Friday, November 24, 2023

NAIBU WAZIRI BYABATO AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KOREA

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Bi. Oh Youngju walipokutana kwa mazungumzo pembezoni mwa Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.


Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato, amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Bi. Oh Youngju, pembezoni mwa Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea kwa manufaa ya pande zote mbili.

Akizungumza katika mkutano huo Naibu Waziri Mhe. Byabato alimuelezea Bi. Youngju kuridhishwa kwa Tanzania juu ya ushirikiano na uhusiano uliopo kati yake na Jamhuri ya Korea na kuahidi kuendelea kushirikiana na nchi hiyo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

Naye Bi. Youngju alimuelezea Naibu Waziri Byabato juu ya mpango wa Jamhuri ya Korea wa kuandaa Mkutanoo kati ya Nchi yake na Viongozi wa Bara la Afrika uliopangwa kufanyika mapema mwezi Juni 2024 na kwamba anaialika rasmi Tanzania ishiriki katika mkutano huo.
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Bi. Oh Youngju walipokutana kwa mazungumzo pembezoni mwa Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Bi. Oh Youngju yaliyofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.
Mazungumzo yakiendelea

KISWAHILI NYENZO MUHIMU KATIKA KUKUZA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA MALAWI

Serikali ya Tanzania itaendelea kukuza na kuhamasisha matumizi ya Lugha ya Kiswahili ili kuimarisha biashara inayovuka mipaka hususan katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ikiwemo Malawi.



Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola alipokitembelea Chuo Kikuu cha Biashara na Sayansi cha nchini humo kwa lengo la kujadiliana na Uongozi wa Chuo hicho kuhusu namna bora ya kuanzisha ushirikiano baina na taasisi za elimu za Tanzania hususani katika kufundisha Lugha ya Kiswahili.



Katika mazungumzo yake na Mkuu wa Kitivo cha Elimu, Mawasiliano na masuala ya Habari wa Chuo hicho, Dkt. Kizito Elijah, Mhe. Balozi Kayola alisema kuwa, upo mwingiliano mkubwa wa kibiashara baina ya Tanzania na Malawi unaosababisha mahitaji makubwa ya kujifunza lugha ya Kiswahili ili kurahisisha mawasiliano katika biashara.



Aliongeza kusema Serikali ya Tanzania itaendelea kusimamia na kutekeleza makubaliano yote yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini humo mwezi Julai 2023 ikiwemo masuala ya ufundishaji wa Kiswahili nchini Malawi.



Kwa upande wake, Dkt. Elijah alisema kuwa, Chuo hicho kimepanga kuanzisha Kituo cha Lugha na kuonesha nia ya kushirikiana na Tanzania hususan Taasisi za Elimu na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ili kutekeleza azma ya kufundisha Lugha ya Kiswahili chuoni hapo na kwamba chuo hicho kipo tayari kuanzisha ushirikiano na Vyuo Vikuu vya Tanzania ikiwa ni pamoja na kubadilishana wakufunzi na wanafunzi.



Wakati huohuo, Mhe. Balozi Kayola ameitembelea Kampuni ya Kitanzania ya Bakhresa ambayo imewekeza nchini Malawi tangu mwaka 2003 katika viwanda vya uzalishaji Unga wa ngano, sabuni za kufulia na inatarajia kukamilisha kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia mwezi Mei 2024.



Akiwa katika Kampuni hiyo Mhe. Balozi Kayola amepongeza uwekezaji mkubwa uliofanyika na kuwahamasisha kuendelea kukuza wigo wa uwekezaji wa bidhaa mbalimbali nchini humo kwani mahitaji bado ni makubwa.



Kadhalika, Mhe. Balozi Kayola alipata fursa ya kukutana na Jumuiya ya Watanzania waishio katika Mkoa Kusini, Malawi ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuiwakilisha Tanzania nchini humo.



Katika mazungumzo yake na Jumuiya hiyo aliwaasa kuendelea kuwa wawakilishi wazuri wa nchi yao kwa kufuata sheria za nchi waliyopo  ili kulinda taswira nzuri ya Tanzania.



Pia alisisitiza umuhimu wa wao kuendelea kujiandikisha kwenye Mfumo wa Kidigitali wa kuwatambua Diaspora (Diapora Digital Hub) ili iwe rahisi kuwaunganisha na fursa mbalimbali za biashara, masoko, na uwekezaji zilizopo nchini pamoja na kurahisisha utoaji wa msaada wakati wa dharura zinazoweza kuwapata katika nchi wanazoishi.



Mhe. Balozi Kayola alitumia fursa hiyo pia kuwajulisha kuhusu hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa  na Mhe. Rais Dkt. Samia huku akitaja Miradi mikubwa inayokamilishwa ikiwemo Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Nyerere, Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR na miradi mingine kwenye sekta ya Kilimo, Biashara na Uwekezaji.



