Mazungumzo yakiendelea |
Thursday, November 9, 2017
Wednesday, November 8, 2017
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Mjumbe Maalum kutoka Norway
Mazungumzo yakiendelea. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanne Marie Kaarstad. |
Prof. Mkenda na Balozi Oyen wakimsikiliza Balozi Kaarstad mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao |
Prof. Mkenda akiagana na Balozi Oyen |
Katibu Mkuu Prof. Mkenda afanya Mazungumzo na Balozi wa Japan Nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akiwa katika mkutano na Balozi wa Japan nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida alipomtembelea Wizarani leo tarehe 08 Novemba,2017. Katika Mkutano huu walizungumzia masuala mbalimbali yanoyohusu uhusiano kati ya Tanzania na Japan hasa katika eneo la uwekezaji.
Prof.Mkenda akipokea zawadi ya Kalenda ya Mwaka 2018 kutoka kwa Mheshimiwa Balozi Yoshida, kalenda hiyo ni maalum yenye picha zinazoelezea utamaduni wa Japan.
Katibu Mkuu Prof. Mkenda na Mhe. Balozi Yoshida pamoja na maafisa kutoka Wizarani na Ubalozi wa Japan wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya Mkutano.
Waziri Mahiga amkaribisha rasmi Wizarani Katibu Mkuu mpya Prof.Mkenda
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Waziri Mahiga (hayupo pichani) |
Sehemu nyingine ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia kikao |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akiwasalimia Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) mara baada ya kukaribishwa rasmi Wizarani. |
Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) |
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara |
Watumishi wengine wa Wizara |
Tuesday, November 7, 2017
Waziri Mahiga akutana na Kamishna wa Umoja wa Ulaya
Mkuu wa mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Roeland van de Geer pamoja na afisa wa Ubalozi huo wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea. |
Afisa Mambo ya Nje, Bw. Salvatory Mbilinyi na Afisa aliyeambatana na kamishna wakifuatilia mazungumzo. |
Picha ya pamoja. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Friday, November 3, 2017
Msichana wa Kitanzania kuiwakilisha nchi Mkutano wa Dunia wa Vijana
Picha ya pamoja |
Thursday, November 2, 2017
Balozi Mbarouk akabidhi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran
Wednesday, November 1, 2017
Naibu Waziri Mhe.Dkt Suzan Kolimba afanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Wizarani
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan Kolimba(Mb) akiwa katika mkutano na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya simu ya Halotel nchini Bw. Pham Dinh Quan alipomtembelea Wizarani jana tarehe 31 Oktoba,2017, Dar es salaam.
Katika Mazungumzo yao Bw. Quan alisema kampuni ya halotel hadi sasa imewekeza katika eneo kubwa la Tanzania hasa vijijini, alisema hadi sasa Kampuni hiyo imewekeza asilimia 80 ya eneo la Tanzania na wana mpango wa kuongeza uwekezaji zaidi katika eneo ambalo halijafikiwa. Mhe. Dkt. Kolimba alipongeza kampuni ya Halotel kwa uwekezaji huo mkubwa ambao umesaidia kurahisisha mawasiliano nchini hasa Vijijini.
Mkutano huo ukieendelea.
Saturday, October 28, 2017
Waziri Mahiga azitaka taasisi kutoa fursa za ajira kwa vijana
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga leo ameongea na vijana kupitia kongamano la Ubalozi Youth Forum lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Waziri Mahiga katika hotuba yake amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Taasisi mbalimbali za Kimataifa na za ndani na makampuni binafsi. Waziri Mahiga amezitaja baadhi ya fursa hizo kuwa ni nafasi za ufadhili wa masomo ya elimu ya juu (scholarship) na mafunzo mbalimbali kama vile ujasiriamali, teknolojia, ajira na biashara.
Kongamano hilo lililenga kuwaelimisha vijana kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye Taasisi za Kimataifa zilizopo nchini na Makampuni binafsi na kuwahamasisha kuchangamkia fursa hizo. Vilevile kongamano hilo lilihudhuriwa na Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini Tanzania ambapo, vijana walipata fursa ya kuzungumza nao na kujifunza masuala mbalimbali kutoka kwa Wanadiplomasia hao.
Aidha katika Kongamano hilo vijana walipata fursa ya kuonesha bidhaa na huduma mbalimbali walizo zibuni, pia kuonesha bidhaa walizozalisha kutokana na miradi mbalimbali inayofadhili na Mashirika ya kimataifa. Miongoni mwa bidhaa zilizooneshwa ni mazao ya kilimo yaliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa (UN) chini ya mradi wa"ajira stahiki kwa vijana vijijini" (decent rural employment) ambapo hadi sasa jumla ya vijana 480 wamenufaika na mradi huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifuatilia kongamano la Ubalozi Youth Forum |
Sehemu ya Wanadiplomasia kutoa nchi mbalimbali Duniani wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakifuatila Kongamano |
Waziri Mhe.Mahiga akihutubia hadhira ya Ubalozi Youth Forum |
Waziri Mhe.Mhiga akiangalia moja ya bidhaa iliyobuniwa na kutengenezwa na kijana kwenye maonesho ya kongamano la Ubalozo Youth Forum yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam |
Friday, October 27, 2017
Program ya Uendelezaji wa Sekta ya Uchukuzi kwa njia ya Barabara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya Utatu wa COMESA-EAC-SADC yazinduliwa.
