Wednesday, June 25, 2014

Kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika, Malabo, Equatorial Guinea

Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania akitoa mchango wa Tanzania kwenye Kikao cha Mawaziri wa Umoja wa Afrika. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja wa Afrika Mhe. Naimi Aziz na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza wakifuatilia mchango huo kwenye mkutano unaoendelea Mjini Malabo Equatorial Guinea tarehe 23-24 Juni 2014.



Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye mazungumzo ya faragha na Mawaziri wenzake wa Mambo ya Nje wa Botswana (juu) Mhe. P.T.C. Skelemani na (chini) Mhe. Netumbo Nandi Ndaitwah wa Namibia pembezoni mwa mikutano ya Mawaziri wa Umoja wa Afrika Mjini Malabo, Equatorial Guinea tarehe 23-24 Juni 2014.



Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akifuatilia majadiliano ya vikao vya wataalam kabla ya Kikao cha Mawaziri kuanza. Wengine pichani ni maafisa wa Mambo ya Nje Sam Shelukindo, Elisha Suku  na Zuleha Khamis. 


Tuesday, June 24, 2014

Makamu wa Rais wa China afungua Kongamano la Taasisi ya Utamaduni Barani Afrika na kuweka Jiwe la Msingi la Ubalozi wa China nchini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Pamoja kwa Taasisi za Confucius Barani Afrika. Taasisi ya Confucius  inajishughulisha na ukuzaji utamaduni na lugha mbalimbali za Afrika  na China ambapo kwa hapa nchini ina matawi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kile cha Dodoma.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala akimkaribisha Mhe. Dkt. Bilal kuhutubia wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa kongamano hilo.
Mhe. Dkt. Bilal akizungumza.

Wajumbe wakimsikiliza Mhe. Dkt. Bilal (hayupo pichani
Mhe. Li naye akizungumza

Mhe. Dkt. Bilal akimsikiliza Mhe. Li (hayupo pichani)

Vikundi vya burudani vikitumbuiza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pamoja kwa Taasisi za Confucius Barani Afrika. Juu ni kikundi cha ngoma kutoka Mkoa wa Dodoma na chini ni Vijana kutoka Chuo Kikuu cha UDOM wakionesha utamaduni wa Kichina wa Kung-Fu.
Mhe. Dkt. Bilal na Mhe. Li wakifurahia burudani zilizokuwa zikitolewa na vikundi mbalimbali (havipo pichani)
Picha ya pamoja.

......Uwekaji Jiwe la Msingi la Jengo la Ubalozi wa China nchini......

Mhe. Li akisalimiana na raia wa China wanaoishi hapa nchini kabla ya kuweka Jiwe la Msingi la Jengo la Ubalozi wa China hapa nchini
Mhe. Bilal na Mhe. Li kwa pamoja na wajumbe wengine wakichota mchanga kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo la Ubalozi wa China hapa nchini litakalojengwa katika Makutano ya Mtaa wa Sokoine na Shaaban Robert Jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja baada ya kuweka Jiwe la Msingi

Picha na Reginald Philip

Mhe. Rais amwapisha Balozi Sokoine

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi Joseph Edward Sokoine ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Hafla hiyo ilifanyika, Ikulu, Dar es Salaam tarehe 24 Juni, 2014 
Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao walikuwepo kushuhudia kuapishwa kwa Balozi Sokoine. Kutoka kulia ni Bibi Victoria Mwakasege, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Innocent Shiyo, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ulaya na Amerika

Balozi Sokoine akisaini hati ya kiapo mbele ya Mhe. Rais Kikwete
Wageni waalikwa wakishuhudia tukio hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule akisalimiana na Mama mzazi wa Balozi Sokoine ambaye alikuwepo kushuhudia tukio hilo.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Sokoine pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wa balozi huyo.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Sokoine, Katibu Mkuu Haule pamoja na Wakurugenzi na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Picha na Reginald Philip



Balozi Sokoine apokelewa kwa shangwe Wizara ya Mambo ya Nje

Balozi Joseph Sokoine ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika akisalimiana na Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uswisi,  Robert Kahendaguza huku Wafanayakazi wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakishangilia mara baada ya Balozi Sokoine kuwasili Wizarani baada ya kuapishwa.
Balozi Sokoine akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Glory Mboya mara baada ya kuwasili Wizarani baada ya kuapishwa.


