Friday, March 17, 2023
TANZANIA, DRC WAJADILI FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI
Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) na Wakala wa Kitaifa wa Kukuza Uwekezaji (ANAPI) cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamekutana kujadili fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania na DRC.
Akiongea Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, Mkurugenzi wa Utafiti, Mipango na Mifumo ya Habari wa TIC, Bw. Mafutah Bunini amesema ANAPI imekuja Tanzania kuelezea fursa za uwekezaji na biashara zinazopatikana nchini Kongo DRC.
“Kama tunavyofahamu Serikali ya Awamu ya Sita imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji hivyo ndugu zetu wa DRC wamekuja kuangalia fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania ili waweze kuwekeza zaidi,” alisema Bw. Bunini.
Bw. Bunini ameongeza kuwa Tanzania imejipanga kushirikiana na DRC kuwekeza katika sekta za kilimo hususan uzalishaji wa mbegu za mafuta, mazao ya chakula kama mchele, mifugo, madini, utalii pamoja na usafirishaji.
Amesema DRC Kongo ina wawekezaji wake Tanzania na ndiyo maana ANAPI imekuja hapa kuhamasisha wawekezaji wa Tanzania kwenda kuwekeza zaidi nchini Kongo, hivyo uwekezaji na biashara ni wa pande zote mbili.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ANAPI, Bw. Anthony Nkinzo Kamole amesema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuna fursa nyingi za uwekezaji hususan katika sekta za madini, usafirishaji, utalii, nishati, afya na viwanda.
“Tuna makubaliano ya biashara kati yetu (Kongo) na Tanzania na ndiyo maana tumekuja hapa kuelezea fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara zinazopatikana nchini kwetu ili kuwavutia wafanyabiashara na wawekezaji wa Kitanzania kuwekeza zaidi Kongo,” alisema Bw. Kamole
Pamoja na Mambo mengine, Mkurungenzi Mtendaji wa ANAPI aliongeza kuwa “mazingira ya biashara nchini Kongo ni mazuri na yakuridhisha, kwanza tuna sera ya kulinda uwekezaji, tumeboresha pia taratibu za kujisajili kampuni nchini Kongo, tumepunguza kodi kwa wawekezaji ili kuwawezesha kufanya biashara na uwekezaji katika mazingira mazuri na salama zaidi kuliko ilivyokuwa awali,”.
Septemba, 2022 Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zilikutana katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) na kukubaliana maeneo ya ushirikiano yenye tija ya moja kwa moja kwa nchi hizo na watu wake hasa biashara na uwekezaji.
DRC imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika sekta za miundombinu, nishati, utalii, elimu, afya, huduma za kifedha, biashara, uwekezaji, kilimo, maliasili na ufugaji. Aidha, zinashirikiana na kuungana mkono kwenye masuala ya kikanda na kimataifa yenye maslahi kwa pande zote mbili.
Sehemu ya Wafanyabiashara na wawekezaji wakifuatilia Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na DRC. Kongamano hilo limefanyika Jijini Dar es Salaam. |
Mkurugenzi wa Utafiti, Mipango na Mifumo ya Habari wa TIC, Bw. Mafutah Bunini akiwasilisha hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara |
Picha ya pamoja |
Thursday, March 16, 2023
University of Ibadan (UI) Nigeria, and University of Dar es Salaam, Tanzania sign Memorandum of Understanding for teaching Kiswahili.
University of Ibadan (UI) Nigeria, and University of Dar es Salaam, Tanzania sign Memorandum of Understanding for teaching Kiswahili.
The University of Ibadan and the University of Dar es Salaam have signed a Memorandum of Understanding for teaching Kiswahili language.
The symbolic virtual signing of the document was facilitated by the High Commissioner of Tanzania to Nigeria, H.E. Dr. Benson A. Bana, who set up the virtual meeting between the two universities.
Speaking after the signing event, Dr. Bana said it was part of his Commission's efforts to advance Tanzania/Nigeria bilateral ties.
The MoU will take the form of development of joint research activities; exchange of undergraduate and postgraduate students; exchange of staff on sabbatical basis; mutual assistance in the establishment of new programs; exchange of information and publications; and organization of seminars, colloquia, symposia, conferences and workshops.
The Vice-Chancellors of both universities said they were happy about the MoU, given that both institutions are the oldest public universities in their different countries.
