Sunday, July 10, 2016

Waziri Mkuu wa India awasili nchini

Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi akipunga mkono  kusalimia wananchi waliojitokeza kumlaki mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Modi atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 09-10 Julai, 2016
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili nchini. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akisalimiana na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki akisalimiana na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege.

Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana (wa kwanza kulia) akiwaongoza Waheshimiwa Mawaziri Wakuu wakati wa mapokezi 
Mhe. Modi akipunga mkono kuwasalimia wananchi waliojitokeza kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Friday, July 8, 2016

WAZIRI MAHIGA AZUNGUMZIA ZIARA WA WAZIRI MKUU WA INDIA NCHINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza katika Mkutano na wanahabari kuhusu ziara ya Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi anayetarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 9-10 Julai, 2016. Mkutano huo ulifanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz P. Mlima. 
Mstari wa mbele ni baadhi ya Mabalozi na Wakurugenzi kutoka Wizarani wakifuatilia Mkutano 

Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P. Mlima (katikati) akifafanua jambo wakati wa Mkutano na wanaandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kisiga akifafanua jambo kwenye Mkutano na Wanahabari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (wapili kushoto) akitoa maelekezo juu ya masuala mbalimbali kuhusu ziara ya Waziri Mkuu wa India Nchini Mhe. Narendra Modi wakati wa Mkutano na Wanahabari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam Julai.

Tuesday, July 5, 2016

Prof. Mbarawa afungua Semina kuhusu Maendeleo ya Viwanda

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb.) akihutubia kwenye ufunguzi wa Semina ya Kimataifa kati ya China na Afrika kuhusu ushirikiano wa kuendeleza viwanda inayofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Julai 5, 2016.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Susan Kolimba (Mb.) akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa semina ya Kimataifa kati ya China na Afrika kuhusu ushirikiano wa kuendeleza viwanda inayofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing  naye akihutubia kwenye ufunguzi wa Semina hiyo
Baadhi ya Wadau walioshiriki katika Semina ya Kimataifa kati ya China na Afrika kuhusu ushirikiano wa kuendeleza viwanda  iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakifuatilia jambo. Mstari wa mbele kutoka kulia ni Prof. Ibrahim Lipumba, Prof. Moshi na Dkt. Reginald Mengi
Baadhi ya Wakuu wa Idara/Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia semina hiyo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu, Bw. Paul Kabale; Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Bw. Lucas Suka; Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka Luvanda; na Mkurugenzi Idara ya Diaspora, Balozi Anisa Mbega.
Sehemu nyingine ya Wakuu wa Idara/Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wa pili kutoka kulia ni mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki, na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu, Bw. Nigel Msangi nao wakisikiliza kwa makini hotuba zilizokuwa zikiendelea kutolewa kwenye Semina hiyo
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Raslimali watu, Bw. Hamid Mbegu; Mkurugenzi wa Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii, Bw. Eliab Chodota na Mkuu wa Kitengo cha Teknologia ya Mawasiliano, Bibi. Achentalika Maunda wakifuatilia jambo wakati wa Semina.
Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (tai nyekundu), Bw. Adam Isara naye akisikiliza hotuba za ufunguzi katika semina hiyo
Sehemu ya Washiriki wa Semina ya Kimataifa kati ya China na Afrika kuhusu ushirikiano wa kuendeleza viwanda iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakifuatilia Jambo.
Sehemu ya Waandishi wa Habari walio hudhuria ufunguzi wa Semina ya Kimataifa kati ya China na Afrika kuhusu ushirikiano wa kuendeleza viwanda wakitekeleza majukumu yao
Mhe. Kolimba na akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Kimataifa kati ya China na Afrika kuhusu ushirikiano wa kuendeleza viwanda
Naibu Waziri, Mhe. Suzan Kolimba akizungumza na Chombo cha Habari cha Kimataifa cha CCTV na kuelezea Faida na Madhumuni ya Semina hiyo
Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Ufunguzi wa Semina






TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Semina kuhusu Maendeleo ya Viwanda

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amesema kuwa bila ya ujenzi wa miundombinu ya uhakika, Tanzania haitaweza kutimiza malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025.