Balozi Sokoine akisalimiana kwa furaha na Bw. Kelvin Kheri mmoja wa Wafanayakazi Wizarani.

Mapokezi yakiendelea.

Balozi Sokoine akisalimiana na Wafanyakazi wa Wizara walipompokea kwa furaha 
Balozi Sokoine akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Irene Kasyanju mara baada kuwasili.

Picha na Reginald Philip



Monday, June 23, 2014

Makamu wa Rais wa China afungua rasmi Kongamano la Uwekezaji

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe Li Yuanchao akifungua rasmi Kongamano la Pili la Uwekazaji kati ya Tanzania na China. Ufunguzi wa Kongamano hilo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2014. Ufunguzi huo ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwekezaji, Mhe. Mary Nagu, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bi. Julieth Kairuki, Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na Taasisi Binafsi na wadau mbalimbali.
Wajumbe mbalimbali wakifurahia hotuba ya ufunguzi ya  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (hayupo pichani).
Mhe. Pinda, Mawaziri na wajumbe wengine wakimsikiliza Makamu wa Rais wa China, Mhe. Li Yuanchao (hayupo pichani) alipokuwa akifungua Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na China
Wajumbe wakifuatilia ufunguzi
Mhe. Li Yuanchao (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na  Mhe. Pinda (mwenye tai nyekundu), Mhe. Nagu (wa pili kushoto), Mhe. George Mkuchika (wa kwanza kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Youqing (wa kwanza kulia) na Bi. Kairuki. Mkurugenzi wa TIC.
Picha ya pamoja na Wajumbe wa Kongamano

Picha na Reginald Philip

Sunday, June 22, 2014

Makamu wa Rais wa China awasili nchini kwa ziara ya kikazi



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimlaki kwa furaha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2014 kwa ajili ya kuanza rasmi ziara yake ya kikazi  ya siku tano hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju aliyekuwepo Uwanjani hapo kwa ajili ya mapokezi ya Makamu huyo wa Rais.
Mhe. Li Yuanchao akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki mara baada ya kuwasili Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa China Mhe. Li Yuanchao akipita  katikati ya Gwaride la Heshima wakati wa mapokezi yakehuku  akisindikizwa na Mwenyeji wake Mhe. Dkt. Bilal.
Mhe. Li akifurahia kikundi cha burudani kilichokuwa uwanjani hapo (hawapo pichani) wakati wa mapokezi yake.
Moja ya vikundi vya burudani vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais wa China alipowasili hapa nchini.
Picha na Reginald Philip

Friday, June 20, 2014

Waziri Membe azungumza na Balozi wa Oman nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe (Mb), akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Soud Al Mohammed Al-Ruqaish alipofika kwa ajili ya mazungumzo yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili mapema leo tarehe 20 Juni, 2014, Jijini Dar es Salaam.
Waziri Membe akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Oman nchini
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga na Afisa Mambo ya Nje, Batholomeo Jungu wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Balozi wa Oman  hapa nchini (hawapo pichani)
Waziri Membe pamoja na Balozi wa Omani wikifurahia jambo wakati wa mazungumzo yao wa kwanza kushoto ni Afisa aliyeambatana na na Balozi wa Oman.
Picha ya pamoja.


Picha na Reginald Philip



Thursday, June 19, 2014

Balozi mpya wa Marekani nchini ajitambulisha rasmi kwa Waziri Membe


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkaribisha kwa furaha na kwa mara ya kwanza ofisini kwake Balozi wa Marekani hapa nchini, Mhe. Mark Childress alipofika e kwa ajili ya kujitambulishana pia kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani.
Mhe. Membe na Mhe. Childress katika picha ya pamoja.
Mhe. Childress akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili Ofisini kwa Mhe. Membe
Mhe. Membe na Balozi Childress wakiwa katika mazungumzo
Mhe. Childress na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Picha ya pamoja kati ya Mkhe. Membe na Mhe. Childress pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia).