Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) ukiendelea jijini Durban, Afrika Kusini. |
Friday, September 16, 2022
BALOZI MINDI ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA WANAWAKE WA AFRIKA KATIKA UONGOZI
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga ameelezea uzoefu wa Tanzania kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia na uongozi wakati akiwasilisha mada katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) unaoendelea jijini Durban, Afrika Kusini.
Mkutano huo ambao umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 15-17 Septemba 2022, chini ya wenyeji wa kiongozi wa Jimbo la KwaZulu-Natal Bi. Nomusa Dube-Ncube, hufanyika kila mwaka kwa kuwaleta pamoja viongozi wanawake kutoka Bara la Afrika ili kujadili masuala yanayohusu usawa wa kijinsia na uongozi.
Miongoni mwa waliohuduhuria mkutano huo ni pamoja na viongozi mashuhuri katika siasa, Sekali na makampuni binafsi kutoka nchini. Liberia, Nigeria, Tanzania, Cameroon, Rwanda, na wenyeji Afrika Kusini.
Kongamano lijalo linatarajiwa kufanyika Agosti 2023 jijini Arusha, Tanzania.
Thursday, September 15, 2022
MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR AFUNGA MKUTANO WA WANAWAKE NA VIJANA KATIKA BIASHARA WA AfCFTA
Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya kufunga mkutano huo. |
Sehemu nyingine ya washiriki wakifuatilia hotuba ya kufunga mkutano huo.
|
WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA MABALOZI WATEULE WA FINLAND, CANADA NA HISPANIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiendelea na mazungumzo na Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa baaada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho jijini Dar Es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Hispania nchini Tanzania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Hispania nchini Tanzania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez |
Balozi Mteule wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alipowasili ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimpokea Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe aliyekuja ofisini kwake kufanya mazungumzo kuhusu ushiikiano wa mataifa yao
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiendelea na mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe |
TANZANIA NA DRC ZAAHIDI UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA MKUTANO WA JPC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisoma hotuba ya kufunga Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) uliofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022
|
Waziri wa Mtangamano wa Kikanda na Nchi zinazozungumza Kifaransa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Didier Mazenga Mukanzu akisoma hotuba ya kufunga Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) uliofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula na Waziri wa Mtangamano wa Kikanda na Nchi
zinazozungumza Kifaransa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Didier Mazenga Mukanzu wakisaini Taarifa ya Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) uliofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula na Waziri wa Mtangamano wa Kikanda na Nchi zinazozungumza Kifaransa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Didier Mazenga Mukanzu wakibadilishana Taarifa ya Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) uliofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimpa zawadi ya picha za kuchora za twiga Waziri wa Mtangamano wa Kikanda na Nchi zinazozungumza Kifaransa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya Kongo (DRC), Mhe. Didier Mazenga Mukanzu |
Picha ya pamoja ya viongozi Wakuu walioshiriki Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) uliofanyika jijini Dar Es Salaam |
WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui katika Ofisi Ndozo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Septemba 2022. Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa yao katika sekta za uwekezaji, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu, biashara, usafiri na uchukuzi, nishati, kilimo, uchumi wa blue, elimu na utamaduni. Pia wamejadili umuhimu wa kuwa na kamati za kitaifa kwa ajili ya ufuatiliaji wa masuala ya msingi ya utekelezaji yaliyokubaliwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Ufarasa mwezi Februari 2022, pamoja na masuala mengine ya ushirikiano baina ya nchi zao. Vilevile wamejadili juu ya mchango unaotolewa na serikali ya Ufaransa katika masuala ya ulinzi wa amani pamoja na nafasi ya tanzania katika kusimamia masuala ya ulinzi na amani kikanda hususan katika Nchi wanachama za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC), Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na katika Umoja wa Afrika (AU). |
Mhe. Nabil Hajlaoui akimweleza Mhe. Balozi Liberata Mulamula jitihada zinazofanya na Serikali yake katika kuunga mkono jitihada za kusaidia shughuli za maendeleo barani Afrika kwa kushirikiana na mataifa mengine ya Ulaya walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Septemba 2022. |
Mhe. Balozi Mulamula akiagana na Mhe. Nabil Hajlaoui baada ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Septemba 2022. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Picha ya Pamoja, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa pili kulia), Mhe. Nabil Hajlaoui (wa pili kushoto) na maafisa waliombatana nao katika mazungumzo yao. |
TANZANIA YAPONGEZWA KWA KUWA MWANACHAMA HAI WA UMOJA WA AFRIKA
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Monique Nsanzabaganwa alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula pembezoni mwa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) uliofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 Jijini Dar es Salaam.
