Thursday, February 15, 2018
Wednesday, February 14, 2018
Wabunge wa EALA wafanya Ziara Nchi za Afrika Mashariki
Wabunge wa EALA wafanya ziara Nchi za Afrika Mashariki
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) wanafanya ziara ya siku 12 kwa ajili ya kupitia na kuangalia maendeleo na changamoto mbalimbali za Mtangamano pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia vyombo vya habari.
Ziara hiyo ilianza tarehe 12- 23 Februari,2018, katika ziara hiyo waheshimiwa Wabunge wamegawanyika katika makundi mawili, kundi la kwanza linafanya ziara katika ukanda wa kati ( Cetral Corridor) , ziara hii itahusisha Zanzibar na Mikoa ya Dar es salaam, Kilimanjaro, Pwani, Arusha, Dodoma, Shinyanga na Kagera, kundi la pili watatembelea ukanda wa Kaskazini ( North Corridor) ziara hiyo itaanzia Kenya, Uganda na kumalizikia Rwanda ambapo ndipo wanapotarajia kukutana kwa kwa ajili ya kikao cha wiki mbili kwa ajili ya majumuisho ya ziara.
Waheshimiwa Wabunge wanaotemebelea Ukanda wa Kati walianzia safari yao Zanzibar ambapo walifanya ziara katika Bandari ya Zanzibar na pia kufanya mazungumzo na Uongozi wa Taasisi ya Kiswahili Kamisheni. Aidha, wakiwa Dar es salaam walipata fursa ya kutembelea Bandari ya Dar es salaam na kukutana na viongozi wa Bandari pamoja na wadau mbalimbali wanaotumia bandari. Akiongea katika mkutano huo Kaimu Meneja wa Bandari Bw. Feddy Liundi, alisema hadi sasa kuna mafanikio makubwa sana katika Bandari ya Dar es Salaam kwani bandari hiyo inahudumia zaidi ya nchi nane na kati ya hizo Rwanda na Malawi wanaongoza kwa matumizi ya bandari ya Dar es salaam.
Kwa upande wao Waheshiwa walisifia maboresho ya bandari na kusema ndio yamechangia bandari hii kuwa kinara na kivutio kwa wasafirishaji wa mizigo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Waheshimiwa Wabunge pia walipata nafasi ya kutembelea eneo la mradi wa maboresho ya bandari ya Dar es salaam wa Dar es salaam Maritime Gateaway Project (PMGP) pamoja na kitengo cha Kontena cha TICTS.
Waheshimiwa wabunge walipongeza uongozi wa bandari kwa maboresho makubwa yaliyofanyika na kuahidi kufanyia kazi changamoto zote zilizoainishwa ambazo ni za Kimtangamano. Jumla ya Waheshimiwa Wabunge 21 kutoka nchi sita (6) za Jumuiya Ya Afrika Mashariki wanashiriki katika ziara hii kwa upande wa Ukanda wa kati(Cetral corridol).
========================================================================
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ( EALA) wakiwa katika Mkutano na Uongozi wa Bandari ya Dar es salaam, kutoka kushoto ni Mhe.Maryam Ussi (Tanzania), Mhe. Wanjiku Muhia (Kenya) (ambaye pia ni kiongozi wa Msafara katika ziara hii) na wa mwisho kulia ni Kaimu Meneja wa bandariBw. Freddy Liundi, wakiwa katika Mkutano. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Bandari, tarehe 13 Februari,2018.
Mhe. Josephine Lemoyan (Tanzania) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya mkutano, wanaofuatilia ni Mhe. Wanjiku (kushoto), na Mhe. Musamali Paul Mwasa (Uganda)
Waheshimiwa Wabunge na wadau wengine wakiwa katika Mkutano huo
Wadau mbalimbali wakifuatilia Mkutano huo
Waheshimiwa Wabunge, wafanyakazi wa bandari pamoja na wadau wengine wakiwa katika picha ya pamoja.
