Saturday, December 6, 2014
Friday, December 5, 2014
Press Release
Naibu Katibu Mkuu afungua Mkutano wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi za Maziwa Makuu
Sehemu ya Wajumbe wakimsikiliza Balozi Gamaha alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo. Wajumbe hao wanahusisha Maafisa kutoka nchi wananchi, Vyama vya Kiraia na Wafanyabiashara. |
Wajumbe wengine wakiwemo Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. |
Mkurugenzi wa Idara ya Demokrasia na Utawala Bora katika Sekretarieti ya Maziwa Makuu, Balozi Ambeyi Ligabo akizungumza wakati wa mkutano wa 6 wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi Wanachama wa Maziwa Makuu. |
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Peter Karasila nae akisema jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
Kaimu Mkuugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Innocent Shiyo akiwakaribisha Wajumbe kwenye mkutano |
Mkutano ukiendelea
Balozi Gamaha (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi za Maziwa Makuu................Matukio kabla ya mkutano |
Balozi Gamaha akisalimiana na Balozi Ligabo alipofika Wizarani kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 6 wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi za Maziwa Makuu. |
Balozi Gamaha akizungumza na Balozi Ligabo alipofika Wizarani |
Ujumbe uliofuatana na Balozi Ligabo walipofika Wizarani akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi za Maziwa Makuu, Bw. Peter Karasila (mwenye tai nyekundu) |
Thursday, December 4, 2014
Hon. Membe, Kinana on special mission over South Sudan
Membe, Kinana on special mission over South Sudan
Sudan and Kenya have endorsed Tanzania’s efforts to reunite factions of the Sudan People’s Liberation Movement (SPLM), whose antagonism is central to the civil war in South Sudan.
Presidents Omar Al-Bashir and Uhuru Kenyatta said separatey during meetings with Special envoys of President Kikwete-- the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Hon. Bernard Membe, and CCM Secretary General Abdulrahman Kinana, that the CCM-brokered mediation in Arusha had great potential to resolve the South Sudan crisis.
“It will be a difficult process, but if Arusha does not succeed there may be no peace in South Sudan,” declared President Al-Bashir, when the Special envoys called on him at the State House in Khartoum on Tuesday evening.
But the two leaders emphasized that the Arusha dialogue should be complementary to the South Sudan peace talks being conducted by the Inter-Governmental Authority for Development (IGAD).
Hon. Membe and the CCM Secretary General are on a mission to reassure IGAD leaders that the Arusha initiative, which was requested by South Sudan President Salva Kiir last September, is not in conflict with the separate peace negotiations in Addis Ababa spearheaded by the regional grouping.
Mr. Kinana reassured the Sudan and Kenya leaders that the Arusha mediation conducted October 12-20 and set to resume next week, was not competing against the IGAD process.
Hon. Membe told reporters in Khartoum that while the peace talks under IGAD conducted at the AU Headquarters in Addis Ababa involved 10 parties to the conflict in South Sudan, Arusha was focused on the SPLM factions led by President Kiir, his fired deputy Riek Machar and Ex-detainees. The bloody conflict has seen thousands of people killed and hundreds others displaced.
During the meeting with President Kenyatta at the State House in Nairobi yesterday, the Kenyan leader told the Special Envoys that the warring parties in South Sudan must not take advantage of the new initiative in Arusha to ignore the decisions reached at IGAD.
One of the decisions is that the killing of civilians should stop immediately. “They must not hide under the Arusha dialogue and continue the killings,” President Kenyatta warned.
The two leaders agreed that CCM could use its experience spanning over 50 years to reconcile the warring factions in SPLM, seen as the core of the conflict in Juba. Tanzania hosted the liberation movements of Angola, Mozambique, Namibia, Zimbabwe and South Africa.
The Special Envoys yesterday held talks with South Sudan President Kiir in Juba. The President reaffirmed his commitment to the dialogue in Arusha and assured CCM and the Tanzania government that he will respect and fully implement the decisions to be taken.
The Special Envoys are scheduled to wind up their mission today after consulting Uganda President Yoweri Museveni in Entebbe.
Ends
Wednesday, December 3, 2014
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar afanya ziara nchini Comoro
Mhe. Hamad akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Silima Haji |
Monday, December 1, 2014
Waziri wa Mambo ya Nje amuaga Balozi wa Australia
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akizungumza na Balozi wa Australia ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.