Vilevile, Mhe. Balozi Kayola aliwaeleza Diapora hao kuwa, Ubalozi upo tayari kushirikiana nao na kuwasisitiza kuwa huru katika kuwasilisha maoni, mapendekezo na ushauri kwa manufaa mapana ya Tanzania. 

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola akizungumza  na Mkuu wa Kitivo cha Elimu, Mawasiliano na masuala ya Habari wa Chuo Kikuu cha Biashara na Sayansi cha Malawi,  Dkt. Kizito Elijah alipokitembelea Chuo hicho kwa lengo la kujadiliana na Uongozi wa Chuo hicho kuhusu namna bora ya kuanzisha ushirikiano baina na taasisi za elimu za Tanzania hususani katika kufundisha Lugha ya Kiswahili.
Mkuu wa Kitivo cha Elimu, Mawasiliano na masuala ya Habari wa Chuo Kikuu cha Biashara na Sayansi cha Malawi,  Dkt. Kizito Elijah wakati wa mkutano kati yake na Balozi Kayola (hayupo pichani)
Mhe. Balozi Kayola akiagana na Dkt. Elijah mara baada ya kukamilisha mazungumzo baina yao 

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola akipata maelezo alipotembelea Kampuni ya Kitanzania ya Bakhresa iliyowekeza nchini Malawi tangu mwaka 2003 kwenye viwanda vya kutengeneza unga wa ngano na sabuni za kufulia.
Mhe. Balozi Kayola akiendelea kupata maelezo wakati wa ziara yake kwenye moja ya kiwanda cha Kamapuni ya Kitanzania ya Bakhresa ambayo imewekeza nchini Malawi

Mhe. Balozi Kayola akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Bakhresa Malawi Limited akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Mahesh Josyabhatla (wa pili kulia)
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola akizungumza na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Mkoa wa Kusini mwa Malawi alipowatembelea kwa ajili ya kujitambulisha ikiwa ni mara ya kwanza tangu ateuliwe kuiwakilisha Tanzania nchini humo
Sehemu ya Watanzania wanaoishi Mkoa wa Kusini, Malawi wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Balozi Kayola (hayupo pichani)

Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi Mkoa wa Kusini Malawi, Bw. Suleiman Marijani akizungumza wakati wa Mkutanoo kati ya Jumuiya hiyo na Balozi Kayola




 

RAIS SAMIA ASHIRIKI MAJADILIANO YA JUU YA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA USALAMA WA CHAKULA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifafanua jambo kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto na Rais wa Burundi Mhe. Evereste Ndayishimiye kushiriki Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha.

Mkutano huo wa ngazi ya juu wa majadiliano uliandaliwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiwa ni mkutano wa pembezoni kuelekea Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika terehe 24 Novemba 2023.

Majadiliano hayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo kuongeza Ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa usalama wa chakula na mazingira endelevu kwa Ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Mkutano huo wa Majadiliano ya Juu ulilenga kupata msimamo wa pamoja wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maalum kwa ajili ya Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mikataba wa Umoja wa Matanda kuhusu Mabadiliko Tabianchi (COP28) utakaofanyika kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Disemba 2020 mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu

Msimamo huo wa pamoja unatarajiwa kupitishwa katika Mkutano wa 23 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 24 Novemba 2023 jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifafanua jambo kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Balozi Dkt. Bernard Kibesse akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifurahia jambo na Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto alipowasili kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto akisisitiza jambo kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evereste Ndayishimiye na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akisisitiza akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha
Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula ukiendelea

Thursday, November 23, 2023

BALOZI NAIMI AWASILISHA HATI KWA RAIS WA AUSTRIA

 

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz (kulia) akiwasilisha  Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van Der Belen (kushoto) tarehe 21 Novemba, 2023


Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz (kulia) akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van Der Belen (kushoto) baada ya kuwasilisha  Hati za Utambulisho tarehe 21 Novemba, 2023

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz akikagua gwaride maalum alipowasili Ikulu jijini Vienna kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria tarehe 21 Novemba, 2023

 

 

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na Katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van Der Belen tarehe 21 Novemba, 2023.

Baada ya kuwasilisha Hati hizo za utambulisho Serikali ya Jamhuri ya Austria ilimuahidi ushirikiano Mhe. Balozi  Aziz kwa kipindi chote atakachohudumu katika kituo hicho na kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na hivyo kuendelea kuimarsiha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Austria.

Naye Mhe. Balozi Aziz alishukuru na kuahidi kushirikiana na Serikali ya Austria katika utekelezaji majukumu yake na kuhakikisha uhusiano kati ya Tanzania na Austria unafikia hatua za juu