Thursday, April 10, 2014

Mhe.Membe akutana na Gavana wa Jimbo la Maryland nchini Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Gavana wa Jimbo la Maryland la nchini Marekani, Mhe. Martin O'Malley walipokutana jijini Washington D.C kwa mazungumzo kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Jimbo hilo na Tanzania katika masuala ya uchumi, jamii na siasa. Mhe. Membe alipata fursa ya kukutana na Gavana huyo alipokuwa mjini humo kwa ajili ya kumwakilisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye upokeaji Tuzo ya Kiongozi mwenye Mchango Mkubwa zaidi katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa Mwaka 2013.
Mhe. Gavana O'Malley akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula
Mhe. Waziri Membe akitoa salamu maalum kwa wajumbe kabla ya mkutano kuanza. Pembeni ni Mhe. Gavana O'Malley.

Mhe. Membe akizungumza huku Gavana O'Malley akimsikiliza.
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo huku Mhe. Gavana O'Malley na wajumbe wengine wakimsikiliza.

Mhe. Gavana O'Malley akizungumza.
Balozi Mulamula akiwa na wajumbe wengine wakimsikiliza Gavana O'Malley (hayupo pichani)
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salvatory Rweyemamu akimsikiliza Gavana O'Malley (hayupo pichani). Wengine ni Balozi wa Nigeria nchini Marekani Prof. Adebowele Adufye pamoja na Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wajumbe wengine wakati wa mkutano kati ya Mhe. Membe na Gavana O'Malley (hawapo pichani). Kushoto ni Bw. Thobias Makoba, Katibu wa Waziri Membe na Bi. Redemptor Tibaigana, Afisa Mambo ya Nje.
Wajumbe wengine
Mhe. Membe akimweleza jambo Mhe. Gavana O'Malley mara baada ya mazungumzo yao.
Mhe. Membe akisalimiana na Bw. John Kennedy Opara, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mahujaji Wakiristo wa Nigeria ambaye pia ni Mshauri wa Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo kuhusu Uhusiano wa Kidini nchini Nigeria. Bw. Opara pia alipokea Tuzo ya Heshima siku hiyo.
Mhe. Gavana O'Malley katika picha ya pamoja na Bal. Mulamula
Mhe. Gavana O'Malley katika picha ya pamoja na Bi. Kasiga.
Mhe. Membe na Mhe. Gavana O'Malley katika picha ya pamoja na wajumbe wengine.

Viongozi wa CCM Tawi la DMV, Marekani wasalimiana na Mhe. Membe

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) (hawapo pichani), Tawi la DMV, Marekani waliofika kumsalimia katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Mhe. Membe alikuwa nchini humo kwa ajili ya kupokea Tuzo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mwenyekiti wa CCM, Tawi la DMV, Bw. George Sebo akitoa salamu za wanachama kwa Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mhe.Membe na wajumbe wengine waliokuwepo kwenye mkutano huo wakimsikiliza Bw. Sebo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Tawi la DMV Bi. Salma Moshi nae akieleza jambo wakati wa mkutano wao na Mhe. Membe (hayupo pichani)
Picha ya pamoja


Mhe. Membe azungumza na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili Ubalozi wa Tanzania mjini Washington D.C, Marekani kwa ajili ya kuzungumza na Wafanayakazi wa Ubalozi huo. Mhe. Membe alikuwa nchini Marekani kwa ajili ya kupokea Tuzo ya Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 kwa niaba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ametunukiwa Tuzo hiyo.
Mhe. Membe akisaini Kitabu cha Wageni Ubalozini Washington D.C huku Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula akishuhudia.
Mhe. Membe akizungumza na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani (hawapo pichani)
Mhe. Balozi Mulamula (kushoto) akiwa na Mkuu wa Utawala Ubalozini, Bibi. Lily Munanka (katikati) pamoja na Bi. Redemptor Tibaigana, Afisa Mambo ya Nje wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozugumza nao.
Wafanyakazi wengine wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakati wa mkutano na Mhe. Membe (hayupo pichani). Kutoka kushoto ni Bw. Suleiman Saleh, Bi. Mindi Kasiga na Bw. Abbas Misana.
Wafanyakazi wengine wa Ubalozi huo akiwemo Dkt. Mkama (kulia), Mama Kijuu (kushoto) wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao.