The the two Universities have shared antecedents. The University of Ibadan was established as a college of the University of London in 1948 and became a full-fledged University in 1962. The University of Dar es Salaam was established as a campus of the University of London in 1961 but became a full-fledged University in 1970.
The Vice Chancellor of Dar es Salaam University, Professor William A. L. Anangisye said the understanding will afford both institutions to learn more about each other.
He added he was pleased that the MoU would allow the teaching of Kiswahili, the lingua franca of Tanzania, and one of the official languages of the Organization of African Unity.
The Vice-Chancellor of the University of Ibadan, Professor Kayode O. Adebowale, mni, FAS, was represented at the ceremony by the Deputy Vice-Chancellor, Research Innovation and Strategic Partnerships, Professor Oluyemisi A. Bamgbose, SAN.
Professor Bamgbose stated that mutual understanding had existed between the University of Ibadan and Tanzania long before now.
She recalled that the University of Ibadan in 1976 conferred the Honorary Doctor of Laws on the late President Julius Mwalimu Nyerere in recognition of his contributions to the development of Africa. She said this was an indication that the two countries shared values.
Professor Bamgbose appreciated the efforts of the High Commissioner to strengthen the relationship between the two countries.
The newly signed MoU will lead to the teaching of Kiswahili as an African language in the University of Ibadan's Department of Linguistics and African Languages.
The Head of the Department, Professor Oye Taiwo, assured that necessary steps will be taken to ensure that the course is approved soon by the University of Ibadan Senate
Deputy Vice-Chancellor, Research Innovation and Strategic Partnerships, Professor Oluyemisi A. Bamgbose, SAN at the signing ceremony of Memorandum of Understating (MoU) |
A delegation from the University of Ibadan poses in a group photo after the signing event |
A delegation from the University of Ibadan poses in a group photo after the signing event |
BALOZI SHELUKINDO ATETA NA BALOZI WA UTURUKI
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Mehment Gulluoglu katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuboresha uhusiano baina ya Tanzania na Uturuki na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo mawili
Wednesday, March 15, 2023
MAWAZIRI WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI WASHIRIKI MKUTANO WA PILI WA TUME YA PAMOJA YA USHIRIKIANO
Mawaziri wa kisekta wa Serikali za Tanzania na Afrika Kusini
wamekutana jijini Pretoria, Afrika kusini kushiriki Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja
ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation - BNC) ngazi ya Mawaziri kati ya nchi
hizo uliofanyika tarehe 15 Machi 2023.
Mkutano huu wa siku moja ulitanguliwa na mkutano ngazi ya
wataalamu uliofanyika tarehe 13 na 14 Machi 2023 ambao pamoja na mambo mengine
ulikuwa na jukumu la kuandaa taarifa kwa ajili ya mkutano wa ngazi ya Mawaziri.
Mkutano wa Mawaziri umepitia na utawasilisha taarifa katika
itakayojadiliwa na kufanyiwa maamuzi katika mkutano wa Wakuu wa Nchi hizo
unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Machi 2023.
Mkutano wa pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri
ulifunguliwa kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Mwenyekiti mwenza Waziri wa
Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Dkt. Naledi Pandor
ambao wameongoza ujumbe wa nchi hizo mbili katika mkutano huo.
Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Dkt. Tax ameeleza kuwa Mkutano
wa Pili wa Tume ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaonesha nia
ya dhati ya mataifa hayo ya kuendeleza ushirikiano wa kihistoria na kidiplomasia
uliopo.
“Mkutano huu unatoa fursa ya kujadili na kuamua masuala ya
msingi ya kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya nchi na watu kupitia muingiliano
uliopo katika shughuli mbalimbali za kijamii, biashara na uwekezaji” alisema
Dkt. Tax
Pia akaeleza mkutano huo wa BNC utaweka msisitizo katika masuala
ya ustawi wa jamii wa mataifa hayo mawili pamoja na watu wake.
Mkutano huo utajadili masuala ya ushirikiano yenye tija kwa nchi
hizo na kupelekea maamuzi yatakayoleta matokeo chanya na kutoa ufumbuzi wa changamoto
za wananchi.
Dkt. Tax amesema sekta binafsi ni chachu katika kuendesha uchumi
wa nchi, pia ni wadau muhimu kwa sekta za umma hivyo ni jukumu la Serikali
kuwezesha upatikanaji wa mazingira mazuri ya biashara ili ziweze kukuza uchumi wa
nchi.
