Tuesday, February 13, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - Fursa za Ufadhili wa Masomo kwa Watanzania na Tuzo ya Utalii kwa Tanzania


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki Profesa Adolph Mkenda 



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO KWA WATANZANIA NA TUZO YA UTALII KWA TANZANIA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mapema mwezi Februari imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda mfupi na muda mrefu katika kada mbalimbali kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea, Serikali ya Misri na Malaysia.

Kwa upande wa ufadhili wa masomo ya muda mfupi, Serikali ya Korea imetoa nafasi nne (4) kwa ajili ya Watumishi wa Umma katika Sekta ya Afya. Nafasi hizo ni kwa ajili ya Mafunzo ya Uganga (Clinical Experts) nafasi mbili (2), Utawala katika masuala ya Afya (Health Administrator)  nafasi moja (1) na Afisa Mwandamizi katika masuala ya Afya nafasi moja (1). 

Mafunzo hayo ambayo yanafadhiliwa na Korea Foundation for International Healthcare yapo chini ya program ya “Dr. Lee Jong-wook fellowship program” kwa mwaka 2018. Maombi ya nafasi hizo yaelekezwe Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambao ni waratibu wakuu katika sekta ya afya.

Kutoka Serikali ya Misri, Wizara imepokea nafasi mbili (2) za mafunzo ya muda mfupi kwa Watangazaji kutoka nchi za Afrika “19th Basic Training Course for the African Broadcasters”. Mafunzo yatafanyika Misri kuanzia tarehe 25 Februari, 2018 hadi 25 Machi, 2018. Mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Halikadhalika, Wizara imepokea nafasi mbili (2) za Mafunzo ya muda mfupi katika Teknolojia ya Uchakataji Madini (Minerals Processing Technology) yatakayofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 18 hadi 29 Machi, 2018. Mratibu wa Mafunzo haya ni Wizara ya Madini.

Kutoka nchini Malaysia, Wizara imepokea mwaliko wa nafasi mbili (2) za kushiriki Mashindano ya 60 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quran ya 1439H/2018 yatakayofanyika Kuala Lumpur, Malaysia kuanzia tarehe 07 hadi 12 Mei, 2018. Mashindano hayo yanaratibiwa na Ofisi ya Mufti, zanzibar na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA).

Kuhusu mafunzo ya muda mrefu, Wizara imepokea  fursa za ufadhili wa masomo kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu katika kozi mbalimbali kwa ajili ya Watanzania wote kutoka Jamhuri ya Korea.

Fursa hizo za masomo ambazo zinafadhiliwa na Wizara ya Elimu ya Korea zinapatikana kupitia tovuti ya    “2018 Global Korea Scholarship” ambayo ni http://www.studyinkorea.go.kr. Tovuti hii imeainisha taarifa na taratibu zote za namna ya kuomba. Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni tarehe 15 Machi, 2018. Aidha,  nakala ngumu ya fomu za maombi ziwasilishwe Ofisi za Ubalozi wa Korea nchini mara baada ya kukamilisha maombi ya mtandaoni (online application).  Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao mapema kabla ya tarehe tajwa hapo juu. Mratibu mkuu wa fursa hizi ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Katika hatua nyingine, Wizara imepokea nafasi tano (5) za ufadhili wa mafunzo kwa ngazi ya shahada ya kwanza na nafasi mbili (2) za ufadhili wa mafunzo kwa ngazi ya shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Helwan cha nchini Misri. Mafunzo ya Shahada ya kwanza yanatolewa kwenye fani za Utalii na masuala ya Hoteli, Biashara, Uhandisi, Kompyuta na Teknolojia. Aidha, ufadhili masomo ya shahada ya uzamili unatolewa kwenye fani za Sanaa na Muziki (Fine Arts and Music).   

Mafunzo  hayo yatafanyika kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Maombi yote yaelekezwe Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania ambao ndio waratibu wakuu.

Wizara inatumia fursa hii kuwahimiza wale wote watakaoomba nafasi hizo kuhakikisha wanatimiza vigezo na masharti ya maombi hayo ili mamlaka zinazohusika na uchambuzi wa ubora ziweze kupata Watanzania wenye sifa kwa ajili ya kuwajengea uwezo na kuliletea taifa maendeleo.

