Wabunge wa EALA wafanya ziara Nchi za Afrika Mashariki
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) wanafanya ziara ya siku 12 kwa ajili ya kupitia na kuangalia maendeleo na changamoto mbalimbali za Mtangamano pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia vyombo vya habari.
Ziara hiyo ilianza tarehe 12- 23 Februari,2018, katika ziara hiyo waheshimiwa Wabunge wamegawanyika katika makundi mawili, kundi la kwanza linafanya ziara katika ukanda wa kati ( Cetral Corridor) , ziara hii itahusisha Zanzibar na Mikoa ya Dar es salaam, Kilimanjaro, Pwani, Arusha, Dodoma, Shinyanga na Kagera, kundi la pili watatembelea ukanda wa Kaskazini ( North Corridor) ziara hiyo itaanzia Kenya, Uganda na kumalizikia Rwanda ambapo ndipo wanapotarajia kukutana kwa kwa ajili ya kikao cha wiki mbili kwa ajili ya majumuisho ya ziara.
Waheshimiwa Wabunge wanaotemebelea Ukanda wa Kati walianzia safari yao Zanzibar ambapo walifanya ziara katika Bandari ya Zanzibar na pia kufanya mazungumzo na Uongozi wa Taasisi ya Kiswahili Kamisheni. Aidha, wakiwa Dar es salaam walipata fursa ya kutembelea Bandari ya Dar es salaam na kukutana na viongozi wa Bandari pamoja na wadau mbalimbali wanaotumia bandari. Akiongea katika mkutano huo Kaimu Meneja wa Bandari Bw. Feddy Liundi, alisema hadi sasa kuna mafanikio makubwa sana katika Bandari ya Dar es Salaam kwani bandari hiyo inahudumia zaidi ya nchi nane na kati ya hizo Rwanda na Malawi wanaongoza kwa matumizi ya bandari ya Dar es salaam.
Kwa upande wao Waheshiwa walisifia maboresho ya bandari na kusema ndio yamechangia bandari hii kuwa kinara na kivutio kwa wasafirishaji wa mizigo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Waheshimiwa Wabunge pia walipata nafasi ya kutembelea eneo la mradi wa maboresho ya bandari ya Dar es salaam wa Dar es salaam Maritime Gateaway Project (PMGP) pamoja na kitengo cha Kontena cha TICTS.
Waheshimiwa wabunge walipongeza uongozi wa bandari kwa maboresho makubwa yaliyofanyika na kuahidi kufanyia kazi changamoto zote zilizoainishwa ambazo ni za Kimtangamano. Jumla ya Waheshimiwa Wabunge 21 kutoka nchi sita (6) za Jumuiya Ya Afrika Mashariki wanashiriki katika ziara hii kwa upande wa Ukanda wa kati(Cetral corridol).
========================================================================
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ( EALA) wakiwa katika Mkutano na Uongozi wa Bandari ya Dar es salaam, kutoka kushoto ni Mhe.Maryam Ussi (Tanzania), Mhe. Wanjiku Muhia (Kenya) (ambaye pia ni kiongozi wa Msafara katika ziara hii) na wa mwisho kulia ni Kaimu Meneja wa bandariBw. Freddy Liundi, wakiwa katika Mkutano. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Bandari, tarehe 13 Februari,2018.
Mhe. Josephine Lemoyan (Tanzania) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya mkutano, wanaofuatilia ni Mhe. Wanjiku (kushoto), na Mhe. Musamali Paul Mwasa (Uganda)
Waheshimiwa Wabunge na wadau wengine wakiwa katika Mkutano huo
Wadau mbalimbali wakifuatilia Mkutano huo
Waheshimiwa Wabunge, wafanyakazi wa bandari pamoja na wadau wengine wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.