Tuesday, February 13, 2018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI -Tanzania Mwenyeji wa Mkutano wa Baraza la Wakimbizi Duniani
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika kikao cha Baraza la Wakimbizi Duniani kinachofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - Fursa za Ufadhili wa Masomo kwa Watanzania na Tuzo ya Utalii kwa Tanzania
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki Profesa Adolph Mkenda |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
FURSA
ZA UFADHILI WA MASOMO KWA WATANZANIA NA TUZO YA UTALII KWA TANZANIA
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki mapema mwezi Februari imepokea fursa za
ufadhili wa masomo ya muda mfupi na muda mrefu katika kada mbalimbali kutoka
Serikali ya Jamhuri ya Korea, Serikali ya Misri na Malaysia.
Kwa upande wa ufadhili wa
masomo ya muda mfupi, Serikali ya Korea imetoa nafasi nne (4) kwa ajili ya
Watumishi wa Umma katika Sekta ya Afya. Nafasi hizo ni kwa ajili ya Mafunzo ya
Uganga (Clinical Experts) nafasi mbili (2), Utawala katika masuala ya Afya
(Health Administrator) nafasi moja (1)
na Afisa Mwandamizi katika masuala ya Afya nafasi moja (1).
Mafunzo hayo ambayo yanafadhiliwa
na Korea Foundation for International
Healthcare yapo chini ya program ya “Dr. Lee Jong-wook fellowship program”
kwa mwaka 2018. Maombi ya nafasi hizo yaelekezwe Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambao ni waratibu wakuu katika sekta ya afya.
Kutoka Serikali ya Misri,
Wizara imepokea nafasi mbili (2) za mafunzo ya muda mfupi kwa Watangazaji
kutoka nchi za Afrika “19th Basic Training Course for the African
Broadcasters”. Mafunzo yatafanyika Misri kuanzia tarehe 25 Februari, 2018 hadi
25 Machi, 2018. Mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo.
Halikadhalika, Wizara
imepokea nafasi mbili (2) za Mafunzo ya muda mfupi katika Teknolojia ya
Uchakataji Madini (Minerals Processing Technology) yatakayofanyika nchini Misri
kuanzia tarehe 18 hadi 29 Machi, 2018. Mratibu wa Mafunzo haya ni Wizara ya
Madini.
Kutoka nchini Malaysia,
Wizara imepokea mwaliko wa nafasi mbili (2) za kushiriki Mashindano ya 60 ya
Kimataifa ya Kuhifadhi Quran ya 1439H/2018 yatakayofanyika Kuala Lumpur,
Malaysia kuanzia tarehe 07 hadi 12 Mei, 2018. Mashindano hayo yanaratibiwa na
Ofisi ya Mufti, zanzibar na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA).
Kuhusu mafunzo ya muda
mrefu, Wizara imepokea fursa za ufadhili
wa masomo kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu katika kozi mbalimbali kwa
ajili ya Watanzania wote kutoka Jamhuri ya Korea.
Fursa hizo za masomo
ambazo zinafadhiliwa na Wizara ya Elimu ya Korea zinapatikana kupitia tovuti
ya “2018
Global Korea Scholarship” ambayo ni http://www.studyinkorea.go.kr.
Tovuti hii imeainisha taarifa na taratibu zote za namna ya kuomba. Tarehe ya mwisho
ya kutuma maombi ni tarehe 15 Machi, 2018. Aidha, nakala ngumu ya fomu za maombi ziwasilishwe
Ofisi za Ubalozi wa Korea nchini mara baada ya kukamilisha maombi ya mtandaoni
(online application). Waombaji
wanatakiwa kuwasilisha maombi yao mapema kabla ya tarehe tajwa hapo juu.
Mratibu mkuu wa fursa hizi ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Katika hatua nyingine,
Wizara imepokea nafasi tano (5) za ufadhili wa mafunzo kwa ngazi ya shahada ya
kwanza na nafasi mbili (2) za ufadhili wa mafunzo kwa ngazi ya shahada ya
uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Helwan cha nchini Misri. Mafunzo ya Shahada ya
kwanza yanatolewa kwenye fani za Utalii na masuala ya Hoteli, Biashara,
Uhandisi, Kompyuta na Teknolojia. Aidha, ufadhili masomo ya shahada ya uzamili
unatolewa kwenye fani za Sanaa na Muziki (Fine Arts and Music).