Picha na Reginald Philip
==========================================
Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo ameagana na Mhe.Geoffrey Tooth Balozi wa Australia nchini Tanzania ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini. Katika mazungumzo yao. Waziri Membe alimueleza Balozi Tooth kuwa wakati wa kipindi chake cha uwakilishi, uhusiano baina ya nchi hizi mbili umeimarika. Mhe. Membe pia amemshukuiru Balozi Tooth kwa ushirikiano mzuri alioutoa katika kipindi chote na kusisitiza kuwa Tanzania ni nyumbani kwake sasa na asisite kurudi nchini kutembea au kwa mapumziko mara apatapo fursa ya kufanya hivyo.
Kwa upande wake, Balozi Tooth ambaye amekuwa akiiwakilisha nchi yake hapa Tanzania kutokea Nairobi Kenya, kuanzia Desemba 2010 amemshukuru Mhe. Membe, uongozi wa Wizara na wafanyakazi wote kwa ushirikiano mzuri alioupata wakati wote. Alisifu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuleta maendeleo na kukuza mahusiano baina ya Tanzania na nchi nyingine.
Balozi Tooth aliyeongozana na Bi. Freya Carlton, Katibu wa Tatu wa Ubalozi huo, anatarajiwa kuondoka nchini wiki hii kurejea Australia ambapo atakuwa mshauri wa Serikali kwenye masuala ya mazingira na mabadiliko wa tabia nchi.
|
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 3 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3
tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana
Novemba 29, 2014
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais
wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi
wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika
kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati
wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
wengine walioshiriki katika mkutano huo.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa
Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa
KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika
jijini Nairobi, Kenya jana Novemba 29, 2014.
(Picha na OMR)
==========================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Novemba 29, 2014 aliiwakilisha Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo, kwa mujibu wa utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unafanyika kila baada ya miaka miwili na lengo lake kuu ni kufanya tathmini juu ya miradi ya miundombinu inayoshirikisha nchi washirika, sambamba na kutazama fursa ya kutanua miundombinu mipya katika nchi hizi kwa lengo la kukuza uchumi wa pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki.
Tathmini hii ya Miundombinu inafanyika kwa kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora katika nchi hizi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi, sambamba na kutanua mtengamano wa nchi hizi na hivyo kuwafanya wananchi wanaoishi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuzidi kuwa wamoja.
Mkutano wa jana uliongozwa na Kaimu Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, Waziri Mkuu wa Rwanda pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda. Viongozi wengine waliopata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Mheshimiwa Balozi Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri wa Wizara hiyo kutoka Tanzania, Mheshimkiwa Samwel Sitta, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Donald Kaberuka, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika, Bwana Makhtar Diop, Katibu Mtendaji wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi na Baalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Balozi Filiberto Sebregondi. Pia mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa nchi za China, Marekani, Japan na nyinginezo ambazo ni wadau wakubwa wa ujenzi wa miundombinu katika nchi za Afrika Mashariki.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Kaimu Rais wa Kenya, William Ruto alifafanua juu ya umuhimu wa kuhakikisha Afrika Mashariki inaunganishwa kwa miundombinu imara ili kukuza uchumi na akapongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kufanikisha azma hiyo huku pia akiomba nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuendelea kuungana katika kutekeleza miradi ya miundombinu na kujitahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
Mkutano huu pia uliambatana na kupokea ripoti ya utekelezaji wa maagizo ya Wakuu wa Nchi za EAC kuhusu Miundombinu kutoka kwa Mawaziri wa Nchi za Jumuiya. Wakuu wa Nchi katika Mkutano huu walipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo waliyoyatoa katika mkutano wa pili uliofanyika mwezi Novemba, 2012 na kuidhinisha miradi 72 ya miundombinu ya kipaumbele ya Barabara, Reli, Nishati na Bandari.
Kwa upande wa utekelezaji; miradi 16 imekamilika, 39 inaendelea kutekelezwa na 17 ipo katika hatua za awali za kutafutiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake.
Kwa upande wa Tanzania miradi minne imekamilika ambayo ni Umeme katika mji wa Kibondo, mradi wa barabara ya Mbezi-Shule-Tangibovu-Makutano ya Nelson Mandela na barabara ya Tabata. Barabara nyingine iliyokamilika ni Nyangunge – Musoma – Sirari na sehemu ya Simiyu - Musoma inayounganisha Kenya na Tanzania huko ujenzi unaendelea.
