Wednesday, December 6, 2017

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la China

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China, Mhe. CAO Weizhou alipofika Wizarani tarehe 06 Desemba, 2017. Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kindugu uliopo kati ya Tanzania na China. Pia Mhe. Dkt. Kolimba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kwa misaada mbalimbali inayotoa kwa Tanzania hususan katika sekta ya ujenzi wa miundombinu.
Sehemu ya ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou wakifuatilia mazungumzo. Wa pili kutoka kulia ni Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke.
Sehemu nyingine ya Ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou.
Sehemu ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutoka kushoto ni Bi. Justa Nyange, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia,  Bw. Charles Faini, Katibu wa Naibu Waziri,  na Bw. Halmesh Lunyumbu, Afisa  Mambo ya Nje 
Mhe. Dkt. Kolimba akiagana na Mhe. CAO mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Picha ya pamoja

Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Nigeria nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Nigeria nchini, Mhe. Dkt. Sahabu Isah Gada. Tukio hilo limefanyika Wizarani tarehe 06 Desemba, 2017.
Mhe. Dkt. Mahiga akionesha Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Gada mara baada ya kuzipokea.
Mhe. Dkt. Mahiga akiwa katika mazungumzo rasmi na Dkt. Gada
Sehemu ya ujumbe kutoka Ubalozi wa Nigeria.
Sehemu ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Balozi Gada (hawapo pichani). Kushoto ni Bw. Suleiman Saleh, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Bw. Nicholaus Joseph, Afisa Mambo ya Nje.
Mhe. Dkt. Mahiga akiagana na Balozi Mteule wa Nigeria nchini, Mhe. Dkt. Gada mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
Mhe. Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Gada na Mkewe mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi huyo.

Tuesday, December 5, 2017

Mhe. Waziri afanya mazungumzo na Balozi wa Korea nchini

    Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Augustine Mahiga (Mb) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Balozi Song,Geum-Young, alipomtembelea Wizarani, Dar es Salaam, tarehe 05/12/2017. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha mahusiano kati ya Korea na Tanzania.
 
    Mazungumzo yakieendelea


Mhe. Waziri na Mhe. Balozi wakipeana mkono baada ya mazungumzo

Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Poland nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Poland, Mhe. Krzysztof Buzalski. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mahiga akiongea na Mhe.Buzalski ambapo katika mazungumzo yao amemuhakikishia kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake awapo nchini.


Mazungumzo yakiendelea.

Waziri Mahiga amuaga balozi wa U.A.E aliyemaliza muda wake wa uwakilishi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiongea na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini (U.A.E), Mhe Abdulla Ibrahim Alsuwaidi alipomtembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Disemba 2017.

Mhe. Abdulla Ibrahim Alsuwaidi amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Mahiga amemshukuru kwa ushirikiano mzuri aliouonyesha alipokuwa nchini. Pia amemtakia safari njema na utekelezaji mwema wa majukumu mapya atakayopangiwa.

Mhe. Abdulla Ibrahimu Alsuwaidi akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Waziri Mahiga ambapo alitumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ujumla kwa kumwezesha kutekeleza vema majukumu yake katika muda wake wote wa uwakilishi hapa nchini. Pia akaahidi U.A.E itaendeleza kudumisha ushirikiano wa kidiplomasia pamoja na ushirikiano katika sekta za miradi ya maendeleo.

Mazungumzo yakiendelea.

Waziri Mahiga akimuga Balozi wa U.A.E aliyemaliza muda wake wa Uwakilishi nchini.

Mhe. Waziri akutana na Ujumbe wa Kamati ya Haki za Wapalestina

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga(Mb) akiongea katika mkutano na Ujumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Msingi za Wapalestina(Committee on the exercise of Inalienable rights of the Palestinian People), kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mwakilishi wa kudumu wa Senegal katika Umoja wa Mataifa, kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Deusdedit Kaganda. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 04/12/2017.