Mafunzo
hayo yatafanyika kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Maombi yote yaelekezwe
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania ambao ndio waratibu wakuu.
Wizara inatumia fursa hii
kuwahimiza wale wote watakaoomba nafasi hizo kuhakikisha wanatimiza vigezo na
masharti ya maombi hayo ili mamlaka zinazohusika na uchambuzi wa ubora ziweze
kupata Watanzania wenye sifa kwa ajili ya kuwajengea uwezo na kuliletea taifa
maendeleo.
Wizara inauhakikishia umma
wa Watanzania kuwa itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika
kuhakikisha inasimamia upatikanaji wa fursa za ufadhili wa masomo na ajira
mbalimbali zinazowasilishwa na nchi rafiki, Mashirika ya Kikanda na Kimataifa
na kuhakikisha zinawafikia Watanzania ili wanufaike na fursa hizo.
Wakati
huohuo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea
Tuzo kutoka Serikali ya Urusi kama mshindi wa pili wa mashindano ya dunia katika kigezo cha nchi nzuri zaidi
kutembelea duniani.
Tuzo hizi ambazo hutolewa
na National Geographic Traveler Awards
ni tuzo mashuhuri zaidi nchini Urusi katika sekta ya uchukuzi na utalii. Aidha,
kupitia Jarida Mtandao la Utalii la nchini Urusi, wasomaji 270,000 walipata
nafasi ya kupiga kura na matokeo kutangazwa tarehe 30 Novemba, 2017.
Hii ni mara ya pili katika
kipindi cha miaka 6 ambapo wapiga kura nchini Urusi wanaichagua Tanzania kama
nchi nzuri zaidi kutembelea. Mwaka 2011 Zanzibar ilipokea tuzo ya aina hii kwa
nchi za Afrika.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
13 Februari, 2018
Ziara ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Wizara ya Mambo ya Nje
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akifungua Mafunzo ya siku moja kwa wanachuo wa chuo cha Taifa cha Ulinzi yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, tarehe 12 Februari,2018. Lengo la mafunzo hayo ilikuwa kuwapa uelewa wanachuo hao kuhusu majukumu ya Wizara.
Major General Yacoob Mohamed Commandant, Mkuu wa chuo cha Taifa cha Ulinzi akitoa hotuba baada ya ufunguzi wa Mafunzo
Wajumbe wakifuatilia mada katika mafunzo hayo
Sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mafunzo hayo
Balozi Innocent Shiyo akitoa mada katika ziara hiyo kuhusu baadhi ya majukumu ya Wizara
Sehemu ya Wanachuo wakifuatilia mafunzo
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizarani wakifutialia mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Wizarani akitoa mada katika mafunzo hayo Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea
Katibu Mkuu Prof. Adolf Mkenda na Balozi Peter Kalaghe wakifuatilia mafunzo hayo
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizarani wakifuatilia mafunzo hayo
Baadhi ya wajumbe wa mafunzo hayo wakifuatilia mada
Katibu Mkuu Prof. Adolf Mkenda na Balozi Peter Kalaghe wakifuatilia mafunzo hayo
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizarani wakifuatilia mafunzo hayo
Baadhi ya wajumbe wa mafunzo hayo wakifuatilia mada
Major General Mohamed akikabidhi zawadi kwa Katibu Mkuu Prof Mkenda
Bi. Robi Bwiru Afisa Habari kutoka Wizarani akielezea ratiba ya Mafunzo hayo.
Picha ya Pamoja baada ya Mkutano
Monday, February 12, 2018
Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini
Balozi Cooke naye akielezea jambo kwa Prof. Mkenda |
Mazungumzo yakiendelea, wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika na Ulaya Bw. Salvatory Mbilinyi, na wa kwanza kushoto ni Naibu Balozi Ubalozi wa Uingereza Bw. Matt Sutherland |
Subscribe to:
Posts (Atom)