Wizara inauhakikishia umma wa Watanzania kuwa itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha inasimamia upatikanaji wa fursa za ufadhili wa masomo na ajira mbalimbali zinazowasilishwa na nchi rafiki, Mashirika ya Kikanda na Kimataifa na kuhakikisha zinawafikia Watanzania ili wanufaike na fursa hizo. 

Wakati huohuo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea Tuzo kutoka Serikali ya Urusi kama mshindi wa pili wa mashindano ya  dunia katika kigezo cha nchi nzuri zaidi kutembelea duniani. 

Tuzo hizi ambazo hutolewa na National Geographic Traveler Awards ni tuzo mashuhuri zaidi nchini Urusi katika sekta ya uchukuzi na utalii. Aidha, kupitia Jarida Mtandao la Utalii la nchini Urusi, wasomaji 270,000 walipata nafasi ya kupiga kura na matokeo kutangazwa tarehe 30 Novemba, 2017.  

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miaka 6 ambapo wapiga kura nchini Urusi wanaichagua Tanzania kama nchi nzuri zaidi kutembelea. Mwaka 2011 Zanzibar ilipokea tuzo ya aina hii kwa nchi za Afrika.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
13 Februari, 2018

Ziara ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Wizara ya Mambo ya Nje

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda  akifungua Mafunzo ya siku moja kwa wanachuo wa chuo cha Taifa cha Ulinzi yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, tarehe 12 Februari,2018. Lengo la mafunzo hayo ilikuwa kuwapa uelewa wanachuo hao kuhusu majukumu ya Wizara.


Major General Yacoob Mohamed  Commandant, Mkuu wa chuo cha Taifa cha Ulinzi akitoa hotuba baada ya ufunguzi wa Mafunzo

 Wajumbe wakifuatilia mada katika mafunzo hayo

Sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mafunzo hayo


Balozi Innocent Shiyo akitoa mada katika ziara hiyo kuhusu baadhi ya majukumu ya Wizara 

 Sehemu ya Wanachuo wakifuatilia mafunzo

 Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizarani wakifutialia mafunzo hayo

 Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Wizarani akitoa mada katika mafunzo hayo Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea


Katibu Mkuu Prof. Adolf Mkenda na Balozi Peter Kalaghe wakifuatilia mafunzo hayo 

Baadhi ya  Wakurugenzi kutoka Wizarani wakifuatilia mafunzo hayo

Baadhi ya wajumbe wa mafunzo hayo wakifuatilia mada

Major General Mohamed akikabidhi zawadi kwa Katibu Mkuu Prof Mkenda

Bi. Robi Bwiru Afisa Habari kutoka Wizarani akielezea ratiba ya Mafunzo hayo.

Picha ya Pamoja  baada ya Mkutano

Monday, February 12, 2018

Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke, alipomtembelea Wizarani tarehe 12 Februari,2018, Dar es Salaam
Prof. Mkenda akizungumza na Mhe. Balozi Cooke,katika mazungumzo hayo Prof. Mkenda  alisema Mahusiano ya Uingereza na Tanzania yana historia ndefu, nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana katika maeneo mbalimbali kama vile biashara, uwekezaji, utalii na elimu.

Naye Mhe. Balozi Cooke alimweleza Prof Mkenda namna yeye na Wanadiplomasia wenzake  walivyofurahishwa na maandalizi ya hafla ya mwanzo wa mwaka kwa Mabalozi (Sherry Party), vilevile Mhe. Cooke alisema Serikali yake inaunga mkono Serikali ya Tanzania kwa juhudi inazofanya ili kufikia uchumi wa viwanda, alisema Uingereza  itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya maendeleo. 

