, Italia tarehe 9 Juni, 2023.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwake jijini Roma, Italia. Akishuhudia nyuma yao ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahamoud Thabit Kombo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na mwenyeji wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake jijini Roma, Italia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na ujumbe wake upande wa kulia wakizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani na ujumbe wake walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwake jijini Roma, Italia.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Italia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani ofisini kwake jijini Rome nchini Italia tarehe 9 Juni,2023 

Akizungumza na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Tax ameelezea kuridhishwa na uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Italia na kuishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo kupitia maeneo ya elimu, afya, kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa na uchumi wa buluu.

Mhe. Dkt. Tax ameihakikishia Italia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Tanzania na kuhakikisha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Italia unakuwa na kufikia ngazi ya juu.

Dkt. Tax amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Italia ambao utatumika kama jukwaa la kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizo kwa maslahi mapana ya pande zote.

“Nafahamu kuwa nchi zetu hazina mfumo wa majadiliano wa kisiasa na kidiplomasia licha ya kuwa na uhusiano mzuri wa siku nyingi, napendekeza tuanzishe mfumo wa majadiliano ya kisiasa kati ya nchi zetu, mfumo ambao utatumika kama jukwaa la kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizi kwa maslahi ya pande zote,” alisema Dkt. Tax.

Dkt. Tax ameipongeza Serikali ya Italia kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa mpango mkakati wa maendeleo na sera za taifa na kuishukuru kwa mikopo ya masharti nafuu wenye nia ya kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mafunzo ya ufundi na kuwezesha vijana kujiajiri katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Mwanza, Songwe, Zanzibar na Dar es Salaam. 

Pia ameelezea shukurani za Serikali ya Tanzania kwa Serikali ya Italia kwa mkopo wa masharti nafuu kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ambao utawezesha utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usajili wa Taarifa muhimu kwa Tanzania Bara ambapo watoto chini ya miaka MITANO watasajiliwa.

Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri Mkuu wa Italia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa Mhe. Anthonio Tajan amesema Italia itaendelea kushirikiana na Tanzania kama mdau mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi na kuahidi kuwa Serikali ya Italia itaandaa kongamano la wafanyabiashara ili kuwawezesha wafanyabiashara wa Nchi hizo mbili kufahamiana na kupata fursa za kufanya kazi kwa pamoja. 

Amemuhakikishia Mhe Waziri kuwa Serikali ya Italia imedhamiria kuendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania na nchi za Afrika kwa ujumla katika sekta mbalimbali. 

WAZIRI TAX: WATUMISHI TEKELEZENI DIPLOMASIA YA UCHUMI KWA BIDII


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha wageni aliposili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Italia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Stergomena Tax amewataka watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Akizungumza na watumishi hao katika Ofisi za Ubalozi huo Jijini Roma, Mhe. Dkt. Tax amesema Serikali inawategemea wao kama wadau wa kubwa katika kutekeleza diplomasia ya uchumi ili kuinufaisha nchi.

“Wizara inategemea Balozi katika kutekeleza diplomasia ya uchumi, kwa hiyo mna wajibu wa kuhakikisha mnafanya kazi hii kwa ukamilifu” alisema Dkt.Tax.

Aidha, Dkt. Tax ameupongeza Ubalozi huo kwa kuandaa mkakati wa kutekeleza diplomasia ya uchumi katika eneo lake la uwakilishi na kuzitaka Balozi nyingine za Tanzania kuiga mfano huo.

“Nimesikia hapa mmeandaa mpango mkakati wa kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika eneo lenu, hili ni jambo zuri niwapongeze kwa hilo na balozi zetu nyingine hazina budi kuiga mfano huu,” alisema Dkt. Tax

Aliongeza kuwa Wizara inatengeneza mkakati wa kitaifa wa utekelezaji wa diplomasia ya uchumi, tutawaletea muuone na mtoe maoni yenu ili kuuboresha zaidi.

