Wednesday, August 12, 2015

Simple Hope Foundation wamtembelea Balozi Mulamula Wizara ya Mambo ya Nje

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Bi. Pamela A. Schwalbach, mmoja wa waanzilishi wa Shirika la (Simple Hope East Africa) linalo fanya kazi za kijamii na  wakina mama wa Kabila la Hadzabe, Mkoani Manyara.  
Bi. Pamela (katikati) na Bi Karen J. Puhl (Kushoto)  wakiwa kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu Mambo ya Nje ambapo alipata wasaa wa kupokea taarifa ya kazi za shirika hilo lisilo la kiserikali la Marekani, Jimbo la Wisconsin. 
Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Bi. Pamela A. Schwalbach (wa pili kushoto), Bi. Karen J. Puhl (wa pili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje Bi. Felista Rugambwa (wa kwanza kushoto)



Picha na Reginald Philip

Tuesday, August 11, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UTEUZI NA UHAMISHO WA MABALOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:

(i)   Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).
(ii) Balozi Wilson Masilingi aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini Mexico
(iii)                Balozi Irene Kasyanju aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na uhamisho huu unaanzia tarehe 07 Agosti, 2015.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


11 Agosti, 2015

Monday, August 10, 2015

Katibu Mkuu amuaga rasmi Balozi wa Finland aliyemaliza muda wa kazi nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Libarata Mulamula akizungumza mbele ya Mabalozi na Wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga rasmi Balozi wa Finland aliyemaliza muda wa kazi nchini, Mhe. Sinikka Antila. Katika hotuba yake Balozi Mulamula alimshukuru Balozi Antila kwa mchango wake wa  kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Finland. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Balozi Mulamula akiendelea kuzungumza.
Balozi Antila (Wa kwanza Kulia), Balozi wa Demokrasia ya Kongo nchini Balozi Juma Mpango (Wa pili Kutoka kulia), Balozi wa Uingereza Mhe. Dianna Melrose (Wa tatu kutoka kulia), Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Segore Kayihura (Wa tatu kutoka kushoto), Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Egon Kochanke (Wa pili kutoka kulia) na Balozi wa Canada nchini Mhe. Alexandre Leveque wakimsikiliza Balozi Mulamula hayupo pichani 
Sehemu ya Wageni walioudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani).
Balozi Antila akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo aliishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chote alichokuwepo nchini.
Katibu Mkuu Mhe. Balozi Mulamula (Wa kwanza kushoto) kwa pamoja na, Mkurugenzi Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine (Wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregond (Wa pili kutoka kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bwa. Alvaro Rodriguez  wakimsikiliza Balozi Antila (hayupo pichani).
Balozi Antila akiendelea Kuzungumza
Balozi Mulamula na Balozi Antila wakitakiana afya njema kwa kugonganisha Glasi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga ambaye alikuwa mshereheshaji wakati wa hafla hiyo akizungumza.
Balozi Mulamula akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlango wa Zenji Balozi Antila.
Wageni waliohudhuria Hafla hiyo wakifurahia kwa kupiga makofi wakati Balozi Mulamula akimkabidhi Balozi Antila zawadi ya picha (Hawapo pichani).  
Balozi Mulamula (Wa pili kulia), Balozi Mpango (Wa kwanza kushoto), Balozi Antila (Wa pili kutoka kushoto), na Balozi Sokoine wakiwa katika picha ya pamoja.
Balozi Mulamula na Balozi Antila wakiwa katika Picha ya Pamoja na wageni walioudhuria hafla hiyo.

Picha na Reginald Philip

Mkurugenzi wa Ushirikano wa Kimataifa awashauri vijana kufanya kazi na Mashirika ya Kimataifa

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akitoa mada katika  Kongamano la Vijana. Wakati wa kongamano hilo Balozi Mushy amewashauri vijana kufanya kazi na Taasisi za Umoja wa Mataifa ili kujipatia uzoefu wa kujielezea ikiwa ni pamoja na kujiamini. Kongamano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania Dkt. Natalia Kanem (Wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (wa kwanza kulia) wakimsikiliza Balozi Mushy (Hayupo pichani) wakati akiwasilisha Mada.
Juu na Chini ni picha ya Vijana waliohudhuria Kongamano hilo wakimsikiliza Balozi Mushy (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada.
Balozi Mushy akimwelezea jambo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi katika Kongamano la Vijana
Balozi Mushy (Katikati mwenye suti nyeusi) alipokuwa akiwasilisha mada ambapo pia alitaka kujua ni vijana wangapi wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2015, huku ikionekana idadi kubwa ya vijana waliohudhuria Kongamano hilo wamejiandikisha