Alitoa kauli hiyo leo, wakati wa semina ya maendeleo ya viwanda iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa China na kufanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mhe. Waziri alisema kuwa ili miundombinu imara iweze kujengwa nchini, katika mwaka huu wa fedha, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi trilioni 11.8 kwa ajili ya bajeti ya maendeleo na kati ya hizo asilimia 46 ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu. “Asilimia 46 ya bajeti ya maendeleo ni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa miradi ya miundombinu mbalimbali kama barabara, reli ya kiwango cha kimataifa, ununuzi wa ndege na meli”.  

Prof. Mbarawa aliyashukuru makampuni ya China kwa kuwekeza nchini katika miradi mbalimbali mikubwa lakini bado alitoa wito kwa makampuni mengine kutoka nchi hiyo kuja  kuwekeza kwa wingi hapa nchini.

Aliyashauri makampuni kutoka nchini China yaje kuingia ubia na makampuni ya hapa nyumbani katika uendelezaji wa miradi mbalimbali kama ya reli barabara na nishati. Aliendelea kueleza kuwa ili kuendeleza sekta ya viwanda nchini, tunahitaji msaada wa mtaji, utaalamu na elimu ya ufundi kutoka kwa marafiki zetu kama nchi ya China.

Aidha, Prof. Mbarawa alisisitiza umuhimu wa kuboresha kiwango cha uzalishaji katika sekta ya kilimo ambayo ndio imeajiri Watanzania wengi hapa nchini. “Sekta ya kilimo imekuwa ikikua kwa asilimia 4 hadi 5 hapa nchini lakini ukuaji huo haujajikita hasa katika kiwango cha uzalishaji (productivity)”. Prof. Mabarawa alisema ili watu wetu waweze kufaidika na kilimo lazima kiwango cha uzalishaji kiboreshwe na  Serikali ya awamu ya tano imejipanga kulifanyia kazi suala hilo.

Mhe. Waziri alihitimisha hotuba yake kwa kuahidi kuwa Serikali itazingatia utunzaji wa mazingira itakapokuwa inatekeleza ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo iliyomo kwenye Mwaka wa Fedha 2016/2017 na miaka mingine itakayofuata.

Akizungumza awali, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba (Mb) aliishukuru Serikali ya Watu wa China kwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo. Alirejea dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kushirikiana na China hususan katika Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika (FOCAC). Alisema Tanzania kuchaguliwa kuwa miongoni mwa nchi 4 ambazo China itahamishia viwanda vyake ni ushahidi wa wazi kuwa nchi hizi mbili zina uhusiano mzuri wa kihistoria.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing alisisitiza umuhimu wa kukuza sekta ya viwanda hapa nchini. Alisema sekta ya viwanda ikikua, itapelekea kufikiwa kwa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, itaongeza ajira, mapato ya Serikali na hivyo kuifanya nchi kujitegemea kifedha. Alimalizia kwa kuihakikishia Tanzania kuwa nchi yake itatimiza yale yote iliyoyaahidi kwenye Mkutano wa FOCAC uliofanyika Afrika Kusini mwaka 2015.
 