Amesema anaamini kuwa kupitia mkakati huo Wizara itajifunza kitu na hivyo kuja na mkakati bora wa utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

Mhe.Waziri amewasihi watendaji wa ubalozi kuhakikisha wana shirikisha sekta binafsi katika kutekeleza kazi zao kwani kufanya hivyo kutasaidia kuondoa uwiano mdogo wa kibiashara uliopo kati ya Tanzania na Italia.

Awali akizungumza katika kikao hicho Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alisema ubalozi unaendelea kusimamia na kutekeleza diplomasia ya uchumi kupitia utalii,kilimo,uwekezaji, biashara na masoko ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchini inazowakilisha.

Alisema ubalozi pia unashirikisha Diaspora katika shughuli za maendeleo ya nchi na kupongeza mpango wa kusajili Diaspora wa Tanzania kwa njia ya Kidigitalia

Mhe. Dkt. Tax yuko nchini Italia kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Italia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akifuatilia taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Kombo wakati wa kikao kazi watumishi wa Ubalozi huo. Kushoto ni Mkurugezi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme na kulia ni Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Utalia Bi. Jubilata Shao
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Kombo wakiwa picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Kombo wakiwa picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi 

Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud T. Kombo akielezea jambo kwa Waziri Tax alipokuwa akitembelea maeno ya Ubalozi

Tuesday, June 6, 2023

NAIBU WAZIRI, BALOZI MBAROUK AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA WIZARA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab alipowasili eneo la Mtumba inapojengwa jengo la ofisi la Wizara hiyo kwa ajili ya kujionea maendeleo ya ujenzi.

Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Majengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi John Kiswaga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma M. Rajab kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara katika eneo la Mtumba

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili eneo la Mtumba kujionea maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akiangalia ngazi za kuingilia lango kuu la jengo la Ofisi ya Wizara linalojengwa Mtumba jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akiangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma M. Rajab wakiongea na wakandarasi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara katika eneo la Mtumba jijini Dodoma

Hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara linalojengwa eneo la Mtumba jijini Dodoma. Jengo limefikia zaidi ya asilimia 70 ambayo ni hatua inayokwenda sambamba na Mkataba wa ujenzi 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara Mtumba jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma M. Rajab wakiongea na wakandarasi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara katika eneo la Mtumba jijini Dodoma



Saturday, June 3, 2023

HADHI MAALUM NI NINI?


 

DKT. TAX AMWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA 10 WA DHARURA WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA JUMUIYA YA NCHI ZA MAZIWA MAKUU JIJINI LUANDA, ANGOLA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 10 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 03 Juni, 2023. 

Mkutano huo wa dharura ulitanguliwa na Mkutano wa Mawaziri uliofanyika tarehe 2 Juni, 2023 umejadili na kuangalia hali ya amani na usalama katika katika Ukanda wa Maziwa Makuu hasa katika nchi za Jamhuri ya Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mkutano huo umeitishwa na Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) Mheshimiwa Joao Manuel Lourenco ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa 16 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Mei 2022 jijini Malabo, Equatorial Guinea. 

Mwezi Julai 2022, Jumuiya ya Kikanda ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) ilitoa Mpango wa Mchakato wa Mazungumzo ya Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliolenga kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na kisiasa na kujiridhisha kuhusu tuhuma mbalimbali zinazotolewa hususan ushirikiano wa Serikali ya Rwanda na kikundi cha M23 na ushirikiano wa Serikali ya DRC na kikundi cha FDLR. 