Akifafanua shughuli za utekelezaji zinazofanywa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Nchi Wanachama Mhe. Nsanzabaganwa alieleza kuwa Tanzania ni miongoni mwa wadau muhimu katika Umoja wa Afrika ambapo, licha ya nafasi yake ya kuunga mkono uanzishwaji wa umoja huo pia imekuwa ikikamilisha michango yake ya uanachama kwa wakati.
"Ukamilishaji wa michango kwa wakati kutoka kwa Nchi wanachama unawezesha uendeshaji wa shughuli za Sekretarieti kutekelezeka kwa tija na kusaidia kupatikana kwa maslahi ya watumishi." alisema Mhe. Nsanzabaganwa.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amemuhakikishia Mhe. Nsanzabaganwa kuwa Tanzania itaendelea kuheshimu makubaliano yaliyokubaliwa katika Umoja wa Afrika sambamba na kuhakikisha inanufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana kama vile ajira na biashara.
Pia ameshukuru kwa jitihada zinazofanywa na Umoja wa Afrika kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) kwa kumtambua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Kinara wa Uhamasishaji wa Masuala ya Wanawake na Vijana katika biashara, sambamba na heshima iliyotolewa kwa Tanzania ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika.
Aidha, Mhe. Waziri amesema kuwa mkutano huo ni muhimu sana kwakuwa umebeba agenda ya wanawake na vijana yenye lengo la kujenga haki na usawa wa kijinsia katika ajira, kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira, kuwajengea uwezo na kushirikishana uzoefu katika biashara na kuingia katika ushindani wa biashara kitaifa, kikanda na kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Monique Nsanzabaganwa katika ofisi za Wizara jijini Da es Salaam tarehe 14 Septemba 2022. |
Mazungumzo yakiendelea |
Picha ya pamoja baada ya mazungumzo. |
Wednesday, September 14, 2022
Tuesday, September 13, 2022
BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDONESIA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele mapema leo tarehe 13/09/2022 amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Indonesia Mhe. Joko Widodo katika hafla iliyofanyika kwenye Kasri la Merdeka jijini Jakarta.
Katika hafla hiyo, wawili hao walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji.
Hatua hiyo ya Mhe. Balozi Makocha Tembele kuwasilisha hati zake za utambulisho inaashiria kuanza rasmi kwa utumishi wake katika nchi hiyo.
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo |
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akiwasili katika Kasri la Merdeka jijini Jakarta ambapo aliwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Indonesia Mhe. Joko Widodo |
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akisalimiana na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo |
Monday, September 12, 2022
TANZANIA YASISITIZA KUBORESHA MIFUMO KUWAINUA WANAWAKE NA VIJANA KIUCHUMI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kusimamia mifumo ya utendaji kazi katika Serikali yake ili kuwawezesha wanawake na vijana washiriki kikamilifu katika biashara.
Ahadi hiyo imetolewa wakati wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara ulioandaliwa na Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) na kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022.
Akiongea katika mkutano huo, Mhe. Rais Samia ameeleza baadhi ya maeneo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita imeyafanyia maboresho ili biashara zinazofanywa na Wanawake na Vijana nchini zilete matokeo chanya sambamba na kuinua kipato chao na uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Maeneo hayo ni pamoja na: Kuondoa vikwazo vya biashara, kuwawezesha wanawake kupata mikopo ya riba nafuu, maboresho katika mifumo ya tozo katika sekta mbalimbali kama vile kilimo na madini, kuwezeshwa kupata vyeti vya ubora kwa ajili ya kuingia katika ushindani wa soko la kimataifa na kupunguza ushuru unaotozwa na mamlaka mbalimbali za Serikali.
Aidha, Mhe, Rais Samia amesema kuwa Serikali yake inatoa nafasi za upendeleo kwa sekta binafsi kushiriki katika shughuli za maendeleo, na kwa sasa Tanzania imetoa kipaumbele kwa wanawake ambapo asilimia 30 ya manunuzi yote makubwa ya Serikali yanatolewa kwa makampuni ya wanawake.