Ujumbe huo uliwasili nchini tarehe 02/12/2017, dhumuni la ziara hiyo ni kuendeleza mahusiano ya kisiasa na kidiplomasia kati ya Tanzania na Palestina, pamoja na kutoa elimu ya uelewa kwa jamii ya Watanzania kuhusu hali ya Wapalestina chini ya utawala wa Israel.
 
    Mhe. Waziri akipokea kitabu chenye  kuelezea Historia ya Watu   
  wa  Wapelestina kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati,
   Mhe. Riyad Mansour ambaye pia ni mwangalizi wa kudumu 
   kutoka Umoja wa Mataifa wa hali ya Palestina.

    Mhe. Waziri akiwa na Ujumbe wa Tanzania na Ujumbe wa  
   Kamati wakieendelea na Mazungumzo
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Mindi Kasiga wa  
   kwanza   kushoto, anayefuata ni Bi. Ellen Maduhu kutoka Idara 
   ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Gerald Mbafu Msaidizi wa 
   Waziri na nyuma yao ni waandishi wa Habari wakifuatilia    
  mazungumzo hayo.

   Ujumbe wa Kamati ukifuatilia mazungumzo hayo.

    Mhe. Waziri akizungumza na vyombo vya habari (hawako   
   pichani) baada ya Mkutano.

Thursday, November 30, 2017

Naibu Waziri afanya Mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia nchini

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Suzan Kolimba(Mb) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Balozi Mohammed M. Almalik alipomtembelea wizarani tarehe 30/11/2017. Lengo la Mazungumzo hayo ni kuzungumzia mahusiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia, Mhe.Balozi alisema hadi sasa Saudi Arabia wana jumla ya miradi  6 katika eneo la maji na afya, kati ya hiyo 3 iko Tanzania bara na 3 Zanzibar.

 
Mhe. Naibu Waziri Dkt Kolimba na Mhe. Balozi Almalik wakiendelea na mazungumzo, wanaofuatilia mazungumzo hayo ni Bw. Charles Faini Msaidizi wa Naibu Waziri(kulia) na anayefuata ni Bw. Odilo Fidelis, Afisa Mambo ya Nje.

Monday, November 27, 2017

Waziri Mahiga akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni alipomtembea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Novemba 2017.

Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Italia. Pia wamejadili mikakati ya kuboresha ushirikiano katika sekta ya elimu hususan elimu ya ufundi, miundombinu, utalii, biashara na uwekezaji.
Mazungumzo ya Kiendelea.



Saturday, November 25, 2017

Katibu Mkuu ashiriki Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na China

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Prof.Adolf Mkenda (kulia) akizungumza katika  wa Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na China

Katibu Mkuu Prof.Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Serikali ya Tanzania na wa Serikali ya Watu wa Jamhuri ya China mara baada ya kuhitimisha Mkutano na Benki ya Uwekezaji ya Asia.

Katibu Mkuu Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika Mkutano wa Ukanda Maalum wa Kiuchumi wa Uwanja wa ndege wa Hanan (Hanan Airport Special Economic Zone) uliofanyika nchini China.

Wajumbe wakifuatilia Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na China

Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza kwenye Mkutano wa  Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na China

Friday, November 24, 2017

Wizara kuongeza wigo wa matumizi ya kiswahili Afrika Mashariki

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba leo  akiongea na Wanachama wa Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA) amesema Wizara inaendelea na jitihada za kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo hadi sasa tayari baadhi ya nchi wanachama zimeshaweka lugha ya Kiswahili katika mitaala ya Elimu katika shule za Msingi na Sekondari  hatua ambayo itawezesha kuongeza wigo wa matumizi ya lugha hii katika Jumuiya yetu.

Mhe. Dkt Kolimba akizungumza katika kongamano hilo amewapongeza Viongozi na Wanachama wa Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki kwa kuwahusisha baadhi ya Ofisi za Balozi zilipo nchini katika hatua za kufanikisha Kongamono hilo. Kwa namna ya pekee alitumia fursa hiyo kumpongeza  Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Jaseem Al Najem na Watumishi wa Ubalozi huo kwa kukubamwaliko wa kushiriki Kongamano na kwa mchango waliotoa kufanikisha Kongamano hilo.

