Thursday, March 26, 2020

KATIBU MKUU BALOZI KANALI IBUGE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA VIETNAM

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Balozi Col. Wilbert A. Ibuge katikati akimkaribisha Balozi wa Vietnam chini Mhe. Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara  Jijini Dodoma alipofika kuitikia wito wa Katibu Mkuu kulia ni Kaimu Mkurugenzi anayeshughulikianchi za Asia na AustralasiaBw. Ceasar Waitara.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Balozi Col. Wilbert A. Ibuge (kulia) akizungumza na Balozi wa Vietnam chini Mhe. Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara  Jijini Dodoma alipofika kuitikia wito wa Katibu Mkuu

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Balozi Col. Wilbert A. Ibuge (kulia) akizungumza na Balozi wa Vietnam chini Mhe. Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara  Jijini Dodoma alipofika kuitikia wito wa Katibu Mkuu

Balozi wa Vietnam chini Mhe. Nguyen Kim Doanh (katikati) akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Balozi Col. Wilbert A. Ibuge (kulia) alipofika katika ofisi za Wizara  Jijini Dodoma kuitikia wito wa Katibu Mkuu kushoto ni afisa ubalozi wa Vietnam aliyefuatana na Mhe. Balozi Nguyen.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Wilbert Ibuge na Balozi Nguyen Doanh wa Vietnam wakiangalia nyaraka mbalimbali walipokutana Ofisini jijini Dodoma kuzungumzia namna ya kuimarisha na kuboresha mahusiano ya kihistoria yaliyopo baina ya Tazania na Vietnam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Wilbert Ibuge na Balozi Nguyen Doanh wa Vietnam wakiagana walipomaliza mazungumzo yao Ofisini jijini Dodoma .


Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Balozi Col. Wilbert A. Ibuge leo tarehe 26 Machi, 2020 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara, Makao Makuu, Jijini Dodoma.

Balozi Doanh alikuja jijini Dodoma kufuatia wito wa Balozi Ibuge na kufanya mazungumzo yaliyohusu mambo mbalimbali kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam, likiwemo suala la uwekezaji wa Vietnam nchini kupitia Kampuni ya simu ya Halotel. 

Katika mazungumzo yao,  viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya Nchi mbili hizo, ikiwemo uendelevu wa mawasiliano ya Kidiplomasia ambapo mahusiano ya Tanzania na Vietnam yamefikisha miaka 55 mwaka huu huku  fursa za uwekezaji nchini zikiendelea kuimarishwa na hivyo kuiwezesha Serikali ya Vietnam ambayo ni mmiliki wa Kampuni ya Simu ya mkononi ya Halotel kuwekeza nchini na kuendesha shughuli zake.  

  
Balozi Ibuge pia alimjulisha Mhe. Balozi Doanh kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara itaendelea kuhimiza uwekezaji kutoka Vietnam na kusisitiza uwekezaji huo  kuzingatia sheria za nchi, kwa lengo la kuwepo tija kwa pande zote zinazohusika. 

Kufuatia kikao hicho, Mhe. Balozi Doanh aliahidi kuendelea kuyasisitiza makampuni ya Vietnam Nchini ikiwemo kampuni ya Halotel kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni zilizowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika.

Nafasi za Kazi Sekretariati ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa - Geneva


Wednesday, March 25, 2020

BALOZI KANALI IBUGE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA PAKISTAN

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Kaimu Balozi wa Pakistan nchi Bw. Mohammad Saleem alipowasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma. Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali ya kudumisha na kukuza uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge na Kaimu Balozi wa Pakistan nchi Bw. Mohammad Saleem wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye Ofisi za Wizara jijini Dodoma. Wengine ni  Caesar C. Waitara Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia (Wa kwanza kulia) na Afisa kutoka Ubalozi wa Pakistan nchini (Wa nne kushoto). 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akielezea jambo kwa Kaimu Balozi wa Pakistan nchi Bw. Mohammad Saleem walipo kutana kwa mazungumzo katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Kaimu Balozi wa Pakistan nchi Bw. Mohammad Saleem walipo kutana kwa mazungumzo katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma
Mazungumzo yakiwa yanaendelea

Friday, March 20, 2020

WIZARA YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI KWA MWAKA 2019/2020


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Wizara ya Mpango wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2019/2020 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika moja ya kumbi za Bunge jijini Dodoma.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Salim Mwinyi Rehani (mwenye suti nyeusi) wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi hayupo pichani aliyekuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Wizara ya mwaka 2019/2020


 WIZARA YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI KWA MWAKA 2019/2020

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/2020.