“Mapema mwezi Mei 2022 nikiwa nchini Ghana kwenye mkutano ulioratibiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Ghana ambao uliwakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali nilipewa heshima ya kuwa kinara wa hamasa ya kuinua Wanawake na Vijana kwenye biashara, hivyo naahidi kuendelea kusimamia mapambano hayo”. Alisema Mhe. Rais Samia.
Akieleza zaidi, Mhe. Rais Samia ameeleza kuwa ili kufikia malengo ya kuinua biashara ni vema sasa nchi za Afrika zikawekeza kwenye miundombinu ili ziweze kufikika na kurahisisha shughuli za biashara kwa wananchi wake ambapo sehemu kubwa ya wajasiliamali wake ni wanawake na vijana.
Pia amesisitiza kuwa manufaa ya itifaki ya Wanawake na Vijana katika biashara kwenye Mkataba wa Eneo Huru Barani Afrika hayawezi kupatikana moja kwa moja kama mipango ya kitaifa ya nchi wanachama haitowajumuisha wanawake na vijana katika utekelezaji wake.
Hivyo, ni vema nchi wanachama zikawekeza pia kwenye tafiti ili kufahamu namna bora ya kuondoa changamoto kwenye uhalisia wa jambo husika ambapo alieleza kwa nyakati tofauti Tanzania imefanya tafiti katika masoko ili yaweze kunufaisha wanawake na kusaidia kuwajengea miundombinu wezeshe kwa shughuli za biashara.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais ameeleza kuwa Tanzania inaandaa mpango wa kusimamia usawa kwa kizazi kijacho ili kuwawezesha wanawake kupata fursa sawa na wanaume na kuhakikisha wanawake na vijana wanawezeshwa kiuchumi na kuwekewa mfumo utakaowawezesha kupata ajira rasmi na zenye ujira utakaowainua kiuchumi kwa maendeleo ya Taifa.
Mhe. Rais Samia pia alitumia fursa ya mkutano huo kunadi fursa za uwekezaji zilizopo nchini katika sekta za kilimo cha mazao ya chakula, matunda na mbogamboga, sekta ya mifugo hususan nyama na bidhaa za ngozi, madini na utalii.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Mhe Balozi Liberata Mulamula katika mkutano huo aliongoza majadiliano yaliyokuwa na mada isemayo “Kuunga mkono Uongozi wa Wanawake na Vijana katika Biashara” (Supporting Women and Youth’s Leadership in Trade).
Mjadala huo ulihusisha viongozi wakuu wanawake wa nchi za Afrika ambao ni: Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Joyce Banda, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Dkt. Jewel Taylor-Howard, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo, Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika,Mhe. Wamkele Mene na Naibu Mwenyekiti, Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Dkt. Monique Nsanzabaganwa.
Washiriki wengine wa mkutano huo ni pamoja na: Mabalozi, Mawaziri wanaohusika na Biashara na Mawaziri wanaohusika na masuala ya jinsia. wanawake na vijana wanaojishughulisha na masuala ya biashara, watunga será na wadau wa maendeleo.
Sanjari na mkutano huo, wajasiriamali zaidi ya 80 wameshiriki kwenye maonesho ya bidhaa mbalimbali ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina washiriki wapatao 72.
==============================================================
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
|
Sehemu ya Mawaziri na Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. |
|
Katibu wa Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Bw. Seif Kamtunda akifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. |
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akisherehesha wakati wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. |
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akisalimiana na sehemu ya Mawaziri walioshiriki Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. |
Picha ya pamoja |
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongoza majadiliano yaliyokuwa na mada isemayo “Kuunga mkono Uongozi wa Wanawake na Vijana katika Biashara” (Supporting Women and Youth’s Leadership in Trade) wakati wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. |
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Joyce Banda akichangia hoja kwenye majadiliano yaliyokuwa na mada isemayo “Kuunga mkono Uongozi wa Wanawake na Vijana katika Biashara” (Supporting Women and Youth’s Leadership in Trade) wakati wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. |
Majadiliano yakiendelea. |
Picha ya pamoja, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Joyce Banda (wa pili kushoto) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Dkt. Jewel Taylor-Howard (wa pili kulia), Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo (katikati) na Naibu Mwenyekiti, Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Dkt. Monique Nsanzabaganwa (wa kwanza kushoto). |
Subscribe to:
Posts (Atom)