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Mhe. Faustine Archange Touadera  Makamu wa Rais wa Uganda Mhe. Jessica Rose Alupo Epel, Waziri Mkuu wa Rwanda Mhe. Eduoardo Ngirente,  Waziri wa Kenya Mhe. Musalia Mudavadi, Waziri Ofisi ya Rais wa Sudani Kusini Barnaba Marial Benjamin, Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo Mhe. Jean Cloude Gakosso, Waziri wa Ulinzi wa Zambia Mhe. Ambrose Lufuma, Mjumbe Maalumu wa Serikali ya Jamhuri ya Sudan Mhe. Balozi Daffa Alla Elhag Ali Osman, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mhe. Moussa Faki Mahamat na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesimama wakati Wimbo wa Taifa wa Angola unaimbwa kwenye Mkutano wa 10 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika jijini Luanda, Angola
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akifuatilia Mkutano wa 10 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) uliokuwa ukiendelea jijini Luanda, Angola

Mkutano wa 10 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) ukiendelea jijini Luanda, Angola

Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) Mheshimiwa Joao Manuel Lourenco akifungua mkutano wa 10 wa Dharura wa Jumuiya hiyo
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mhe. Moussa Faki Mahamat akifuatilia Mkutano wa 10 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo akifuatilia Mkutano wa 10 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu uliokuwa ukiendelea jijini Luanda, Angola

DKT. TAX AWASILI ANGOLA KUMWAKILISHA MHE. RAIS DKT SAMIA KATIKA MKUTANO WA ICGLR

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na   Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Tete Antonio alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa 4 de Fevereiro jijini Luanda, Angola kuhudhuria Mkutano wa 10 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR)


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Angola Bw. Mbwana Mziray (kulia) na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mhe.Moussa Faki Mahamat (kushoto) alipowasili jijini Luanda, Angola kuhudhuria Mkutano wa 10 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR).


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Mjumbe Maalum wa Serikali ya Sudan Balozi Dafallah Al-Hajj wakati wa kikao cha maandalizi cha  Mkutano wa 10 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) utakaofanyika jijini Luanda  Angola tarehe 3 Juni 2023.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akishiriki kikao


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewasili jijini Luanda , Angola kuhudhuria Mkutano wa 10 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR).

 
Mkutano huo utakaofanyika tarehe 03 Juni 2023 utajadili na kuangalia hali ya amani na usalama katika katika Akanda wa Maziwa Makuu hasa katika Jamhuri ya Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Friday, June 2, 2023

SERIKALI YAKABIDHI ENEO LA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imekabidhi eneo la ujezi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa Mkandarasi ambaye ni CRJE (East Africa) Ltd na Mshauri Elekezi Aru Built Environment Consulting Company Ltd (ABECC) katika eneo la Lakilaki, Jijini Arusha.

Hafla ya makabidhiano ya eneo hilo la ujenzi imeongozwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ambaye amekabidhi eneo hilo kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya makabidhiano hayo Dkt. Shelukindo amesema kuwa Serikali imetoa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 26 hivyo Wizara itaendelea kutoa usaidizi wa karibu katika usimamizi wa ujenzi wa mradi huu ambao katika hatua ya awali unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilllingi billioni nane (8) na utakamilika baada ya miaka miwili kulingana na mkataba wa mradi huo. 

“Ujenzi wa majengo ya mahakama hiyo utakuwa wa kisasa kwa kuwa umezingatia taratibu na vigezo vya ujenzi wa majengo ya ofisi za kimataifa ambapo pamoja na jengo kuu, kutakuwa pia na jengo la mahakama, hospitali, shule na mengine yanayoendana na huduma za mahakama hiyo,” alisema Dkt. Shelukindo

Naye Rais wa Mahakama wa Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud alieleza kuwa amefurahishwa na hatua hiyo iliyofikiwa na Serikali ya kukabidhi eneo la ujenzi wa mradi huo lililosubiriwa kwa muda mrefu.

‘’ Tunaishukuru na kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa hatua hii itaiwezesha Mahakama kuwa na majengo ya kisasa na ofisi za kudumu kwa ajili ya kutoa huduma zake na tunatarajia ujenzi wa maradi huu utakamilika kwa wakati na salama” alisema Mhe. Jaji Aboud.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella ameishukuru pia Serikali kwa kuitimza ndoto yake ya miaka mingi ya kujenga mahakama hiyo nchini ambayo italiletea fursa nyingi Jiji la Arusha ikiwemo ajira za mafundi, walinzi pamoja na kuongeza taswira nzuri ya jiji hilo la kitalii.