Kwa upande wa Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa
Afrika Kusini, Mhe. Dkt. Nalendi Pandor ameeleza kuwa uhusiano kati ya Tanzania
na Afrika kusini umejengwa na historia yenye uhalisia iliyoasisiwa tangu enzi
za harakati za kupinga ubaguzi wa rangi pamoja na za ukombozi wa Kusini mwa
Afrika.
Ameongeza kuwa Afrika Kusini itaendelea kushirikiana na Tanzania
hususan katika shughuli za kijamii, kiuchumi na masuala ya kiutamaduni.
“Napongeza jitihada za mshikamano zilizooneshwa na
wafanyabiashara wa Afrika Kusini na Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania
kwa kusaidia madawati 400 katika shule za Wilayani Kongwa na vifaa wezeshi vya
usafi katika shule ya miyembeni mwaka 2018” alisema Dkt. Pandor.
Aidha, akaeleza kuwa Tanzania na Afrika Kusini zina matamanio
makubwa ya kukuza uchumi utakaotengeneza ajira na kuondoa umasikini na kujenga
usawa wa hali ya kimaisha kwa wananchi wake.
Vilevile, Tanzania na Afrika Kusini zina mtazamo unaofanana
katika masuala ya usalama, uchumi na misimamo ya kimaendeleo ya kikanda na
kimataifa hivyo, BNC ni sehemu ya jitihada zitakazowezesha kuongezeka kwa miradi
ya maendeleo na mshikamano imara utakaopelekea kukuza na kuimarisha ushirikiano
uliopo.
Mkutano wa BNC unajadili na kutathmini hatua za utekelezaji zilizofikiwa
katika sekta mbalimbali za ushirikiano zilizokubaliwa na nchi hizo. Sekta hizo
ni pamoja na; Siasa na Diplomasia, Ulinzi na Usalama, Fedha na Uchumi, Nishati, Mifugo na Uvuvi, Madini, Habari, Mawasiliano
na teknolojia ya mawasiliano, Kilimo, Uchukuzi, Elimu na Mafunzo, Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Utalii, Maji na Misitu, na Afya.
Kwa pamoja viongozi hao walizitaka sekta zilizopo katika maeneo
hayo ya ushirikiano kuhakikisha wanatekeleza na kutatua kwa wakati masuala ya
kiutendaji ili kuruhusu sekta hizo kustawi kiuchumi na kuyafikiwa kwa wakati
malengo ya Wakuu wa Nchi katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania na Afrika
Kusini.
Mkutano huu unaenda sambamba na kongamano la biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini litakaalofanyika tarehe 16 Machi 2023 na kuhusisha maonesho ya huduma na biashara kutoka sekta za umma na sekta binafsi ambapo washiriki wapatao 136 wanatarajiwa kushiriki katika kongamano na maonesho hayo jijini Pretoria, Afrika Kusini.
Tuesday, March 14, 2023
Monday, March 13, 2023
MAKATIBU WAKUU WA SADC WAKUTANA KINSHASA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye ni Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC ngazi ya Makatibu Wakuu akiwa katika meza ya Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa SADC unaofanyika Kinshasa, Jamhui ya Kidemokrasia ya Congo |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye ni Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC ngazi ya Makatibu Wakuu akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa SADC kinachofanyika Kinshasa, Jamhui ya Kidemokrasia ya Congo. |
Wajumbe wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wanaoshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC, ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika Kinshasa, Jamhui ya Kidemokrasia ya Congo. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mtangamano wa Kikanda wa DRC ambaye ni Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu, Balozi Songhu Kayumba akisoma hotuba ya ufunguzi ya kikao hicho. |
TANZANIA NA AFRIKA KUSINI KUONGEZA MAENEO MAPYA YA USHIRIKIANO
Tanzania
na Afrika Kusini zimekubaliana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika
sekta za fedha na uchumi, kilimo, madini, maji, utalii, siasa na diplomasia,
mawasiliano na uchukuzi, teknolojia ya habari, uchumi, nishati, elimu, wiwanda,
biashara na uwekezaji, ujenzi, utalii, kilimo, uvuvi, afya, elimu na utamaduni.
Makubaliano
hayo yamefikiwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya
Ushirikiano (Bi-National Cooperation) kati ya Tanzania na Afrika Kusini
unaofanyika tarehe 13 – 16 Machi 2023 jijini Pretoria, Afrika Kusini.