Saturday, July 2, 2016

Rais Kagame afungua maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa

Rais Paul Kagame akihutubia katika halfa ya ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam, ambapo alikuwa mgei rasmi katika maonyesho hayo.
Sehemu ya viongozi wa Serikali, Mabalozi, wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na wafanyabishara kutoka mataifa mbalimbali walioshiriki katika maonyesho hayo wakifuatilia hafla ya ufunguzi.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, pembeni akishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (wa kwanza kulia) wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wakishangilia kwa kupiga makofi wakati Mhe. Rais Kagame akitoa Zawadi kwa washindi mbalimbali waliohudhuria katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa
Rais Kagame akibonyeza Kitufe maalumu kilichoandaliwa kuashiria ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba 
Mhe.Rais Kagame na Mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli wakitembelea Mabanda yaliyopo katika viwanja hivyo vya sabasaba na kujionea thamani mbalimbali zikiwemo vitanda vilivyotengenezwa kwa mbao zitokanazo na mti wa Mnazi
Kaimu Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana(wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, kushoto kwao ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Joseph Mwasota 
Rais Kagame akisalimiana na Mtoto aliyejitokeza katika maonyesho hayo katika viwanja vya sabasaba.
Mama Janeth Magufuli na Mgeni wake Mama Jeannette Kagame nao wakiendelea kutembelea mabanda yaliyokuwepo katika viwanja hivyo vya sabasaba

Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Rais - Hotuba Bw. Bujiku Sakila akiwa pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Batholomeo Jungu na Bw. John Pangipita

 

Rais Magufuli na Kagame washiriki dhifa ya Kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, akitakiana afya njema na ushirikiano ulio imara na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame kwenye dhifa ya kitaifa,iliyofanyika Jijijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, Wenza wa Marais Mama Janeth Magufuli na Mama Jeannette Kagame, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na viongozi wengine wakuu wa Serikali.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu (wa kwanza kulia) na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Rwanda mama Jeannette Kagame(wa kwanza kushoto) wakiwa wamesimama wakati nyimbo za taifa zikipigwa 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) (katikati), Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Loiuse Mushikiwabo (wa kwanza kulia) na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Othmani Chande nao wakiwa wamesimama wakati nyimbo za taifa zikipigwa
Mhe. Rais Magufuli akizungumza kwenye Dhifa ya kitaifa ambapo alimshukuru Mhe.Rais Kagame kwa kuitikia mwaliko wake na Kufungua maonyesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).
Mhe. Rais Kagame naye akizungumza katika Dhifa hiyo ambapo alimshukuru mwenyeji wake Mhe. Magufuli kwa mapokezi na kuahidi kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Rwanda yaliyodumu kwa muda mrefu.
Sehemu ya Viongozi wa Serikali waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa na Waheshimiwa Marais.
Sehemu nyingine ya viongozi wa Serikali waliohudhuria Hafla hiyo wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na Waheshimiwa Marais
Balozi wa China nchini Tanzania (wa pili kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (wa kwanza kushoto) pamoja na maafisa kutoka Ubalozi wa China hapa nchini pia walishiriki katika hafla hiyo.  
Rais Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Sinde Warioba na Rais Kagame akisaliamiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ackson Tulia.
Rais Kagame akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt.Susan Kolimba(Mb)

Friday, July 1, 2016

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ampokea Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe.Paul Kagame

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mhe. Paul Kagame yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia leo, ambapo anatarajiwa kufungua Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam 
 Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akiwa na mkewe mama  Jeannette Kagame wakipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam.


Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege. 
Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam.
 Waheshimiwa Marais wa Tanzania na Rwanda wakiangalia vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgeni wake wakisalimia wananchi waliofika viwanja vya Ikulu  kumlaki mgeni mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (wa sita kulia), akiwa katika Mkutano na Mgeni wake Mhe. Rais Paul Kagame pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali wa pande zote mbili.
 Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Mhe. Rais Dkt. Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb)(kushoto) na  Rwanda Mhe. Louise Mushikiwabo wakipongezana mara baada ya kukamilisha zoezi la kuwekeana saini makubaliano ya ushirikiano yaliyofikiwa katika kikao cha Tume ya pamoja ya kudumu ya Ushirikiano baina ya serikali ya Tanzania na Rwanda, kilichofanyika mwishoni mwa mwezi April. 
Uwekaji saini ni moja ya shughuli zilizoshuhudiwa na Wahemiwa Marais wa Tanzania na Rwanda.