Waziri Bernard Membe aongelea swala la Uraia Pacha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb) akiongoza mazungumzo ya Raia Pacha alipokuwa akiongea na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bw. Idd Sandaly na katibu wake Amosi Cherehani ( Hawapo pichani) wakiwemo baadhi ya Maafisa Ubalozi na wanaDMV kwenye Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani siku ya Jumanne April,2014 alipo karibishwa chakula cha jioni Ubalozini hapo huku Naibu Spika Mhe. Job Ndungai akiongezea mawili matatu 

Waziri Membe akiongelea swala la Uraia Pacha kulia ni Naibu Spika Job Ndungai akifuatilia mazungumzo hayo

Kushoto ni Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Rais Idd Sandaly na Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakifuatilia mazungumzo

Kikao kikiendelea

Waziri Membe akutana na wafanyakazi wa Ubalozi Tanzania nchini Marekani


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe (Mb) akikaribishwa na balozi wa Tanzania nchin Marekani Balozi Mulamula. Membe yupo Marekani mjini washington DC, ambako atapokea Tuzo ya Africa's Most Impactful Leader of the Year kwaniaba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mindi Kasiga afisa Ubalozi wa Washington DC akiongea machache kuhusu ujio wa Mhe.Bernard Membe kabla ya Balozi ya Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberatta Mulamula kumtambulisha kwa wageni waalikwa walio jumuika na Waziri Bernard Membe kwenye chakula cha jioni na baadae kuongea Mhe. Membe kuongea machache na ujio wa safari yake

Waziri Bernard  Membe akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya watanzaniaDMV Rais Idd Sandaly

Waziri Membe akimtambulisha naibu spika Job Ndungai kwa maafisa wa Ubalozi wa Washington DC

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndungai akisalimiana na Bwana Mulamula
Picha ya Pamoja



Tuesday, April 8, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atapokea tuzo ya Africa’s Most Impactful Leader of the Year kwa niaba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania mjini Washington D.C, Marekani tarehe 09 Aprili, 2014.

Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Taasisi ya Uchapishaji ya African Leadership Magazine yenye makazi yake nchini Marekani kwa viongozi wa Afrika wanaofikia vigezo vilivyowekwa na Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia utawala bora, demokrasia na kuheshimu haki za binadamu kwa Mwaka 2013 inatolewa kwa Mhe. Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa Taasisi ya African Leadership Magazine, Tuzo hiyo inatolewa kwa Mhe. Rais Kikwete kutokana na namna ya pekee ya uongozi wake wenye matokeo yanayopimika kiutawala bora hususan kwa mwananchi wa kawaida wa Tanzania. Aidha, uongozi wake umeiletea Tanzania heshima kubwa kimataifa na kuiweka Tanzania kama chaguo muhimu kwa wawekezaji kutokana na ukuaji uchumi na maboresho ya sera.

Tuzo hiyo tayari imewahi kutolewa kwa Marais na Viongozi wengine mbalimbali wa Afrika wakiwemo Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa Liberia, Mhe. James Michel, Rais wa Shelisheli na Rais Mstaafu wa Ghana, Mhe. John Kuffor.

Ujumbe wa Mhe. Membe utamhusisha Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salvatory Rweyemamu, Waandishi wa Habari na Maafisa wa Serikali. Mhe. Membe atarejea nchini tarehe 11 Aprili, 2014.

 


Imetolewa na: KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

 

8 APRILI, 2014

Thursday, April 3, 2014

Tanzania na EU zasaini Mkataba wa Kubadilishana washitakiwa wa Uharamia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.  Bernard K. Membe (Mb) na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya wa Mambo ya Nje na Usalama, Bi. Catherine Ashton wakiweka saini  Mkataba wa Kubadilishana Maharamia wanaokamatwa Bahari Kuu. Mkataba huo ulisainiwa mjini Brussels, Ubelgiji hivi karibuni. Mhe. Membe amefuatana na  ujumbe wa Rais kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Ulaya na Afrika unaofanyika mjini Brussels.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Benard K. Membe (Mb.) na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya wa Mambo ya Nje  na Usalama, Bi. Catherine Ashton wakipeana mkono mara baada ya kusaini mkataba huo.

