Wednesday, October 17, 2012

Mhe. Balozi Maajar akutana na Watanzania mjini Iowa‏



Mhe. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (kulia), Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania (Singo na Godlisen) waliokutana naye kwenye Chuo Kikuu cha Des Moines Jimboni Iowa kabla ya kuanza Mkutano wa Iowa - Tanzania mjini Des Moines tarehe 16 Oktoba, 2012.

Mhe. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (kushoto) akisalimiana na Dkt. Allan Hoffman, Rais Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Santa Barbara, Carlifornia ambaye naye alijumuika na Watanzania kwenye mazungumzo hayo na Balozi Maajar kabla ya Mkutano wa Iowa - Tanzania kuanza.


Rais wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ijulikanayo kama Empower Tanzania, Bw. Phil Latesa akizungumza na Dkt. Allan Hoffman na Bw. Singo baada ya mkutano na Mhe. Balozi Maaar (hayupo pichani).


Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar akisalimiana na Watanzania waishio Des Moines Iowa.


Mhe. Balozi Maajar akiwa katika picha na Bw. Singo, alipokutana na Watanzania kabla ya kuhudhuria Mkutano wa II wa Iowa – Tanzania pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Chakula ujulikanao kama World Food Prize unaoendelea mjini Des Moines, Iowa. 


Mhe. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akiwa katika picha ya pamoja na Bi. Mindi Kasiga (kulia), Afisa Mwandamizi (Mawasiliano) katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico kabla ya kuhudhuria Mkutano wa II wa Iowa – Tanzania pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Chakula ujulikanao kama World Food Prize unaoendelea mjini Des Moines, Iowa.


Picha na habari kutoka kwa Mindi Kasiga, Ubalozi wa Tanzania - Washington, DC.





Mhe. Balozi Maajar akutana na Watanzania mjini Iowa‏

Des Moines, Iowa
16 Oktoba, 2012

BALOZI wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar amewaasa Watanzania waishio Jimbo la Iowa mjini Des Moines kujitokeza na kutoa maoni yao kuhusu suala la uraia wa nchi mbili kwenye mchakato wa mabadiliko ya katiba unaoendelea nchini.
Balozi aliyasema hayo alipokutana na Watanzania hao kabla ya kuhudhuria Mkutano wa II wa Iowa – Tanzania pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Chakula ujulikanao kama World Food Prize unaoendelea mjini Des Moines, Iowa.
Alitoa mfano wa kwake binafsi alipokuwa mwanasheria na mwanaharakati ambapo kupitia taasisi mbalimbali walifanikiwa kushawishi na hatimaye kubadilisha sheria zilizowabana wanawake kuwa na haki sawa na wanaume nchini Tanzania.
“Hakuna ushawishi mzuri kama ule unaotoka kwenu nyie wenyewe Wana Diaspora, kwani nyie ndio mliovaa kiatu cha uraia wa nchi mbili na mnajua kinabana wapi” alisisitiza Balozi na kuwaomba wajitokeze kwa wingi kutoa maoni yao sasa wakati muda unaruhusu kufanya hivyo.
Aliongeza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba amethibitisha ugumu uliopo kwa wajumbe wa tume hiyo kusafiri nje ya nchi kukusanya maoni, hivyo aliwataka Watanzania waishio nje ya nchi watembelee tovuti ya mabadiliko ya katiba na kutoa maoni yao http://www.katiba.go.tz
Sambamba na kutoa maoni, Mhe. Maajar aliwaasa Watanzania wa Des Moines kujipanga ili kuunda umoja wa Watanzania ili waweze kushughulikia masuala yanayowahusu kwa pamoja. Alisema Marekani ni nchi kubwa na Watanzania waishio majimbo mengine wameitikia wito huo na sasa kuna Jumuiya za Watanzania kwenye majimbo mengi nchini Marekani.
“Kwenye jimbo hili, ni muhimu sana kuwa na Jumuiya madhubuti ili kutumia fursa hii inayojitokeza kila mwaka ya Mkutano wa World Food Prize, kukutana na viongozi wanaokuja kutoka nyumbani au hata sisi kutoka ubalozini” alihimiza.
Kwa upande wao, Watanzania waishio mjini hapa walimshukuru Balozi Maajar kwa kukutana nao na kuahidi kutekeleza yale yaliyoongelewa. Pia walipendekeza ubalozi wa Tanzania Washington D.C. ujaribu kuboresha njia za mawasiliano ya kisasa kama vile Facebook na Tweeter ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi ambao kutokana na kubanwa na kazi, hawapati nafasi ya kutembelea tovuti ya ubalozi.
Mhe. Balozi yupo mjini Des Moines, IA kwa siku mbili ambapo baadaye leo atahutubia Mkutano wa II wa Iowa – Tanzania kama mgeni rasmi ulioandaliwa na Empower Tanzania, Taasisi isiyo ya Kiserikali yenye makao makuu yake hapa Des Moines, Iowa. Kesho tarehe 17 Oktoba 2012, ataendesha mjadala wa Kukata Njaa kabla ya kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano huu wa World Food Prize.

Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 67 ya Umoja wa Mataifa yazinduliwa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule, akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa ambayo kilele chake ni tarehe 24 Oktoba, 2012. Maadhimisho ya kilele yatafanyika jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karimjee.
Wengine katika picha, aliyekaa ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, Bw. Alberic Kacou na aliyesimama pembeni mwa Katibu Mkuu ni Bw. Songelaeli Shilla, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katikaWizara ya Mambo ya
Nje.


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, Bw. Alberic Kacou (kushoto) akielezea umuhimu wa maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani). Kulia ni Bw. John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Baadhi ya Waandishi kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari wakimsikiliza kwa makini Bw. Kacou (hayupo pichani).

Menejimenti ya Wizara yatembelea Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere

Jengo la Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) linavyoonekana baada ya kukamilika. Kituo hiki kinachomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kimejengwa Jijini Dar es Salaam kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.

Moja ya Kumbi za Mikutano katika Kituo hicho.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M.Haule (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara wakati ujumbe huo ulipotembelea Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

Katibu Mkuu (mwenye suti) akimsikiliza kwa makini Bi. Bertha Lynn, mmoja wa Wataalam walioshiriki katika ujenzi wa Kituo hicho kutoka China alipokuwa akifafanua jambo.Wengine katika picha ni Bw. Huang Mei Luan (kushoto kwa Katibu Mkuu), Mkurugenzi wa Mradi wa ujenzi wa Kituo hicho kutoka China na Bw. Isaya Kapakala, Afisa anayesimamia mradi huo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M.Haule akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara na Wataalam wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

Monday, October 15, 2012

Balozi wa Japan hapa nchini aongoza ujumbe kuonana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia

Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akifafanua jambo kwa wageni waliofika kumtembelea Ofisini kwake leo. Kulia kwa Balozi Kairuki ni Mhe. Masaki Okada, Balozi wa Japan hapa nchini akifuatiwa na Bw. Yoshiyasu Mizuno, Mshauri wa masuala ya Maendeleo ya Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ya hapa nchini. Anayewatazama ni Bw. Takuya Osada kutoka Kampuni ya Global Business Division ya Japan.

Balozi Kairuki (katikati) akiwa na Balozi Okada (kushoto) na Bw. Mizuno wakimsikiliza Bw. Takuya (hayupo pichani) wakati ujumbe huo ulipofika kumtembelea Balozi Kairuki Ofisini kwake leo.

Bw. Takuya akimsikiliza kwa makini Balozi Kairuki (hayupo pichani) alipokuwa akimweleza masuala mbalimbali baada ya kumtembelea ofisini kwake. Anayendika ni Afisa kutoka Ubalozi wa Japan hapa nchini.


Balozi Kairuki akifurahia jambo na Bw. Mizuno wakati wa kuagana baada ya mazungumzo yao.

Mkurugenzi wa Asia akutana na Mwakilishi wa Heshima wa Australia hapa nchini

Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimkaribisha Ofisini kwake Bw. Thiery Murcia, Mwakilishi wa Heshima wa Australia hapa nchini alipomtembelea leo.

Balozi Kairuki akiwa katika mazungumzo na Bw. Murcia.

Balozi Kairuki akimsikiliza kwa makini Bw. Murcia alipokuwa akizungumza nae.

Balozi Kairuki akipitia moja ya nyaraka muhimu alizokabidhiwa na Bw. Murcia wakati wa mazungumzo yao.

Saturday, October 13, 2012

Mhe. Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Ireland hapa nchini

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Fionnuala Gilsenan, Balozi mpya wa Ireland hapa nchini. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam jana.

Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Mhe. Balozi Gilsenan, Bibi Grace Shangali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Anayeshuhudia pembeni mwa Bibi Shangali ni Bi. Felista Rugambwa, Afisa Mambo ya Nje.

Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Gilsenan mara baada ya kupokea hati za utambulisho za Balozi huyo.

Mhe. Rais Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Gilsenan mara baada ya kupokea hati za utambulisho za Balozi huyo. Pembeni mwa Balozi ni Bw. Nicholas Michael, Afisa katika Ubalozi wa Ireland hapa nchini.

Mhe. Balozi Gilsenan akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais.

Mhe. Balozi Gilsenan akisikiliza na kufurahia wimbo wa Taifa lake ulipokuwa ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais. Wengine katika picha kulia kwa Balozi ni Bw. Shaaban Gurumo, Mnikulu na Bw. Japhet Mwaisupule, Kaimu Mkuu wa Itifaki.

Mhe. Balozi Gilsenan akisalimiana na Kiongozi wa Bendi ya Polisi, Inspekta Billy Kachalle mara baada ya kumaliza kupiga nyimbo za mataifa ya Tanzania na Ireland kwa heshima ya Balozi huyo.

Mhe. Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Cuba hapa nchini

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo, Balozi mpya wa Jamhuri ya Cuba hapa nchini.Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam jana.

Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha Mhe. Mahadhi Juma Maalim (kushoto wanaosalimiana), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mhe. Balozi Tormo. Anayeshuhudia pembeni mwa  Mhe. Naibu Waziri ni Bibi Grace Shangali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Mhe. Balozi Tormo mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi huyo. Pembeni mwa Balozi ni Mke wake Bibi Maria Griselda Herviz.

Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Tormo na mkewe Bibi Herviz mara baada ya kupokea hati za utambulisho za Balozi huyo.

Mhe. Balozi Tormo akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.

Mhe. Balozi Tormo akisikiliza Wimbo wa Taifa lake uliokuwa ukipigwa na Bendi ya Polisi (haipo pichani) kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais. Wengine katika picha ni Bw. Shaaban Gurumo (kulia kwa Balozi), Mnikulu na Bw. Japhet Mwaisupule (kushoto kwa Balozi), Kaimu Mkuu wa Itifaki.

Mhe. Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Korea hapa nchini

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisubiri kupokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Chung IL, Balozi mpya wa Jamhuri ya Korea hapa nchini. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam jana.

Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Mhe. Balozi  IL mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi huyo. Kulia kwa BaLozi IL ni mkewe Bibi Junghwa Moon.

Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi IL na mkewe Bibi Junghwa Moon mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi huyo.

Mhe. Balozi IL akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.

Mhe. Balozi IL akisikiliza Wimbo wa Taifa lake uliokuwa ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu. Wengine katika picha ni Bw. Shaaban Gurumo (kulia kwa Balozi) ambaye ni  Mnikulu na Bw. Japhet Mwaisupule (kushoto kwa Balozi), Kaimu Mkuu wa Itifaki.

Friday, October 12, 2012

Mhe. Naibu Waziri apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi wa UNICEF hapa nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kushoto) akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Bw. Jama Gulalid, Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) hapa nchini.

Mhe. Naibu Waziri akifafanua jambo wakati wa mazungumzo  na Bw. Gulalid mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho.

Bw. Gulalid akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kukabidhi Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Naibu Waziri (hayupo pichani).

Mhe. Naibu Waziri akifurahia jambo wakati wa kuagana na Bw. Gulalid mara baada ya mazungumzo yao.

Naibu Waziri akutana na Balozi wa India hapa nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia) akisalimiana na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Debnath Shaw aliyefika ofisini kwa Mhe. Naibu Waziri kwa lengo la kujitambulisha ambapo pia walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

Mhe. Naibu Waziri (kulia) akizungumza masuala mbalimbali na Mhe. Balozi Shaw wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha.

Mhe. Balozi Shaw (kushoto) akizungumza  huku  Mhe. Naibu Waziri akimsikiliza kwa makini.

Mhe. Balozi Shaw akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili ofisini kwa Mhe. Naibu Waziri.

Mhe. Naibu Waziri akiendelea na mazungumzo na Mhe. Balozi Shaw. Wengine katika picha ni Bw. Charles Faini (kushoto kwa Mhe. Naibu Waziri), Afisa Mambo ya Nje na Bw. D.K. Pant (kulia kwa Mhe. Balozi) Afisa kutoka Ubalozi wa India hapa nchini.