“Jiji la Arusha limebahatika kuwa mwenyeji wa taasisi za kimataifa zinazojengwa katika eneo hili la Lakilaki hivyo Mkoa utatoa usaidizi wakati wa ujenzi wa mradi huu ili ukamilike kwa ubora na wakati na kuyafikia malengo yaliyowekwa na Serikali” alisema Mhe. Mongella. 

Hafla hiyo ya makabidhiano ilihudhuriwa pia na Meneja wa Mradi kutoka CRJE (East Africa) Ltd, Bw. Zhang Cuishan, Mshauri elekezi kutoka chuo cha Ardhi, QS. Dkt. Godwin Maro, viongozi na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja watumishi kutoka Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

Mwaka 2005 Umoja wa Afrika uliridhia kuwepo na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambapo Tanzania ilijitolea kuwa mwenyeji wa Mahakama hiyo na kuanzia wakati huo Serikali imekuwa ikikamilisha taratibu mbalimbali za nyaraka za eneo la mradi ambao utajengwa katika eneo la Lakilaki nje kidogo ya jiji la Arusha.

Viongozi wakiwasili katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha tayari kwa ajili ya kumkabidhi Mkandarasi CRJE (East Africa) Ltd na Mshauri Elekezi Aru Built Environment Consulting Company Ltd (ABECC) eneo la ujenzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akimkabidhi nakala za mitakaba ya ujenzi wa jengo la Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Meneja wa Mradi kutoka CRJE (East Africa) Ltd, Bw. Zhang Cuishan. Ujenzi wa mahakama hiyo utakuwa katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella pamoja na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud, viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na maafisa waandamizi kutoka Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akimkabidhi nakala za mitakaba ya ujenzi wa jengo la Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Rais wa Mahakama hiyo, Mhe. Jaji Imani Aboud


Viongozi na watumishi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja






Thursday, June 1, 2023

DKT. MPANGO AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA BURUNDI KUJA KUWEKEZA NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Mpango amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Burundi kuja kuwekeza nchini na kuitaja Tanzania kama sehemu salama ya kuwekeza mitaji yao.

Mhe. Dkt. Mpango ametoa wito huo alipokutana kwa mazungumzo na timu ya wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa 17 wa Burundi ambao wameonesha nia ya kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo za madini, ufugaji, kilimo na  viwanda vya mbolea na saruji.

Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara ikiwa ni pamoja na kuzifanyia kazi changamoto za kisera na kisheria.

Ameongeza kusema  uchumi wa Tanzania upo imara,huku mazingira na miundombinu kwa ujumla kama maji, umeme, barabara na reli vikiboreshwa ili  kukidhi mahitaji ya wawekezaji.

Amesema uwekezaji ni gharama na kwamba Serikali inaboresha mazingira ili mwekezaji yeyote apate faida lakini pia na nchi ifaidike na uwekezaji huo.  Hivyo katika kuhakikisha azma hiyo inafikiwa Serikali iliandaa Mpango wa maboresho ya biashara ambao umejumuishaa maoni na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wadau  wa biasharana  uwekezaji.

Pia amesema kupitia mpango huo Serikali imefanikiwa kubadilisha mifumo mbalimbali na kuondoa kero mbalimbali kama upatikanaji wa leseni, ulipaji kodi ili ieandane na wakati uliopo ikiwemo banadari, kituo cha uwekezaji Tanzania na sekta nyingine.

“Nimefurahi sana Kampuni 17 kuja kuwekeza Tanzania ni jambo zuri na pia ninafarijika na kampuni za Tanzania pia zilizowekeza hapa Burundi. Naendelea kusisitiza badala ya kufanya biashara na nchi za mbali huko tufanye biashara wenyewe kwa wenyewe  kwani tuna mengi ya kubadilisha katika biashara ili pia tuwaunge mkono Wakuu wa Nchi za Afrika waliofanya uamuzi wa makusudi wa kuanzisha Ukanda Huru wa Biashara Barani Afrika. Kuna bidhaa zinapatikana Tanzania, Burundi hazipo lakini pia kuna bidhaa zinapatikana Burundi, Tanzania hazipo hivyo tufanye biashara,  alisisitiza Mhe. Dkt. Mpango.