EU Tanzania signs Piracy Transfer Agreement


Signing Ceremony of the Agreement between the European Union and the United Republic of Tanzania on the conditions of transfer of suspected pirates and associated seized property from the European Union led naval force to the United Republic of Tanzania. The Government of Tanzania was represented by Honorable Bernard K.Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Cooperation and Ms. Catherine Ashton, First Vice President of the European Union represented the EU.

Monday, March 31, 2014

Tanzania: Sports Diplomacy Will Transform Local Athletes



TANZANIA has embarked on sport diplomacy to enable its athletes perform better and bring in medals from international events including the Commonwealth Games set for July, this year in Glasgow, Scotland.

The diplomacy which is meant to enhance capacity building amongst the sportsmen and women will include sending local athletes to other countries and learn new tactics and improve their performance.
Minister for Foreign Affairs and International Relations, Bernard Membe, said that at the moment the country does not have international standard facilities for training its athletes and this has prompted the government to seek assistance from advanced countries.
To start with, the government will send 50 athletes and about 16 coaches abroad to train. A total of ten athletes will train in Ethiopia, ten in New Zealand, ten in China and ten others in Turkey and the government will provide tickets and per diem allowances while the rest of the expenses will be covered by the host countries.
We applaud the government for coming up with this brilliant idea and as Minister Membe said, this is indeed good news for the country's ambitious plan to revive the ailing standard of sports.
Previously, our sportsmen and women were training on facilities that don't meet international standards and this led to their dismal performance in international competitions but now, the government is committed to bring to an end scenario of failure to win medals in big games.
Yes! The embarrassing failure has to end now and the country should retain its old lost glory, especially in such events as Commonwealth Games, where the country has a history of performing well.
Without our sportsmen and women winning in sports competitions, locally and internationally, Tanzania will not be able to make any diplomatic sports impact at home and abroad.
We should remember that sports diplomacy has helped a number of countries in the world in pushing forward their agendas, some of which had absolutely nothing to do with sports.
However, at this juncture, the major focus should remain on helping our athletes step up and improve their career and instil winning mentality. We always believe that good preparations will definitely pay off.

Wednesday, March 26, 2014

Mhe. Membe azungumzia miaka 50 ya Muungano na mafanikio ya Wizara

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe (Mb) akizungumza na Waandishi wa Habari, kuhusu Mafanikio ya Wizara kwa kipindi cha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964 katika nyanja mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi, ushiriki wa Tanzania kwenye harakati za ukombozi na utatuzi wa migogoro Barani Afrika na Diplomasia ya Michezo .
Waandishi wa Habari waliokuwepo wakati wa mkutano kati yao na Waziri Membe (hayupo pichani).
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa  wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (katikati) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga wakifuatilia mazungumzo ya Waziri Membe  na Waandishi wa Habari.
Waziri Membe (Mb) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) huku Naibu wake Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akisikiliza.
Mazungumzo yakiendelea.(Picha na Reginald Kisaka)




WIZARA IMEJIPANGA KUTEKELEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI: WAZIRI MEMBE

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa sasa imejipanga katika kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje inayoweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi hususan katika kukuza biashara, kuhamasisha uwekezaji na kuvutia watalii kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Hayo yalisemwa na Mhe. Bernard Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam alipozungumza na Waandishi wa Habari kuwaeleza mafanikio ya Wizara yake yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo maadhimisho yatafikia kilele tarehe 26 Aprili, 2014.

Mhe. Membe alisema kuwa mara baada ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 na kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 Sera ya Mambo ya Nje ilijikita katika masuala ya ulinzi na usalama na pia ukombozi wa Bara la Afrika, ambapo viongozi wengi kutoka nchi mbalimbali za Kusini mwa Afrika zikiwemo Namibia, Angola, Msumbiji na nyingine walitumia ardhi ya Tanzania katika kupigania uhuru wa mataifa yao.