Akizungumza katika Mkutano huo Makamu wa Rais amezitaka nchi wanachama kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Miundombinu ili kusaidia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja, ambayo inalenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria. “Tusiishie kubakiza mipango hii katika karatasi, tusiishie kuzungumza tu bali huu ni wakati wa kuhakikisha tunarahisisha ufanyaji biashara katika nchi zetu na kupunguza vikwazo visivyo vya lazima,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais pia aliambatana na Mheshimiwa Dkt. Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui. Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake tayari wamerejea nyumbani Tanzania ambapo kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, maadhimisho yanayofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Novemba 30, 2014
|
Konseli Mkuu wa Tanzania Dubai afanya mazungumzo na Konseli Mkuu wa Saudi Arabia Dubai
Konseli Mkuu wa Tanzania, Dubai, Bw. Omar Mjenga amekutana na Konseli Mkuu wa Saudi Arabia, Dubai, ambaye pia ndio Mkuu wa Makonseli Wakuu waliopo Dubai (Dean of Diplomatic Corps), Bw. Emad A. Madani katika ofisi za Koseli Kuu wa Saudi Arabia. |
Konseli Mkuu Bw. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Konseli Mkuu wa Saudi Arabia Dubai Bw. Bw. Emad A. Madani Konseli Mkuu wa Tanzania, Dubai, Bw. Omar Mjenga amekutana na Konseli Mkuu wa Saudi Arabia, Dubai, ambaye pia ndio Mkuu Makonseli Wakuu waliopo Dubai (Dean of Diplomatic Corps), Mhe. Emad A. Madani katika ofisi za Koseli Kuu ya Saudi Arabia.
Bw. Mjenga alienda kumtembelea ili kuomba ushiriki wake pamoja na Makonseli Wakuu wote kwenye kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya Utalii nchini Tanzania, litakalofanyika tarehe 17 Disemba 2014.
Bw. Emad Madani amesema atashiriki vikamlifu kwenye kongamano hilo huku akisema kuwa Tanzania na Saudi Arabia ni nchi rafiki wa siku nyingi, na hivyo basi wapo tayari kuomba taasisi ya utalii ya Saudi Arabia kushiriki pia.
Aliahidi kuwaomba Makonseli Wakuu wote washiriki.
Kongamano hilo limeandaliwa na Koseli Kuu ya Tanzania uliopo Dubai kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
|
Wednesday, November 26, 2014
Watanzania kupata punguzo la asilimia 40 kwa matibabu katika Hospitali ya Irani iliyoko Dubai
Konseli Mkuu, Bw. Omar Mjenga wa Konseli Kuu ya Dubai kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Irani iliyopo Dubai (Iranian Hospital Dubai), wakiweka saini makubaliano ya pamoja ambayo yatatoa punguzo la asilimia 40 ya matibabu kwa Mtanzania yeyote yule atakayetibiwa katika hospitali hiyo. Makubaliano hayo yamewekwa saini katika hospitali ya Irani iliyopo Dubai, maeneo ya Jumeirah. |
Konseli Mkuu Omar Mjenga wa Tanzania, Dubai pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Irani, Dubai wakionyesha makubaliano mara baada ya kumaliza kutiliana saini. |
Tuesday, November 25, 2014
Rais Kikwete apokea salamu za kheri toka kwa Rais Obama
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula akiwasilisha kwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete salamu za kumtakia afya njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. |
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Washington DC uliomtembelea kumjulia hali na kuwasilisha salamu maalumu za pole za Rais Barack Obama jijini Baltimore, Maryland. |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafosa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri ya afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafosa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri ya afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. |
Rais Prof. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula na Maafisa Waandamizi wa Ubalozi Tanzania, nchini Marekani (Picha na Freddy Maro) |
Friday, November 21, 2014
Waziri Membe azindua Chama cha Urafiki wa Tanzania na China
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba ya uzinduzi wa Chama cha Urafiki wa Tanzania na China. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika Jijini Dar es Salaam na kuhuduhuriwa na Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim, Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Yongqing na Viongozi wengine. |
Mhe. Membe akihutubia. |
Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Yongqing akihutubia wakati wa hafla hiyo. |
Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Salim nae akizungumza wakati wa hafla hiyo |
Mhe. Membe kwa kushirikiana na Balozi Lu Yongqing wakizindua Chama hicho kwa mara nyingine. |
Waziri Membe, Balozi Lu na Dkt. Salim pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo. |
Waziri Membe pamoja na Wageni waalikwa wakiinua glasi juu kutakiana heri |
Waziri Membe akijadiliana jambo na Dkt. Salim |
Hafla ikiendelea |
Subscribe to:
Posts (Atom)