Wednesday, February 9, 2022
Tuesday, February 8, 2022
RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AFDB) DKT. ADESINA AWASILI DODOMA
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
akisalimiana na Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi
Adesina alipowasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma akiwa
katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini.
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina awasili jijini Dodoma akiwa katika ziara ya
kikazi ya siku tatu nchini. Katika uwanja wa ndege wa Dodoma Dkt. Adesina
amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba.
Dkt.
Adesina yuko nchini kwa ziara ya siku tatu ambapo
tarehe 09 February 2022 atashiriki katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara za
mzunguko zinazojengwa katika jiji la Dodoma utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Ujenzi
wa barabara hizo za mzunguko zenye urefu wa kilomita 112.3 unagharamiwa kwa
pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na benki hiyo. Ujenzi wa barabara hizo utalifanya jiji la Dodoma kuwa na barabara za aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
MKUTANO WA 15 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA NISHATI LA EAC WAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA KATIKA NGAZI YA WATAALAMU
Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika
Mashariki umefunguliwa leo tarehe 8 Februari 2022 jijini Arusha, Tanzania
katika ngazi ya Wataalamu.
Mkutano huu utafanyika katika ngazi tatu ambapo umeanza na;
Mkutano Ngazi ya Wataalamu unaofanyika tarehe 8 hadi 9 Februari 2022,
utafuatiwa na Mkutano Ngazi wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 10 Februari
2022 na utamalizika kwa Mkutano Ngazi ya Mawaziri utaofanyika tarehe 11
Februari 2022.
Lengo la Mkutano huu ni kupitia na kuandaa
taarifa ya hali ya utekelezaji wa Maamuzi/Maagizo ya mikutano iliyopita; Hatua
iliyofikiwa hadi sasa katika sekta za Nishati Umeme, Nishati Mafuta, na Nishati
Jadidifu; pamoja na Utekelezaji wa Miradi/Programu mbalimbali za Kitaifa na
Kikanda ya Sekta za Nishati inayotekelezwa ndani ya
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Ujumbe wa Tanzania katika
Mkutano Ngazi ya Wataalamu unaongozwa na Kamishna Msaidizi Maendeleo ya
Umeme kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila ambaye ameambatana
na Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota,
Mkurugenzi Idara ya Nishati na Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini
Zanzibar, Mhandisi Said H. Mdungi pamoja na maafisa wengine Waandamizi kutoka
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye dhamana katika sekta ya nishati.
Mkutano Ngazi ya Wataalamu
na Ngazi ya Makatibu Wakuu ni sehemu ya mikutano ya awali kwaajili ya
maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la
Jumuiya ya Afrika Mashariki utaofanyika tarehe 11 Februari 2022.
Kushoto ni Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika Mkutano Ngazi ya Wataalamu na Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme katika Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akifafanua jambo wakati wa majadiliano ya mkutano huo. |
Mwenyekiti wa Mkutano Ngazi ya Wataalamu na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu kutoka Jamhuri ya Kenya, Mhandisi Benson Mwakina (Kushoto) akiongoza majadiliano, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Bw. Christophe Bazivamo. |
Kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Mgeta Sabe na wajumbe wengine wa Tanzania wakifatilia majadiliano. |
Ujumbe wa Tanzania. |
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania. |
WAZIRI MULAMULA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA 46 WA DHARURA WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC
Mkutano ukiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine (katika) na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Balozi Stephen Mbundi wa Wizara hiyo wakifuatilia Mkutano wa 46 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea |
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 46 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendele |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea kwenye Mkutano wa 46 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akichangia hoja kwenye Mkutano wa 46 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao. |
Monday, February 7, 2022
WAZIRI MULAMULA: TUTAENDELEA KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA NISHATI NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Edwin Rutageruka (wa kwanza kusho), Mkurugenzi wa Diplomasia Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje, Makamu wa Rais wa Kampuni ya dmg event ya nchini Uingereza Bw. Damian Howard (wa pili kushoto) na Bw. Abdulsamad Abdulrahim (kulia) Mkurugenzi wa Kampuni ya Ocean Business Partners Tanzania Ltd walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma. |
Mazungumzo yakiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma |
Friday, February 4, 2022
MAAFISA JWTZ WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALIA
Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira pamoja na Col. Abdallah Khalfan wametembelea Ubalozi wa Tanzania Jijini Roma, Italia.
Wakiwa Ubalozini walipokelewa na mwenyeji wao Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ambapo pamoja na mambo megine wamezungumzia masuala ya ushirikiano. Maafisa hao walikuwepo nchini Italia kwa shughuli za kikazi.
