Thursday, November 22, 2018

Mhe. Dkt. Ndumbaro awa mgeni rasmi maadhimisho ya Mshikamano na Taifa la Palestina


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Mshikamano na Taifa la Palestina akitoa hotuba yake kwenye maadhimisho hayo ambayo yalifanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 21 Novemba, 2018.  Katika hotuba yake, Mhe. Naibu Waziri alisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na Taifa la Palestina ili kuhakikisha taifa hilo linaondokana na hali zote za kuonewa na kugandamizwa na kuwa huru.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mhe. Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani).
Sehemu nyingine ya wageni waalikwa akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Dkt. Bashiru Ali (wa pili kushoto) wakifuatilia hotuba ya Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina.
Wageni waalikwa wakiwemo watoto ambao ni raia wa Palestina wanaoishi nchini wakiwa kwenye maadhimisho hayo


Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hamdi Abu Ali akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina yaliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

Mhe. Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro kwa pamoja na Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu wakifuatilia hotuba ya Balozi Abu Ali (hayupo pichani).


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ali naye akizungumza wakati wa maadhimisho hayo

Afisa Habari kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) nchini, Bi. Stella Vuzo nae akitoa salamu za Ofisi hiyo kuhusu maadhimisho hayo


Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza Mhe. Dkt. Salim alipokuwa akimweleza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina


Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza Mhe. Dkt. Salim. Pembeni ni Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hamdi Abu Ali


Viongozi wa meza kuu wakiwa wamesisima kwa heshima wakati nyimbo za Taifa la Tanzania na Palestina zikiimbwa wakati wa maadhimisho hayo

Katibu Mkuu wa CCM, Mhe. Dkt. Bashiru Ali (kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi (katikati) na mmoja wa wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina

Balozi Mwinyi akimweleza jambo  Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Charles Faini wakati wa maadhimisho hayo

Sehemu ya Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioshiriki maadhimisho hayo

Mhe. Naibu Waziri akimkabidhi zawadi Bi. Zaheeda Alishan ambaye ni mshindi wa kwanza wa shindalo la uchoraji wa picha zinazoelezea matukio mbalimbali kuhusu  Palestina

Viongozi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Bw. Jaykesh Rathod (mwenye mfuko) ambaye ni mshindi wa pili wa  shindano la kuchora picha zinazoelezea matukio mbalimbali ya Palestina

Mhe. Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez ambaye nae alishiriki maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina


Mhe. Dkt. Ndumbaro akipata maelezo ya picha kutoka kwa mshindi wa kwanza, Bi. Alishan

Mshindi wa kwanza, Bi.Alishan (kulia) akiwa pamoja na wageni waalikwa kwenye picha yake iliyompatia ushindi.

Mhe. Dkt. Ndumbaro akipata maelezo kutoka kwa mshiriki mwingine wa shindano la kuchora

Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza mshiriki wa maonesho hayo ya picha kuhusu Palestina

Mhe. Dkt. Ndumbaro akipata maelezo kutoka kwa mshiriki mwingine
Mhe. Dkt. Ndumbaro akikaribishwa na Mhe. Balozi Hamdi mara alipowasili kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina

Mhe. Dkt. Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo

Wednesday, November 21, 2018

Tanzania wins the Best Tourist Destination Award in Russia


 PRESS RELEASE

Tanzania wins the Best Tourist Destination Award in Russia

Tanzania has won the Award for the ‘’Best Destination to the World’’ in the Category of Exotic Destination 2018.

Today, on 21st November, 2018, the Ambassador of Tanzania to Russia, His Excellency Maj. Gen. (Rtd) Simon Mumwi on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania will be receiving a Russian National Geographical Traveler Award at the ceremony scheduled to be held in Moscow.

Tanzania won the Award after online voting conducted by the Russian version of National Geographic Magazine that involved 263,000 online readers.

Tanzania is winning this Award for the third time since 2011 where Zanzibar was chosen as the Best Beach Tourist Destination in Africa and therefore awarded the Star Travel Award. Last year, Tanzania also received a National Geographical Travel Award as the second best destination in the world in the category of exotic destination.

These achievements reflect efforts made by the Government of Tanzania through its Embassy in Russia, Ministries of Tourism and Natural Resources both in Tanzania Mainland and Zanzibar and other Institutions in tourism industry.