Picha na Reginald Philip 

Friday, August 7, 2015

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika akutana na Ujumbe wa EU nchini

Mkurugenzi Idara ya  Ulaya na Amerika katika Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine akimsikiliza Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Egon Kochanke alipokuwa akiongea kwa niaba ya Mabalozi wa Umoja wa  Ulaya (EU) walipokutana kwa mazungumzo Wizarani hivi karibuni.
Sehemu ya Ujumbe huo kutoka Umoja wa Ulaya hapa wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Sokoine na Balozi Kochanke
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda,  Bw. Innocent Shio (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Bi. Grace Martin, na Bi. Shamim Khalfan, Maafisa Mambo ya Nje (kulia) wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Balozi Sokoine na Balozi Kochanke (hawapo pichani).
Afisa Mambo ya Nje, Bi Felista Rugambwa (wa kwanza kushoto) akinukuu mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kwenye Mkutano huo.
Mkutano ukiendelea


Picha na Reginald Philip.

Wednesday, August 5, 2015

Waziri Membe amuaga rasmi Balozi wa Hispania aliyemaliza muda wa kazi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza mbele ya Mabalazi na Wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga rasmi Balozi wa Hispania aliyemaliza muda wa kazi nchini, Mhe. Luis Manuel Cuesta Civis.  Katika hotuba yake Mhe. Membe alimshukuru Balozi Luis kwa mchango wake wa  kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Hispania. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Agosti, 2015.
Balozi Luis (kulia) kwa pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye pia ni Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe. Juma Halfan Mpango (wa pili kulia), Balozi wa Zimbabwe na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kushoto) wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Balozi Luis akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo pamoja na mambo mengine aliishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiririkiano wa Kimataifa na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano aliopata katika kipindi chote alichokuwepo nchini.
Sehemu ya Mabalozi na wagenui waalikwa wakimsikiliza Balozi Luis (hayupo pichani)
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine akizungumza machache wakati wa hafla hiyo
Mhe. Waziri Membe kwa pamoja na Mhe. Balozi Luis, Mabalozi na wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Sokoine ambaye haonekani pichani
Bi. Kasiga ambaye alikuwa mshereheshaji wakati wa hafla hiyo akizungumza
Balozi Luis akimweleza jambo Waziri Membe
Maafisa Mambo ya Nje walioshiriki hafla hiyo. Kushoto ni Bi. Olivia Maboko na Bi. Tunsume Mwangolombe

Mhe. Membe na Mhe. Luis wakitakiana afya njema
Mhe. Membe akimkabidhi zawadi Balozi Luis
Waziri Membe akizungumza na Balozi Luis
Waziri Membe akiagana na Balozi Luis mara baada ya hafla hiyo
Balozi Luis akiagana na Balozi Sokoin
Picha ya pamoja

Friday, July 31, 2015

Marais wastaafu wajadili uongozi wa Afrika

Rais Yoweri Museveni na Mhe. Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa wakiwa na baadhi ya  marais wastaafu wa Afrika waliohudhuria mkutano huo akiwemo Mhe. Festus Mogae (wa kwanza kushoto), Rais Mstaafu wa Botswana, Mhe, Olusegun Obasanjo (wa pili kushoto), Rais Mstaafu wa Nigeria,  Mhe. Jerry Rawlings (wa tatu kutoka kulia), Rais Mstaafu wa Ghana, Mhe. Bakili Muluzi (wa pili kulia), Rais mstaafu wa Malawi na Mhe. Hifikepunye Pohamba (wa kwanza kulia), Rais Mstaafu wa Namibia
===========================================
MARAIS WASTAAFU WAJADILI UONGOZI WA AFRIKA

Marais wastaafu wa nchi sita za Afrika wamekutana Jijini Dar es Salaam jana kutafakari mustakabali wa Bara lao wakizingatia mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia ulimwenguni. Mjadala huo ulioitishwa na Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Benjamin Mkapa, ulifunguliwa rasmi na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni.

Ulihudhuriwa na Marais Wastaafu wa Nigeria, Mhe. Olusegun Obasanjo, Ghana, Mhe Jerry Rawlings, Malawi, Mhe. Bakili Muluzi; Botswana, Mhe. Festus Mogae, na Namibia, Mhe. Hifikepunye Pohamba.

