Mazungumzo yakiendelea. Kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi wa Marekani. |
Tuesday, October 24, 2017
Waziri Mahiga akutana kwa mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini
Friday, October 20, 2017
Ujumbe wa Mfalme wa Oman watembelea eneo la EPZA-Bagamoyo
Mhe. Ndikilo akipokea zawadi kutoka kwa Mhe. Dkt. Mohammed. |
Wakati huo huo Ujumbe wa Mfalme wa Oman ulipata fursa ya kutembelea eneo la kihistoria la Kaole Wilayani Bagamoyo, ambapo waliweza kusikia mengi kuhusiana na historia ya eneo hilo na kujionea maeneo mbalimbali yanayohusisha historia ya Tanzania na Oman.
Mhe. Dkt. Mohammed akinywa Maji katika kisima ambacho maji yake huwa hayakauki na hivyo iliaminika kuwa ukinywa maji hayo unaongeza siku zako za uhai. |
Mkutano na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Suzan Kolimba (Mb) akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari( Hawako pichani) kuhusu maadhimisho ya Miaka 72 ya Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC), tarehe 19 Oktoba,2017, Dar es Salaam, kulia kwake ni Bw. Alvaro Rodriguez Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini na kushoto ni Balozi Celestine Mushy Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa . Mwaka huu siku hii itaadhimishwa katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam Oktoba 24,2017 , Maadhimisho hayo yatafikia kilele katika tukio litakalofanyika katika Kisiwa cha Unguja, Zanzibar. Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo mwaka huu ni "Maeendeleo ya Viwanda hayana budi kuzingatia Utunzaji Mazingira ili kuleta Maendeleo endelevu".
Baadhi ya maafisa wa Wizara na Umoja wa Mataifa, wakifuatilia mkutano huo, wa kwanza kulia ni Bi. Wendy Bigham - Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Sihirika la Chakula Duniani(WFP), Bw. Jestus Nyamanga Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na mwisho ni Bw. Charles Faini Katibu wa Naibu Waziri.
Thursday, October 19, 2017
Watanzania wahimizwa kudumisha na kuuenzi utamaduni wao
Kikundi cha ngoma kutoka nchini Oman ambacho ni sehemu ya ujumbe wa Mfalme wa Oman uliopo nchini kwa ziara kikitumbuiza jukwaani. |
Mhe. Dkt. Kigwangalla na Mhe. Dkt.Mohammed wakijadiliana jambo. |
Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima akifuatilia buruduni iliyokuwa ikitolewa na kikundi cha ngoma kutoka Oman. Wengine ni sehemu ya ujumbe wa Serikali ya Tanzania na Oman. |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Oman ikifuatilia burudani. |
Bendi ya Jeshi kutoka nchini Oman ambayo pia ni sehemu ya ujumbe huo ilitoa burudani kwa wananchi waliohudhuria hafla hiyo. |
=======================================================================
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla amewataka Watanzania kuwa
mabalozi wazuri katika kuzitangaza na kuzidumisha mila, tamaduni na desturi zao
kwakua ndio nguzo na utambulisho wa Mtanzania popote Duniani.
Waziri
Kigwangala aliyasema hayo katika sherehe za muziki wa utamaduni wa Oman
zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam tarehe 18
Oktoba 2017.
Sherehe
hizo ambazo Mgeni rasmi alikuwa Mhe. Dkt. Kigwangalla, ziliandaliwa na ujumbe wa Mfalme wa Oman uliokuja na Meli ya Mfalme huyo nchini kwa ziara ya siku
sita inayotarajiwa kumalizika siku ya Jumamosi tarehe 21 November 2017.
Mhe.
Kigwangala alisema kupitia tamasha hilo la muziki na ziara nzima kwa ujumla,
Oman inapata fursa ya kujitangaza na kuutumia utamaduni wao kama sehemu ya
utalii na kwamba hii ni nafasi ya pekee kwa Watanzania kujifunza namna gani watu wa mataifa
mengine wameweza kutumia utamaduni wao kwa tija na kuongeza pato la Taifa.
Aidha,
alisisitiza ni wakati sasa makundi yote ya utalii yaliyopo nchini kama utalii wa kwenye maji,
utalii wa misitu hususan kwa kutumia upekee wa mazingira yetu, fukwe na hata
historia ya binadamu vikaendelea kuhifadhiwa na kupatiwa ubunifu zaidi wa namna
ya kuvitangaza na kupata mfumo wa kisasa kwa ajili ya kuwezesha watalii wengi kuingia
na kutoka nchini kwa namna bora zaidi.
Halikadhalika
akaongeza kwa kusema “Nchi yetu imebarikiwa sana kwa kuwa na idadi kubwa ya
vivutio vya utalii ukilinganisha na Oman, katika fursa niliyopata ya kukutana
na Naibu Waziri wa Utalii wa Oman ambaye ameambatana na ujumbe huu nimeweza
kuzungumza naye mengi ambayo tutayaweka katika utekelezaji ili sekta ya utalii
iweze kuongeza fedha za kigeni zaidi.”
Kwa upande wake Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Bw. Mohammed bin Hamad
Al-Rumhy ameahidi kuwa Serikali ya Oman itaendeleza undugu huo kwa kufanya
biashara na kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuweza
kuingia katika soko la ushindani duniani.
Lengo
kuu la ziara ya ujumbe huo ni kutangaza amani katika ukanda wa Afrika Mashariki
sambamba na kudumisha undugu uliopo baina ya Tanzania na Oman ambapo utamaduni
wa mataifa haya mawili umekuwa ukifanana hususan katika ukanda wa pwani kufuatia
historia na muingiliano wa wananchi wake katika shughuli mbalimbali za kiuchumi
na kijamii.