Amesema mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika kuhusu  ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Uvinza-Msongati hadi Gitega yanaendelea vizuri na kwamba kukamilika kwa reli hiyo kutarahisha biashara na nchi jirani. Pia ameeleza kuwa, ujenzi wa Barabara ya lami kutoka Uvinza hadi Malagarasi unaendelea huku zikiwa zimebakia kilomita 52 pekee kukamilika.

Pia alitoa rai kwa Wawekezaji hao kuendelea kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania  uliopo nchini humo kwa kuwasilisha changamoto zao ili ubalozi nao uziwasilishe kwa wahusika kila inapohitajika.

Kwa upande wake, Kiongozi wa wawekezaji hao ambaye pia ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bujumbura, Bw. Fredrick Siwale amemshukuru Makamu wa Rais kwa kutenga muda na kuzungumza nao. Pia alieleza kuwa Benki hiyo imewekeza mtaji wa Dola za Marekani Milioni 210 kwa ajili ya kuwawezesha wawekezaji hao kuwekeza nchini.

Ameongeza kusema katika kutekeleza suala zima la uwekezaji nchini Tanzania kwa wawekezaji kutoka Burundi, wamekuwa wakiwapatia mikopo baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa nchi hiyo  ili kutumia mikopo hiyo kuwekeza Tanzania ambapo hadi sasa wafanyabiashara hao wamewekeza kwa kujenga kiwanda cha Mbolea cha Intracom jijini Dodoma, kiwanda cha kutengeneza saruji mjini Kigoma na ujenzi wa hoteli  ya kitalii mjini Tanga.

Wawekezaji hao pia wamempongeza Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko na wafanyakazi wa Ubalozi kwa ushirikiano wanaopata kila wakati wanapohitaji msaada.

Mhe. Dkt. Mpango alikuwa nchini Burundi kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa 21 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Phillip Mpango akizungumza na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Burundi alipokutana nao jijini Bujumbura, Burundi pembezoni mwa Mkutano Maalum wa 21 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo alishiriki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wawekezaji hao wameonesha ya kuja nchini kuwekeza kwenye sekta za kilimo, madini, ufagaji, ujenzi wa viwanda vya saruji na mbolea na ujenzi wa hoteli.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa mkutano huo
Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko akitoa taarifa kwa Mhe. Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mpango kuhusu wawekezaji hao kutoka Burundi
Kiongozi wa Wawekezaji hao ambaye pia ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bujumbura, Bw. Fredrick Siwale akizungumza wakati wa kikao kati yao na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mpango
Kikao kikiendelea. huku viongozi mbalimbali kutoka Tanzania akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi (wa tatu kushoto) na Mhe. Balozi Maleko (kushoto) wakifuatilia
Sehemu ya wawekezaji hao wakifuatilia kikao
Sehemu nyingine ya wawekezaji
Picha ya pamoja kati ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mpango (wa pili kushoto), Dkt. Mnyepe (wa pili kulia), Mhe. Balozi Maleko (kushoto) na Bw. Siwale (kulia)
Picha ya pamoja kati ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mpango (katikati), Dkt. Mnyepe (wa pili kulia), Mhe. Balozi Maleko (wa pili kkushoto) na wawekezaji (kushoto na kulia) kutoka Burundi ambao wamewekeza kwenye Kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Intracom kilichopo jijini Dodoma
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja

Picha ya pamoja kati ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mpango, Dkt. Mnyepe, Mhe. Balozi Maleko na baadhi ya wawekezaji kutoka Burundi wenye nia ya kuwekeza Tanzania