Mkutano
huu uliofunguliwa katika ngazi ya Maafisa Waandamizi unafanyika tarehe 13 na 14 Machi 2023 pia ni mkutano wa awali kwa
ajili ya kuandaa taarifa zitakazopitiwa na kujadiliwa na mkutano ngazi ya
Mawaziri utakaofanyika tarehe 15 Machi 2023.
Mkutano
wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini
unalenga kujadili na kutathmini hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika
masuala mbalimbali ya ushirikiano yaliyokubaliwa kwenye mkutano wa kwanza wa
BNC uliofanyika mwezi Mei 2017 jijini Dar es salaam.
Akihutubia
wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano huu, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania
katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na
Afrika Kusini, ngazi ya Maafisa Waandamizi, Balozi Fatma Rajab ameeleza kuwa
mkutano huu unatoa nafasi ya kupitia hali halisi ya utekelezaji wa maeneo ya
ushirikiano yaliyokubaliwa katika kikao cha kwanza na kuweka mikakati imara ya
kusonga mbele kimaendeleo.
“Kikao hiki kitahusisha majadiliano
yatakayowezesha kufikiwa kwa makubaliano katika maeneo mbalimbali ya
ushirikiano ya kisekta yatakayo rasimishwa kwa ajili ya utekelezaji na kuruhusu
maeneo mapya ya ushirikiano” alisema Balozi Fatma.
Vilevile,
akaeleza kuwa mkutano huu ni muhimu kwakuwa ushirikiano wa nchi zetu umejengwa
katika misingi imara iliyopiganiwa kwa jasho na damu tangu enzi za ubaguzi wa
rangi na hivyo BNC hiyo ni chachu ya kuimarisha na kuharakisha ushirikiano wa
kiuchumi na kijamii katika maeneo yatakayokubaliwa.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini na
Mwenyekiti mwenza za kikao hicho Bw. Zane Dangor, alieleza kuwa BNC inatoa
fursa ya kuimarisha ushirikiano hususan katika masuala ya biashara na
uwekezaji.
“Jukumu
letu ni kuimarisha ushirikiano katika masuala yenye maslahi makubwa kwa mataifa
yetu na kufungua fursa ya maeneo mapya ya ushirikiano” alisema Bw. Dangor.
Matarajio
ya Wenyeviti wa Mkutano huu ngazi ya Maafisa Waandamizi ni kuhakikisha wajumbe
wanawasilisha michango yenye tija ya kisekta katika majadiliano ili kuifikia
hatua ya juu ya kimaendeleo kupitia ushirikiano uliopo.
Pia
viongozi hao wamesisitiza kuwa Tanzania na Afrika Kusini zinauchukulia kwa
upekee ushirikiano huo kwakuwa nchi hizo zina masuala mengi ya kushirikishana
kupita uanachama wake katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC
na kwa lengo la kujenga uchumi wa kanda hiyo na Afrika kwa ujumla.
Tanzania
na Afrika Kusini zilikubaliana kuanzisha Tume ya Marais ya Uchumi (Presidential
Economic Commission-PEC) mwaka 2005 na mwaka 2011 nchi hizo zilisaini Tume ya
Ushirikiano wa Pamoja (Bi-National Commission) ambayo ilichukuwa nafasi ya PEC.
|
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (BNC) kati ya Tanzania na Namibia, ngazi ya Maafisa Waandamizi, Balozi Fatma Rajab akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika jijini Pretoria, Afrika Kusini tarehe 13 hadi 16 Machi 2023. |
Katibu Mkuu Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini na Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (BNC) kati ya Tanzania na Afrika Kusini, Bw. Zane Dangor akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika jijini Pretoria, Afrika Kusini tarehe 13 hadi 16 Machi 2023 |
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab na Katibu Mkuu Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini, Bw. Zane Dangor wakifafanua juu ya utaratibu wa mkutano huo ambapo walieleza kuwa majadiliano ya mkutano yanafanyika katika makundi manne ambayo ni; Siasa na Diplomasia; Ulinzi na Usalama; Fedha na Uchumi, na Huduma za kijamii. |
Mkurugenzi Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz akifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (BNC) kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaofanyika jijini Pretoria Afrika Kusini tarehe 13 hadi 16 Machi 2023. |
Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe akifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (BNC) kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaofanyika jijini Pretoria Afrika Kusini tarehe 13 hadi 16 Machi 2023. |
TANZANIA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA YA MADOLA KUKABILI CHANGAMOTO ZA KIDUNIA
Tanzania imeahidi kushirikiana na Jumuiya ya Madola kukabiliAna na changamoto za kidunia zikiwemo mabadiliko ya tabianchi, Uviko 19, migogoro, ugaidi na umasikini
Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo aliposhiriki maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Balozi Shelukindo amesema licha ya uhusiano wetu na historia ya pamoja kama wanachama wa Jumuiya ya Madola tunaamini kuwa kwa umoja wetu tunaweza kuzikabili changamoto za kidunia kwa urahisi zaidi.
“Kila mmoja wetu akitimiza wajibu wake kwa wakati, itakuwa rahisi kuzikabili changamoto za kidunia hususan mabadiliko ya tabianchi, Uviko 19, migogoro, ugaidi na umasikini,” alisema Balozi Shelukindo
Kwa Upande wake, Balozi wa Uingereza hapa Nchini, Mhe. David Concar amesema Jumuiya ya Madola imekuwa na mchango mkubwa kwa Tanzania hususan vijana ambao ndiyo taifa la kesho wamekuwa wakinufaika na ufadhili wa masomo kwa ngazi mbalimbali, biashara na uwekezaji pamoja na ajira.
Balozi Concar amesema Jumuiya ya Madola imefurahishwa na hatua ambazo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikizichukua katika masuala ya demokrasia, haki za binadamu na utawala bora, ulinzi na usalama na utawala wa sheria.
“Tanzania imeboresha sana masuala ya demokrasia, haki za binadamu na utawala bora, ulinzi na usalama na utawala wa sheria….. mtakumbuka hivi karibuni mikutano ya kisiasa imeruhusiwa pamoja na uhuru wa vyombo vya Habari umeongezwa jambo ambalo linaashiria kukua na kukomaa kwa demokrasia,” alisema Balozi Concar.
Balozi Concar ameongeza kuwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya biashara na uwekezaji nchini na hivyo kuchangia uchumi wa Tanzania kukua.
Maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Madola yamehudhuriwa pia na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba pamoja na baadhi ya wanamichezo wa Tanzania walioshiriki kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola.
Maadhimisho yameongozwa na Kauli Mbiu isemayo ‘Kujenga mustakabali endelevu na wenye amani wa pamoja’.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo azungumza na Balozi wa Uingereza hapa Nchini, Mhe. David Concar pamoja na Balozi wa Rwanda Nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba alipowasili katika makazi ya Balozi wa Uingereza Jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Uingereza hapa Nchini, Mhe. David Concar akiwasilisha salamu za Jumuiya ya Madola wakati wa maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akiwasilisha hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Uingereza hapa Nchini, Mhe. David Concar akichangia jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam |
Picha ya pamoja |
Saturday, March 11, 2023
BALOZI KOMBO AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA JAMHURI YA MALTA
Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella katika Ikulu ya Malta.
Baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Vella viongozi hao walizungumza ambapo pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yaliakisi kuimarisha ushirikiano zaidi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kisiasa na azma ya nchi ya Malta kuwa daraja baina ya Afrika na Umoja wa Ulaya.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao walisisitiza suala la kuibua fursa zenye manufaa kwa pande zote mbili katika maeneo ya elimu, utalii, utamaduni, uvuvi, usafiri wa majini, biashara na uwekezaji.
Uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Malta ulianza mwaka 2015 na tangu wakati huo, juhudi za kukuza uhusiano huo zimekuwa zikifanyika kupitia sekta za elimu, utalii na usafiri wa anga; na kupitia katika majukwaa ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Madola ambazo nchi zote mbili ni wanachama.
Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta |
Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta |
Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta, mara baada ya Balozi Kombo kuwasilisha Hati za Utambulisho |
Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta, mara baada ya Balozi Kombo kuwasilisha Hati za Utambulisho |
Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta |
TANZANIA NA NAMIBIA ZASAINI HATI ZA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri Namibia zimesaini Hati za Makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya usalama, mishati na mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia.
