Wednesday, July 19, 2023

WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA WA CANADA AWASILI NCHINI

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 19 – 23 Julai, 2023. 

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mhe. Sajjan alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo.

Akiwa nchini, Mhe. Sajjan pamoja na ujumbe wake anatarajia kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali na kujadiliana nao masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Canada.

Aidha, Waziri Sajjan anatarajia kukutana kwa mazungumzo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Waziri wa Afya pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Canada.

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo



Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasilis katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akisalimiana naKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam


Tuesday, July 18, 2023

TANZANIA NA HUNGARY ZAAINISHA MAENEO YA KUSHIRIKIANA





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Hungary Mheshimiwa Katalin Novák

Rais wa Hungary Mheshimiwa Katalin Novák akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Hungary, Mheshimiwa Katalin Novák wakizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mazungumzo yao 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknoloji Prof. Adolf Mkenda akipongezana na Waziri wa Nchi wa Hungary Azbej Tristan  baada ya kusaini Hati ya Makubaliano (MoU) 




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akiteta jambo na Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo Ikulu Jijini Dar es Salaam 

Rais wa Hungary Mheshimiwa Katalin Novák akipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) kwenye makazi ya Mwakilishi wa Heshima wa Hungary nchini Tanzania, Bw. Solomon Kimaro Jijini Dar es Salaam 

Rais wa Hungary Mheshimiwa Katalin Novák akisalimiana na  Mwakilishi wa Heshima wa Hungary nchini Tanzania, Bw. Solomon Kimaro kwenye makazi yake Jijini Dar es Salaam 

 

Monday, July 17, 2023

RAIS WA HUNGARY AWASILI TANZANIA

Rais wa Hungary Mheshimwa Katalin Novák, amewasili leo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne itakayomalizika tarehe 20, Julai 2023.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Mheshimiwa, Novák amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) 

Akiwa nchini, tarehe 18 Julai 2023 Mheshimiwa Novák anatarajia kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na kufanya mazungumzo rasmi na baadae viongozi hao kuzungumza na Waandishi wa Habari.

Mheshimiwa Novák ni Rais wa kwanza mwanamke kuongoza Hungary ambapo alichaguliwa mwezi Mei, 2022. Aidha, ni Rais wa kwanza kutoka Hungary kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania.

Ziara hiyo ni matokeo ya jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Mataifa mbalimbali duniani.

Tanzania na Hungary zimekuwa zikishirikiana katika sekta za biashara, elimu, utalii, kilimo, utangazaji na viwanda.

Viongozi wengine walioambatana na Dkt. Tax kumpokea Rais wa Hungary ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Muliro Jumanne, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani anayeiwakilisha pia Tanzania nchini Hungary, Mhe. Abdallah Possi, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme pamoja na Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.








MKUTANO WA 25 WA KAMATI YA MAWAZIRI WA SADC KWA NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAANZA JIJINI WINDHOEK

Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) utafanyika jijini Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17 hadi 21 Julai, 2023

 

Mkutano huo umetanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu unaofanyika tarehe 17 na 18 Julai 2023 ambapo ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kamati hii unaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Faraji Mnyepe.

 

Akifungua Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Balozi Penda Naanda amewakaribisha Wajumbe nchini Namibia na kuwaomba kujadili agenda zilizopo mezani kwa umakini ili hatimaye kuziwasilisha kwa Kamati ya Mawaziri kwa hatua zinazofuata.

 

Ameongeza kusema kuwa, vikao vya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ni muhimu kwani huzikutanisha nchi wanachama kwa ajili ya kujadili na kutathmini hali ya siasa, ulinzi na usalama ya kanda, demokrasia na utawala bora kwa maslahi mapana ya nchi wanachama. 

 

“Nawakaribisha jijini Windhoek na katika kikao chetu hiki ili kwa pamoja tupokee na kujadili taarifa mbalimbali za vikao vilivyotangulia ili kutathimini hatua zilizofikiwa na kutoa mapendekezo yetu ya namna ya kuendeleza mtangamano wa Jumuiya yetu kupitia vikao hivi” alisema Balozi Naanda.

 

Akichangia hoja wakati wa Mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Samwel Shelukindo  amesema ni matarajio ya Tanzania kuwa, vikao hivyo ambavyo hufanyika kila mwaka vitaendelea kutoa mchango chanya katika kukuza na kuimarisha masuala mbalimbali ya Jumuiya ikiwemo demokrasia katika Kanda; hali ya Siasa, ulinzi na usalama; mapambano dhidi ya uhalifu wa kupangwa, rushwa na usafirishaji haramu wa binadamu.

 

Aidha, ametoa rai kwa Jumuiya ya SADC kuendelea kutilia maanani changamoto ya ongezeko la vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu na wimbi la utekaji nyara Watoto kwa kuwa ni changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zinaathiri vijana ambao ndio nguvu kazi ya Kanda.

 

“Ni vyema Kanda yetu ikaendelea kujiwekea mikakati madhubuti ya kudhibiti changamoto hizi ikiwemo kutafuta fedha za kuwasafirisha wahamiaji haramu wanapomaliza vifungo vyao, manunuzi ya magari na vifaa kwa ajili ya kufanyia doria za pamoja za udhibiti wa mipaka na utoaji wa mafunzo kwa taasisi husika” alisisitiza Balozi Fatma.

 

Kuhusu athari zitokanazo na migogoro ya ndani na nje ya Afrika ikiwemo mgogoro wa Urusi na Ukraine ambao umeathiri usalama wa chakula, Balozi Fatma ameziomba nchi wanachama kuchukua hatua mbalimbali za kujitegemea kwa kuhakikisha zinazalisha chakula cha kutosha, kuimarisha mifumo ya ubora wa mazao, kuwa na soko la Kanda la kuuziana mazao na kuuza nje ya nchi kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni.

 

Mkutano wa 25 unalenga pamoja na mambo mengine kupokea na kujadili agenda mbalimbali zikiwemo mapitio ya utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa 24 wa MCO na Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC; Hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya kanda; masuala ya demokrasia; mapambano dhidi ya uhalifu wa kupangwa, rushwa na usafirishaji haramu wa binadamu.

 

Nchi Wanachama 16 za SADC zimeshiriki Mkutano huo wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Balozi Penda Naanda akifungua rasmi Mkutano wa Kamati hiyo uliofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 17 Julai 2023
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Balozi Penda Naanda akiwa na wajumbe wa meza kuu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kamati ya Makatibu Wakuu wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC uliofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 17 Julai 2023
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC wakati wa mkutano uliofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 17 Julai 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab.
Balozi Fatma Rajab wakati wa Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC. Balozi Fatma alitoa mchango wa Tanzania kuhusu umuhimu SADC kuendelea kutilia maanani changamoto ya ongezeko la vitenfo vya usafirishaji haramu binadamu na wimbi la utekaji nyara watoto ambazo kwa kiasi kikubwa zinaathiri vijana ambao ni nguvu kazi ya kanda
Mjumbe wa Angola akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,
Mjumbe wa Botswana akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,
Mjumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,
Mjumbe wa Lesotho akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,
Mjumbe wa Namibia akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,
Mjumbe wa Afrika Kusini akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,
Mjumbe wa Zimbabwe akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,

Wajumbe wa Sekretarieti ya SADC wakishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,

Sehemu ya Washiriki wakati wa Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,

Mkutano ukiendelea