Aliongeza kuwa, tangu kipindi hicho cha harakati za ukombozi hadi sasa Tanzania imeweka historia duniani katika utatuzi wa migogoro na ulinzi wa amani ambapo imekuwa mstari wa mbele kwenye kuchangia Vikosi vya kulinda amani katika nchi mbalimbali zinazokabiliwa na migogoro ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Comoro, Sudan (Darfur) na Lebanon.

“Katika kudumisha amani, vyombo vyetu vimevuka mipaka kisheria ili kuhakikisha amani inapatikana, hivyo ninatoa pongezi kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kazi nzuri ya ulinzi wa amani”, alisema Mhe. Membe.

Mhe. Membe aliongeza kuwa, kwa sasa Wizara inakwenda vizuri katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Idara na Taasisi nyingine imekuwa mstari wa mbele kutafuta wawekezaji na wafanyabiashara wenye vigezo na sifa ambao wana nia ya kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo gesi. “Wizara inajitahidi kwenda duniani kutafuta wawekezaji, kwani ni kipindi cha kufanya hivyo, na wale wenye sifa na vigezo tunavyovihitaji watachukuliwa”, alisisitiza Mhe. Membe.

Aidha, Mhe. Membe alieleza kuwa, kutokana na hali ya amani na utulivu hapa nchini pamoja na jitihada za Serikali katika kuimarisha Sekta ya Uchukuzi, Utalii utaendelea kuongezeka.

Katika hatua nyingine, Mhe. Membe alisema kwamba ili kukuza vipaji vya michezo kwa vijana hapa nchini,  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inahamasisha Diplomasia ya Michezo kwa kuzishirikisha nchi marafiki katika kuchangia sekta hiyo kiufundi, kitaaluma, vifaa na masuala mengine yanayohusu sekta hiyo.

Alifafanua kuwa, kwa sasa Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la sehemu za kufanyia mazoezi zenye hadhi ya kimataifa kwa ajili ya kuwawezesha wanamichezo kufanya mazoezi kabla ya kwenda kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa. 

Aidha, aliongeza kuwa kwa jitihada za Wizara nchi nne ambazo ni Uturuki, Ethiopia, China na New Zealand zimekubali kuwapokea wanamichezo 50 na Walimu wao kuanzia mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu kwa ajili ya kwenda kujifua tayari kwa kushiriki mashindano ya michezo ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Glasgow, Uingereza mwezi Jalai 2014.

“Kutokana na Tanzania kukosa viwanja vyenye hadhi ya kimataifa kwa ajili ya mazoezi na ili kuwawezesha vijana wetu kufanya vizuri michezoni, Wizara ilianza kutafuta maeneo nje ya nchi kwa ajili ya mazoezi ambapo tayari nchi za Ethiopia, New Zealand, China na Uturuki zimekubali tupeleke vijana 50 kwa ajili ya mazoezi, nchi tatu kati ya hizo zitapokea vijana kumi kila moja na China itapokea vijana 20”. Alisisitiza Mhe. Membe.

Mhe. Membe alieleza kuwa ana imani mkakati huu utasaidia Tanzania kuanza kupata medali na pia utaamsha ari ya vijana kupenda na kushiriki michezo kikamilifu.

Wakati wa mkutano huo, Mhe. Membe pia alitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ikiwemo Mgogoro wa Mpaka katika Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi ambapo alisema, baada ya kukutana na Jopo la Usuluhishi chini ya Rais Mstaafu wa Msumbiji, Mhe. Joachim Chissano hivi karibuni, nchi hizo mbili zimeachwa ziangalie faida na hasara za mpaka kupita katikati au pembezoni mwa Ziwa hilo. Hiki ni kikao cha kwanza cha usuluhishi ambapo pande mbili zilikutana ana kwa ana. Aidha, baada ya uchaguzi mkuu nchini Malawi mwezi Mei mwaka huu, kikao kingine kitapangwa.

