Monday, January 5, 2015

MEMBE APONGEZA ANGLIKANA KUPINGA USHOGA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamillius Membe akizindua sherehe ya miaka 50 ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano, jijini Dar es salaam jana Jumapili, Januari 4, 2015, akishuhudiwa na  Dk. Valentine Mokiwa, Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam.
Waziri Membe akizungumza katika sherehe hiyo
Wachungaji wakimsikiliza Mheshimiwa Membe kwa makini wakati akiongea.
Masista nao wakifuatilia  
Askofu Mokiwa akitoa mahubiri katika ibada ya uzinduzi wa sherehe ya miaka 50 ya Diyosisi ya Dar es Salaam. .
Waziri Membe akisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakitolewa na Askofu Valentino


Mahubiri yakiendelea.
Mwimbishaji kwaya akiwaimbisha nyimbo wanakwaya waliovalia majoho ya rangi ya blue na nyeupe.
Mcheza kinanda akisindikiza kwaya ya kanisa






Waziri Membe akikaribishwa na Askofu Mokiwa kwaajili ya utoaji wa vitabu vya kuchangishia fedha kwa ajili ya miradi ya Dayosisi
Waziri Membe aliaanza kumkabidhi kitabu cha Harambee Askofu Mokiwa
Ibada ikiendelea.

Picha na Reginald Philip

======================================

MEMBE APONGEZA ANGLIKANA KUPINGA USHOGA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amelipongeza Kanisa la Anglikana Tanzania kwa kusimama kidete kupinga ndoa za jinsia moja, hata pale makanisa mengine ya Anglikana duniani yalipounga mkono suala hilo.
Akizindua sherehe za Miaka Hamsini tangu kuanzishwa kwa Dayosisi ya Dar es Salaam ya Kanisa hilo jana, Mhe. Membe alisema msimamo huo wa Kanisa na Watanzania uliipa serikali nguvu kukataa shinikizom kutoka nchi za Magharibi kwamba iidhinishe ushoga hapa nchini.
"Mlinitia nguvu sana pale niliposimama kidete kuwaambia rafiki zetu wa nje kuwa katika hilo la ndoa za jinsia moja, Tanzania tunaomba tukubaliane kutokukubaliana," alisema Mhe. Waziri, wakati wa uzinduzi huo uliofanyikia kwenye kanisa la Mtakatifu Albano, jijini Dar es Salaam. Sherehe za Miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es Salaam zitafikia kilele Julai, mwaka huu.
Mhe. Membe alisema serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la Anglikana na madhehebu mengine ya dini kuboresha maisha ya Watanzania. "Naomba muendelee kushirikiana na serikali katika kutoa huduma kwa wananchi," aliwaambia waumini na waalikwa wengine waliohudhuria misa maalum ya uzinduzi iliyoongozwa na Askofu Valentine Mokiwa.
Aliwataka viongozi wa dini kuombea nchi umoja na  amani, na kuhimiza waumini wao kushiriki kikamilifu katika matukio mawili muhimu yanayolikabili taifa mwaka huu -- Kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.
Uchaguzi wa Rais ni muhimu kwa sababu "Rais wa Awamu ya Tano atategemewa kuendeleza mema ya Awamu ya Nne na awamu zilizopita, na kutoa majawabu kwa changamoto za sasa na zijazo na kutusogeza karibu zaidi na Tanzania njema tunayoitamani, Tanzania yenye neema tele. Hatuko mbali na nchi yetu hiyo ya ahadi," alisema.

Mhe. Membe alishambulia rushwa na ifisadi kuwa ndivyo vinavyodidimiza nchi na kuongeza umasikini kwa wananchi licha ya Tanzania kuwa na rasilimali lukuki. "Tuchague viongozi waadilifu, wazalendo, wachapa kazi, wasio na uchu wa madaraka kwa ajili ya kujinufaisha wao binafsi na marafiki zao," alisema.
Alitaka vijana waandaliwe vyema kushiriki ujenzi na ulinzi wa taifa kwani ndio warithi. "Tukiwaandaa vyema,mustakabali wa taifa letu na watu wake utakuwa kwenye mikono salama. Tukishindwa leo, tutalia na kusaga meno kesho," alionya.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.