Sehemu ya wajumbe wa Tanzania wakifuatilia mkutano, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko. |
Sehemu ya wajumbe kutoka nchi wanachama wakifuatilia mkutano. |
Meza kuu wakiongoza Mkutano. |
Mkutano ukiendelea. |
Thursday, October 26, 2017
Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Mawaziri wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (TRIPARTITE)
Sehemu nyingine ya Wajumbe kutoka nchi Wanachama wakifuatilia Mkutano. |
Mkutano ukiendelea. |
Picha ya pamoja. |
============================================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MHE. WAZIRI MAHIGA AFUNGUA RASMI MKUTANO
WA KWANZA WA MAWAZIRI WENYE DHAMANA YA MASUALA YA MIUNDOMBINU WA NCHI WANACHAMA
WA JUMUIYA YA UTATU WA COMESA-EAC-SADC (TRIPARTITE) UNAOFANYIKA HAPA DAR ES
SALAAM LEO TAREHE 26 OKTOBA 2017
Mkutano wa
Kwanza wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC
umefanyika hapa Dar es Salaam, Serena Hoteli leo tarehe 26 Oktoba 2017. Mkutano
huo unahusisha jumla ya nchi 26 Wanachama wa Umoja huo. Mkutano huu unafanyika
hapa Tanzania kwa kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ndiyo Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC.
Mkutano huu
umefunguliwa na Mhe. Dkt. Augustine Phillip Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Mhe. Prof. Makame Mbarawa
(Mb), Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Kufanyika kwa Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya
Miundombinu kunatokana na maazimio ya Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi
Wanachama wa COMESA, EAC na SADC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini tarehe
14 Juni, 2011 ambao ulipitisha maeneo matatu ya kutekelezwa kwenye ushirikiano
wa Utatu wa COMESA – EAC – SADC. Maeneo hayo ni: 1) Kuunganisha Soko; 2)
Kuendeleza Miundombinu ili kuunganisha Nchi Wanachama kwa miundombinu iliyo
bora; na 3) Kukuza Viwanda.
Kwa upande wa Sekta za Miundombinu, huu ni Mkutano wa
Kwanza wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa
Utatu wa COMESA, EAC na SADC. Mkutano huu katika Ngazi ya Wataalam ulijadili
hatua zilizofikiwa na Nchi Wanachama katika uendelezaji wa miundombinu na
kupendekeza maamuzi ya kisera kwenye sekta za miundombinu ya uchukuzi
(barabara, reli, bandari, anga); teknolojia ya habari na mawasiliano; na
nishati.
Kwa ujumla Mkutano wa Mawaziri umepita na kujadili programu kuu
zifuatazo:
i.
Programu
ya Uendelezaji wa Sekta za Uchukuzi kwa njia ya Barabara kwa
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (Tripartite Transport and Transit
Facilitation Programme (TTTFP);
ii.
Taarifa
za utekelezaji wa miradi na programu kuhusiana na Sekta ya Miundombinu ya
Uchukuzi (Anga, Barabara, Reli na Bandari); Sekta ya Mawasiliano na Sekta ya
Nishati;
iii.
Maendeleo ya Kanda za Uchukuzi (Corridor Development) za Jumuiya ya Utatu wa COMESA, EAC na SADC,
ambapo hatua mbalimbali za Utekelezaji wa Vituo vya Kutoa Huduma kwa Pamoja
Mipakani (OSBPs) kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya hizo zimejadiliwa;
iv.
Utekelezaji
wa Programu ya Kikanda wa Uendelezaji wa Miundombinu katika Ukanda wa Afrika
Mashariki, Ukanda wa Afrika Kusini na Ukanda wa Bahari ya Hindi (Regional Indicative Programme for Eastern
Africa, Southern Africa and the Indian Ocean (2014 – 2020); na
v.
Utekelezaji wa Miradi ya NEPAD Presidential Infrastructure Championship Initiative (PICI);
vi.
Rasimu ya Mpangokazi wa shughuli za utatu wa COMESA-
EAC- SADC hususan uratibu wa mikutano ya miundombinu;
vii.
Utafutaji raslimali fedha za kuwezesha shughuli za
utatu wa COMESA- EAC- SADC; na
viii.
Uzinduzi rasmi wa Programu ya Uendelezaji wa Sekta za Uchukuzi kwa njia ya
Barabara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (Tripartite Transport
and Transit Facilitation Programme (TTTFP).
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Waziri Mahiga, pamoja na
kuwakaribisha Mawaziri nchini Tanzania na jijini Dar es Salaam, amesisitiza
umuhimu wa kuwa na miradi ya pamoja ya kuendeleza sekta ya miundombinu baina ya
Jumuiya za kikanda kama njia madhubuti ya kuwaletea maendeleo ya haraka
wananchi. Mhe. Mahiga pia amesisitiza kwamba Tanzania inathamini ushirikiano wa
kanda na hivyo itaendelea kushiriki kikamilifu katika juhudi za maendeleo za
kikanda ikiwemo zile za Jumuiya ya Utatu (Tripartite) kama njia mojawapo wa
utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda. Mwisho, Mhe. Mahiga amewatakia
mkutano mzuri Mawaziri wa Miundombinu akiwaomba kuibua mikakati na mapendekezo
madhubuti katika kuendeleza miundombinu katika eneo lote la UTATU.
Aidha, Mawaziri kwa pamoja, wakiongozwa na Mhe. Aggrey Henry Bagiire,
Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi wa Jamhuri ya Uganda na ambaye atakuwa ni
Mwenyekiti wa Mkutano huo kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, watazindua rasmi Programu
ya Uendelezaji wa Sekta za Uchukuzi kwa njia ya Barabara kwa Nchi Wanachama wa
Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (Tripartite Transport and Transit Facilitation Programme (TTTFP).
Uzinduzi huu utafanyika
leo tarehe 26 Oktoba, 2017 saa 9.00 Alasiri na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali
wa Serikali na Sekta Binafsi.
I
Imetolewa na,
KITENGO CHA MAWASILIANO
YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI,
TAREHE 26/10/2017
Subscribe to:
Posts (Atom)