Tokea mwaka 2004 hadi sasa Kiswahili kimekuwa lugha ya kwanza ya Afrika kutumika katika vikao vya Ngazi ya Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika, hii ni kufuatia jitihada na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Jitihada hizo ilikuwa ni pamoja na kugharamia wakalimani kwa fedha za ndani, na mwaka 2008 Wizara iliishawishi Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuchukua jukumu hilo.

Aidha Mhe. Dkt. Kolimba amewahakikishia Viongozi na Wanachama wa CHAKAMA kuwa nia ya Serikali ya kufungua vituo vya kufundishia lugha ya  kiswahili  sehemu mbalimbali nje ya mipaka ya Tanzania bado iko palepale, "tayari tulishafungua kituo kimoja mwaka 2012 katika Ofisi za Kamisheni ya Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia" amesema Mhe. Dkt. Kolimba.

CHAKAMA imehitimisha Kongamano lake leo lililofanyika kwa muda wa siku mbili mjini Dodoma ,likiwa na kauli  mbiu ya "Kiswahili na Maendeleo ya Afrika Mashariki" chama hiki kinaundwa na nchi Wanchama za Jumuiya ya Afrika pia kinahusisha wanachama kutoka nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo Ghana na Zimbabwe.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba akihutubia washiriki wa kongamano la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki lililofanyika katika Hoteli ya African Dream mjini Dodoma

Naibu Waziri Mhe.Dkt. Susan Kolimba akimkabithi cheti cha ushiriki mmoja wa wajumbe wa Kongamo la CHAKAMA

Naibu Waziri Mhe.Dkt. Kolimba  akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kongamano



Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa akutana na Msajili wa UN-MICT

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akizungumza na Msajili wa Mfumo wa Kimataifa wa kumalizia mashauri masalia ya iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (MICT), Dkt. Olufemi Elias alipotembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Novemba 2017.

Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Caroline Chipeta na Maafisa mambo ya nje wakifuatilia mazungumzo.

Maafisa walioambatana na Msajili wa UN-MICT wakifuatilia mazungumzo.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje ziarani China kushiriki Mkutano wa FOCAC

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akifungua Mkutano wa kuvutia wawekezaji uliofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini China na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Makampuni 100 yenye nia ya kuwekeza Barani Afrika. Prof. Mkenda yupo nchini China kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC unaofanyika kwa ngazi ya Watendaji.
Prof. Mkenda akizungumza na Kiongozi wa Benki ya AIIB iliyoanzishwa kwa lengo  la kutoa mikopo kwa miradi ya miundombinu kwa nchi wanachama wa Belt and Road. Benki hiyo imeikaribisha Tanzania kujiunga nayo ili iweze kufaidika na fursa za mikopo nafuu. Vilevile, Prof. Mkendaamekutana na uongozi wa Kampuni ya Hainan Group inayomiliki mashirika mbalimbali ya ndege na Hoteli zaidi ya 1000 ulimwenguni. Katika mazungumzo hayo Prof. Mkenda amewashawishi wawekeze kwenye ujenzi wa Hoteli katika maeneo ya Utalii Zanzibar na Tanzania Bara.
Ujumbe ukifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Kiongozi wa Benki ya AIIB (hawapo pichani).  Kutoka kushoto ni Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Lu Yongqing, aliyekuwa Balozi wa China nchini Tanzania na Mhe. Mbelwa Kairuki, Balozi wa Tanzania nchini China.
Ujumbe kutoka Benki ya AIIB
Prof. Mkenda akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua Mkutano wa Kuvutia Wawekezaji uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini China.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Chen Xiaodong akifungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika unaofanyika tarehe 24 Novemba, 2017 Beijing, China. Baada ya ufunguzi kiongozi huyo amefanya mazungumzo ya kukuza ushirikiano na nchi nne Tanzania ikiwa ya kwanza kukutana nayo. Katika mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Mhe. Xiaodong, China imeahidi kuendeleza ushirikiano katika nyanja  za uchumi hususan kwenye ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. CHEN Xiaodong mara baada ya kukamilisha mazungumzo ya ushirikiano kati ya Tanzania na China.