Tuesday, October 17, 2017
Taarifa kuhusu kuzingatia sheria katika katika kuingiza au kutoa mifugo nchini kwa ajili ya malisho na maji.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KUHUSU KUZINGATIA SHERIA KATIKA KUINGIZA
AU KUTOA MIFUGO NCHINI KWA AJILI YA
MALISHO NA MAJI
Hivi karibuni, tumeshuhudia kuibuka kwa wimbi kubwa
la uungizaji wa mifugo kutoka nchi jirani kuingia nchini kwa ajili ya malisho
na maji bila kufuata sheria za nchi. Uingizaji wa mifugo kutoka nchi moja
kwenda nyingine una madhara mengi, ikiwemo kiusalama, uharibifu wa mazingira na
kueneza magonjwa ya mifugo.
Ikumbukwe kuwa tarehe 13 Oktoba, 2017, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa agizo la kuondoa
mifugo yote iliyo nchini kinyume cha sheria ndani ya siku saba (7). Kutofanya hivyo kutapelekea
mifugo hiyo kutaifishwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kufuatia agizo hilo, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatoa
wito kwa Watanzania wote wenye mifugo nchi jirani wafuate taratibu za kisheria
na kama kuna mifugo kwenye malisho nje ya Tanzania waiondoe mara moja ili
kuepusha hasara na usumbufu.
Aidha,
wizara inatoa wito kwa Watanzania hususan wanaoishi Mikoa iliyopakana na
nchi jirani kuwa wazalendo kwa kutokushirikiana na raia wa nchi za kigeni
kuvunja sheria mbalimbali za nchi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam
17 Oktoba, 2017
Monday, October 16, 2017
Meli ya Mfame wa Oman yawasili Jijini Dar es Salam kwa ziara
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Dkt. Aziz Mlima akisalimiana na Mhe. Dkt. Mahammed. |
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima akisalimiana na Waziri Mahammed. Pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaniva. |
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Ayoub Mndeme akisalimiana na Waziri Mahammed. |
Mhe. Waziri Mwinyi akikaribishwa ndani ya Meli na Mhe. Waziri Mahammed. |
Mhe. Waziri Mwinyi pamoja na Dkt. Kolimba wakiwa katika mazunguzo na Mhe. Waziri Mohammed mara baada ya kuingia ndani ya meli. |
Balozi Dkt. Mlima akifatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea baina ya Mawaziri Mwinyi na Waziri Mahammed. Kushoto kwake ni Balozi wa Oman nchini, Mhe. Ali Abdullah Al-Mahruqi. |
Viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Tanzania na Oman wakijadiliana ndani ya Meli. |
Vikundi vya ngoma vikitumbuiza katika viwanja vya bandari mara baada ya Meli kuwasili. |
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakifuatilia hafla ya mapokezi ya Meli ya Mfalme wa Oman. |
Waziri Mwijage akutana na Balozi wa India nchini
Mhe. Dkt. Kolimba akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Waziri Mwijage na Balozi Arya. |
Mazungumzo yakiendelea |
Saturday, October 14, 2017
Taarifa kuhusu ziara ya meli ya Kifalme kutoka Oman nchini
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa kuhusu ziara ya meli ya Kifalme kutoka Oman nchini
Meli ya Kifalme ya FULK AS SALAAM ya Mfalme Qaboos Bin Said Al Said wa Oman iliyo katika ziara ya kirafiki katika Pwani ya Afrika Mashariki itatia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam kwa ziara ya siku sita kuanzia tarehe 16 hadi 21 Oktoba, 2017. Lengo kuu la ziara hiyo ni kueneza ujumbe wa amani, upendo na kuimarisha urafiki uliodumu kwa muda mrefu kati ya Oman na Tanzania.
Meli hiyo ambayo imeanzia Zanzibar tarehe 12 hadi 15, 2017 inatarajiwa kuja na ujumbe wa zaidi ya watu mia tatu (300) ukiongozwa na Mhe. Mohammed bin Hamad Al Rumhy, Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman ambaye ataongozana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Umma ya Kukuza Uwekezaji nchini Oman, Dkt. Salim Al Nasser Ismaily na Mhe. Maitha Al Mahrouqi, Katibu Mkuu wa Utalii.
Mara baada ya kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam, Meli hiyo itapokelewa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Hussein Ali Mwinyi (Mb.) na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Aidha, tarehe 17 Oktoba, 2017 kutakuwa na hafla maalum ya chakula cha mchana ndani ya Meli hiyo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Tarehe 18 Oktoba, 2017 kutakuwa na tukio la Muziki wa Kitamaduni utakaopigwa mubashara na Bendi kutoka Oman katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Pia tarehe 19 Oktoba, 2017 wananchi wakiwemo wanafunzi wataruhusiwa kufanya ziara ya kutembelea Meli hiyo kwa utaratibu maalum. Pamoja na kutembelea Tanzania, Kenya ni nchi nyingine iliyopewa nafasi ya kutembelewa na Meli hiyo ya Kifalme.
Meli hiyo itaondoka Bandari ya Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2017 kuelekea Mombasa, Kenya.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam
14 Oktoba, 2017
Thursday, October 12, 2017
Balozi wa Hispania atembelea Wizara
Mazungumzo yakiendelea. |
Wednesday, October 11, 2017
Tanzania na Cuba kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano
Mkutano ukiendelea |
Subscribe to:
Posts (Atom)