Wednesday, February 17, 2016

Waziri Mahiga azungumzia mafanikio ya Wizara katika siku 100 za Awamu ya Tano

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akikaribishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Mlima katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mkutano na Vyombo vya Habari juu ya mafanikio yaliyopatikana katika Wizara ndani ya siku 100 za kwanza za Serikali ya Awamu ya Tano.
Dkt. Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Wizara katika kipindi cha siku 100 za kwanza za Serikali ya Awamu ya Tano. Mafanikio hayo ni  pamoja na mchango wa Tanzania katika utatuzi wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi; Tanzania kuwa miongoni mwa nchi nne za Afrika zilizochaguliwa wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na China (FOCAC) kwa China kuwekeza kwenye  Viwanda; Kubana matumizi kwa kupunguza safari nje; na kuimarisha Balozi ili ziweze kuiwakilisha Tanzania kikanda na kimataifa.
Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Wizara na Mafanikio yake ndani ya siku mia moja katika Serikali ya awamu ya tano.









Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya  Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akimkaribisha Mhe. Waziri katika mkutano na kumtambulisha kwa Waandishi wa Habari hawapo pichani ili aweze kuzungumza nao. 
Sehemu ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, wakifuatilia Mkutano kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Waandishi wa Habari, Balozi Celestine Mushy (kushoto) Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (katikati), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia na Balozi Innocent Shio, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda. 
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi wakifuatilia Mkutano huo.

Mhe.  Dkt. Mahiga akiagana na Wakurugenzi wa Wizara mara baada ya kumaliza Mkutano na Waandishi wa Habari. Anayeshuhudia mwenye suti ya bluu ni Katibu Mkuu, Balozi Mlima.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.