Through these efforts, the volume of Russian tourists visiting Tanzania has been increasing. For instance; last year (2017) 10,060 tourists from Russia visited Tanzania as compared to only 4,021 tourists in 2012.

More concerted efforts will be made by the Ministry of Foreign Affairs and other stakeholders to promote Tanzania as the best tourist destination in the world and looking forward to see more Russian tourists choosing Tanzania as their best destination for tourism.





Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma
21st November 2018.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania yashinda Tuzo ya Utalii nchini Urusi

Tanzania imeshinda tuzo ya utalii kwa kuonekana ni eneo bora zaidi la utalii duniani nchini Urusi kwa mwaka 2018 (The Best Destination to the World in the Category of Exotic Destination 2018).

Leo tarehe 21 Novemba 2018, Balozi wetu nchini Urusi Mhe. Maj. Gen. (Mst). Simon Mumwi atapokea Tuzo hiyo kutoka Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine” jijini Moscow kwa niaba ya nchi.   

Tanzania imepata ushindi huo kutokana na kura zilizopigwa kwenye mtandao wa jarida hilo la “National Geographic Magazine” lililoshirikisha wapiga kura 263,000 kwa njia ya mtandao.

Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka saba tokea mwaka 2011, raia wa Urusi kupitia jarida hilo wanaichagua Tanzania kama eneo bora zaidi la utalii. Mwaka 2011, Zanzibar ilipata tuzo ya ‘Star Travel’ kama eneo bora zaidi la utalii wa ufukweni katika bara la Afrika na mwaka jana, Tanzania ilipata tuzo ya NGT na Tanzania ilishinda nafasi ya pili katika tuzo hiyo  katika kundi la eneo bora la utalii duniani.

“National Geographic Traveller Awards” (NGT Awards) ni tuzo ya kifahari zaidi katika sekta ya utalii nchini Urusi na hutolewa na Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine”.

Mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wetu Urusi, Wizara za Utalii za Tanzania Bara na Zanzibar, na Taasisi zote zinazosimamia masuala ya utalii za ndani na nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.

Kupitia juhudi hizi, idadi ya watalii wanaokuja Tanzania kutoka Urusi imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, idadi hiyo imeongezeka kutoka watalii 4,021 mwaka 2012 hadi watalii 10,060 mwaka 2017.  

Wizara kupitia Ubalozi wetu itaendelea kuongeza juhudi za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na tunategemea kwa kushirikiana na wadau wengine katika juhudi hizi, idadi ya watalii kutoka Urusi wanaokuja nchini itaongezeka zaidi.




Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
21 Novemba 2018


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Iran nchini


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Iran nchini, Mhe. Mousa Farhang alipofika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Mhe. Naibu Waziri kwa kuteuliwa kwenye wadhifa huo na kuzungumzia uhusiano kati ya Tanzania na Iran.
Mhe. Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Balozi Farhang kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Iran.
Ujumbe uliofuatana na Balozi Farhang kutoka Ubalozi wa Iran hapa nchini ukifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Balozi Farhang (hawapo pichani)


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Zainab Angovi (kushoto) kwa pamoja na Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Charles Faini na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Kisa Mwaseba wakifuatilia na kunukuu mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Balozi Farhang (hawapo pichani).

Mazungumzo yakiendelea

Balozi Farhang akimpatia Mhe. Dkt. Ndumbaro zawadi ya sanaa ya kutengenezwa kwa mkono kutoka Iran


Wawekezaji kutoka Uturuki wajionea fursa za uwekezaji jijini Dodoma



Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi akitoa taarifa ya fursa za uwekezaji zinazopatikana jijini Ddodma kwa wafanyabiashara wakubwa kutoka Uturuki ambao wameonesha dhamira ya kuwekeza katika jiji hilo. Fursa zilizoelezwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli yenye hadhi ya nyota tano, ujenzi wa maduka makubwa (shopping malls), masoko makubwa, shule za kimataifa na nyumba za kuishi. Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dodoma (DOWASA walikuwepo kuwahakikishia wawekezaji hao kuwa nishati ya umeme na maji sio tatizo jijini Dodoma. wawekezaji hao wamekuja kufuatia jitihada zinazofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo.  


Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Maduka Kessy alifungua mkutano kikao hicho kwa kuwahahakishia wawekezaji hao ushirikiano unaohitajika ili dhamira yao iweze kutimia.
Sehemu ya wawekezaji hao wakimsikiliza kwa makini Bw. Kunambi.
Wawekezaji wakimsikiliza kwa makini Bw.  Kunambi aliyekuwa akielezea maeneo mbalimbali ya uwekezaji katika jiji la dodoma.
Juu na Chini ni Sehemu ya watumishi wa Serikali na Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji wakimsikiliza Bw. Kunambi.

Wawekezaji kutoka Uturuki walipata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali mara baada ya kupata maelezo juu ya maeneo mbalimbali ya uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma.


Majadiliano yakiendelea wakati wa mkutano.
Wawekezaji walipata fursa ya kutembelea kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika jiji la Dodoma.
Wawekezaji kutoka Uturuki wakipata maelezo ya ramani ya eneo la uwekezaji kutoka kwa Mchumi na Mratibu wa Maswala ya Uwekezaji katika Halmashauri ya jiji, Bw. Abel Msangi.
Hili ndio eneo la uwekezaji lililotembelewa na wawekezaji hao kutoka uturuki.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Maduka Kessy akiwaelezea jambo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bw. Jestas Nyamanga pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi
Wawekezaji kutoka Uturuki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wao.













Monday, November 19, 2018

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania, Perth pamoja na Balozi wa Kenya nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Konseli wa Heshima wa Tanzania kwenye Jimbo la Perth nchini Australia, Bw. Didier Murcia alipofika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba, 2018 kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Naibu Waziri  pamoja na kumweleza utekelezaji wa majukumu yake katika kuiwakilisha Tanzania, Perth. 

Ujumbe uliofuatana na Bw. Murcia. Kutoka kushoto ni Bw. James Chialo na Bw. Thierry Murcia kutoka Kampuni ya Ndovu Resources ya jijini Dar es Salaam

Bw. Murcia akimweleza jambo Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa mazungumzo yao

Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Katibu wa Mhe. Naibu Waziri, Bw. Charles Faini.



..........................Mkutano kati ya Naibu Waziri na Balozi wa Kenya nchini


Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Dan Kazungu. Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba 2018. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia Balozi Kazungu alitumia fursa hiyo kumweleza Mhe. Naibu Waziri kuhusu Mkutano wa Kimataifa kuhusu  Rasilimali Endelevu za Majini utakalofanyika nchini Kenya kuanzia tarehe 26 hadi 28 Novemba 2018

Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Charles Faini (kushoto) akiwa na Bw. Medard Ngaiza, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Balozi Kazungu ambao hawapo pichani

Mhe. Balozi Kazungu akimweleza jambo Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa mazungumzo yao

Mhe. Balozi Kazungu akimkabidhi Mhe. Dkt. Ndumbaro moja ya nyaraka kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Rasilimali Endelevu za Majini utakaofanyika nchini Kenya.

Mhe. Dkt. Ndumbaro akiagana na Balozi Kazungu mara baada ya mazungumzo kati yao

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Namibia nchini



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi akisalimiana na Balozi wa Namibia nchini, Mhe. Theresa Samaria alipofika Wizarani kwa ajili ya kumsalimia na  kuzungumzia kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia kwenye sekta mbalimbali ikiwemo biashara, kilimo, uvuvi na mifugo. Mazungumzo hayo yamefanyika tarehe 19 Novemba, 2018.
Mhe. Balozi Samaria akimweleza Dkt. Kasidi kuhusu fursa mbalimbali za biashara ambazo Tanzania inaweza kuzichangamkia kwenye nchi yake ambayo ina ukame uliokithiri kutokana na kuzungukwa na Majangwa ya Kalahari na Namib. Fursa hizo ni pamoja na biashara ya nyama, matunda, nafaka mbalimbali na korosho.
Mazungumzo yakiendelea huku Afisa aliefuatana na Balozi Samaria akinukuu
Katibu Mkuu, Dkt. Kasidi akisoma nyaraka aliyopatiwa na Balozi Samaria ambayo ni mkataba ulioanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia miaka 20 iliyopita. 

Dkt. Kasidi akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Samaria mara baada ya kumaliza mazungumzo yao


Piacha ya pamoja kati ya Dkt. Kasidi na Balozi Samaria pamoja na  Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Namibia nchini walioshiriki mazungumzo kati ya viongozi hao