Balozi
wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Mkuu
wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira
katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Italia
Balozi
wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Mkuu
wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira
na Col. Abdallah Khalfan
Balozi
wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Mkuu
wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira,
Col. Abdallah Khalfan pamoja na baadhi ya watumishi wa Ubalozi
Thursday, February 3, 2022
WAZIRI MULAMULA AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA SERIKALI YA URUSI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akipokea ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladimirovich Putin |
Mazungumzo yakiendelea. |
Picha ya pamoja Mhe. Waziri na Ujumbe kutoka Serikali ya Urusi. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme, na Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Fredrick Kibuta. Kutoka kulia kwa Mhe. Waziri ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Masuala ya Kibinadamu nchini Urusi, Bw. Evgeny Primakov, Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Yuri Popov pamoja na Mjumbe kutoka serikali ya Shirikisho la Urusi, Bw. Egor Utkin. |
Waziri Mulamula akikabidhi shajara. |
Picha ya Pamoja. |
Wednesday, February 2, 2022
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA SAUDIA ARABIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi
Arabia wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.Kikao hicho kilifanyika ofisini kwa Mhe. Waziri Mttumba jijini Dodoma |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia (walioko kushoto) wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji. |
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (katikati) katika kikao na Wawekezaji kutoka nchini Saudi Arabia(hawapo pichani) kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Hemedi Mgaza na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Balozi Edwin Rutageruka wakati wa kikao na wawkezaji hao |
Waziri Mulamula (katikati) katika picha ya pamoja na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia waliokuja nchini kuangalia fursa za biashara na uwekezaji baada ya kumalizika kwa kikao chao jijini Dodoma |
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini akiwa nje ya jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba akizungumza na wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi
Arabia aliokuja nao Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji baada ya kumalizika kwa kikao chao na Mhe Waziri Mulamulajijini Dodoma |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.
Mhe. Waziri Mulamula amekutana na Ujumbe wa wawekezaji hao ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 02 February 2022. Ujumbe wa wawekezaji hao umeongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia Mhe. Ali Mwadini umeelezea utayari wao wa kuja kuwekeza nchini.
Akizungumza katika kikao hicho Balozi Mulamula amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia mazingira rafiki ya uwekezaji nchini na kwamba Tanzania iko tayari kuwapokea.
Amesema Tanzania na Saudia zina uhusiano wa muda mrefu ambao una historia ya aina yake na kwamba uwekezaji kutoka kwa kampuni hiyo ni sehemu ya kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia.
Kampuni hiyo inayomiliki viwanda mbalimbali nchini Saudi Arabia inajishughulisha na uzalishaji wa pembejeo za Killimo hususan, mbolea za kupandia na kukuzia mimea pamoja na dawa (pesticides) aina ya ‘phosphorus, nitrogen, potassium na sulfur’.
Mbali na uzalishaji wa mbolea na dawa, Kampuni hiyo pia inazalisha vifaa vya kilimo vya plastiki ikiwa ni pamoja na khusambaza bidhaa katika nchini za Saudi Arabia, ukanda wa Mashariki ya Kati na duniani kote.
Wawekezaji hao waliwasili nchini Januari 28, 2022 wametembelea Mikoa ya Mtwara, Lindi Mtwara na Dodoma na kukutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mikoa hiyo, wadau wa sekta binafsi na wakulima wa korosho kuzungumzia biashara na uwekezaji katika nyanja hizo.
Wawekezaji hao wamemuhakikishia Mhe. Waziri Mulamula juu ya nia yao ya kuja kuwekeza Tanzania na kutaja maeneo ambayo ni kipaumbele chao kuwa ni madini, biashara, kilimo na mifugo
WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amefanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Donald Wright leo tarehe 2 Februari 2022 jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani katika sekta za afya, uwekezaji, biashara na uhusiano wa kimataifa. |
Kushoto ni afisa kutoka Ubalozi wa Marekani, Bi. Kristin Mencer akifuatilia mazungumzo. |
Kutoka kulia ni Katibu wa Waziri, Bw. Seif Kamtunda na Afisa Mambo ya Nje Bi. Talha Waziri wakifuatilia mazungumzo. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Picha ya Pamoja. |
WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA ALFA CARE GROUP LIMITED
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kati) amekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Alfa Care Group Limited Bw. Dadkarim Mulla (wa kwanza kushoto) ambaye aliambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo (wa pili kushoto) walipomtembelea Wizarani tarehe 1 Februari 2022 jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Edwin Rutageruka (mwenye tai) na Katibu wa Waziri, Bw. Seif Kamtunda. Katika Mazungumzo yao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kwa lengo ya kuyafikia malengo ya kitaifa kwa ufanisi. Vilevile wamejadili namna ya kuongeza uwekezaji katika miradi ya maendeleo husasani sekta ya afya, miundombinu, teknolojia, utalii sambamba na kukuza ajira kwa watanzania. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Picha ya pamoja |
Mhe. Balozi Mulamula akimkabidhi Mhe. Gambo Calenda na Shajara za Wizara. |
Mhe. Waziri akimkabidhi pia Bw. Mulla calenda ya Wizara |
Saturday, January 29, 2022
BALOZI MULAMULA: MISINGI YA SERA YA MAMBO YA NJE HAIJABADILIKA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akifurahia jambo alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Wizara jijini Dodoma |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Nassor Mbarouk (Mb), akizungumza na watumishi wa Wizara kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na watumishi wa Wizara kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma |
Kutoka kushoto; Naibu katibu Mkuu Mhe. Balozi Fatma Rajab, Naibu Waziri Mhe. Balozi Nassor Mbarouk (Mb), Waziri Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Mkurugenzi Msaidizi Menejimenti ya Rasilimali Watu Bw. Peter Bunyazu wakiwa kwenye kikao na Watumishi wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma |
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo (mstari wa mbele) wakifuatilia Kikao kilichokuwa kikiendelea baina Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na watumishi wa Wizara. |
Kikao kikiendelea |
Kikao kikiendelea |
Picha ya pamoja Meza Kuu na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Picha ya pamoja Meza Kuu na Wakuu wa Taasisi zilipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Picha ya pamoja Meza Kuu na baadhi ya Watumishi wa Wizara |