Akiwasilisha taarifa ya Wizara, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi amesema Wizara katika kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuzingatia maoni na ushauri wa Kamati ya Bunge imeanzisha Kitengo cha Usimamizi wa Majengo ambacho kitakuwa chini ya Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu.

Amesema pamoja na kuanzishwa kwa Kitengo hicho Wizara imeendelea kushirikiana na Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku wakifuata sheria na taratibu zilizopo.

Amesema uamuzi wa kuanzishwa kwa kitengo hicho unatokana na ushauri uliotolewa na Kamati hiyo uliyoitaka Wizara kuhakikisha mipango ya ujenzi wa majengo ya ofisi na makazi ya Balozi mbalimbali nje ya nchi unasimamiwa kitaalamu na kwa ufanisi mkubwa.

“Uamuzi huu umetokana na ushauri ambao Kamati hii iliutoa kwa Wizara katika kuhakikisha suala la ujenzi wa majengo ya Balozi zetu unasimamiwa kitaalamu na kwa ufanisi,” alisema Prof. Kabudi.

Mhe. Waziri amesema Wizara inaendelea na mipango ya kuwashirikisha Watanzania waishio ughaibuni katika mipango na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchininikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira rafiki ya kuchangia maendeleo na kusaidia ndugu na jamaa zao waliopo nchini na kufanya uchambuzi wa mazingira ya ushirikishwaji wao na kuangalia masuala ya kisheria, kitaasisi ushirikiano na sekta binafsi takwimu za Watanzania waishio ughaibuni na uwezo na hamasa ya kuchangia maendeleo ya nchi.



Wednesday, March 18, 2020

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA SADC

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akifungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika uliofanyika kwa njia ya video kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Machi 2020.

Mhe. Waziri Mkuu akitoa salamu kwa Nchi Wanachama wa SADC ambao ni wajumbe wa Mkutano huo unaoongozwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa jumuiya hiyo.
Pamoja na salamu hizo za ufunguzi Mhe. Waziri Mkuu alipongeza jitihada zinazofanywa na Nchi Wanachama katika kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo la ugonjwa wa virusi vya CORONA ambao umewezesha nchi wanachama kushirikiana kutafuta namna bora ya kuendelea na shughuli za utekelezaji kwa ustawi wa kanda na watu wake.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, Mhe. Palamagamba John Kabudi akitoa hotuba ya utangulizi kumkaribisha Waziri Mkuu ili aweze kufungua mkutano wa wa Baraza hilo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jinini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC, Dkt. Stergomena Tax akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya jumuiya hiyo wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC.

Wajumbe wa Mkutano huo ambao ni Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine waandamizi wakifuatilia hafla ya ufunguzi. 


Tuesday, March 17, 2020

DKT. NDUMBARO AKUTANA NA BALOZI WA UBELGIJI, SWEDEN


Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjoberg leo jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo ya Mhe. Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro pamoja na Balozi wa Ubelgiji yalijikita katika masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji hasa kwenye sekta za Kilimo na Madini.

Balozi wa Ubelgiji, Mhe. Acker amesema kuwa Ubelgiji itaendelea kuwekeza katika kilimo cha maharage mkoani Kigoma, na kilimo cha Tumbako katika mikoa ya Tabora, Ruvuma, Katavi na Rukwa.

"kupitia uwekezaji wa kilimo nchi zetu mbili (Tanzania na Ubelgiji) zimekuwa zikinufaika sawa hivyo ni rai yangu kuona uwekezaji huu unaendelea kutoa fursa za ajira kwa mataifa haya mawili," Amesema Balozi Acker.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Tanzania itaendelea kuhakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake na Ubelgiji katika sekta ya Kilimo, Uwekezaji na Biashara ili kuendelea kutoa fursa za ajira na kukuza uwekezaji nchini.

Katika nyingine, Naibu Waziri Dkt. Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjoberg, ambapo mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.  

Pamoja na mambo mengine, Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Sjoberg amemuahidi Naibu Waziri kuwa Sweeden itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa nchi hizi mbili zinapiga hatua katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Kwa upande wake Mhe. Naibu Waziri amemhakikishia Balozi Sjoberg kwamba Tanzania itaendelea kukuza na kuimarisha Ushirikiano na Uhusiano wake na Sweden kwani uhusiano huo wa muda mrefu umekuwa na manufaa kwa nchi zote mbili.


Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao jijini Dar es Salaam



Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam



Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimfafanulia jambo Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam



Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg wakisalimiana bila kushikana mikono kabla ya kuanza kwa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam



Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam



Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimueleza jambo Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam




Monday, March 16, 2020

TEKNOLOJIA YAWEZESHA MKUTANO WA MAAFISA WAANDAMIZI WA SADC KUEPUKA CORONA ( COVID-19)

Mkutano wa Maafisa Waandamizi ambao ni mkutano wa awali wa maandalizi ya Baraza la Mawaziri la nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika tarehe 18 Machi 2020 umefunguliwa rasmi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini  Dar es Salaam.

Akifungua mkutano huu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Waandamizi wa SADC, Balozi Kanali Wilbert Ibuge amewashukuru wajumbe wote kutoka nchi wanachama pamoja na wataalamu wa TEHAMA kwa jitihata walizoonesha kuhakikisha mkutano huu kwa mara ya kwanza unafanyika kwa mfumo wa Video. “ Hii ni uthibitisho siyo tu wa namna ambavyo Teknolojia ya Habari na Mawasilisno imebadilisha na itaendelea kutubadilisha namna tunavyowasiliana bali pia ambavyo matishio ya majanga ya kidunia kama ugonjwa wa Virusi vya CORONA (COVID 19) yanavyotulazimisha kutafuta mbinu mbadala za kufanya mambo yetu kikanda na kidunia pamoja na kuendelea kuimarisha ushirikiano bila kuonana ana kwa ana” alisema Balozi Ibuge
Mkutano huu unahudhuriwa na Maafisa Waandamizi kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) wenye dhamana ya masuala ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha, Uchumi, Mipango pamoja na Viwanda na Biashara.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu unaongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikia na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Waandamizi wa SADC, Balozi Kanali Wilbert Ibuge ambaye ameambatana na maafisa wengine waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Fedha na Mipango Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Wizara ya Viwanda na Biashara Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Maafisa wengine waandamizi walioshiriki ni pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Mambo ya Ndani. Vilevile mkutano huu umehudhuriwa na baadhi ya Mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha katika nchi za SADC ambao ni pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Afrika Kusini.

Mkutano huu utajadili ajenda chache za muhimu kwa wakati huu ambazo ni: Taarifa ya Maandalizi ya Dira ya SADC ya 2050; Mpango Mkakati wa Maendeleo wa SADC 2020-2030; Maadhimisho ya miaka 40 ya SADC tangu kuanzishwa kwake mwaka 1980; Utekelezaji wa maazimio ya vikao vilivyopita; Hali ya michango na kifedha kwa ujumla ya SADC; na Kupokea taarifa ya ukaguzi wa shughuli mbalimbali za Sekretarieti SADC.


Awali mkutano katika ngazi ya Maafisa Waandamizi ulipangwa kufanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Machi 2020 na kufuatiwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri tarehe 17 na 18 Machi 2020. Hata hivyo, kufuatia ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na Mawaziri wa Afya kutoka Nchi Wanachama wa SADC walipokutana kwa dharura tarehe 9 Machi, 2020. Mkutano huo ulijadili na kupendekeza kwa Nchi Wanachama namna ya kuzuia maambukizi ya mlipuko wa ugonjwa hatari wa virusi vya Corona (COVID 19) unaosambaa kwa kasi na kuleta athari kubwa duniani tangu kubainika kwakwe mwezi Desemba.

===================================================================


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Waandamizi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Balozi Kanali Wilbert Ibuge, akifungua mkutano wa Maafisa Waandamizi ambao ni mkutano wa awali wa maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakaofanyika Machi 18, 2020, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Waandamizi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Balozi Kanali Wilbert Ibuge, akifungua mkutano wa Maafisa Waandamizi wa SADC unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ufunguzi wa Mkutano huo umefanyika kwa njia ya video kuepuka maambukizi ya Virusi vya ugonjwa CORONA (COVID 19)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Waandamizi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Balozi Kanali Wilbert Ibuge, akitoa hotuba ya ufunguzi ambapo alitumua nafasi hii kueleza agenda zitakazojadiliwa na wajumbe wa mkutano kutoka nchi wanachama. Pia aliishukuru Sekretariet ya SADC,wajumbe kutoka nchi wanachama, wataalamu wa TEHAMA kutoka nchi za SADC pamoja, na wajumbe wengine kwa ushirikiano wao uliowezesha kufanyika kwa mkutano huo kwa njia ya video. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC, Dr. Stergomena Tax.

Maafisa Waandamizi wa nchi za SADC  wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo uliokuwa ukiendelea kupitia mfumo wa video, unaofanyika katika kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, Tanzania 

Maafisa Waandamizi wa nchi za SADC  wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa mkutano kutokea nchini Tanzania kupitia mfumo wa video  

Mkutano ukiendelea.