Wednesday, January 14, 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari



Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600
              

 

   20 KIVUKONI FRONT,
                 P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,  
                          Tanzania.

 




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) ameondoka nchini tarehe 14 Januari 2015 kwenda Urusi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Mhe. Sergey Lavrov.

Ziara hiyo ya kwanza ya kikazi ya Waziri Membe nchini Urusi, inalenga kwenye kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Urusi.

Akiwa nchini humo, Mhe. Membe anatarajiwa kutumia fursa hiyo kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na Urusi, hususan katika maeneo ya biashara, uwekezaji na ubadilishanaji wa teknolojia. 

Tanzania inaweza kufaidika na utaalamu wa Urusi katika sekta za uzalishaji wa nishati, uvuvi, afya, kilimo na huduma za jamii. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

14.01.2015

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.