Kuhusu uhusiano wa Tanzania na Rwanda, Mhe. Membe alisema kwamba Tanzania haina ugomvi na Rwanda na kwamba tatizo lililopo ni kutokuaminiana kunakotokana na mashitaka na madai ya uongo yanayotolewa na watu wasiozitakia mema nchi hizi. Hivyo alieleza kuwa Tanzania inaamini katika majadiliano ya amani na diplomasia ili kuweza kutatua tatizo hili.

Vile vile, Mhe. Membe alitumia fursa hiyo pia kuwaasa Watanzania wanaopata fursa ya kusafiri au kuishi nje ya nchi kujiepusha kufanya makosa ya jinai kwa kufuata sheria na taratibu za nchi wanazokwenda. Mhe. Membe aliyasema hayo kufuatia taarifa alizopokea wakati wa ziara yake nchini China hivi karibuni kuhusu vijana wadogo wa kike kutoka Tanzania wanajihusisha na biashara haramu ya ukahaba huko Guangzhou, China.

“Tuna Watanzania wapatao milioni tatu wanaoishi vizuri nje ya nchi, hata hivyo wapo wachache wanaofanya mambo mabaya kama ugaidi, ukahaba na biashara za madawa ya kulevya. Nawaomba sana Watanzania wanapokuwa nje waishi kulingana na sheria na taratibu za nchi hizo ili kujilindia heshima na utu na pia heshima ya nchi yetu”, alisisitiza Mhe. Membe.



-Mwisho-



Matukio mbalimbali ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani nchini

Ndege iliyombeba Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Frank-Walter Steinmeier ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Machi, 2014.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akimpokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Frank-Walter-Steinmeier alipowasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja nchini. Lengo la ziara ya Waziri Steinmeier lilikuwa ni kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani hususan katika nyanja za biashara na uwekezaji.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Frank-Walter-Steinmeier  akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. 
Mhe.Steinmeier akiongea na Wahadhiri, Wanafunzi, Mabalozi na watu mbalimbali ( hawapo pichani) kuhusu ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Ujerumani. Katika mjadala huo Mhe. Steinmeier aliipongeza Tanzania kwa kudumisha amani katika Ukanda wa Maziwa Makuu na Afrika kwa ujumla. Mhadhara huo ulifanyika katika Ukumbi wa Nkurumah chuoni hapo.
Waziri Membe pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mhe.Steinmeier ( hayupo pichani ).
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) naye akifuatilia kwa makini hotuba ya Mhe.Steinmeier ambaye hayupo pichani. 
Washiriki mbalimbali waliokuwepo wakati wa Mhadhara uliotolewa na Mhe.Steinmeier (hayupo pichani).  
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu ( kushoto) akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Bw. Reginald Mengi wakifuatilia kwa makini mhadhara uliokuwa ukitolewa na Mhe. Steinmeier ambaye hayupo pichani.
Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bw. Hans Koeppel (wa kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo (wa tatu kulia), Balozi  Dora Msechu, (watano kulia) pamoja na Washiriki wengine wakifuatilia Mhadhara uliokuwa ukitolewa na Mhe.Steinmeier (hayupo pichani)
Baadhi ya  Wajumbe waliofuatana na Mhe. Steinmeier (hayupo pichani) 
Picha ya Pamoja.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianio wa Kimataifa, Bw. John Haule akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Steinmeier.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) pamoja na Mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Steinmeier walipokuwa wakiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)  
Waziri Membe (Mb) akifafanulia jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Steinmeier. Wakati wa ziara hiyo Mhe Steinmeier alimkabidhi Waziri Nyalandu ndege ndogo kwa ajili ya kukabiliana na uwindaji haramu  wa wanyamapori.
Waziri Membe akiagana na Waziri Steinmeier mara baada ya kumaliza ziara yake nchini. 
Mhe. Steinmeier akiagana na Balozi Philip Marmo.
Mhe. Steinmeier akiagana na Balozi Msechu.
Mhe. Steinmeier akipunga mkono kuaga kabla ya kuondoka nchini.


Picha na Reginald Philip