Balozi Cooke naye akielezea jambo kwa Prof. Mkenda
Mazungumzo yakiendelea, wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika na Ulaya Bw. Salvatory Mbilinyi, na wa kwanza kushoto ni Naibu Balozi Ubalozi wa Uingereza Bw. Matt Sutherland 



Hafla ya chakula cha jioni kwa Wajumbe wa Baraza la Wakimbizi Duniani yafana

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni na Wajumbe wa Baraza la Wakimbizi Duniani. Hafla hiyo iliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuhudhuriwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne na Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Wakimbizi Duniani, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wakimbizi Duniani Mhe. Lloyd Axworthy, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani,  Balozi Simba Yahaya (hawapo pichani).  Hafla hiyo imefanyika katika Hotel ya Hyatt Regancy, Jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.
Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Gerald Mbwafu (wa kwanza kushoto), Afisa Mambo ya Nje, Bi.Ramla Hamis (wa pili kutoka  kushoto) pamoja na Mjumbe wa Baraza la  Wakimbizi Duniani nao wakiwa katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wakimbizi Duniani, Mhe. Lloyd Axworthy naye akitoa neno la shukrani kwa Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mapokezi yao hapa nchini.
Mhe. Axworthy akiendelea kuzungumza huku meza kuu wakimsikiliza kwa makini
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza hilo nao wakiendelea kumsikiliza Mhe. Axworthy (hayupo pichani).
Sehemu nyingine ya wageni waalikwa wakiendelea kumsikiliza Mhe. Axworthy alipokuwa akizungumza.  
Bi. Nguse Nyerere, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa akisherehesha kwenye hafla hiyo
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (wa kwanza kulia), pamoja na Mhe. Lloyd Axworthy wakifurahia jambo kwa pamoja.










Saturday, February 10, 2018

Waziri Mahiga awa mgeni rasmi maadhimisho ya miaka 39 ya Taifa la Iran

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati wa maadhimisho ya 39 ya  Taifa la Iran. Mhe. Mahiga ambaye alikuwa alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alitumia fursa hiyo kuelezea mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Iran katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara na elimu. Aidha alilipongeza taifa hilo kwa hatua kubwa ya maendeleo wanayopiga hususan katika matumizi ya teknolojia.
Waziri Mahiga akiendelea kuzungumza kwenye maadhimisho hayo.
Sehemu ya Mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia hotuba ya Waziri Mahiga (hayupo pichani).
Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe.Mousa Farhang naye akitoa hotuba wakati wa maadhimisho hayo ya 39 ya taifa lao
Sehemu ya viongozi wa dini pamoja na wageni waalikwa nao kwa pamoja wakisikiliza hotuba kwenye maadhimisho hayo.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nao wakiwa katika hafla hiyo. 
Sehemu ya raia wa Iran wanaoishi nchini na wageni waalikwa wakifatilia matukio wakati wa maadhimisho hayo
Waziri Mahiga akizungumza jambo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe.Mousa Farhang
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (kulia) pamoja na Katibu wa Waziri Bw. Gerald Mbwafu nao walihudhuria hafla hiyo
Waziri Mahiga akisalimiana na Sheikh al Hadi Musa Salim, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam walipokutana kwenye hafla hiyo.  
Waziri Mahiga akisalimiana na Balozi wa Algeria nchini Tanzania Mhe.Saad Belabed walipokutana nae kwenye hafla hiyo.
Picha ya pamoja.













Matukio ya Hafla ya Mwanzo wa Mwaka kwa Mabalozi ( Sherry Party)

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe.Balozi Augustine Mahiga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda,wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini katika sherehe ya kukaribisha Mwaka mpya 2018 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, tarehe 10 Februari 2018.

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mhe. Balozi Mahiga na Katibu Mkuu Prof. Mkenda wakiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi Wakuu, Wawakilishi wa Heshima na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

 Waheshimwa Mabalozi wakiwa katika mchapalo kabla ya kuanza Tafrija
Katibu Mkuu, baadhi ya Wakurugenzi katika hafla hiyo

Balozi Grace Mujuma akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo

Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Wizarani waliohudhuria hafla hiyo

Sehemu ya Wakurugenzi na  Maafisa wa Wizara

Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizarani


Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mhe. Balozi Mahiga wakiwasalimia na kuwakaribisha Mabalozi 






Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara wakiwa katika hafla hiyo.