Monday, July 22, 2013

Rais Kikwete aongoza Watanzania kuaga miili ya Askari 7 waliouawa nchini Sudan; Waziri Membe pia ahudhuria


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiweka saini kitabu cha maombolezi leo, mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisaini kitabu cha maombolezi mara baada ya kuwasili uwanjani hapo. 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezi.
 Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitafakari kwa kina tukio la mauaji wa Askari wa Tanzania lililotokea katika jimbo la Darfur nchini Sudan. Wengine katika picha ni Mhe. Shamsi Vuai Nahodha (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (wa tatu kushoto) Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na Luteni Jenerali Samwel Ndomba (wa nne kushoto), Mnadhimu Mkuu wa Majeshi nchini.

Mhe. Bernard K. Membe (Mb), (wa pili kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, naye alishiriki katika kuaga miili ya Askari 7 waliouawa nchini Sudan hivi karibuni. 

Mh. Waziri Membe akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa CCM, Mhe. Abdulrahman Kinana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said Meck Sadiki.

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, Mhe. Rais Kikwete akizungumza kwa masikitiko wakati wa kuaga miili ya Askari saba wa kulinda amani waliouawa na waasi katika jimbo la Darfur, nchini Sudan hivi karibuni.  Rais Kikwete amevitaka vikosi vya ulinzi nchini kutokata tamaa kutokana na maafa hayo bali wazidishe moyo na kuendelea kulitumikia kwa ufasaha Taifa lao. 

Miili ya Askari wa kulinda amani wa Tanzania waliouawa katika jimbo la Darfur nchini Sudan, ikiwasili kwenye Viwanja vya Diamond Jubilee tayari kwa kuagwa na wananchi, ndugu, jamaa na marafiki.

Simanzi na majonzi viliwatala kwa familia za Marehemu.

Mhe. Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa miili ya Marehemu.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kulia) na Mke wa Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (katikati), pamoja na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakiwa kwenye majonzi mazito mara baada ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu hao.

Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Davis Mwamunyange akitoa saluti za heshima za mwisho kwa Marehemu hao.

Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania,  Bw. Phillipe Poinso akitoa heshima za mwisho kwa Askari wa Tanzania wa kulinda amani waliouawa jimbo la Darfur nchini Sudan hivi karibuni.  Bw. Poinso alikuwa akimwakilisha Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou.

Umati wa Wanajeshi na Wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Diamond Jubilee leo kuaga miili ya Askari hao saba.


Picha zote na maelezo kwa hisani ya Zainul Mzige wa www.dewjiblog.com


Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza masuala mbalimbali katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na New Zealand alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Murray McCully tarehe 22 Julai 2013. Mhe. McCully na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 21  na 22 Julai, 2013.
Mhe. McCully nae akimweleza Mhe. Membe masuala ya msisitizo katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili ikiwemo ushirikiano katika masuala ya biashara na kilimo.

Mhe. Membe na wajumbe kutoka Tanzania na New Zealand wakimsikiliza Mhe. McCully.

Mhe. Membe  akimkabidhi Mhe. McCully zawadi ya kinyago mara baada ya mazungumzo yao.


Mhe. Membe akiagana na mgeni wake mara baada ya mazungumzo yao.

Sunday, July 21, 2013

Tanzania yadhamiria kushirikiana na New Zealand kukuza sekta ya kilimo



Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Mhe. Murray McCully amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 21- 22 Julai, 2013.

 Wakati wa ziara hiyo, Mhe. McCully atafanya mazungumzo na Viongozi wa Kitaifa wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb); Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb); Wazri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (Mb); na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. William Mgimwa (Mb). 

Mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita katika kuimarisha maeneo ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na New Zealand. Tanzania ina lenga kujifunza kutoka New Zealand kutokana na nchi hiyo kupata mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo hususan ufugaji na viwanda vya kusindika maziwa na mazao mengine.
Eneo lingine ambalo Tanzania inataka kushirikiana na New Zealand ni sekta ya nishati mbadala. Tanzania imedhamiria kukarabisha makampuni ya New Zealand kuwekeza nchini katika uzalishaji wa nishati ya nguvu ya jua na geothermal.

Kukaribishwa kwa makampuni hayo ni moja ya mikakati ya Serikali ya kufikia lengo lake la kuwapatia umeme asilimia 30 ya wananchi wa vijijini ifikapo mwaka 2015.

Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand atua nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili

Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Mhe. Murray McCully (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mberwa Kairuki wakati alipo wasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. McCully yupo nchini kwa ziara ya siku mbili ambapo atajadili na Viongozi wa Kitaifa wa Serikali namna ya kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na New Zealand.

Balozi Kairuki na Mhe. McCully wakielekea chumba maalum kwa ajili ya kufanya mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand (kushoto) akiwa katika maungumzo na Balozi Kairuki.

Saturday, July 20, 2013

Miili ya Askari waliofariki mjini Darfur yawasili nchini


Sehemu ya Masanduku yenye miili ya askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia hivi karibuni mjini Darfur nchini Sudan wakati wakilinda amani, yawasili nchini leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.  

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wanananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia mjini Darfur wakati wakilinda amani.  

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wanananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipakia moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia mjini Darfur wakati wakilinda amani.  

Askari hao waliuwawa kwa shambulio la kushtukiza na kundi la waasi wakati wakiwa kwenye kazi yao ya kulinda amani nchini Sudan.  

Jeshi la JWTZ lilioa taarifa likisema kuwa tukio hilo ni pigo kubwa kwa nchi yetu ya Tanzania ikiwa ni la kwanza kutokea tangu Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007.


Picha na maelezo kwa hisani ya www.issamichuzi.blogspot.com