Hati za Makubaliano hayo zimesainiwa katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JCC) kati ya Tanzania na Namibia uliomalizika jijini Windhoek, Namibia tarehe 10 Machi 2023 katika ngazi ya Mawaziri.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwenye Mkutano huu umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ambaye ameambatana na Naibu Waziri
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. David Silinde(Mb.) na Naibu Waziri Wizara ya
Nishati, Mhe. Steven Byabato (Mb.).
Kadhalika, ujumbe wa Jamhuri ya
Namibia umeongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia,
Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah ambaye ameambatana na Mawaziri wa kisekta na
Makatibu Wakuu wa nchi hiyo.
Mkutano wa Tatu wa JCC kati ya
Tanzania na Namibia umejadili na kutathimini masuala mbalimbali ya utekelezaji
kwenye maeneo ya ushirikiano yaliyokubaliwa baina ya nchi hizi. Maeneo hayo ni
pamoja na; Siasa na Diplomasia, Ulinzi na Usalama,
Uchumi, Nishati, Kilimo, Maendeleo na Miji, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Maliasili,
Utalii na Mazingira, na Uvuvi, Afya, Elimu na Utamaduni.
Aidha, mkutano huu wa Mawaziri umewaagiza
watendaji katika sekta za ushirikiano kukamilisha kwa wakati masuala yote
yanayohitaji utekelezaji ndani ya muda ulioazimiwa na kikao hicho ili kuleta
tija katika shughuli za wananchi na kuwainua kiuchumi.
Vilevile, wamesisitiza umuhimu wa
kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii
katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na Bara la Afrika kwa
ujumla.
Wakihutubia katika ufunguzi wa
mkutano huo Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Namibia Mhe. Dkt.
Stergomena Tax na Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah wamesisitiza umuhimu wa
kukuza mawasiliano baina nchi hizo mbili ili kuweza kurithisha kizazi cha sasa
juu ya historia ya mataifa hayo mawili na kufahamu ndoto kubwa waliyokuwa nayo
waasisi wa matifa haya katika kuyafikia maendeleo ya watu wake.
Mkutano
huu ulitanguliwa na mkutano wa awali wa ngazi ya Maafisa Waandamizi uliofanyika
tarehe 8 Machi 2023 na kufuatiwa na mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika
tarehe 9 Machi 2023.
Mkutano wa Tatu wa JCC kati ya
Tanzania na Namibia umeazimia kuwa mkutano ujao wa JCC utafanyika mwaka 2024
nchini Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Naitwa wakisaini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano katika masuala ya ulinzi, nishati na mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia kati ya Tanzania na Namibia jijini Windhoek Namibia. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Naitwa wakibadilishana Hati za Makubaliano baada ya kukamilisha zoezi la uwekaji saini wakati wa Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia Jijini Windhoek. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Naitwa wakionesha Hati za Makubaliano zilizosainiwawakati wa Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia Jijini Windhoek.. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akihutubia wakati wa Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia jijini Windhoek. Katika hotuba yake amesisitiza umuhimu wa kufanyia kazi kwa wakati maazimio ya mkutano huo ili kuweza kujenga uchumi imara wa kisekta na kujenga mahusiano mazuri baina ya wananchi wa Tanzania na Namibia. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Naitwa akihutubiwa wakati wa mkutano huo, ambapo pamoja na kuhimiza umuhimu wa kurithishwa historia ya ushirikiano wa Tanzania na Namibia amezitaka sekta zenye makubaliano ya ushiriano kufanyia kazi maeneo yote yanayohitaji utekelezaji ili Wizara za Mambo ya Nje ziweze kuratibu ushirikiano uliopo kwa tija na maslahi ya nchi hizo. Kutoka kushoto, Naibu Waziri Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. David Silinde(Mb.) na Naibu Waziri Wizara ya Nishati, Mhe. Steven Byabato (Mb.)wakifatilia majadiliano katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JCC) kati ya Tanzania na Namibia uliofanyika jijini Windhoek, Namibia. Ujumbe wa Tanzania, kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba akifatilia majadiliano katika mkutano huo. Kutoka kushoto, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Bw. Ally Gugu, Mkurugenzi Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Makamba Makamba wakifatilia Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia uliofanyika jijini Windhoek, Namibia. Ujumbe wa Tanzania Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Naitwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Tanzania na Namibia, Makatibu Wakuu walioongoza ujumbe wa Tanzania na Namibia katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JCC) ngazi ya Maafisa Waandamizi na Mabalozi wa Tanzania na Namibia.