Marais wastaafu pamoja na wanazuoni na watu mashuhuri wa Afrika walisisitiza muhimu wa kujenga mtangamano wa bara hilo ili kuleta maendeleo ya haraka ya kiuchumi. Washiriki walikubaliana kuwa juhudi za pamoja zifanywe kudhibiti vikwazo dhidi ya mtangamano, ikiwa ni pamoja na historia ya tawala tofauti za kikoloni; elimu na teknolojia duni, na ukosefu wa utashi wa kisiasa.

Pamoja na kusifia hatua zilizofikiwa kuboresha demokrasia barani Afrika, washiriki walisema maendeleo ya uchumi yanahitaji kasi kubwa zaidi ili wananchi wafaidike na rasilimali nyingi zilizopo.

Uongozi wa nchi za Afrika ulikosolewa kwa kushindwa kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya kiuchumi na kuzembea utekelezaji wa maamuzi yanayochukuliwa kwenye majukwaa mbalimbali ya pamoja, kama vile Umoja wa Afrika na Jumuiya za Maendeleo za kikanda.

Ilishauriwa jumuiya za kikanda ziimarishwe kwa kutengewa rasilimali za kutosha na kupewa uwezo zaidi wa kufanya maamuzi ili ziwe misingi ya kujenga umoja wa kiuchumi.

Washiriki walisifia Mpango Mkakati wa Umoja wa Afrika wa kulifanya bara hilo liongoze  duniani kiuchumi na kiteknolojia ifikapo mwaka 2063, lakini wakasisitiza uwekwe mpango madhubuti wa utekelezaji ili kufikia azma hiyo.

Katika hotuba yake, Rais Museveni alisema Afrika inayo misingi imara ya umoja. Alitupilia mbali madai kuwa bara hilo lina mgawanyiko mkubwa wa kijamii. "Bara hili lina makundi manne tu ya kilugha," alisema.
Kiongozi huyo wa Afrika Mashariki alihimiza juhudi zaidi kuleta mtangamano wa kiuchumi na kisiasa Afrika. "Lazima tujenge mtangamano wa kiuchumi. Pale inapowezekana, tuungane kisiasa pia."

Alisema Afrika ilitawaliwa na wakoloni kwa sababu haikuwa na mtangamano, kitu kinacholifanya bara hilo liendelee kubaki nyuma kimaendeleo. Alitaka hatua za pamoja zichukuliwe kuendeleza viwanda na maliasili za Afrika, ikiwapo madini, mafuta na gesi.
Jana usiku, Mhe. Mkapa aliwaandalia wageni wake hafla ya  chakula cha jioni ambapo pia Jukwaa la Uongozi Afrika lilikabidhi zawadi kwa washidi wa shindano la kuandika insha lililoshirikisha vijana 522 kutoka nchi 11 za bara hilo.

Mshindi wa kwanza ni Munyaradzi Shifetete kutoka Zimbabwe, ambaye alikabidhiwa cheti na fedha taslim. Wengine waliokabidhiwa zawadi na Rais Mstaafu wa Botswana, Mhe. Mogae, ni Vicky Mbabaazi kutoka Uganda, Sholopelo Sholopelo kutoka Botswana, Joseph Wanga kutoka Kenya na Omolo Juema kutoka Uganda

(mwisho)

Press Release

H.E Simonetta Sommaruga, President of Switzerland

 PRESS RELEASE 

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Simonetta Sommaruga, President of the Swiss Confederation on the occasion of the National Day of Switzerland on 1st August, 2015.

The message reads as follows;

“H.E. Simonetta Sommaruga,
President of the Swiss Confederation,
Bern,

SWITZERLAND


Your Excellency,

It is my pleasure and privilege to extend to you, my heartfelt congratulations on the occasion of your country’s National Day. As you celebrate this important occasion, allow me to take this opportunity to express my gratitude on the good relations that exist between our two countries and peoples.

The Government of Tanzania highly values the existing ties and is ready to work with the Government of Switzerland in deepening the friendship between our two countries and strengthening collaboration in bilateral and multilateral frameworks.
        Please accept, Your Excellency, my best wishes for your personal good health and continued peace and prosperity for the people of Switzerland”.

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

31st July 2015

Kaimu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya  Simba akimkaribisha Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Lawrence Tax alipotembelea Wizarani na kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo uanachama wa Tanzania kwenye Jumuiya hiyo.
Balozi Simba akizungumza na Dkt. Tax
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Bw. Innocent Shiyo (Kushoto) na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Upendo Mwasha kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo yaliyo kuwa yakiendelea kati ya Balozi Simba na Dkt. Tax (Hawapo pichani).
Mkutano ukiendelea
Naibu Katibu Mkuu Balozi Simba (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)



Picha na Reginald Philip